UKOSEKANAJI WA UHALISIA KATIKA FILAMU ZA KITANZANIA.
- TATIZO NI UHABA WA ELIMU KATIKA SANAA YA FILAMU?
- TATIZO NI TEKINOLOJIA NDOGO?
- TATIZO NI KULEWA SIFA NA HATIMAYE KUTOKUWA MAKINI KATIKA UIGIZAJ?I
Mr Emmanuel
Myamba katika moja ya washa aliwahi sema kuwa “Ni wazi
ukiangalia filamu zetu zinakosa weledi katika uandishi wa miswada, uongozaji,
uhariri na hata uumbaji wa wahusika. Lazima tukubali udhaifu huu turekebishe” aliendelea kueleza kuwa “Nimekuwa katika
tasnia ya filamu kwa muda sasa lakini kuna changamoto nyingi katika tasnia ya
filamu, na jambo ambalo nimeliona ni wasanii kukosa ujuzi kitaaluma katika
utendaji wa filamu kwa ujumla, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa
ajili ya wasanii maskini wasio na uwezo wa kulipa ada kubwa katika vyuo vilivyopo,
lakini pia kutoa nafasi kwa wale ambao wanafanya kazi lakini taaluma imekuwa
shida kwao, na mwito ni mkubwa kweli,”
“Tatizo kubwa la wasanii
wa Tanzania kushindwa kufaidika na vipaji na ujuzi wao, ni kukosa elimu ya
kutosha ya mambo ya sanaa, kwa mantiki hiyo nikaamua kufungua chuo hiki kwa
ajili ya wasanii, nimeapa kwamba nitaweka ada ndogo ili wasanii wachanga au kwa
ujumla tuseme wasio na uwezo mkubwa wa kifedha waweze kusoma hapa,”
Kati ya waigizaji
wanaoigiza kwa hisia na kuvutia nyoyo za mashabiki hapa Tanzania basi hutakosa
kumtaja Emmanuel Myamba a.k.a Pastor Myamba ambaye
mara nyingi tumezoea kumuona akiigiza kama mchungaji au mtu mwenye maadili ya
dini.
Mimi kama mdau wa senema za
kibongo ninamkubali sana msanii huyu hasa katika kipaji chake cha kuigiza
katika hali ya uhalisia wa maudhui ya kidini na kweli amefanikiwa kuvaa
uchungaji wa kweli ambao ni zaidi ya movie wakati ni movie tu. Kutokana na
kipaji hicho na umakini wa uigizaji wake wadau wengi tunajua kuwa Myamba ni
mchungaji ambaye anakanisa lake, lakini kumbe sio, yeye ni mwigizaji na muumini
wa kawaida tu. Hali hii sis wadau wa filamu ndio tunatamani kuangalia filamu zenye
uhalisia wa namna hii. Katika kundi hili wasanii kama Dr. Cheni, JB, Wema Sepetu na Shamso Ford
ni baadhi ya waigizaji ambao wanakuwa makini katika katika uigizaji wao;unaweza
kufurahi nao au kulia nao ukifikiri kile kinachochezwa ni ukweli mtupu, kumbe
sio ni falamu tu.
Swali ninalojiuliza hapa nini ambacho kinakosekana kwa wasanii
wengi hata wale waanzilishi wa Tasnia hii? je tatizo ni nini? Je ni kweli swala
la elimu linachangia kama?
Pastor Myamba alivyoshauri kuwa “ni vyema kupata elimu kwani elimu inakufanya
ujiamini juu ya unachokifanya na kwa umakini zaidi”.
Nina Imani kuwa kusaka
maarifa ya namana ya kutengeneza sinema zenye uhalisia na visa litasaidia sana
kuleta ushindani sio tu wa ndani bali wa limataifa; ikumbukwe kuwa filamu
ambazo zinakosa uhalisia zinapunguza mvuto, na hivyo kuwafanya watazamaji
kuishiwa na hamu ya kuziangalia filamu hizo na kuwakosesha kipato na kuongeza
umasikini miongoni mwa wasanii.
Kama Gayo alivyowahi
kushauri kuwa “Ikiwa tutaendelea kutengeneza filamu zisizo na weledi, zenye
visa vilevile na zenye kusukumwa na wasambazaji au haja ya kuchuma fedha za
haraka tu watu watatuchoka na baadaye soko litakufa”.
Hivyo kilio cha elimu kwa
wasanii kimekuwa ni kilio cha wadau wengi hapa Gayo anasisitiza kuwa “Pia
wasanii na watendaji wengine wanapaswa kupatiwa mafunzo, kwangu mafunzo ndiyo
kitu cha kwanza muhimu kwa mtu yeyote yule katika kumuongezea stadi zake za
utendaji. Kwa jumla kuna upungufu mkubwa wa mafunzo ya fani mbalimbali za
sanaa, ikiwemo filamu. Wasanii wengi wanajifunza kwa kuiga wenzao. Ingawa hii
ni moja ya njia za kujifunza, tatizo lake ni kuwa huchukua muda mrefu na haina
hakika kama kinachoigwa ni sahihi au la”.
Je ni kweli
sekta hii ni ya watu ambao hawajasoma? Mimi ninasema hapana? Isipokuwa
ni sekta ambayo wahusika wake baada ya kushika pesa kidogo hunogewa na hawataki
kujiendeleza kwa kujipanua katika elimu ya uigizaji; na kwa hiyo ufanisi wa
kazi umekuwa wa chini mno.
Msanii Myamba ametuletea changamoto nzuri ya
kuanzisha chuo cha filamu Tanzania kuppitia chuo hiki wasanii wataweza
kukabiliana na changamoto za uandaji wa filamu kwa wasanii kukubali kujiongezea
ujuzi na masilahi bora.Kwa hiyo eneo hili la mafunzo linahitaji msukumo siyo tu
wa kuongeza nafasi bali pia ubora wake.
Wazungu na kiingereza chao
wanasema "Knowledge" comes from getting
educated.
"Experience"
comes from real life encounters. There is a famous saying that says.
"Experience
is better than knowledge!" and "Experience is the Best Education In
Life."
Experience and knowledge go hand in hand.
Knowledge is
important, because it makes you aware of what is around you. Knowledge also
enables a person to become wealthy.
The more
knowledge we have, the more advanced we can become. Education can give you a
good job and assure you a secure future. The world needs knowledge to discover
new things to help everyone.
Msanii kama kioo halisi
cha jamii inayomzunguka, anatakiwa kuuvaa uhalisia wa fani yake ili Yule anayeamua
kumwangalia aweze kufaidika na tasnia hiyo. Ili kufikia malengo stahiki, wasanii mmoja mmoja au kwa pamoja wakipata
upeo juu ya haya, wataweza kutekeleza ipasavyo majukumu yao na kuwa msaada
mkubwa katika kuielimisha jamii juu ya mambo mbalimbali.
Nachukua nafasi kumpongeza
Msanii Emmanuel Myamba aka Pastor Myamba
kwa kuliona hili na kuanzisha chuo cha kuwaelemisha na kuwapa ujuzi unaostahili
wasanii wengine ili waweze kukabili changamoto za kufanya kazia zao kwa makini
na kwa uhalisia unaotakiwa katika tasinia ya filamu nchini kuptia Chuo
kinachojulikana kwa jina Tanzania Film
Training Center (TFTC) kilichopo Ubungo Dar Es Salaam
ambacho hutoa mafunzo mbailimbali ya filamu,ikiwemo acting, directing, editing,
production management,producing nk.
Nina imani chuo hiki
tutawasaidia wasanii wachanga na wakongwe wapate fursa ya kujiongezea ujuzi
kitaaluma ili kukabiliana na changamoto mbalimbali katika soko la filamu la
ndani na la kimataifa. wazo hili la uanzishaji wa chuo maalum cha uigizaji ni uamuzi wa busara ambao hata serikali inatakiwa kuunga mkono jitihada hizi binafsi. Mungu ibariki Tanzania
hongera sana msanii Myamba determination ni silaha ya kufanya vizuri katika kila jambo; usilemae kwa sifa na ukaanza kuharibu kipaji chako; keep it up
ReplyDelete