WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Monday, October 20, 2014

TAZAMA PICHA ZA MTANANGE WA WATANI WA JADI YANGA NA SIMBA ULIYOCHEZWA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM


 Jaja hakuweza fua dafu...

Mtanange ukiendelea...
 
Kiungo wa timu ya Simba,Amri Kiemba akuchuana vikali na Mshambuliaji wa timu ya Yanga,Andrey Coutinho wakati wa mtanange wa watani wa Jadi Yanga na Simba uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana  ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.Timu hizo zimetoka sare ya bila kufungana.


 Dogo akiwachambua wana Yanga...

 
Shabiki wa Simba akionyesha bango linaloonyesha michezo iliyopita waliowahi kucheza na Yanga na kushinda



 Mashabiki wa Simba

 Mashabiki wa  Yanga Wakifanya Yao

kipa wa timu ya Simba, Manyika Peter (kushoto) akipongezwa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi baada ya kumalizika kwa  mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania  uliochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jana. timu zote zimetoka sare ya bila kufungana. katika michezo mingine iliyochezwa katika viwanja tofauti, Azam FC wameweza kuwafunga, Mbeya City bao 1-0 lililofungwa katika daki ya 18 ya mchezo na Agrrey Moris, mchezo huo ulichezwa katika Uwanja wa Sokonne jijini Mbeya na huko Mtwara katika Uwanja wa Nangwanda, JKT RUVU wameweza kwafunga wenyeji timu ya Ndanda FC bao 3-1 na katika mchezo mwingine uliochezwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Kasoro Bahari mkoani Morogoro kati ya Mtibwa Sugar na Polisi Morogoro, timu hizo zimetoka suru bin suru, Coast Union nayo imeibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mgambo

 
Kipa wa Siba, Manyika Peter akipongezwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya mchezo kumalizika.

 Kocha Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, akiwasalimia mashabiki wa timu hiyo

Makocha wa yanga na Simba, Maximo (kushoto)akisalimiana na Patrick Phili kabla ya mchezo.

PICHA NA OTHMAN MICHUZI NA ANTHONY SIAME

source: haki Ngowi

No comments:

Post a Comment