TUTAENDELEA KUKUMBUKA NA KUKUENZI DAIMA HAYATI BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE 1922 - 1999
"Inawezekana tatizo
la paka kwa panya lingekwisha kama paka angefungiwa kengele shingoni: taabu ni
kumpata panya wa kuifanya kazi hiyo. Na panya watakuwa wajinga sana wakidhani
kuwa paka watajifunga au watafungana kengele shingoni"
"Hakuna umaskini mbaya kama umaskini wa mawazo, ni umaskini mbaya
sana"
'Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!'
'Mtu mwenye akili akikuambia neno la kipumbavu -ukalikubali, anakudharau!'
Tutawasha
Mwenge na kuuweka juu ya Mlima Kilimanjaro, umulike mpaka nje ya mipaka yetu, ulete matumaini
pale pasipo na matumaini, upendo pale
palipojawa na chuki na heshima pale palipojaa dharau –
“TUNAPOZUNGUMZA habari
za uhuru maana yetu nini hasa? Kwanza; kuna uhuru wa nchi,yaani uwezo wa
wananchi wa Tanzania kujipangia maisha yao, wakijitawala wenyewe bila ya
kuingiliwa kati na mtu yeyote asiyekuwa Mtanzania. Pili; kuna uhuru wa
kutosumbuliwa na njaa, maradhi na umasikini. Tatu, kuna uhuru wa mtu binafsi,
yaani haki yake ya kuishi, akiheshimika sawa na wengine wote, uhuru wake wa
kusema na uhuru wake wa kushiriki katika uamuzi wa mambo yote yanayogusa maisha
yake, na uhuru wa kutokamatwa ovyo na kutiwa ndani kwa kuwa tu kamuudhi mkubwa,
japo kama hakuvunja sheria yoyote”.
“Lakini ni dhahiri kwamba mambo hayo
yanategemea maendeleo ya uchumi, madhali nchi yetu bado masikini; na wananchi
hawakupata elimu; na ni wajinga na wanyonge, basi uhuru wetu wa kujitawala
unaweza kuhatarishwa na taifa lolote la kigeni lenye maendeleo na nguvu zaidi.”
...."Kiongozi
anayetufaa Tanzania , ni yule anayejua kuwa nchi yetu ni masikini na watu wake
ni masikini. Na ukimwangalia usoni ...uone anaguswa na umasikini wetu.
Vinginevyo hatufai...."
“Kwa sasa uhuru wa
taifa letu, mara nyingi ni uhuru wa maandishi tu; maana nchi yetu ni maskini
mno, ni nyonge mno kulinganisha na nchi nyingine, hata hatuwezi kutimiza wajibu
wetu kwa ukamilifu kwa binadamu wengine”.
“Watu wenye mawazo
tofauti, hata wakiwa wachache, lazima wawe na haki ya kutoa mawazo yao katika
majadiliano bila ya hofu ya kusumbuliwa; mawazo yao na yashindwe katika hoja za
majadiliano, siyo kwa vitisho au mabavu. Majadiliano yenyewe yatakayoleta uamuzi
lazima yawape nafasi watu kusema kwa uhuru kabisa. Hata baada ya kuamua
jambo, watu wawe na uhuru kuendelea kulizungumza jambo hilo”
“Elimu inayotolewa ni lazima ijenge mambo matatu kwa kila mwananchi, akili ya kuuliza, uwezo wa kujifunza kutoka kwa wengine - na kuyakataa au kuyakubali kutokana na mahitaji yake - na uwezo wa kujiamini kama raia huru na sawa katika jamii, anayethamini wengine na kuthaminiwa kwa anayofanya na siyo kwa anachopata”
No comments:
Post a Comment