WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, March 6, 2012

KATIKA SAKATA LA MADAKTARI VS SERIKALI TATIZO LIKO WAPI?

Msimamo Wa Madaktari Leo


05/03/2012
KAMA TULIVYOTOA TAARIFA KWENYE KIKAO CHA MADAKTARI CHA MARCH
3, NI KWAMBA

MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA NA HATIMAYE KUTIWA SAINI KATI YA
SERIKALI NA
MADAKTARI TAREHE 2/3/2012 NI KUWA, ILI MEZA YA MAZUNGUMZO YA KUJADILI
MADAI
YA MADAKTARI IWEZE KUENDELEA NA HATUA YA PILI NI LAZIMA WAZIRI WA AFYA
(DR MPONDA) NA NAIBU WAKE (DR LUCY NKYA) AMA WAJIUZULU AU WAWAJIBISHWE
KAMA

ILIVYOKUWA IMEAHIDIWA NA MH. WAZIRI MKUU FEBRUARY 9 ALIPOFANYA KIKAO
NA WATUMISHI WA AFYA PALE HOSPITALI YA MUHIMBILI.

AIDHA, KULINGANA NA MAKUBALIANO HAYA KIKWAZO KIKUBWA CHA
KUTOKUENDELEA KWA MAJADILIANO YA MADAI YA MADAKTARI (UBORESHAJI
WA HUDUMA WAPATAZO WAGONJWA,

MAZINGIRA MAZURI YA KUFANYIA KAZI NA MASLAHI KWA UJUMLA WAKE) NI
KUENDELEA KUWEPO KWA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA KWENYE NAFASI ZAO ZA
KIUONGOZI.

HIVYO BASI, KWENYE HUO MKUTANO WA MARCH 3, BAADA YA MAJADILIANO NA
TAFAKARI ZA KINA, ILIKUBALIWA KWA PAMOJA KUWA WATU HAWA WAWILI
WANATAKIWA KUACHIA NGAZI MARA MOJA ILI HAKI ZA WAGONJWA
NA MADAI YA MADAKTARI YAWEZE KUJADILIWA NA KUTEKELEZWA.

HIVYO BASI, ILIAMULIWA KUWA KAMA MPAKA SIKU YA JUMATANO
(MARCH 7) BADO AKINA DR MPONDA NA DR LUCY NKYA WATAKUWA BADO WAPO
MADARAKANI WATAANZA MGOMO RASMI KUSHINIKIZA AMA WAJIUZULU AU
WAWAJIBISHWE ILI TARATIBU ZINGINE ZIWEZE KUANZA.

KAMA ILIVYO TARATIBU YA CHAMA KUTOA TAARIFA KWA WANACHAMA KOTE NCHINI,
IFAHAMIKE KWAMBA MKUTANO ULIAMUA KUWA MADAKTARI WOTE KUWA KUANZIA
JUMATANO (MARCH 7) WATASITISHA KUTOA HUDUMA ZOTE ZA AFYA KATIKA
HOSPITALI ZOTE NCHINI MPAKA HAPO SERIKALI ITAKAPOONESHA UTAYARI KWA
KUTIMIZA AHADI YAKE YA KUWAWAJIBISHA WATAJWA HAPO JUU ILI HATUA
ZINGINE ZA UTEKELEZAJI WA MADAI YA MADAKTARI KWA MANUFAA YA TAIFA
YAWEZE KUANZA KUSHUGHULIKIWA.

IFAHAMIKE KWAMBA CHAMA KINASIKITISHWA SANA NA KITENDO
CHA VIONGOZI WAANDAMIZI WA WIZARA YA AFYA AMBAO WANAJUA
UMUHIMU WA KUWAJIBIKA. KWA MARA NYINGINE TENA WANAWAFANYA
MADAKTARI WAENDELEE KUTETEA HAKI ZA WATANZANIA

KATIKA NJIA NGUMU NA KWA NIA YA KUFANIKISHA MALENGO HAYA KWA FAIDA YA
WATANZANIA WOTE.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAT MAKAO MAKUU.


DR. NAMALA MKOPI RAIS WA MAT
  
Habari kwa hisani ya Mjengwa Blog

Thursday, March 1, 2012

TANZANIA BILA UCHAFU INAWEZEKANA


JE TATIZO LA UCHAFU WA MAZINGIRA UNAOKABILI MIJI YETU NI SEHEMU YA UTAMADUNI WETU?

Tatizo la uchafu wa miji yetu ukiongwozwa na jiji la dare s salaam  limeendelea kuwa ni kero kubwa sana katika jamii yetu; kama wananchi wengi na wanaharakati wameendelea kusema kupiga kelele na kuandika kuwa  “ Kama kuna suala ambalo linakera pia ni uchafuzi wa mazingira. Sio kwamba huwa ni kero tu, lakini uchafu huleta magonjwa mbali mbali na hatimae vifo ambavyo mara nyingi ni vya kujitakia.”



Najiuliza leo tatizo letu kama watanzania ambao tumesherekea miaka 50 ya uhuru wetu kwa amani na utulivu lakini kwa upande mwingine sherehe zilizozungukwa na uvundo wa taka kila mahali sisi kama watanzania tumekosa nini au ni nini tunashindwa kufanya ili hata kupunguza tatizo hili?

Je serikali yetu na viongozi wake hawalione hili, na hali wakeri? Au wao wanaishio katika nchi nyingine tofauti nah ii tunayoilalamikia? Au wako kwenye ya kufikirika ambako wao uchafu hauwakeri na wanashindwa kuusimamia?

Je ni tatizo la pesa za kusiamamia usafi au zile kidogo zinazopatika zinatumika bila kuangalia kipaumbele? Je  miji yetu lina itaweza kuandaa utaratibu mzuri wa kuwa na Vifaa Vya Kuwekwa Takataka hii itakuwa na mwanzo mzuri wa kuanza kuwaelimisha wananchi utaratibu na kuwezesha  Kila  mtu kuweza kutupa  taka taka Popote Alipo.  Wananchi wasipoweza kutafutiwa utaratibu wa kuweza kuwa na ukahika wa wapi watupe takataka tutawapa sababu ya kutoana  kama kuna sababu ya Kujali Usafi Wa Miji miji husika. Je Usafi Wa Miji Yetu Tanzania Inahitaji Pesa Za Kigeni?  Tufanye Nini Ili Tutunze Usafi Wa Miji Yetu

JE TATIZO LA  KUKITHIRI KWA UCHAFU JE VIONGOZI WETU WANAHUSIKA?

viongozi hawawezi kukwepa jukumu lao katika hili Tusijaribu kuwavua wajibu viongozi wetu. Uchafu unaanzia kwao. Je uongozi wa miji yetu kwa nini usiwajibishwe? Kwa nini tunawalaaumu viongozi wetu ? kwa falfasa ya kirahisi tu tunawaona viongozi wetu wanaonyesha kabisa haw anjali kwani wao wanaangalia sasa na sio chanzo. Watasimamia usafi  kwa ajili ya kiongozi mwingine  anayekuja  wa nchi tofauti  kusafisha mazingira na kupamba mji, lakini, baada ya hapo uchafu unabaki pale pale. Hii ni aibu kwetu. Je hata kuweka vifaa vya kutupa taka ndani yake inashindikana? je hata kutunga sheria ndogo za kuwajibisha wachafuzi wa mazingira inashindikana?

Elimu ya usafi wa mazingira yafaa iwashirikishe watendaji wote kuanzia ngazi za chini katika serikali za mitaa, kata hata tarafa. Kama taifa tunahitaji wananchi waelemishwe vya  kutosha kwa wananchi kuhusu usafi wa mazingira. Kwa mfano uchafu katika jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake ni moja ya matatizo makubwa na ambayo ni dhahiri uongozi wa jiji hili unaelekea kuwa umeshindwa kulipatia ufumbuzi. 

JE NINI KIFANYIKE KATIKA KUTATUA TATIZO HILI KWA JUMLA;

Je tunazo sheria za kusimamia usafi wa mazingira?  
Je sheria zetu zinawabanaje  wafanyabiashara ndogondogo ambao wamekuwa wakijiendeshea shughuli zao mahali popote wanapojisikia na sehemu ambazo si rasmi na kufanya kuacha taka ngumu katika maeneo ya  biashara zao?

Je miundo mbinu yetu inafanya kazi vizuri au hatuna mfumo taka  unaoeleweka? Je gharama za kusafisha vyoo vilivyojaa mwananchi wa kawaida amaweza kumudu? Kama hawezi kumudu sheria zetu zinawaruhusu kusafisha vyoo vyao/au kuzibua wakati wa mvua?
Je ushuru amabao wananchi na wafanya biashara unatumika katika kufanya usafi au matumizi makubwa ya ushuru huo unatumika kwa matumizi ya kiofisi?

Kama mwanaharakati mmojai alivyowahi andika kuwa “ Swala la uchafu kukidhiri Dar ni watu kutowajibika Ufisadi tu watu wanalipa ushuru lakini Halimashauri ya jiji wanatupia tumboni.Kama jiji Chafu basi hata watu wenyewe usafi wao binafsi ninawasiwasi mno.Hata hivyo usafi si kila mtu anaweza. Uchafu na harufu mbaya katika jiji hilo umekuwa ni jambo la kawaida, hali hiyo inalitofautisha jiji hilo lenye hadhi Tanzania na majiji mengine makubwa duniani.” 

Waziri wetu Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda (Mtoto Wa Mkulima) baada ya moja ya ziara zake za kutembelea Jiji la Dar es Salaam  aliwahi sema kuwa “hali hairidhishi, Hali hii isipochukuliwa hatua haraka na kupewa kipaumbele kamwe magonjwa ya milipuko kama vile kichocho na kipindupindu hayatodhibitiwa na watu wataendelea kupoteza maisha kwa vitu ambavyo kama kuna mkakati mzuri vinaweza kudhibitiwa”.

MTAZAMO KWA UJUMLA

Tunaweza kufanya miji yetu kung’ara kama kila mtu atajitahidi kuwajibika na kujijengea utamamduni mpya wa kutunza mazingira, na kukataa tabia ya kutupa taka ovyo na kila mtu kuwa mlinzi wa mwenzake na kumkemea yeyoye ambaye atakuwa na tabia ya kutupa taka ovyo;

Wananchi wawajibike kwa upande wao na viongozi wetu nao wawajibike kwa upande wao kwani wao  ndio msingi wa kufanikisha zoezi nzima kwa kuweza kufacilitate utaratibu,

·        Kuandaa sheria ambazo zinatekelezeka;

·        Kuandaa vifaa vya kuwekea taka katika sehemu mbalimbali za jiji ili kuwarahisishia wananchi kutupa taka  na kuwapunguzia wananchi ushawishi wa kutupa taka ovyo;

·        Viongozi waandae magari yanayotakiwa kwa ajili ya kubeba taka na sio magari ambayo baada ya kuondoa tatizo la taka, yanaongeza uchafu kwa kutupa uchafu kila yakiwa yakipita na taka.

·        iko haja ya kuwekwa kwa sheria kali za kudhibiti kwanza utupaji taka hovyo kama ilivyo katika miji mingine ya kitaifa na sheria hizo zisiwe mapambo, bali zitumike kwa vitendo kwa wahusika kuchukuliwa hatua ikibidi kutangazwa ili iwe ifundisho. 

·        Viongozi waweze kuona aibu ya miji yetu kuwa michafu na inanuka

Kama tatizo la uchafu litaendelea kuwa ni tatizo sugu kwa taifa letu swala hili litakuwa ni aibu kwa taifa zima na si kwa wakazi miji husika; kama taifa tuweze kuwatumia wataalamu waliopo  kuwaomba kuaandaa  mikakati bora ya utupaji taka ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kutupia taka ambayo hayapo katika maeneo ya makazi ya watu.

Nafikiri sio jambo la busara kuendelea kutupiana lawama, ni vyema kwa pamoja serikali na wananchi wakakutana kama wadau na kujadiliana namna ya kuondokana na aibu hii. Kwa kufanya hivyo tutaweza kuliepusha Taifa na magonjwa ya mlipuko na kulijengee taifa usalama wa afya  za wananchi.



Naamini kuwa usafi hauhitaji kwenda shule au  ufadhili kutoka nje; bali yatupasa kubadilisha tabia na utamaduni wetu; tunaweza kubadilisha tabia zetu na kubadilisha maisha yetu ya kutoka kuzungukwa na uchafu na kuwa taifa safi na litakalo heshimika kwa utunzaji wa mazingira.

TANZANIA BILA UCHAFU INAWEZEKANA

Hotuba Ya Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete February 2012



Ndugu Wananchi,
Naomba sote tumshukuru Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehma kwa kutuwezesha kuzungumza tena mwisho wa mwezi huu. Katika mwezi tunaoumaliza leo taifa letu lilipata msukosuko mkubwa kufuatia mgomo wa madaktari. Nashukuru mgomo huo umeisha lakini makovu yake yatabaki maisha katika kumbukumbu za historia ya taaluma ya tiba hapa nchini.
Leo, Mheshimiwa Waziri Mkuu amenipa taarifa kuwa Kamati aliyounda kushughulikia madai ya madaktari imekamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa yake kwake. Kuanzia kesho Serikali itaifanyia kazi taarifa hiyo na kuamua ipasavyo kulingana na uwezo uliopo. Nawaomba ndugu zetu madakatari kuwa na moyo wa subira. Napenda kutumia fursa hii kuwahakikishia ndugu zetu madaktari na watumishi wengine wote wa sekta ya afya kwamba Serikali inatambua, inajali na kuthamini kazi wazifanyazo na mchango wao katika kulinda na kudumisha afya za wananchi wa Tanzania. Aidha, narudia kutoa pole zangu za dhati kwa wananchi na hasa wagonjwa nchini kwa mateso waliyoyapata katika kipindi cha mgomo. Ni matumaini yangu kuwa hali kama ile haitajirudia tena katika nchi yetu.
Ndugu Wananchi,
Tukio lingine la kusikitisha ni mauaji ya Songea. Yapo yale yanayohusishwa na imani za ushirikina, na yapo yale ambayo yalitokea kwenye maandamano. Napenda kutumia nafasi hii kuelezea masikitiko yangu kwa vifo hivyo na kutoa pole na rambirambi zangu na za wananchi wa Tanzania kwa ndugu wa marehemu wetu hao. Tupo pamoja nanyi katika misiba hii mikubwa na majonzi. Napenda kuwahakikishia wananchi wa Songea kwamba Serikali kupitia vyombo vyake vya usalama imekuwa inafanya na itaendelea kufanya uchunguzi wa kina wa mauaji haya mpaka wahusika wote wapatikane na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria. Nimearifiwa kuwa, mpaka sasa kwa mauaji 13 yanayohusishwa na imani za ushirikina watuhumiwa 26 wamekwishakamatwa. Na kwa mauaji yaliyotokana na maandamano, askari polisi wanne wamekamatwa na upelelezi unaendelea.
Ndugu Wananchi;
Nashukuru kwamba amani na utulivu vimerejea katika Manispaa ya Songea. Nawapongeza sana viongozi wa ngazi zote na wananchi kwa ujumla kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuwezesha usalama na utulivu kupatikana. Tafadhali endeleeni na juhudi hizo mpaka mambo yatengemae kabisa.
Ndugu Wananchi;
Katika mwezi huu pia, Bunge letu Tukufu lilifanya mkutano wake wa sita na miongoni mwa maamuzi makubwa yaliyofanywa ni kupitisha Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 hususan kuhusu Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuhusu Katiba ya nchi. Nimekwishatia saini marekebisho hayo tarehe 20 Februari, 2012 na hivyo sasa yako tayari kutumika.
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi kwa Wabunge wetu kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya ya kupitisha marekebisho hayo. Aidha, natoa pongezi maalum kwa vyama vya siasa vya CCM, CHADEMA, CUF na NCCR - Mageuzi pamoja na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali kwa maoni na mapendekezo yao ambayo ndiyo yalikuwa chachu ya marekebisho yaliyofanyika. Pia, nawashukuru kwa ushirikiano wao uliowezesha mafanikio kupatikana Tulipotoka

Ndugu Wananchi;
Bila ya shaka mtakumbuka kuwa baada ya Bunge kupitisha Muswada wa Sheria ya Mabadikiko ya Katiba tarehe 18 Novemba, 2011, kulikuwepo na maneno mengi na maoni mbalimbali katika jamii. Wapo baadhi ya wadau hasa baadhi ya vyama vya siasa na asasi za kiraia ambao waliniomba nisitie sahihi Muswada huo kuwa Sheria na badala yake niagize Bunge liuzungumze upya. Aidha, vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF na NCCR – Mageuzi na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali waliomba kukutana nami tuzungumzie mchakato mzima wa Katiba. Sikusita kuwakubalia na kwa nyakati mbalimbali tulikutana na kuzungumza nao.

Ndugu Wananchi;
Katika mazungumzo yangu nao niliwaeleza ugumu niliouona kuhusu kuacha kutia sahihi Muswada huo na kuurudisha tena Bungeni kujadiliwa upya. Nilichelea kuliingiza taifa letu katika mgogoro mkubwa wa kisiasa na kikatiba usiokuwa na lazima. Mgogoro ambao tunaweza kuuepuka kwa kutumia njia nyingine za kikatiba na kisheria kufikia malengo yale yale. Kitendo cha mimi kukataa kutia sahihi kingejenga chuki kwa upande wa Wabunge walio wengi ambao waliujadili Muswada na kuupitisha. Wengeweza kuhisi wamedharauliwa na kuonekana hawana thamani.
Katika mazingira hayo mtakapowarudishia Muswada huo kuujadili kuna hatari ya kutokupata ushirikiano wao na kushindwa kupata kile kinachotarajiwa. Wanaweza kujadili na kuamua kukataa mapendekezo yote mapya na kubakia na msimamo wao ule ule.

Ndugu Wananchi;
Kwa ajili hiyo, busara ilinielekeza kuwa tusitumie njia hii bali tutumie njia za kawaida za kufanya marekebisho ya Sheria zilizotungwa na Bunge. Hakuna Sheria iliyotungwa na Bunge ambayo haiwezi kufanyiwa marekebisho. Kinachotakiwa ni kupeleka mapendekezo ya vifungu au vipengele vya Sheria husika vinavyotakiwa kurekebishwa. Bunge litavijadili na kama hoja zinatosheleza vitafanyiwa marekebisho. Mimi nilipendelea busara na hekima hiyo. Niliwaeleza wadau sababu za kuamua kutia sahihihi Sheria na kuwasihi wakubali tufanye lililo bora zaidi ambalo ni kupeleka Bungeni mapendekezo ya sheria hiyo katika maeneo ambayo tunataka marekebisho hayo yafanywe.

Nilitahadharisha kuwa hata kufanya hivyo kunaweza kuwa na ugumu wake hasa pale dhana zisizokuwa sahihi zitakapopandikizwa kwa Wabunge. Niliwaomba tushirikiane kuhakikisha dhana potofu hazijitokezi na zinapojitokeza tuzisahihishe. Niliwahakikishia utayari wa Serikali kushirikiana nao katika hatua zote, tangu kutayarisha mpaka kuwasilisha mapendekezo hayo Bungeni iwapo watapenda Serikali ifanye hivyo. Aidha, niliwaambia kuwa hata sisi Serikalini tulikuwa na dhamira ya kupeleka marekebisho kwa baadhi ya vifungu vya Sheria hiyo kwa sababu mbalimbali.

Nafurahi kwamba, kwa pamoja licha ya tofauti zetu kuhusu uamuzi wangu wa kutia saini Muswada tulikubaliana kushirikiana kutoa mapendekezo ya marekebisho ya Sheria hiyo, ambayo tuliyawasilisha katika Bunge lililopita. Nafurahi na kufarijika kwamba, baada ya mjadala mkali, na Wabunge kufanya marekebisho kadhaa na hata kuingiza mambo mengine mapya, Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ulipitishwa na Bunge tarehe 10 Februari, 2012. Baadaye uliwasilishwa kwangu na nikatia sahihi kuwa Sheria tarehe 20 Februari, 2012. Sina budi pia kukitambua Chama cha Mapinduzi ambacho kilileta mapendekezo yake. Mapendekezo hayo yalizingatiwa kama ilivyofanywa kwa yale ya wadau wengine.

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kutoa pongezi maalum kwa vyama vya siasa vya CHADEMA, CUF, NCCR – Mageuzi na CCM na Baraza la Taifa la Asasi Zisizokuwa za Kiserikali kwa uelewa wao na ushirikiano wao kulikotuwezesha kufikia hapa tulipo katika mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya kwa usalama, utulivu na kwa maelewano. Kwa kweli, jinsi hali ilivyokuwa huko nyuma, hatuna budi kushukuru na kujipongeza. Ni matumaini yangu na rai yangu kuwa tutaendeleza ushirikiano na utamaduni huu wa mazungumzo tuliouanzisha na kuutumia katika hatua zingine zinazofuata.

Nchi imetulia joto na jazba kuhusu Katiba havipo. Kumbe tukiamua na hasa tukizungumza inawezekana. Naomba wadau wote tuazimie kuwa mambo yaendelee hivi hata katika hatua zijazo za mchakato huu na masuala mengine muhimu kwa maslahi ya nchi yetu na watu wake.
Ndugu Wananchi;

Katika mazungumzo yetu na wadau tulikubaliana kwamba tushughulikie marekebisho ya Sheria hii kwa awamu. Kwa kuanzia tushughulikie mambo yanayohusu Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi Kuhusu Katiba ili iundwe na kuanza kazi. Baada ya hapo tuangalie mambo yahusuyo Bunge Maalum na Kura ya Maoni.

Bahati nzuri Sheria ya sasa inaelekeza kuwa Kura ya Maoni itatungiwa Sheria yake maalum, hivyo mambo yanaweza kusubiri wakati huo. Hivyo basi, baada ya muda si mrefu, Serikali na wadau tutaanza mazungumzo kuhusu mapendekezo ya marekebisho kuhusu Bunge Maalum. Kama yatakuwepo na kama kutafikiwa makubaliano, mapendekezo yatafikishwa katika Bunge letu tukufu kwa hatua zipasazo.

Ndugu Wananchi;
Bahati nzuri pia kuna kipindi kirefu kidogo wakati Tume inaendelea na kazi yake mpaka hapo Bunge Maalum litakapoanza kazi. Tume imepangiwa kukamilisha kazi yake ndani ya miezi 18 na inaweza kuongezwa miezi miwili. Wadau wanaweza kutumia sehemu ya muda huo wa Tume kushughulikia na kufanya marekebisho yahusuyo Bunge Maalum. Hata hivyo, kama mapendekezo yatakamilika mapema ni bora zaidi yafikishwe Bungeni na kushughulikiwa ipasavyo. 

Wadau Kupendekeza Majina

Ndugu Wananchi;
Miongoni mwa marekebisho muhimu yaliyofanywa katika Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika Bunge lililopita ni kuwekwa kwa utaratibu wa wadau kupendekeza kwa Rais majina ya watu wanaoona wanafaa kuteuliwa kuwa Wajumbe wa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni kuhusu Katiba. Nafurahi kutoa taarifa kwamba nimekwishatoa mwaliko kwa wadau husika, yaani vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, jumuiya za kidini, asasi za kiraia pamoja na jumuiya, taasisi na makundi mengine yenye malengo yanayofanana kuleta mapendekezo hayo.
Mwaliko wangu huo umeshatangazwa katika Gazeti la Serikali Namba 66 la Ijumaa tarehe 24 Februari, 2012. Kuanzia kesho itatangazwa katika magazeti ya kawaida. Katika mwaliko huo, wadau wanatakiwa kupendekeza majina yasiyozidi matatu ya watu wanaokidhi sifa zilizotamkwa katika kifungu cha 6 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba. Sifa hizo ni hizi 

zifuatazo:-
(a) Uzoefu katika kufanya mapitio ya katiba na sifa za kitaaluma za wajumbe kwenye mambo ya katiba, sheria, utawala, uchumi, fedha na sayansi ya jamii.
(b) Jiografia na mtawanyiko wa watu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na
(c) Umri, jinsia na uwakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii.
Aidha, nimeelekeza kuwa siku ya mwisho ya wadau kuwasilisha mapendekezo yao ni tarehe 16 Machi, 2012. Wadau wanatakiwa kupitishia mapendekezo yao kwa Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Muungano au Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Nimewapa viongozi watendaji wakuu hao jukumu la kupokea mapendekezo ya majina na kuyawasilisha kwangu. Baada ya hapo nitashauriana na Rais wa Zanzibar kuteua Wajumbe wa Tume pamoja na Mwenyekiti na Makamu wake.

Ndugu Wananchi;
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba pia inatoa fursa kwa Rais kuteua Wajumbe wa Tume kutoka hata nje ya orodha ya wadau. Ilionekana ni vyema kufanya hivyo kwani wapo watu wengine wazuri ambao wanaweza kuwa hawamo katika makundi yaliyotajwa na Sheria hii. Aidha, upo uwezekanao kwa mapendekezo ya makundi kutozingatia baadhi ya mambo ya msingi kama vile jinsia, jiografia na mtawanyiko wa watu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kadhalika. Fursa hii aliyopewa Rais itasaidia katika kuzingatia matakwa haya ya Sheria.
Pamoja na hayo napenda kuwahakikishia kuwa iwapo nitaitumia fursa hiyo watu hao hawatakuwa wengi kuliko wale waliopendekezwa na makundi yaliyotajwa katika kifungu cha 6 (6) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha wadau na wananchi kwa jumla kuwa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni Kuhusu Katiba ina Wajumbe 30 tu wanaopatikana kwa idadi sawa kutoka sehemu zotu mbili za Muungano wetu yaani 15 kutoka Tanzania Bara na 15 kutoka Zanzibar. Unapoongeza Mwenyekiti na Makamu wake kwa jumla Tume itakuwa na wajumbe 32 yaani 16 kila upande. Hivyo basi, fursa ya kila aliyeleta majina kupata nafasi katika Tume si kubwa.

Nayasema haya kutahadharisha juu ya ukweli huu ili tusijipe matumaini makubwa mno na wala tusije tukashutumiana baada ya uteuzi. Hata hivyo, pamoja na ugumu wa kuchagua miongoni mwa orodha ya watu wengi wazuri, nitajitahidi tu Wajumbe wa Tume wawe watu makini, wanaowakilisha sura pana ya jamii za nchi yetu na makundi yake muhimu na utashi wa watu wa Tanzania yetu.
Tunapokwenda
Ndugu Wananchi;
Ni matarajio yangu kuwa zoezi la kuunda Tume litakamilika muda mfupi kadri inavyowezekana, baada ya kupokea mapendekezo ya makundi. Kama nilivyokwishawahi kudokeza siku za nyuma, napenda Tume ikamilike kuundwa katika robo ya pili ya mwaka huu na kuanza kazi muda mfupi baada ya hapo.
Naomba nitumie nafasi hii kutoa wito maalum kwa wananchi wenzangu kuanza kujiweka tayari kutoa maoni yao kwenye Tume. Mambo yataanza miezi michache ijayo. Najua Tume itatengeneza utaratibu wa kuelimisha wananchi kuhusu Katiba. Lakini nawaomba kila mtu binafsi yake aanze kuchukua hatua za kuifahamu Katiba iliyopo sasa ili apate ufahamu wa maudhui muhimu ya Katiba. Kufanya hivyo kutamuwezesha kuamua kwa usahihi anataka kupendekeza nini kiwemo katika Katiba mpya. Nimeagiza Mpiga Chapa wa Serikali kuhakikisha kuwa vitabu vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinachapishwa kwa wingi ili wananchi waweze kuwa navyo na kuvisoma. Inawezekana, Timiza Wajibu Wako.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Mungu Ibariki Afrika!
Mungu Ibariki Tanzania!

Habari kwa hisani ya Mjengwa Blog

Tuesday, February 21, 2012

MUGABE NA DEMOKRASIA



Akitimiza miaka 88 leo Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe aliyetawala toka uhuru wa nchi nchi hiyo1980,  leo amesema bado ataendelea kugombea uraisi wa nchi hiyo mpaka pale atakaposema mwenyewe imetosha..
Habari kwa Hisani ya Mjengwa Blog



Monday, February 20, 2012

LEADERSHIP CORNER

Most people spend more time and energy going around problems than in trying to solve them. - Henry Ford

Sunday, February 19, 2012

Uchambuzi Wa Habari: Dk Mwakyembe Naye Amwaga Sumu!



Ndugu zangu,

Kwenye vyombo vya habari kumekuwa na taarifa zinazochanganya  juu ya kinachomsibu Dk. Mwakyembe.

Na kama utangulizi ufuatao nitauzungumza kama hotuba fupi mbele ya watu wanaojiandaa kwa mlo wa kusheherekea harusi, basi, nina imani, zaidi ya nusu ya wageni waalikwa watainuka kwenye meza zao na kukiacha chakula.

Maana nitaanza kwa kusema;

Mabibi na Mabwana,

Wakati tukijiandaa kwa  mlo ulio mbele yenu ningependa kuwaeleza mafupi juu ya sumu na jinsi sumu inavyoweza kuingia kwenye mwili wako na hatimaye kukudhuru. Na bila shaka wote mnajua kuwa sumu inaua.

Ni hivi; unaweza kuwekewa sumu. Usipoiona na ukaiacha, basi, utakuwa umepona.  Ndio, kama kuna sumu imewekwa usiichukue. Kwa mantiki hiyo hiyo, jiadhari, unaweza ukashikishwa sumu.  Kuwa makini na wanaokupa mikono ya heri, mingine ni mikono ya kifo. Yumkini anayekupa  mkono amevaa glovu yenye sumu.

Ndugu yangu, unaweza pia   ukagusishwa sumu.  Kuwa makini na unayecheza nae muziki baada ya mlo huu. Kumbatio la muziki tulivu laweza kugeuka kuwa ni kumbatio la kifo.

Sumu inaweza  pia kukuingia  mwilini kwa kulishwa.  Uwe makini na anayekulisha kipande cha keki ya harusi. Na kama waweza kulishwa sumu hivyo hivyo waweza ’ kujilisha’ mwenyewe sumu. Chunga sana na anayekupa kipande cha nyama choma. Ukakipokea na hatimaye kukitia mdomoni.

Kama ilivyo kwa kulishwa na kujilisha sumu. Yawezekana pia sumu ikaingia mwilini mwako kwa kunyweshwa au kujinywisha.  Chunga sana na unayekaa karibu naye. Jichunge mwenyewe pia. Ukinywa vodka nyingi ni sawa na ’ kujinywisha’ mwenyewe sumu.

Sumu yaweza pia kukuingia mwilini kwa kumwagiwa. Kaa mbali sana na atakayefungua champeini isije kilichomo kikawa ni sumu.  Na wengine hamfahamu, kuwa   sumu yaweza  pia kukuingia kwa kupuliziwa.  Sahani yako ya chakula yaweza kuwa imepuliziwa sumu…

Ndugu zangu,

kuna njia nyingi sana za sumu kuingia mwilini mwako. Nisiwachoshe, tuendelee na  mlo wetu wa harusi!

Naam. Habari kubwa katika siku mbili hizi ni kadhia ya Dr. Mwakyembe na madai ya  sumu kuingizwa mwilini mwake na wabaya wake. Na kama mlivyoona hapo juu, bado haijawa wazi kama Mwakyembe kalishwa, kawekewa, kanyweshwa au kagusishwa sumu. 
Jitihada za Jeshi la Polisi juzi kutaka kutuambia WaTanzania ukweli juu ya kadhia hii zinaonekana kugonga mwamba  kwa kupingwa vikali na Mwakyembe mwenyewe. Tumesoma kwenye magazeti ya leo.

Nani anaongopa?

Bila shaka, habari hii imekuwa ikiwavutia wengi kwa vile kiu ya jamii ni kutaka kujua ukweli mzima. Jamii inataka kujua; nani anasema kweli na nani anaongopa. Vita inayopiganwa sasa imebaki kuwa ni vita ya maneno kwenye vyombo vya habari.

Kila upande unadai una ushahidi na unachosema lakini ushahidi huo hauwekwi hadharani ukaonekana.  Wanahabari nao wameonekana kusukumwa zaidi na upepo wa vita na kuandika yale ambayo wanadhani yatauza magazeti.  Kimsingi media inaweza ikamaliza vita hii kwa kuwauliza wahusika maswali sahihi na magumu yatakayotokana na  maelezo wanayotoa wahusika

Mfano, DCI Manumba anasema; ” Ukweli kuhusu  kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu , tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya ambayo nayo imewasiliana na  hospitali aliyokuwa amelazwa  Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha  kuwa hakuna sumu  katika maradhi yanayomsibu Mwakyembe.”- ( Mwananchi, Jumamosi, Februari 18, 2012)

Naam, kama DCI Manumba anadai wamethibitishiwa na Wizara ya Afya iliyofanya mawasiliano na hospitali anayotibiwa Dr . Mwayembe nchini India  kwamba Dr Mwakyembe hakukutwa na sumu mwilini ni kwanini wanahabari wasifike Wizara ya Afya kuthibitishiwa juu ya kile ambacho Manumba anadai kuthibitishiwa. Maana, haiyumkini kuthibitishiwa huku kukawa ni kwa mdomo tu.
Na Dk. Mwakyembe anaposema; ” Ripoti inatamka wazi kuwa  kuna kitu kwenye bone marrow ( ndani ya ute wa mifupa) kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua.” ( Mwananchi,  Februari 19, 2012.)

Kwa wanahabari kazi hapa ingekuwa kumbana Mwakyembe  awasaidie kupata maelezo ya ziada kutoka kwa mabingwa hao wa India ili iwasaidie ku-establish, bila mashaka, juu ya dhana ya sumu katika kinachomsibu Mwakyembe.

Vinginevyo, taarifa ya jana ya Dr Mwakyembe inatoa tafsiri pia ya mtu aliyejeruhiwa na aliyeamua ’kumwaga sumu’ hadharani. Taarifa ile ya Mwakyembe imeonyesha jinsi  watendaji wetu wakuu Serikalini na hata kwenye chama tawala wasivyoaminiana. 

Tumeona jinsi Mwakyembe alivyorusha makombora makali dhidi ya jeshi la polisi na kutoa tuhuma nzito ya jinsi  jeshi hilo linavyotenda hujuma . Kwa mtu wa kawaida atajiuliza; kama Mwakyembe Waziri na kada wa CCM analia kuchezewa faulo, je,  hali itakuwaje kwa mtu wa kawaida na kama ni mwanachama wa chama cha upinzani?

Swali lingine; kama baadhi ya mawaziri wa JK kwenye baraza moja wanaonyesha hadharani kuwa hawaaminiani wanamsaidiaje Rais wa nchi? Na je, Mwakyembe au Sitta wakihamishimiwa wizara ya Mambo ya Ndani  watafanyaje kazi na akina Manumba na Said Mwema? Na kuna wengi wanaomtarajia JK kufanya  mabadiliko makubwa  ya Baraza la Mawaziri kwa vile hawaridhishwi na utendaji wa Baraza lililopo.

Na haya yote tunayoyashuhudia  ni ’ maradhi ya taifa’  ya tangu uhuru kwa vile tumekuwa na Katiba yenye mapungufu makubwa na kwa sasa isiyokidhi mahitaji ya wakati uliopo. Tunamshukuru Rais wa nchi kwa kuonyesha dhamira ya kutuanzishia mchakato utakaopelekea kupata Katiba Mpya kwa Taifa la Kisasa.

Katiba ya sasa inaruhusu ’ ubaguzi wa kisiasa’. Inawatenga Watanzania wengine katika ushiriki wa uongozi na ujenzi wa nchi.  Na dhambi ya ubaguzi ndio inayotutafuna sasa hadi tukafikia hata viongozi watendaji wa juu ndani ya chama tawala  kukosa kuaminiana.
Ndio, Watanzania walio wengi  ’ hawajalishwa sumu’, isipokuwa, kwa miaka mingi Watanzania wamekuwa ’ wakibwigizwa ugoro’ uliowafanya wasinzie  kama watu waliopigwa  sindano ya ganzi.

Wengi  sasa , na hususan vijana, wanakataa mchana wa jua kali kubwigizwa ugoro na walio kwenye mamlaka. Wamebumbuluka. Wameanza kusoma katikati ya mistari. Ndio, wameamka na wana kiu ya kuiona Tanzania mpya na inayostawi. 

Maggid Mjengwa,
Dar es Salaam.
Jumapili, Februari 19, 2012.

Habari kwa hisani ya Mjengwa Blog

Thursday, February 16, 2012

WHAT IS LEADERSHIP?


Leadership is understanding people and involving them to help you do a job. That takes all of the good characteristics, like integrity, dedication of purpose, selflessness, knowledge, skill, implacability, as well as determination not to accept failure. - 

Admiral Arleigh A. Burke