WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Friday, December 31, 2010

SALAMU ZA MWAKA MPYA 2011

MAISHA BORA KWA KILA MTAZANZANIA: TUYATEGEMEE KUPTIA KASI MPYA, NGUVU MPYA NA ARI MPYA? AU TUSUBIRI KAULI MBIU NYINGINE?

       Mheshimiwa J.Kikwete - Rais wa Tanzania

Ni desturi kila kiongozi anapoingia madarakani huja na kauli mbiu, ambayo inakuwa ni dira ya utekelezaji wa majukumu yake katika kuwaletea maendeleo wananchi wake, tumeshuhudia kauli mbiu kama : Umoja ni Nguvu, na Utengano ni Udhaifu; Ruksa; Uwazai na Ukweli na hatimaye sasa tuna kauli mbiu ya “Kasi Mpya Nguvu Mpya na Ari Mpya” ambayo lengo la kauli hii kwa jamii ya watanzania ni kuwa na “Maisha bora kwa kila Mtanzania”.

katika tafakari yangu ya leo ikiwa ni salamu za kuaga mwaka wa 2010 na kuukaribisha 2011, maswali ya msingi je kauli hii mbiu inaweza kubadilisha maisha ya watanzania kutoka maisha duni na kuwafanya wayafurahie maisha yaliyo bora? Je serikali yetu inatumia kigezo gani katika kuhakikisha kuwa kauli hii mbiu inaleta changamoto na hata mabadililo katika maisha ya wananchi wake? Na katika kutekeleza Kauli hii mbiu Je tunao viongozi ambao wamejizatiti kuwatumikia wanainchi? Je tunao viongozi ambao wanajisuta wenyewe wanaposhindwa kuwatendea haki wananchi wao? (fear of justice): Kwa nini wataalamu wetu wengi wanaikimbia nchi yetu na kwenda kufanya kazi nchi nyingine? Je wananchi nao wanatimizaje wajibu wao katika kutekeleza kauli Mbiu hii kwa ajili ya maendeleo yao wenyewe? Je Kauli mbiu hii imelenga maisha bora kwa wale ambao tayari wako ndani ya mzunguko wa ari,kasi, na nguvu mpya kutokana na uwezo, wa mali ambazo wamezipata kwa njia ambazo zina utata/sio sahihi?

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa Serikali yoyote duniani, inayoendeshwa kwa misingi ya demokrasia, lengo lake la kwanza ni  ulinzi wa maisha ya wananchi wake na furaha yao, na si uharibifu wake. Kulinda maisha ya wananchi wake ni lengo pekee kwa serikali ya kidemokrasia kwa sababu serikali ipo kwa ajili ya watu na imechaguliwa na watu na inapata madaraka kutoka kwa watu. Aidha, ridhaa ya serikali yoyote kuendelea kukaa madarakani haitokani tu na katiba na sheria iliyoiweka madarakani; bali ridhaa ya wananchi kutawaliwa inatokana zaidi na matendo mema ya serikali hiyo kwa wananchi wake.

Serikali ina changamoto ya kuhakikisha ufisadi nchini unaondolewa ili utajiri wa nchi yetu uwanufaishe wananchi, wakiwemo wafanyakazi. Kama mwandishi mmoja alivyowahi kumnukuu Albert Einsten kuwa : “Ulimwengu pamekuwa mahali pa hatari sana kuishi lakini haitokani na uovu unaotendeka, bali inatokana na wale wanaouona uovu ukitendeka lakini hawachukui hatua yoyote.” Swali je viongozi wetu wanao utashi na uwezo wa kukwemea maovu haya, hata kama watendaji wa maovu haya ni watu wa karibu nao: kama marafiki na ndugu au watoto?
Nakumbuka kauli mbiu hii (Kasi Mpya Nguvu Mpya na Ari Mpya) ilivyotolewa ilishangiliwa sana na watanzania  ilionyesha kuwa na manufaa kwa umma, tatizo ni kuwa furaha hiyo kwa Watanzania kama kawaida imeanza kuzimika kama kibatari kwenye upepo, kwa vile utekelezaji wa kauli mbiu hii hauonyeshi kufikia malengo yake. Inafika mahali ambapo wananchi wanaanza kusema kunatofauti gani ya kule tukiko toka na hapa tulipo?

Kimantiki ni rahisi sana kwa gari ambalo gurudumu zake tayari zinazunguka kupandisha milima kwa haraka  kuliko lile ambalo lilikuwa limesimama litahitaji nguvu zaidi na wakati zaidi katika kuupandisha mlima ule ule; Wakati mwingine msaada wa ziada utahitajika, lakini kwa bahati mbaya iwapo gari ambalo lilikuwa katika mwendo  litakuwa tayari limeshakamilisha kupanda mlima halitaweza kutoa msaada wa haraka; na kama kwa bahati mbaya hata vioo vya kuangalia pembeni pengine havifanyi kazi, ni vigumu sana kujua kama mwenzake aliyemwacha nyuma anakuja au limeshindwa kabisa kupandisha mlima. Hii ni taswira ya viongozi wetu na serikali yao mambo yanapowaendea vizuri hawajali maisha ya wananchi wao mpaka wakati wa chaguzi tena.

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa kama viongozi wetu wanavyosema; maisha bora hayawezi kuja watu wakiwa vijiweni;hayawezi kunyesha kama mvua, ni suala la mchakato. Lakini wananchi wameanza kuona mambo tofauti yanayotokea kwa viongozi wao. Viongozi wa nchi wao maisha yameanza kuwa mazuri baada ya muda mfupi. Wananchi wanashuhudia baadhi ya viongozi walioingia madarakani karibuni ambao walikuwa hoi kabisa lakini sasa wanaishi kama vile wako kwenye paradise ya peke yao.
Viongozi wetu wanageuka mchwa na kusahau waliko toka; wengi hujiingiza katika  Wimbi wa wizi wa mali za umma na ufisadi wa kutisha. Ni vema viongozi wetu, hasa mawaziri, wakaingia kazini kutatua kero ambazo kila mmoja anazifahamu. Kama msanii Mrisho Mpoto alivyoimba katika moja ya nyimbo zake,Mwaka 2005 walitupima viatu na leo wanarudi tena kutuuliza tunahitaji viatu vya aina gani; sisi hatutaki mnapokuja kwetu tena mtuulize, bali tunataka mnaporudi mje na viatu vyetu tena ambavyo vinatutusha .

La msingi tunapoanza mwaka 2011 kukbukuke kuwa maisha bora ya Mtanzania yatapatikakna kama serikali itaweza kuboresha:
·         Elimu kwa watoto wetu, Utajiri mwingi wa Taifa utumike kujenga shule bora kwa watoto wetu, kujenga mazingira bora ya kusomea na mahitaji yote yanayomjenga mtoto kiakili. Kama Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere alivyosema “Elimu bora ndiyo urithi pekee unaoweza kulifanya Taifa kuweza kuboresha maisha ya watu wake”. Na elimu bora ndiyo chemchemu ya maisha bora kwa kila Mtanzania.

·          Hali halisi ya shule nyingi wanafunzi wanakaa nchi kutokana na ukosefu wa madawati ,tatizo la vyoo mashuleni  haviko vya kutosha na kama viko sio visafi Kwahiyo ,wanafunzi  wetu wanakuwa kwenye hatari ya kupata maambukizo kutokana na kutokuwepo na vyoo safi .kuna tatizo la msingi la uwiano wa walimu na wanafunzi. Idadi ya wanafunzi ni kubwa kuliko uwezo wa walimu; tatizo la pili walimu wengi hawana uwezo mkubwa wa kufundisha hivyo hupelekea watoto kumaliza shule wakiwa hawafahamu chochote kama vile kusoma,  kuandika hata kuhesabu

  • Kuna tatizo la huduma za afya  hali halisi ni ile amabayo iko kwenye hopsptiali na zahanati nyingi hapa nchini akina mama wajawazito wanakufa sana hasa wakati wa kujifungua,sababu kubwa ni ukosekanaji wa wakunga na vifaa au wakunga hawapati mafunzo ya kutosha: tatizo pia tunaliona kwa  watoto wetu wanafariki kila kukicha kutoka na kutokuwa na Zahanati nzuri na kubwa yenye huduma bora pamoja na ukosekanaji wa madawa,
  • Tatizo la wataalamu wetu wengi hasa katika sekta ya afya wanvyokimbilia nje ya nchi hii ina dhihirisha kuwa Wataalamu wetu hawathaminiwi na hii inatugharimu sana; pengine wamesomeshwa na pesa za walala hoi lakini hawarudi nchini kuisaidia jamii.
Maisha Bora kwa sasa inawezekana, hili halina pingamizi ila tu utekelezaji wake unahitaji viongozi wetu wavue ubinafsi na wafikirie vizuri, waseme kile ambacho wanaweza kukitenda na si kutumia umasikini wa watu kwa kuwapa matumaini yasiyotekelezeka. tukumbuke kuwa mabadiliko sio rahisi yanahitaji kujitoa muhanga kutekeleza majukumu bila kuogopa vitisho, wala upendeleo: je tunao viongozi wa namna hii katika serikali yetu?

Ni jukumu la serikali ili kufanikisha hii ahadi inatakiwa kuwamulika mawaziri wanaotia mashaka katika kufanikisha sera na adhima ya maisha bora. kwamba ni vyema mtu anayetoboa jahazi akatoswa mapema, kwani kulelewa na kushangilia huku akiendelea na hujuma zake, mwisho wake ni abiria wote, pamoja na nahodha kuzama na kupoteza maisha. Kikwete, wakati wa kuwatosa wote wanaokuangusha ni sasa na usijali urafiki, uswahiba au undugu na watu wa aina hiyo na hapo utakuwa umeokoka na kulitendea haki taifa la Watanzania.

Je picha hizi hapa chini  zinatupa mawazo gani kuhusu  Watanzania? Wanafurahia maisha bora? Wanalaani serikali kwa kushindwa kuwajali? Au wana sema yote sawa tu? Au wanafurahia mafanikio ya Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya: Ni mambo yepi yanahitaji mabadiliko ya haraka kama yako?




Sunday, December 26, 2010

Kona ya Siasa: Ujumbe wa Siku ya X-mass



"Wananchi wanatakiwa wasiiogope Serikali; bali Serikali inatakiwa iwaogope Wananchi wake"

Monday, December 20, 2010

Politics Corner "Debate on Constitution"

The discussion of change of Constitution let remember Hillary Rodham Clinton once said:    

"The challenges of change are always hard. It is important that we begin to unpack those challenges that confront this nation and realize that we each have a role that requires us to change and become more responsible for shaping our own future." 


Philip Crosby reminded us that;



"If anything is certain, it is that change is certain. The world we are planning for today will not exist in this form tomorrow." 


Leadership advise:


People ask the difference between a leader and a boss. . . The leader works in the open, and the boss in covert. The leader leads, and the boss drives. 

- Theodore Roosevelt


Think of managing change as an adventure. It tests your skills and abilities. It brings forth talent that may have been dormant. Change is also a training ground for leadership. When we think of leaders, we remember times of change, innovation and conflict. Leadership is often about shaping a new way of life. To do that, you must advance change, take risks and accept responsibility for making change happen.
§  Charles E. Rice, CEO of Barnett Bank
 

Sunday, December 19, 2010

Politics Corner

The fight for justice against corruption is never easy. It never has been and never will be. It exacts a toll on our self, our families, our friends, and especially our children. In the end, I believe, as in my case, the price we pay is well worth holding on to our dignity.
Frank Serpico

Thursday, December 16, 2010

Remmy Ongala & Orchestra Super Matimila ~ Sika Ya Kufa



BURIANI DOCTOR REMMY ONGALA


NINI TUMEJIFUNZA TOKA KWA HAYATI REMMY ONGALA aka DOCTOR?
Wapenzi wa muziki wa dansi na Muziki wa Injili tumepokea kwa masikitiko habari za kifo cha mkongwe wa muziki/Injili  doctor Remmy Ongala ambacho kimetokea tarehe 13/12/2010.

Swali la msingi kwa nini kifo chake kimewagusa wengi? Majibu ya swali hili ni mengi sana kulingana na kila mtu na mtazamo wake na kwa namna ambavyo alikuwa anamfahamu na Doctor Remmy kupitia nyimbo na maisha yake mengine ya kawaida na kwa namna ambavyo  aligusa hisia zetu.

Kwa upande wangu nitazungumzia hasa URITHI  gani ambao Remmy ametuachia sisi kama wananchi wa Tanzania. Marehemu Remmy ametuachia jambo moja kubwa la kuwa wakweli katika katika kutekeleza majukumu yetu bila kumwogomba mtu yeyote Yule; ni Mwenyezi Mungu tu wa kuogopewa. Remmy alikuwa mkweli, muungwana na mwelimishaji wa aina yake.

Aliweza kukitumia kipaji chake katika kuwatetea wanyonge kwa kupitia musiki wake, alikuwa anajitahidi sana kutoimba sana nyimbo za mapenzi na badala yake kuimba zaidi nyimbo zilizokuwa zinagusa na kueleza matatizo ya wanyonge watu wa kipato cha chini, ambao hawana sauti amabyo wakiitumia inaweza kuwasaidia kutatua mataizo yao.

Aliwahi kusema huko nyuma kuwa dunia hii ni gereza wanyonge ambao hawana uwezo wa kuyafurahia maisha kwa vile hawana uwezo hivyo wao ni wakuamuriwa tu nini wafanye ni sawa na wafungwa. Mafanikio ya wanyonge lazima yatokane na furaha ya matajiri ambao furaha yao ndio nafuu ya wanyonge na hasira yao ni kiyama kwa wanyonge.

Doctor Remmy kwa kweli Alifanikiwa sana kueleza ukweli wa maisha wa wanyonge kama umasikini, tatizo la ukimwi na namna ya kujikinga na maambukizo, ukiukwaji wa haki za msingi za binadamu, rushwa mapenzi na uvumilivu kwa kupitia muziki wake; ndio maana kumbi zake zilikuwa zinawapenzi wengi wa Muziki.

Nakumbuka sana ule wimbo wake wa Mambo kwa soksi ambao ulikuwa unahamasisha sana watu watumie kondom katika swala la mapenzi ili kujikinga na maambukizo ya ukimwi; wimbo huu ulionekana kupingana na maadili kwa wakati huu, lakini ukweli Doctor Remmy ulikuwa miongoni mwa elimishaji wa ngono salama kwa jamii. Aliitumia sanaa yake kuwa kweli ni kioo cha jamii katika kutatua tatizo. Hatukuwa tayari kuukubali ukweli huu, tukitumia kigezo ujumbe huu ulikuwa umewasilishwa kunyume na utamaduni wetu. Bila kuogopa ukweli huu Remmy aliuweka bayana, je leo hii Jamii yetu tunaielimisha vipi? Tukubali au tukatae myonge myongee lakini haki yake mpe Remmy alikuwa ameona mbali na alikuwa anawaonyesha wanyonge haki hiyo ya gharama nafuu kwa usalama wa maisha yao;

Yako mengi ya kusema la msingi tu muziki ambao ulikuwa ukipigwa na kutungwa na Doctor Remmy ulikuwa na hisia kali za kuelimisha kulingana na mazingira; tutamkumbuka sana kupitia nyimbo zake; tutamkosa kwa sababu hatutapata tena mashairi na na uimbaji wa hisia kwama wake;

Mwenyezi Mungu amempa Baraka za maisha yake kwa kazi kubwa ambayo ametufanyia kwa kumuwezesha kutumia muda wake wa kutosha kabla ya kifo chake kumwimbia yeye; na kwa kulisoma neno lake kwa utulivu zaidi na kwa makini ampaka pale alipowita kwake katika mapumziko ya milele; kama wengi walivyosema tumempenda sana mpendwa wetu Remmy lakini Mungu amempenda zaidi; Yeye alitoa na Yeye Ametwaa, jina lake na lihimidiwe milele Amin 


Thursday, December 9, 2010

KWA NINI BADO TUNAHITAJI ELIMU YA URAIA KWA WATANZANIA HASA WAISHIO VIJIJINI?



Demokrasia ina gharama kubwa sana, ambayo pengine haionekani kwa haraka sana, kwa wananchi wa kawaida; mfumo huu wa maisha unawahusisha wananchi katika kutekeleza sehemu hii kubwa ya uchaguaji wa viongozi wao. Wananchi wengi hawapendi sana kujihusisha na swala hili kwa vile wanaamini kuwa sio lazima sana wao wahusike wakati kuna wengine wengi wanaweza fanya hivyo. Hivyo kila mmoja humsukumia mwenzake swala la upigaji wa kura. Kuchagua kiongozi mzuri kwao hakuna maana yeyote kwao  na haina manufaa kwao mimi naungana na kundi hili kwa sababu ambazo nitazieleza hapo baadae.

Leo nitazungumzia kwa nini wananchi wengi hawajitokezi wakati wa zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa rais na wabunge wake: Tumeshuhudia katika uchaguzi huu uliomalizika October 2010 kumekuwa na malalamiko ya  wananchi kuto kujitokeza kwa wingi katika upigaji wa kura, swali ni kwa nini?

Mtazamo wangu unalenga zaidi katika  ukosekanaji wa elimu ya uraia;
Kwa nini tunahitaji elimu ya uraia? Je hatuna kabisa mashirika au idara za serikali au za watu binafsi au Mashirika yasiyo ya Kiserikali ambayo yanajishughulisha na ufundishaji wa elimu hiyo? Kama tunayo kwa nini hakuna mabadiliko ya msingi ya uelewa huu kwa wananchi kwa ujumla hasa wale wanaoishi vijijini? Je idara na mashirika hayo yamelenga zaidi katika ufundishaji wa elimu gani kwa ustawi wa demokrasia?

Lengo kubwa la elimu ya uraia ni kuleta na kuimarisha uelewa wa wananchi katika kuzielewa na haki zao zitokanazo na upigaji wa kura; Elimu ya uraia vile vile husaidia sana katika kuondoa fikra tofauti ambazo zinaweza kuletwa na chama au vyama katika kujinadi hasa wakati wa kampeni za uchaguzi, kama tu wananchi wameiva katika kuelewa haki zao. Wananchi hawajui hata kama wao ndio wafanyanyi wa maamuzi makubwa sana ya maendeleo yao;


Kwa nchi kama Tanzania kwa hivi sana umasikini ndio umekuwa kielelezo cha kuwachagua viongozi, ukizingatia kuwa kutokana na ugumu huo pesa utumika kununua kura, ambazo huwachagua wawakilishi wa watanzania walio wengi ambao wanakuwa hawana sauti katika kujua hatima ya maendeleo yao. Wananchi walio wengi hawana elimu kabisa ya uraia na hawajui namna gani kura zao zina thamani kwa maendeleo ya nchi. Kwa mfano katika wananchi takribani karibu million  19 waliojiandikisha kupiga kura ni ni pungufu ya nusu ndio waliopiga kura. Je hii inamaanisha nini?
Inaelekea kuwa elimu kama inatolewa haitolewi kwa ukamilifu hasa kwa wananchi wa vijijini, ndio maana hata leo katika nchi ya Tanzania bado kuna wananchi ambo wanafahamu fika kuwa Mwalimu J. Nyerere bado ni rais wa Tanzania; je REDET wako wapi? Serikali na mashirika yake pamoja na NGOS wako wapi katika kueleimisha hili? Ifahamike kuwa kuto kumpa mwananchi elimu ya uraia ni kumnyanyasa kifikra na kimaendeleo. Kwa ufupi kukosekana kwa elimu ya uraia kumesababisha :
·        wananchi wasione umuhimu wa kwenda kupiga kura kwa kujua kuwa kupiga kwao kura ama sivyo hakuwezi kubadilisha chochote.
·        Wananchi hawajioni ni kama wanaweza kudai haki yao kwa njia sahihi  ya kupiga kura


Wakati umefika wa kuwauliza wote wanaohusika na utoaji huo wa elimu je kipimo cha ufanisi au ubora wa kazi yao ni nini? Kwa mwanafunzi kipimo cha elimu aliyepewa ni kuelewa alichofundishwa, kufanya tathimini  na hatimaye kuweza kufaulu mitihani yake, je kwa vikundi vyote vinavyojihusisha na utoaji wa elimu  hii kipimo chao ni nini. Je wanaweza kuwapimaje wale wananchi hasa wa vijijini ambao wanahitaji sana elimu hiyo je wako;
·        Chini ya kiwango (below Basic) hawa ni wale wenye elimu kidogo au hawana kabisa.
·        Wastani(basic) wana elimu ya kutosha kuhusu mada nzima
·        Juu ya kiwango (advanced) wamebobea katika elimu ya uraia wanaijua nini wanataka na watapata vipi.



Bado tunasafari ndefu lakini inahitaji umakini mkubwa sana; ambao unahitaji wannanchi makini ambao ndio wanaweza kutuletea viongozi makini, maendeleo yetu yataletwa na sisi wenyewe na sio mtu mwingine yeyote Yule? Tukumbuke kuwa kama hatutachukua hatua ya haraka katika kuwaelimisha watu wetu kuhusu  elimu ya uraia tunaemdelea kuwajaza wananchi wetu na ujinga hivyo na tutaendelea kuwajaza hofu katika kufanya maamuzi, hivyo hakuna namna yeyote wataweza kumchagua  mtu sahihi kwa namna wao wanavyoona; watamchagua mtu kupitia ulipaji wa fadhila kwa vile ulinipa hiki name nakupa hiki. elimu ya uraia ikifundishwa vyema ni rada ya kuongozea demokrasia katika nchi kwani huipeleka nchi katika njia sahihi kwa faida ya taifa na sio tija binafsi wa wanjanja wachache.

Wananchi wazuri ambao wanaelewa taarifa kuhusu mwelekeo wa serikali na siasa katika nchi yao hawajezaliwa hivyo bali wamepikwa kutokana na elimu ya uraia.

Thursday, December 2, 2010

JE NI KWELI KUWA SIASA NI MCHEZO MCHAFU? ( IS IT TRUE THAT POLITICS IS A DIRTY GAME?)

Siasa ni mfumo ambao unahusisha zaidi uongozi wa watu kwa kufuata kanuni, sheria, sera, uwajibikaji, uwazi na ugawaji wa rasilimali sawa kwa wnanchi wake;katika kuwaleta maendeleo  wadau wakuu ambao ni wananchi.

Kwa msingi wa utashi huu, wananchi wanakichagua kikundi cha watu ambao wanawaamini na kuwapa uwezo wa kuunda serikali ili iwaongoze kwa niaba yao.  Kwa hivyo hakuna nchi yeyote hapa duniani ambayo haina serikali. Tofauti inayoweza kujitokeza ni namna serikali hiyo inavyoundwa katika misingi ipi? Na inatekeleza vipi kanuni na taratibu zake? Je kuna uwazi katika shughuli zake? Viongozi wanabebe dhamana ya watu katika utendaji wao na wawajibikaje kwa wananchi ambao ndio waliowaweka ofisini; na viongozi wanatakiwa wawajibike na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

Siasa kama siasa sio mchezo mchafu;siasa inageuka kuwa mchezo mchafu pale tu serilali ambayo imekabidhiwa dhamana na wananchi inaanza kwenda kinyume na utaratibu na kanuni sahihi,  na kuto fuata   maadili ya uongozi (code of conduct) ndipo tafsiri ya siasa inaanza kugeuka na kuwa mchezo mchafu. 
                                                                        Amin Dada



Misingi ya siasa chafu imechochewa sana na mwanasalsafa Machiavelli  ambaye aliandika katika maandishi yeke kuhusu viongozi na madaraka; kitabu chake kinawanufaisha sana viongozi katika kuimarisha  nafasi zao za uongozi, amewafundisha viongozi namna ya kuwa waongo (liar), wakatili, wanafiki,  kuwa na uchu wa mali, na hata ikibidi kuua ili kupata madaraka na kuudumisha adhima yao ya kuendelea kunyonya na kujitajirisha. mwongozo huu wa Machiavelli unatumiwa sana na watawala wa mabavu (dictators), kutoka nchi mbalimbali ambao waliongoza au wanaongoza nchi zao kwa manufaa binafsi na sio kuwaletea maendeleo wananchi bali huwajengea hofu na kuwasababishia wananchi wao maisha magumu, watawala kama; Idd Amin Dada, Mabuto, na kadhalika. Katika mlengo huu hakuna kuwajibishana, kinachofanyika hapa wananchi ni kusikiliza na kutii tu



                                                                                        Mabutu                                                                                

Uchafu wa siasa ni pale tunapoilinganisha siasa kama wapiganaji katika mchezo wa mieleka ule ambao hauna kanuni yeyote ili ushinde, unaweza kumchezee au kumpiga au kumwangusha mpinzani wako kwa namna yeyote ile uwezayo ili mradi tu wewe uwe mshindi; hapa hakuna  kanuni yeyote inayohitajika refarii yuko pale kutangaza mshindi tu kwani hana kanuni yeyote ambayo anafuata; hapo ndipo tafsiri ya mchezo mchafu inapoanza.je nini kazi ya wanasheria wetu? Utetezi au uonevu? Tatizo la mchezo huu ukiuanza huwezi kuuacha. Ushauri kama huuwezi kamwe usiucheze waache wanaouweza waucheze,  watu wenye kiburi na wasiojali utu hata mara moja. Na ukiamua kuucheza kamwe usiuache au usiwasaliti wenzako ukifanya hivyo safari yako yakuendelea kufurahia maisha ya siasa yataishia kaburini.


Je siasa zetu zinalenga wapi tunaoutaratibu ambao tunaweza kumwajibisha hata kiongozi wa juu wa    nchi anapokiuka maadili ya uongozi? mkumbuke Nixon na “Watergate scandal” kwa kosa lolote lile ambalo alifanya akiwa kama kiongozi mkuu wan nchi alikiuka maadili ya uongozi kulingana na taratibu za serikali ya Marekani kilichofuata ni kumpigia kura ya kutomwamini na kumwondoa ofisini kama Raisi; alikwenda kwenye ziara kama Raisi wa Marekani ndani ya "Airforce One" lakini alirudi nyumbani kama raia wa kawaida kwa kutumia ndege ya kawaida ya abiria.



                                                                                    Nixon
                                                                   
Siasa sio mchezo mchafu kwa watu ambao ni wanyeneykevu na wenye huruma ya kuwahurumia wanyonge, watu wanaomwogopa Mungu, na daima sio wala rushwa, siasa kama kazi ni sawa na kazi nyingine zinazotakiwa kufuata taaratibu, tukumbuke kuwa iwapo mtu mwenye haki anaongoza nchi kila mtu atafurahia matunda na maziwa yatokanayo na rasilimali ya nchi hiyo, lakini iwapo nchi itaongozwa na mtu mwovu, fisadi wanyonge wataumia sana na wenye nacho wataongezewa. Na hapo tutakendelea na kilio cha kila siku kwanini sisi ni masikini katika nchi hii iliyojaa maziwa na asali na wakati huo huo inawatajirisha watu au inchi nyingine?


Tukumbuke kwa wale ambao wamesoma kitabu cha sharkespear  nini alikifanya Macbeth kwa kusababisha umwagaji wa damu ambao ulikuwa hauna sababu kwa sababu tu ya  siasa  za ubinafsi na hatimaye kutekeleza mwonekano wa siasa kuwa mchezo mchafu ambao mwisho wa siku ulimgeukia mwenyewe na kuuwawa. Tatizo la uchafu wa siasa pengine huanzia kwa serikali kuona kuwa ofisi zao ndio biashara yao hivyo hata ile mishahara ambayo wamewekewa kisheria haiwatoshi na huanza kujiingiza katiak rushwa, mikataba mibovu ambayo inawapa masilahi wao binafsi, na kuwaongezea nguvu ya kipesa na uwezo wa kuongoza kwa masilahi ya watu wachache.

Katika nchi zetu ambazo umasikini umekidhiri, tatizo la kukosekana kwa ajira, kupeana kazi na vyeo kwa kufuata undugu na urafiki na sio sifa za elimu, kuwanunua watu kwa kuwapa zawadi wakati wa kampeni na hatimaye wakati wa upigaji wa kura, kwa misingi hiyo sio rahisi baada ya uchaguzi kwa wananchi kuwawajibisha viongozi wao. Siasa taalumu nzuri sana na muhimu kwa jamii ikiwa itawapata viungozi wazuri na waungwana ambao wamewaeka wananchi mbele ya maendeleo yao, lakini siasa ikiwapata viongozi wabovu wala rushwa nchi imekwisha na wanyonge hawana chao ndipo hapo siasa inapokuwa ni mchezo mchafu. Kwa msingi huu ni kuwa siasa sio mchezo mchafu ni mchafu tu ikipata watu wala rushwa  na sio waaminifu, walafi wa madaraka,

Ni mchezo mchafu tu kama utaratibu wote wa uchaguzi haukwenda vizuri na matokeo yake baada ya hapo ni chuki binafsi baina ya vyama na hiyo mwisho wa siku itamaanisha kuwa chama tawala na  chama cha upinzani ni maadui na hakuna wa umuhimu wa chama kingine kuwapo, vyama vya siasa katika nchi vinaweza kuiongoza kwa kupokezana ni kama huko Marekani wakati wananchi wanapoona kuwa nchi iko amani yao ina mashaka wanakipigia Republican lakini wakiona uchumi wao unayumba wanakipigia Democratic;

Tukumbuke maneno ya Raisi JF Kennedy wa Marekani alivyosema” hakuna mtu ambaye atanishawishi mimi kufanya kitu ambacho nafikiri sio kwa masilahi ya nchi yangu, kama wewe au mtu mwingine anafikiri kuwa ndiye, basi huyo ni Mwendawazimu” Hii ndio tofauti ya kiongozi ambaye kwake siasa ni mchezo mzuri kwa masilahi ya wananchi wake na taifa lake, ambaye ni mkweli mwadilifu na ambaye anaweza kutoa maamuzi mazito kwa faida ya nchi yake, LAKINI pale tunapokosa maadili ya uiongozi tunakaribisha sana  urafiki, undugu na kugeuza ofisi zetu ambazo zimewekwa kwa masilahi ya Taifa kuwa sehemu za biashara na kuwakaribisha zaidi wenye fedha kututawala kwa kutoa mwongozo nini kifanyike hapo ndipo tunabadilisha tafsiri sahii ya siasa kuwa mchezo mchafu. Pengine bora hata kiongozi ambaye ni mbabe wa maendeleo ya taifa ambaye anapinga uzembe na hana rafiki wala ndugu ndugu yake ni maendeleo ya nchi yake. Je tunao viongozi wa namna hii hasa barani Afrika. tumkumbuke Mzee wetu, Mandela Nyerere na wengine wa namna kama yao

                                                                                         Mandela
                                                                                
Nukuu:


Politics is the gentle art of getting votes from the poor and campaign funds from the rich, by promising to protect each from the other.
Oscar Ameringer



Politicians are like diapers. They both need changing regularly and for the same reason.
Author Unknown



Blessed are the young, for they shall inherit the National Debt."
Herbert Hoover



Richard Nixon is a no good, lying bastard. He can lie out of both sides of his mouth at the same time, and if he ever caught himself telling the truth, he'd lie just to keep his hand in."
Harry S. Truman.