UVUMILIVU HUJENGWA NA MISINGI GANI?
Naanza kwa kujiuliza kuwa
“tulichonacho sisi wananchi je ni subira?; na
baadhi ya viongozi wetu je wanao uvumilivu?
Kwa haraka haraka tu Uvumilivu ni
uwezo wa, au ni mazoezi ya, kutambua na kuheshimu imani au matendo ya wengine;
uvumilivu uko katika kila nyanya ya maisha yetu, kuanzia maisha yetu ya kila
siku;TATIZO
katika maisha ya kawaida sana, swala la uvumilivu halizungumzwi sana, kwani uvumilivu
unahusishwa na familia au kikundi kidogo cha watu; katika level hii uvumilivu
huzungumzwa sana katika kuimarisha maisha ya ndoa;
Uvumilivu huongelewa sana kwa mapana hasa katika
maswala ya uongozi, uongozi ni hali ya kuongoza nchi katika mwelekeo wa kuleta
maendeleo na ni ukweli kama mwandishi mmoja alipowahi sema kuwa “ KUONGOZA watu na hasa wa watu wazima ni kazi nzito
inayohitaji mtu anayepewa jukumu hilo kuwa makini, vinginevyo mambo yanaweza
kuwa magumu na hatimaye kuangukia katika mtego wa udikteta. Hii inatokana
na kukosekana mambo makubwa matatu ambayo ni ufahamu au maarifa, hekima
na hasa uvumilivu. Kiongozi asiye mvumilivu anaweza kujikuta anatumia
mabavu kutawala ili watu wajue kuwa yupo, ana nguvu na ana mamlaka”.
Ni ukweli ulio wazi
kuwa kiongozi anatakiwa kuwa, mtulivu,
mvumilivu na anayetumia zaidi hekima kuliko mabavu”, kiongozi anatakiwa Kuwa
na msimamo wa uvumilivu ni moja ya kazi
ngumu zaidi miongoni mwa viongozi dhidi ya wananchi katika jamii. Ni ukweli
ambao haufichiki kuwa viongozi hawakuzaliwa
wakiwa wavumilivu, lakini lazima tujifunze kuwa wavumilivu. Katika siasa uvumilivu
wa kisiasa unakuza utamaduni wa utawala
bora na ukomavu wa demokrasia; na Kwa demokrasia kufanya kazi vizuri, wananchi
lazima kuwa tayari kuvumilia na kuvumiliana.
Dhana ya uvumilivu ni ya
msingi sana kwa maendeleo kwani inaruhusu mawazo mapya ndani ya jamii; kupitia
dhana hii ya uvumilivu, kiongozi anakuwa
tayari kukubali na kuheshimu maoni na mawazo ya watu wengine na haki zao
kwa uwazi na uhuru. Katika hali hii,uvumilivu huruhusu kuwepo kwa vyombo huru vya habari kutumika kama chombo muhimu kuwahabarisha
wananchi na kuwasilisha madai yao kwa viongozi wao. Demokrasia inahitaji vyombo
vya habari amabvyo hugeuka kuwa daraja la mawazo kati ya viongozi na waongozwa.
Vyombo huru vya habari husaidia wananchi kuelewa taratibu ambazo zinaimarisha
demokrasia.uvumilivu wa viongozi huru utasaidia kueneza demokrasia na uwajibikaji kwani wananchi wataweza kukosoa
serikali na ujumbe kufikishwa serikalini bila kuogopa.
ni ukweli kuwa Falsafa ya Uvumilivu hufunza na kuwakumbusha viongozi wanatakiwa kuishi kulingana na fikira njema. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hayuko tayari kuamsha fikra mbaya za udikteta bali daima atajitaidi kuziepusha kwa kuendeleza uamuzi wa uwazi na kwa kutumia njia ya utulivu wa hekima kupitia uzoefu makini wa kimantiki: Kiongozi mwenye uvumilivu daima hutafakari, na kuziweka fikira mahali pamoja kabla ya kufanya uamauzi.Msingi wa kimaadili wa falsafa ya uvumilivu kama mtaalam mmoja alivyo wahi kusema kuwa "zuri liko katika hali ya nafsi, yenyewe, inaonyeshwa katika hekima na kujidhibiti, hivyo kuboresha ustawi wa kiroho: Fadhila inatokana na nia ambayo inawiana na Maumbile. Kanuni inatumika katika uhusiano wa kibinafsi, yaani: kuwa huru kutokana na hasira, na wivu"
kwa ufupi tunaweza
kusema kuwa uvumilivu umesheheni nini?
·
Tendo lililojaa subira
kubwa,
·
Tendo ambalo kama
linafanywa na kiongozi wa nchi basi anatoa uhuru mkubwa kufanya mambo bila
kuingiliwa na nguvu za Ikulu,
·
Tendo lililojaa utu,
·
Tendo kwa serikali kuwa
tayari kukosolewa na watu binafsi au vyombo vya habari.
·
Tendo ambalo
linaashiria uwajibikaji wa serikali na utumishi wenye tija katika kwa taifa na
wananchi wake katika kukuza demokrasia
Ni ukweli ambao
haufichiki kuwa viongozi wetu wakiwa wavumulivu katika uwajibikaji wao mara
moja hurudisha imani ya wananchi dhidi
ya serikali yake, upendo na matumaini katik ya viongozi na wananchi huongezeka
pia: Tukumbukwe kuwa Ingawa watu wengi kufikiria uvumilivu ni upole na kuto wajibika la hasha uvumilivu ni
uwajibikaji ulio jaa busara na subira;
Swali lakujiuliza
tunavyoelekea kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Taifa letu je viongozi wetu katika
awamu zote katika serikali yetu ya Muungano waliutumiaje uvumilivu katika
kutekeleza majukumu yao?
Je uvumilivu wa
kipindi cha mapambano ya uhuru wa taifa letu Bara na visiwani katika miaka hiyo ni sawa na
uvumilivu wa leo?
Je uvumilivu baiana
ya vyama vya kisiasa ukoje? Ni kweli kuwa wanavumiliana katika kuchangia hoja
katika mambo mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Taifa letu?
Je hali ya viongozi
wetu na vyama vyao wakati wa chaguzi mbalimbali uvumilivu hutawala kampeni zao?
Kuna maswali mengi
sana ya kujiuliza hasa katika kipindi hiki cha kuelekea miaka 50 ya uhuru wa
taifa letu na nini kifanyike baadaya ya sherehe hizo kwa manufaa ya taifa letu
la Tanzania
MUNGU IBARIKI TANZANIA KUELEKEA MIAKA
50 YA UHURU