WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, November 2, 2015

RAISI MTEULE WA WA AWAMU YA TANO - HAPA NI KAZI TU




MHESHIMIWA DR. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI NA TANZANIA MPYA: 2015- 2020


JE RAISI WA AWAMU YA TANO MHESHIMIWA Dr. JOHN POMBE MAGUFULI ATAKUWA  KAMA RAISI  PARK  CHUNG   ALIYEIJENGA SOUTH KOREA KWA MUDA MFUPI KIMAENDELEO?


MAENDELEO YA NCHI YANATEGEMEA SANA MAONO (VISION) YA KIONGOZI AMBAYE YUKO MADARAKANI.
JE FALSAFA YA MHESHIMIWA MAGUFULI NI SAWA NA USEMI HIZI?

Give a person a fish: you have fed the person for today.  Teach a person to fish: you have fed the person for a lifetime.”

Kumpa mtu samaki utakuwa umemlisha katika siku ya leo; ukiweza  Kumfundisha mtu  namna ya kuvua samaki  utakuwa umeweza kumsaidia kumlisha katika maisha yake yote.

Teach the person how to process and package fish for export and market it, and you have stimulated economic development.

Ukiweza kumfundisha mtu namna ya kutengeneza na kusafirisha na kuweza kuuza samaki katika masoko ya nje; utakuwa umefanikiwa kuchochea maendeleo ya kiuchumi

Park Chung Hee
 alikuwa kiongozi wa Korea ya Kusini kuanzia mwaka 1961-1970 alipo uwawa.Park Chung Hee alikuwa dikteta lakini alikuwa Rais ambaye alifanya Korea ya Kusini leo hii kuonekana tajiri. Alipoingia madarakani mwaka 1961 alikuwa na vision na vipaumbele ya maendeleo ya nchi yake kwa kutilia mkazo maendeleo ya  Elimu, kukuza technologia (ICT),Kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwa na nidhamu ya kazi (discipline) na kusimamia ukuaji wa Nishati.

Kwa taathimini ya kiuchumi wakati Park anaingia madarakani uchumi wa Korea ya Kusini ulikuwa sawa na  hali ya uchumi tunaoulaamikia sisi watanzania yaani uchumi duni na maisha magumu;


Kutokana vision na uzalendo wake kwa kujitoa kwa utendaji bora  na usimamiaji bora wa rasilimalia za taifa lake  leo hii Korea ya Kusini ni moja ya nchi zenye uchumi imara dunia na inashindana na hata kuogopewa na nchi ambazo ni tajiri duniani.

Ni takribani zaidi ya miaka 30 toka alipouwawa lakini tafiti zinaonyesha kuwa amebaki kuwa na rekodi bora ambayo imeisaidia nchi yake katika umaarufu ambao Korea ya Kusini inafurahia leo; Park alisaidia sana katika kusimamia ukuaji wa uchumi na usambazaji wa kasi  wa uwiano wa kipato, ikilinganishwa na mataifa mengine.  Kwa usimamiaji wake bora wa maendeleo kwa wote, Rais Park ilijulikana kama "unforgettable" miongoni mwa Wakorea kwa sababu ya ujuzi wake na nguvu ya usimamiaji wa maendeleo kwa wote.


Kwa nini alifanikiwa katika kuboresha uchumi wa nchi yake?
Rais Park alikuwa na tabia moja mimi naiona ni nzuri ambayo iliwashangaza waandishi wengi  ndani ya ofisi yake kuwa kuta zilitapakaa michoro ya takwimu, ikiwa ambazo zilikuwa zikionyesha  mwenendo wa biashara, ukusanyaji wa kodi na taarifa za maendeleo ya viwanda ambayo katika nchi yeyote ile ni nguzo imara ya maendeleo. Kiongozi yeyote mwenye  maono ya  namna hii lazima awe kiongozi bora kwa maendeleo ya nchi yake. Kila kiongozi mwenye dhamana alitakiwa kila mara kuje kumweleza repoti ya maendeleo ya wizara yake au sehemu yake ya kazi kwa kumweleza kwa maneno maandishi na michoro takwimu ya utendaji wake kwa manufaa ya watu wa korea ya kusini.

Swali hapa viongozi wetu wanatumia muda wao mwingi wakiwa ofisini wanakuwa wanawanasomo repoti gani za aina gani? Wanafuatiliaje utekelezaji wa maendeleo ya wizara zao au idara zao au 
Kusoma magazeti tu? 

Je viongozi wetu wanakuwa na muda wowote wa kufuatilia ukuaji wa uchumi wa taifa kupitia ofisi zao?



Jambo jingine ambalo ni msingi sana ambalo pengine viongozi wetu wanatakiwa kulitilia mkazo wanapo yaangalia maendeleo ya kiuchumi kwa nchi yetu kwa  kuendelea kutilia mkazo katika kujenga uwezo wa kiufundi unaotokana na elimu ubora katika fani ya sayansi na teknolojia. Uwezo wetu wa kiufundi ni nguvu itakayo liwezesha Taifa kuendelea kwa kasi ya haraka na kututoa katika udidimizi wa uchumi ambao tunaulalamikia leo: umasiki wa taifa letu hautaondoka kwa kelele za kisiasa, utaondoka kwa utendaji na kuwa na watendaji wazuri ambao wanaona kuwa umasikini na janga la taifa na unawakera;

Kama taifa “pengine” tuna tunatumia misaada vibaya, lengo la misaada ambayo nchi Hisani hutoa kwa taifa ni katika katika kutatua kero ya uchumi unaotusumbua na na kuyafanya maisha ya watanzania kuendelea kuwa duni. Matumizi bora ya misaada ya kigeni, katika miradi ya miundombinu sahihi ni suluhisho namba moja wa umasikini wetu.

Watendaji wetu kuanzia Kiongozi wa juu kabisa wa Serikali yaani Rais na wengine wote wanaomfuata wanatakiwa wawe na uwezo wa Kujenga kuboresha uchumi, kupitia sera  na  kuhakikissha kuwa wanakuwa na  mitazamo yakimaendeleo kwa kukuza mifumo ya kiutawala na sera zinazolenga zaidi katika kusimamia maisha na ukuaji wa uchumi wa nchi ili tuweze kuondokana na tatizo kubwa la umasikini wa Taifa letu.

Nimejaribu kueleza hayo yote ili kuonyesha kuwa bila kuwa na uongozi wenye maono usiotafuta faida yake wenyewe, usiokuwa tayari kuwawajibisha watendaji wabovu na wanaokiuka maadili uvunja sheria  hatuwezi kutoka hapa tulipo, tutaendelea kufurahia
kauli mbiu ambazo hazina maana wala msingi mkubwa kwa maendeleo ya Taifa. Kama historia inavyo onyesha kuwa Rais Park aliingia madarakani kwa kupindua uongozi ulikuwa madarakani lakini lengo lake lilikuwa maendeleo ya Korea kusini katika hali yeyote na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kipindi chake kama kiongozi wa nchi.

Katika kampeni zilizokuwa zikifanyika katia ya Chadema na CCM tumejifunza mengi na kama taifa hatimaye tumefanya uamuzi sahii wa kumchagua kiongozi mwadilifu ambaye katika makala iliyopita nilizioredhesha sifa za kiongozi ambaye Taifa la Tanzania linamwitaji kwa sasa;

Mheshimiwa John Pombe Magufuli katika kipindi chote cha kampeni ameweza kuelezea ilani ya chama chake na kufafanua jinsi ambavyo atawezesha kulivusha Taifa la Tanzania katika mabadiliko ya maendeleo ambayo kama taifa tunayahitaji kwa sasa;


Kwangu Mimi Mheshimiwa Magufuli ni Park Mwingine ambaye anauchungu sana na nchi hii; ametuahidi kuwa atakuwa msimamizi wa khali ya juu wa utekelezaji wa mpango wa mabadiliko ambayo kama taifa tunayahitaji kwa sasa; katika kampeni alituhahidi kuwa  hana mchezo hata kidogo katika hili  na hatakuwa na msamaha kwa wale wote ambao hawakufikia malengo ambayo serikali yake na chama kimeainisha katika ilani ya uchaguzi. Ameshatoa onyo kwa viongozi na wafanyakazi kuwa hayuko tayari kuona kuwa rasilimali ya taifa inachezewa na wajanja
wachache, ikibainika serikali yake itawafukuza kazi bila huruma;
Kwa Dr, Magufuli  ufanisi ulikuwa unapimwa kwa uwajibikaji na sio propaganda za kisiasa.

Mheshimiwa Magufuli amepania kurudisha kwenye kamusi maneno uwajibikaji na uwajibishaji kwa watendaji wa serikali katika taasisi zake na idara zake,  na ameamua kuondoa kabisa kwenye kamusi maneno utashi wa kisiasa urafiki na undugu ambao ndio ulikuwa unatawala uwajibikaji wa utumishi wa watendaji wa serikali.

Mheshimiwa Magufuli anaamini kuwa  hakuna maendeleo ya kweli kama ututaendelea kuendekeza utashi wa kisiasa; ni dhahiri kuwa tuhesabu kuwa hakuna maendeleo ya haraka yatapatika katika nchi yetu; tukumbuke kuwa majukumu  ya kiserikali yakizingatia zaidi, urafiki na undugu basi tujue kuwa hakuna uwajibishai wowote utakao fanyika kutoka ndani ya serikali na kama utafanyika basi utatokana na shinikizo kubwa kutoka kwa wananchi; tuandike maumizu katika kulitoa Taifa hili kutoka katika dimbwi la umasikini na  vision za viongozi wetu zitabaki zaidi za kwenye makaratasi ambazo zinakosa sana kipaumbele na kuthubutu. Hivyo Mheshimiwa Magufuli amethubutu na yuko tayari kulisimamia hili kwa ajili ya maendeleo ya taifa hasa katika kuwasaidia wanyonge masikini katika kunufaika na rasilimali za taifa lao.

Mheshimiwa Magufuli katika kauli yake ya kushukuru mara baada ya kuchaguliwa kuwa mgombea wa chama cha mapinduzi  kauli mbiu imeendelea kuwa  sitawaangusha hapa ni kazi tu; katika imani kuwa ameona umasikini na tabu ya Taifa hili hivyo kama watanznia walivyojenga imani kwake hivyo naye ameweka juhudi zote katika jusimamia kwa dhati kabisa rasilimali za Taifa ili kurudisha matumaini  makubwa na serikali yake kwa wananchi kwa maendeleo yao.

Binafsi kama mtanzania na mfuatiliaaji wa utendaji wa kazi  Dr.
John Pombe Magufuri pamoja na mapungufu yake kama binadamu amekuwa miongoni mwa viongozi wachachce ;
ambaye daima hana tabia ya kupenda kuona watendaji ambao wako chini yake wanatenda kazi kwa mazoea; daima ameonyesha kuthubutu katika kutekeleza sheria na kuwashugulikia watendaji wabovu  huku akiwa tayari kufuata sheria na kujielimisha ili aweze kuzielewa zaidi sheria za nchi na wizara husika;  kwa keli ni ni msimamiaji mzuri wa sheria katika utendaji hata kama wakati mwingine maamuzi yake yanakuwa kero kwa kwa watendaji wenzake wanaomzunguka.


Kimsingi kama nilivyoainisha hapo juu inawezekana magufuli
akawa na madhaifu yake lakini huwezi kuondoa ukweli kuwa ni miongoni mwa viongozi wachache ambap wametumikia taifa hili   
vizuri kiutendaji na hata kuchukua hatua kali kwa wakati za kiutendaji pale ilipotakiwa. Hilo hata wananchi wa kawaida wanalijua na jamii ndio inayo msafisha daima.

Angalia jinsi anavyosimamia sheria namba 18 ya mwaka 2007 ambayo ilisainiwa na Rais mwenyewe ambayo inakataza watu kuingilia eneo la hifadhi ya barabara kwa kujenga makazi au kufanya biashara; pamoja na Mheshimiwa Rais na waziri Mkuu kumpunguza kasi lakini msimamo wake uko pale pale.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadiki aliwahi sema kuwa “Hatukatai hata kama ana upungufu wake, basi apewe sifa katika yale mazuri anayoyafanya, lakini ukweli ni wazi kuwa Magufuli ni kiongozi mchapakazi na msimamizi mzuri wa sheria na hilo halipingiki,” Akiendeleza sifa hizo Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka, alisema siku zote utendaji kazi wa Magufuli unafuata sheria na taratibu “Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, wengi tunamtambua Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya, tunakuomba uendelee kufanya hivyo hivyo wala hutofeli na ukiendelea na moyo huo sote hatutafeli,” aliongeza Kabaka.


Serikali mpya ya Mheshimiwa Magufuli inatakiwa ichukue tahadhari mapema wasiendelee kufanya kazi na watendaji wabovu; Kumbuka, samaki mzuri akichanganyika na samaki waliooza lazima achafuke uvundo. Viongozi wetu ambao watapata dhamana ya kuongoza katika hii awamu mpya  wanatakiwa wajipange upya waache porojo za kujitetea kwa maneno matendo yao ndio yatakuwa utetezi wao;  wajitete kwa vitendo ambavyo vina tija kwa wananchi kwa maendeleo ya Taifa;

Watanzania wamemchagua mheshimiwa Magufuli kwa sababu utendaji wake kazi mzuri na kuwa kiongozi ambaye ameonyesha kiwango cha juu cha maadili; na ameonyesha katika kampeni zake kuwa yuko tayari kuwavusha wananchi  kuelekea katika bandari ya salama na yenye amani na maisha bora.

Magufuli ameonyesha upendo wa juu kabisa sio tu kwa wana ccm bali kwa watanzania wote bila kujali itikadi zao au dini zao au makabila yao. Ni kiongozi ambaye anaonyesha  upendo kwa wananchi wote; kwake uongozi ni kwa ajili ya wote na sio watu wachahce tu.

 

Tukumbuke kuwa kuwa uongozi ni dhana nzito ya kuaminiwa ambayo unakabiziwa na watu; lakini na kwa  kuwa uongozi wa kweli ni matokeo ya kuwa na maadili mazuri. Tukumbuke kuwa kuweza kutekeleza majukumu yako vizuri, Lazima kuwe na uhuisano wa karibu kati ya uongozi na mwongozo.

Mheshimiwa Magufuli tunaweza sema kuwa  amejitambua mwenyewe kuwa kazi moja ambayo anakabiliwa nayo ni kuwaletea mabadiliko wananchi wa Tanzania hivyo amejiaamini wewe mwenywe kuwa anaweza kufanya hivyo hivyo anayo mizizi ya huruma na uvumilivu ndani  na ni mtu ambaye haogombi kushindwa

Kiongozi bora atahangaika kuhakikisha kuwa maisha ya wananchi wake yanasonga mbele na kuwa na misha bora. Ukiwa mnyonyaji wewe ni kiongozi mbovu; viongozi ni viashiria vya mabadiliko katika jamii, na kuendeleza mafanikio tukumbuke kuwa sio vigumu kumtawala mtu ila jukumu ni kumwendeleza mtu.

Viongozi wanaishi kwa kuelewa mazingira na tabia za watu; kiongozi lazima awe tayari kuyapokea mabadiliko kila kitu kinaendelea kubadilika; kiongozi lazima ajue kuwa haitakiwi kuogopa awe tayari kujifunza na kamwe ahitimu shule ya mabadiliko, kiongozi lazima awe tayari kuishi na mabadiliko  na kuonyesha mfano wa yeye kuwa kinara wa mabadiliko. kiongozi mzuri anajua mapungufu ya watu wake, mapungufu yetu yanakamilishwa na wengine ambao wanautaalamu zaidi.

 

uvumilivu ni nguzo muhimu kwa viongozi wazuri ( role model). kiongozi mzuri lazima ajue kuwa kushindwa ni sehemu ya uongozi bora kwani inakupa nguvu ya kuanza upya, unawapenda watu wako bila kuchagua au kubagua jinsia yao na kabila zao au dini zao na vyama gani vya siasa wanavyoshabikia ila mradi tu hawavunji sheria dhamana ya uongozi bado unatakiwa kuwajali.

mheshimiwa Magufuli ameoonyesha kuwa yuko tayari kama kiongozi kujifunza na sio mvivu wa ufuatiliaji wa mipango ya serikali,  mhsehimiwa Magufuli anaonekana kuwa ni kiashiria cha mabadiliko na na yuko tayari kusimamia maendeleo kwa wananchi wote wa Tanzania. 

Mheshimiwa Magufuli anayo mawazo mazuri ya kimaendeleo na kujua namna ya kuyatumia kwa ajili ya maendeleo ya watu wa Tanzania; na nina uhakila kuwa anatambua na anauelewe kuwa yale uliyojifunza shuleni wakati mwingine hayafanayi Kwa ufanisi wa speed yake na yuko tayari kufanya  mabadiliko  ili kuendana na kasi na utamaduni utakaowawezesha wafanyakazi kufany kazi kwa bidii ili kuliletea taifa mabadiliko na maendeleo yanayotakiwa.

VIVA MAGUFULI TUNAKUJUA WEWE NI:

  • Ni Jembe:
  • Ni Tingatinga
  • Ni Mtumishi wa watanzania wote
  • Unayajua mapungufu yako.
  • Unaongoza kwa usemi wa sisi sisi.
  • Ni Mnyenyekevu na mtumishi wa watu wote.
  • Ni team player
  • Unakumbukumbu nzuri,
  • Ni mwadilifu
  • Mtu wa watu hasa wanyonge
  • Ni Mwogopa Mungu


VIVA MHESHIMIWA  JOHN POMBE MAGUFULI RAISI MTEULE WA AWAMU YA TANO MWENYEZI MUNGU AKUPE NGUVU YA KULIVUSHA SALAMA TAIFA LA TANZANIA KATIKA MIAKA HII MITANO KATIKA MAENDELEO AMBAYO SISI WATANZANIA TUMEYASUBIRI KWA MIAKA MINGI SANA;


UKADIRIFU INAKUTAKIA UONGOZI BORA 

No comments:

Post a Comment