Ili kuona matokeo ya CSEE, bofya hapa na kwa matokeo ya QT, bofya hapa
Katibu Mtedaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk Charles Msonde
ametangaza matokeo ya mitihani ya Shule za Sekondari ya Kidato cha Nne
ya mwaka jana na kusema, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10
ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013.
Dk Msonde amesema kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kutoka asilimia
58.25 hadi asilimia 68.33 kumetokana na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa
(Big Results Now - BRN).
Dk Msonde ameishukuru Serikali kwa BRN na Walimu kwa jitihada zilizofanikisha kupatikana kwa matokeo hayo.
Matokeo haya yametolewa kwa kutumia mfumo mpya wa wastani wa pointi
badala ya madaraja kama ilivyozoeleka kwa miaka iliyotangulia.
Baraza hilo limewafutia metokeo watahiniwa 128 wa kujigetemea kutoka
vituo vya Kisesa mkoani Mwanza na Lubabo huko Zanzibar kutokana na
udanganyifu uliokithiri.
No comments:
Post a Comment