WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 15, 2011

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUWEZESHA KUTIMIZA MIAKA 17 YA NDOA LEO NOVEMABER 16 2011










Tunapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kutuwezesha kutimiza miaka 17 ya maisha ya ndoa; mwezi  wa November Tarehe 16, 2011 ni sawa na miaka 17 iliyopita  Mke wangu Mpendwa Grace Peter Myamba (Teacher au Mama Rose) pamoja nami Emmanuel Alois Turuka  tuliunganishwa kuwa  mwili mmoja katika ndoa Takatifu;


Tarehe 16 November 2011 tunamshukuru  Mungu kwa kutuwezesha kutimiza miaka 17 ya ndoa  iliyojaa upendo na furaha pamoja na binti yetu mpendwa Rose Turuka.
Tulikuwa vijana wakati tunaoana na tunazidi kumshukuru Mungu kwani wakati tulio nao ndoa nyingi  hazidumu kwa muda mrefu au kwa miaka mingi.

Katika miaka hii 17 ya ndoa Grace amekuwa kiongozi, mshauri na mama  mtendaji ndani ya familia yetu na nje ya familia yetu amekuwa kimbilio la wale wenye mahitaji ambayo yako ndani ya uwezo wake wa kusaidia kulingana na neema ya Mungu kwa maneno mengine Katika hii miaka 17 Grace amekuwa Mama  wa watoto yatima na wale wanaohitaji msaada bila kujali imani yao au wapi wanatoka;


Ni ukweli ambao haupingiki kuwa ndoa yenye Baraka na inayodumu inahitaji sana matunzo ya hali ya juu na ujasili wa kuifanya iwe bora,(commitment); na ndoa bora hutengenezwa na wana ndoa wenyewe na si vinginevyo,; ndoa bora hujengwa katika mafiga matatu figa la upendo, figa la  msaamaha na figa la mawasiliano bora.


Katika miaka hii 17 tumejifunza kuwa Ndoa bora hujengwa katika msingi wa mawasiliano mazuri miongoni mwa wanandoa wenyewe, bila mawasiliano hakuna ndoa bora. 


katika miaka hii 17 Daima tumekuwa na mawasiliano ya karibu kuhusu nini kifanyike na kinachoendelea katika maisha yetu familia. Mawasiliano baina ya mume na mke yanajumuisha daima mipango iliyokusudiwa au kuimarisha zaidi mitazamo hasi au chanja. Mawasiliano pekee, yatasaidia kubadilisha tabia ambayo sio nzuri ambayo inaweweza kufoofisha uimara wa ndoa;


Katika hii miaka hii 17 tumejifunza kuwa Ndoa bora hujenga katika misingi ya furaha kama vile mazungumzo yanayopelekea vicheko, utani, na vitu vya namana hii ambavyo ni silaha muhimu sana katika kuimarisha ndoa bora;




Katika hii miaka 17 tumejifunza kuwa  ndoa inakuwa na matarajio tofauti ya kulea zaidi familia ambayo imepata kibali mbele ya Mungu. Pamoja na mafanikio yote ambayo yanaweza kuwepo katika ndoa bora  lakini kujitoa bila unafiki wa kila mtu ni jambo la muhimu zaidi na zaidi katika kudumisha ndoa bora.




Katika miaka hii 17 tumejifunza kuwa sisi kama wanadamu ambao tumeunganishwa na Ndoa Takatifu bado tunatakiwa kumshinda  ibilisi dhidi  udhaifu au mapugufu yetu  na yatupasa kujua kuwa sisi ni binadamu ambao sio wakamilifu tuna mapungufu mengi ambayo yataweza tu kwisha kwa upendo, msamaha na neema ya Mungu. “Majani yanakuwa ya kijani kama yanamwagiliwa, na ndoa bora ni ile ambayo inaudumiwa kulingana na bibilia inavyotufundisha”. 


Katika miaka hii 17 tumejifunza kuwa Mtikisiko ndani ya ndoa si mwisho wa ndoa bora ni kama tu dhoruba ambayo inaweza kuepushwa kwa kufahamu kwa nini tatizo lilitokea na kujirekebisha mara baada ya kosa kutokea. Ni ukweli ambao haupingiki kuwa pale ambapo udhaifu  hujitokeza  na wana ndoa wakashinda udhaifu huu  ndoa bora hujengwa katika msingi huo. Tunamshukuru Mungu kwani yeye alijua alichotupangia, kwa ajili yetu, na akatuandalia kalenda bora ambayo bado tunaendelea kutembea juu yake ama kweli  kila alichokichagua Mungu ndicho sahihi.

Tumejifunza kuwa katika miaka hii 17, Kumweka Mungu kwanza katika ndoa, huleta furaha ya kweli (joy) faraja na ulinzi. Kumweka Mungu kwanza maana yake mume na mke wanaishi kwa utii na kufuata amri za Mungu mwanzilishi wa ndoa; tunamshukuru Mungu katika kipindi hiki chote tumekuwa tukiwanaomba Mungu pamoja na kuwa na mahusiano yanayoongozwa na Mungu. Kwa vipimo vya kibinadamu huwezi kuwa na furaha siku zote kwa safari ndefu kama ya ndoa furaha ya kweli hupatikana kwa kumuweka Mungu namba moja.


“Mwanandoa mwenye busara hawezi kumuaibisha mwenzi wake bali ataongea kwa hekima na kumaliza tofauti zozote kwa upendo. Kawaida wana ndoa bora hawaangalii mapungufu zaidi bali wanaangalia uwezo na kurekebisha udhaifu wa mwenzake; Biblia inakumbusha kuwa kwa maombi udhaifu hujitenga ”. "Macho ya Bwana ni juu ya haki, na masikio yake husikiliza sala zao, lakini uso wa Bwana ni juu ya watendao maovu" (1 Petro 3:12).

Mungu anajua maumivu na furaha ya ndoa, naye anaelewa tamaa za mwili, yote yanawezekana kwa utia na kusikilizana. Utii kwa Mungu daima huleta furaha (Warumi 16:19).

Katika miaka hii 17 tumeishi kwa kutekeleza wajibu miongoni mwetu, tumejitoa kutimiza mahitaji, kwa njia ya furaha na kuvumiliana; uvumilivu hujenga msingi bora wa upendo, na kuisaidia Ndoa takatifu kusimama imara, kwani mume na muke wanaahidi kubaki pamoja katika mapendo mpaka kufa;

katika hii miaka 17 tumejifunza kuwa inatupasa sisi kama wanandoa kufanya maamuzi wa ya kila siku kwa kuweka Mungu  mbele  kwa kufanya hivyo na, ndoa yako itakuwa na uwezo wa kukabili aina yeyote ile ya dhoruba ambayo inaweza haribu ndoa hiyo. mgogoro haina maana ndoa imeshindikana. Migogoro ni kama dhoruba  kubwa, inatisha na ni hatari. migogoro ndani ya ndoa inaweza kuwa mwanzo mpya. Tumejifunza kuwa  kutokana na maumivu yanayoweza kutokea ndani ya ndoa, NDOA bora huzaliwa.

Mwenyezi  Mungu, asante sana kwa kutuchagua sisi kuwa wanandoa na kutusaidia kuishi pamoja katika miaka hii 17. Tunajua kwamba ulikuwa na mpango na kusudi kwa ajili ya ndoa yetu, na sisi tunazidi kukuomba uzidi kutujalia neema ya utakaso katika maisha yetu ya kila siku ya ndoa; utujalie neema ya kuendelea kusameheana na kuondoa ubinafsi miongoni mwetu. 


Tunazidi kukuomba uendelee kutupa neema ya kukuweka wewe  kwanza katika kila jambo tufanyalo; tunaomba uzidi kubariki ndoa yetu mingi inayokuja  nasi kama wana ndoa tuzidi kupendana na kudumisha amani na kuendelea kuilea familia yetu kulingana na mafundisho yako kama tulivyoagizwa kupitia Bibilia Takatifu 


Sunday, November 6, 2011

JE UWAJIBIKAJI WA PAMOJA WA KICHAMA HOZOROTESHA UADILIFU?


UWAJIBIKAJI WA PAMOJA WA WANASIASA NA VYAMA VYAO JE UNAPUNGUZA  UWAJIBIKAJI WA MWANASIASA MMOJA MMOJA KATIKA KUTETEA  MASILAHI YA WANANCHI?

Ni kweli kuwa Wanasiasa wengi huwa na uadilifu wa kutosha kupinga matendo maovu ambayo mengine hufanywa na viongozi ndani ya chama chao kama ufisadi na rushwa; lakini wakati mwingine nguvu hizo huishia ukingoni kutokana na shinikizo kubwa la chama chake, pale anapolazimishwa kufuata msimamo wa pamoja wa chama katika kufanya maamuzi; na pale itakapo tokea tu muhusika huyo amefanya maamuzi kinyume na uwajibikaji wa pamoja wa chama ni rahisi sana kutengwa na kuonekana msaliti: 




Kutokana na shinikizo hilo baadhi ya wanansiasa wazuri na waadilifu watetezi wa wanyonge hubaki  wamevaa ngozi ya unafiki. kwa msimamo huu ni kweli ambao haufichiki kuwa  sio kila mwanasiasa ni mla rushwa au fisadi bali baadhi ya wanasiasa huwa na sifa mbaya kwa sababu nguvu ya uwajibikaji wa pamoja wa kichama.


Nafikiri inafurahisha sasa kuona kuwa Wanasiasa wengi wameanza kuhodhi sifa mbalimbali za utaalam “professionalism” tumeanza kuona namana wabunge wenye sifa hizo wanavyoweza kujenga hoja na kuvuta hisia za watu wengi, na hata kuleta changamoto katika shughuli zao za siasa. Jingine ambalo tumejifunza tumeona kuwa “professionalism” husaidia kuzingatia maadili ya utendaji kazi na hulka ya kujiamini na kuwa tayari kukosoa ,kukosolewa  na kufanya maamuzi mazito hata wakiwa katika msimamo wa  pamoja ya kichama hawaburuzwi kihoja.


Pamoja na dhana ya kuwa lengo la kuwa chama cha siasa chochote, lengo la kwanza kabisa ni kushinda uchaguzi. Na kuna tofauti kati ya mwanansiasa mtaalam njisi ambavyo ana fanya kampeni walio wengi maadili ya husadia kupunguza kampeni chafu. Maadili ni muhimu zaidi na katika siasa na kwa maendeleo ya wananchi. Maadili ya kweli yatapunguza wanasiasa kujishughulisha na rushwa.

Katika demokrasia wananchi ndio wenye dhamana na uwezo wa mwisho wa kumrejesha mwanasiasa kuendelea kuhozi madaraka; pamoja na umaarufu wake, uadilifu na utaalam katika kushughulikia maswala ya siasa bila ridhaa ya mwananchi sio rahisi kurejea madarakani;

historia ya vyama vingi na chaguzi za Zambia zinaainisha kuwa ukomavu wa demokrasia ndani ya Zambia wananchi ndio wenye sauti ya mwisho wananchi wa Zambia wanapima na kuamua kulingana na utendaji wa viongozi wao na sio ushabiki wa vyama;
Tatizo la kushabikia sana vyama ndilo linaloponza sana maendeleo ya nchi nyingi za kiafrika; wananchi wanakumbatia zaidi chama na sio utendaji wa viongozi wa vyama vyao;

Kama wananchi tunatakiwa kuanza kuangalia upya maamuzi yetu dhidi ya viongozi wetu; tunahitaji viongozi waadilifu na viongozi wa namna hii  wataweza kuchukua hatua kwa maslahi ya jamii kwa manufaa ya wote, na wanaweza kubaki madarakani kwa muda mrefu iwezekanavyo kulingana na utaratibu wa nchi husika na kukendelea kukubalika kwako kwa masilahi ya wengi; Katika mfumo wa kidemokrasia wa serikali, ambapo nguvu ya utawala ina inapatika upya kila baada ya miaka mitano na wananchi ndio wenye dhamana ya kuwarejesha madarakani.

Nchi ya Zambia imetufundisha kuwa  hakuna kiongozi anayemiliki watu, hakuna chama chenye hatimiliki ya kuwa na kundi la wananchi kama itakuwa hivyo basi kuna tatizo na wananchi katika nchi hiyo; wananchi mara zote wanategemea na wanataka  mabadiliko makubwa ya kiuchumi hawahitaji propaganda za chuki, wanahitaji kufaidi raslimali zao  wazambia walikuwa wanashangaa utajiri wote unaotokana na shaba unakwenda wapi? Pale ambapo hawakuridhika hawakuwa na papara walisubiri tu wakati ulipofika walimweka pembeni kiongozi na kumpa dhamana kiongozi mwingine. Lazima tukubali kuwa katika nchi zilizopo kusini mwa Afrika  Zambia ni moja ya changamoto za mabadiliko ya kisiasa:

Maamuzi ya wananchi katika awamu tofauti Zambia umeendelea kuwashangaza viongozi walioko madarakani kuanzaia enzi  Kaunda, pamoja na ukongwe wake wa kutawala kwa miaka 27 hadi awamu ya Banda; Kiini cha msukumo huu nini? Wananchi wanatamani kupata maisha bora; na kuwa viongozi wenye kiwango cha juu kabisa cha uadilifu kuweza kuwatumikia wananchi na kuleta maendeleo sio kwa nadharia bali vitendo;


Viongozi wetu wa vyama vya siasa wamesahau kuwa, Kimsingi, raia huzaliwa wakiwa huru dhidi ya mikingamo ya kijamii, kwa lugha ya kitaalamu tabula rasa. Lakini mikingamo hii ya kijamii huingizwa katika fikra za wananchi kupitia itikadi na elimu ya siasa katika vyama ambavyo wanafuata; na wakati mwingine hata kupitia shule na sehemu za ibada.

Cha ajabu haitoshi kuivuruga jamii peke yake tumeona na tunaendelea kuon kuwa viongozi wetu wa kisiasa hapa nchini wamekuwa wakigombana kila mara katika mambo ya msingi na yasiyo na msingi. Kugombana si kubaya kama kunaleta tija, lakini kule kugombana kunakofanywa kwa misingi ya kujitafutia umaarufu kunasabaisha viongozi kushindwa kutekeleza majukumu yao ambayo yanatokana na ahadi wakati wakiomba ridhaa ya kuchaguliwa na wananchi, ni dhambi ambayo haiwezi kuvumilika hata kidogo. 

Wakati tunaelekea kusherekea miaka hii 50 ya uhuru wetu  itakuwa busara kama serikali kwa upande mmoja , vyama vya siasa kwa upande mwingine kupunguza matumizi nguvu ya kiuchumi katika maswala yanayohusu zaidi umaarufu wa kisiasa na kupeleka nguvu hizo katika maswala ya kijamii; bado wananchi wetu hali zao bado ziko duni sana (masikini), tunahitaji barabara bora; huduma za afya nzuri, elimu bora kwa vijana wetu; ajira za kutosha kwa wenye sifa za kuajiriwa;


Kama Rais Kenedy wa Marekani alivyowahi kusema ‘Wewe UMELIFANYIA NINI TAIFA LA TANZANIA’ ni wajibu wa msingi kabisa kwa wale wote ambao wamepata ajira ya serikali kutimiza wajibu wao; ni aibu kubwa pale inapogundulika kuwa wafanyakazi wengi wa serikali wanafanya kazi chini ya masaa nane; tusitarajie maisha bora kama sisi kama watumishi wa umma hatutawajibika ipasavyo; tutimize wajibu wetu kwa maisha bora kwa kila mtu,

MUNGU IBARIKI TANZANIA TUNAVYOELEKEA KUSHEREKEA MIAKA 50 YA UHURU

Friday, November 4, 2011

TAFSIRI YAKO IMEKAAJE KATIKA PICHA HII

Je picha hii ya viongozi wetu wa juu wa serikali unaweza ukaitolea maelezo gani? Au wanatafakari nini viongozi wetu huku wakitabasamu?


  • Je wanafurahia miaka Hamsini ya Uhuru na wamefanikiwa kuanzisha mchakato wa Kuandikwa kwa katiba upya?




  • je wanafurahia kufanikiwa kuwawajibisha viongozi wa serikali ambao wamekuwa na tabia ya kutumia madaraka vibaya?




  • je wanapanga mikakati ya namna ya kupunguza ugumu wa maisha kwa watanzania




  • Au lolote na liwe kazi na dawa, ngoja tucheke kidogo tupunguze "stress" za kazi ili tukirudi ofisini tuwe fresh na tutawajibika ipasanya katika kutekeleza kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtu kupitia   kasi,nguvu na ari mpya?



Friday, October 28, 2011

JE UVUMILIVU NI KARAMA AU MAZOEA


UVUMILIVU HUJENGWA NA MISINGI GANI?



Naanza kwa kujiuliza kuwa “tulichonacho sisi wananchi je ni subira?; na baadhi ya viongozi wetu je wanao uvumilivu?  

Kwa haraka haraka tu Uvumilivu ni uwezo wa, au ni mazoezi ya, kutambua na kuheshimu imani au matendo ya wengine; uvumilivu uko katika kila nyanya ya maisha yetu, kuanzia maisha yetu ya kila siku;TATIZO katika maisha ya kawaida sana, swala la uvumilivu halizungumzwi sana, kwani uvumilivu unahusishwa na familia au kikundi kidogo cha watu; katika level hii uvumilivu huzungumzwa sana katika kuimarisha  maisha ya ndoa;


Uvumilivu huongelewa sana kwa mapana hasa katika maswala ya uongozi, uongozi ni hali ya kuongoza nchi katika mwelekeo wa kuleta maendeleo na ni ukweli kama mwandishi mmoja alipowahi sema kuwa “ KUONGOZA watu na hasa wa watu wazima ni kazi nzito inayohitaji mtu anayepewa jukumu hilo kuwa makini, vinginevyo mambo yanaweza kuwa magumu na hatimaye kuangukia katika mtego wa udikteta.  Hii inatokana na kukosekana mambo makubwa matatu ambayo ni ufahamu au maarifa, hekima na  hasa uvumilivu. Kiongozi asiye mvumilivu anaweza kujikuta anatumia mabavu kutawala ili watu wajue kuwa yupo, ana nguvu na ana mamlaka”.


Ni ukweli ulio wazi kuwa  kiongozi anatakiwa kuwa, mtulivu, mvumilivu na anayetumia zaidi hekima kuliko mabavu”, kiongozi anatakiwa Kuwa na  msimamo wa uvumilivu ni moja ya kazi ngumu zaidi miongoni mwa viongozi dhidi ya wananchi katika jamii. Ni ukweli ambao haufichiki kuwa  viongozi hawakuzaliwa wakiwa wavumilivu, lakini lazima tujifunze kuwa wavumilivu. Katika siasa uvumilivu wa kisiasa unakuza  utamaduni wa utawala bora na ukomavu wa demokrasia; na Kwa demokrasia kufanya kazi vizuri, wananchi lazima kuwa tayari kuvumilia na kuvumiliana.



Dhana ya uvumilivu ni ya msingi sana kwa maendeleo kwani inaruhusu mawazo mapya ndani ya jamii; kupitia dhana hii ya uvumilivu, kiongozi anakuwa  tayari kukubali  na kuheshimu  maoni na mawazo ya watu wengine na haki zao kwa uwazi na uhuru. Katika hali hii,uvumilivu huruhusu kuwepo kwa vyombo  huru vya habari kutumika kama chombo muhimu kuwahabarisha wananchi na kuwasilisha madai yao kwa viongozi wao. Demokrasia inahitaji vyombo vya habari amabvyo hugeuka kuwa daraja la mawazo kati ya viongozi na waongozwa. Vyombo huru vya habari husaidia   wananchi kuelewa taratibu ambazo zinaimarisha demokrasia.uvumilivu wa viongozi huru utasaidia kueneza demokrasia  na uwajibikaji kwani wananchi wataweza kukosoa serikali na ujumbe kufikishwa serikalini bila kuogopa.


ni ukweli kuwa Falsafa ya Uvumilivu hufunza na kuwakumbusha viongozi wanatakiwa kuishi kulingana na fikira njema. Mwenye kuifuata falsafa ya uvumilivu hayuko tayari kuamsha fikra mbaya za udikteta bali daima atajitaidi kuziepusha kwa kuendeleza uamuzi  wa uwazi na kwa kutumia njia  ya utulivu wa hekima kupitia uzoefu makini wa kimantiki: Kiongozi mwenye uvumilivu daima hutafakari, na kuziweka fikira mahali pamoja kabla ya kufanya uamauzi.Msingi wa kimaadili wa falsafa ya uvumilivu  kama mtaalam mmoja alivyo wahi kusema kuwa "zuri liko katika hali ya nafsi, yenyewe, inaonyeshwa katika hekima na kujidhibiti, hivyo kuboresha ustawi wa kiroho: Fadhila inatokana na nia ambayo inawiana na Maumbile. Kanuni inatumika katika uhusiano wa kibinafsi, yaani: kuwa huru kutokana na hasira, na wivu"

kwa ufupi tunaweza kusema kuwa uvumilivu umesheheni nini?
·        Tendo lililojaa subira kubwa,
·        Tendo ambalo kama linafanywa na kiongozi wa nchi basi anatoa uhuru mkubwa kufanya mambo bila kuingiliwa na nguvu za Ikulu,
·        Tendo lililojaa utu,
·        Tendo kwa serikali kuwa tayari kukosolewa na watu binafsi au vyombo vya habari.
·        Tendo ambalo linaashiria uwajibikaji wa serikali na utumishi wenye tija katika kwa taifa na wananchi wake katika kukuza demokrasia

Ni ukweli ambao haufichiki kuwa viongozi wetu wakiwa wavumulivu katika uwajibikaji wao mara moja  hurudisha imani ya wananchi dhidi ya serikali yake, upendo na matumaini katik ya viongozi na wananchi huongezeka pia: Tukumbukwe kuwa Ingawa watu wengi kufikiria uvumilivu ni upole  na kuto wajibika la hasha uvumilivu ni uwajibikaji ulio jaa busara na subira;


Swali lakujiuliza tunavyoelekea kusherekea miaka 50 ya uhuru wa Taifa letu je viongozi wetu katika awamu zote katika serikali yetu ya Muungano waliutumiaje uvumilivu katika kutekeleza majukumu yao?

Je uvumilivu wa kipindi cha mapambano ya uhuru wa taifa letu Bara  na visiwani katika miaka hiyo ni sawa na uvumilivu wa leo?

Je uvumilivu baiana ya vyama vya kisiasa ukoje? Ni kweli kuwa wanavumiliana katika kuchangia hoja katika mambo mbali mbali yanayohusu maendeleo ya Taifa letu?


Je hali ya viongozi wetu na vyama vyao wakati wa chaguzi mbalimbali uvumilivu hutawala kampeni zao?

Kuna maswali mengi sana ya kujiuliza hasa katika kipindi hiki cha kuelekea miaka 50 ya uhuru wa taifa letu na nini kifanyike baadaya ya sherehe hizo kwa manufaa ya taifa letu la Tanzania

MUNGU IBARIKI TANZANIA KUELEKEA MIAKA 50 YA UHURU

Sunday, October 23, 2011

HONGERA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUTUNUKIWA SHAHADA ZA HESHIMA


“HONORIS CAUSA”



Kama ilivyoelezwa na wataalum wa vyuo vikuu ambavyo ndio watoaji wa Shahada ya Heshima “ Honoris Causa” kuwa;

shahada ya heshima ni ile itolewayo kwa mtu mwenye vigezo stahiki na aliyetoa mchango mkubwa wa maarifa, elimu au ujuzi katika eneo fulani la kitaaluma.

Kwa kawaida shahada hizi hutolewa kama njia ya kuheshimu na kutambua michango ya watu hao katika maarifa, ujuzi au eneo la kitaaluma kwa mfano, afya, uchumi, mazingira, sayansi au fasihi,
mtunukiwa wa shahada hiyo hapasi kuwa na uhusiano wa awali na taasisi inayompa heshima hiyo.

Mtu anayependekezwa kupewa shahada katika chuo chetu ni yule aliyetoa mchango mkubwa kwa umma au kwa taifa na sio lazima mchango katika taaluma bali ni kazi ya ziada yenye manufaa kwa umma nje ya wajibu wake wa kazi.

Mheshimiwa Dr. Jakaya Mrisho Kikwete toka alipochagualiwa kuwa rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania amekuwa kiongozi ambaye amepata shahada zaidi ya moja nje ya nchi na ndani ya nchi;

Kwa maneno mengine ni kuwa Dr. Kikwete amekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya jamii katika mfumo wa moja kwa moja (direct) na kwa kupitia viongozi wengine ( in direct) katika kuonyesha njia na kutekeleza majukumu amabayo amekabidhiwa kwa kulingana na katiba yetu;

Shahada hizi zote ambazo amepata zinahusiana na utendaji wa kazi ambao unampa sifa yeye kufikia kilele hiki na utekelezaji wa majukumu.  Kwa wale wote ambao wanakaa darasani na kufanaya utafiti na hatimaye kufanikiwa kutunikiwa shahada mbalimbali lengo kubwa na la msingi wake ni kuwawezesha  kuelewa na mambo mbali mbali kupita uchambuzi wa vitabu na utafiti na kutumia elimu hiyo katika kutatua matatizo ya jamii inayowazunguka;

Lakini kwa upande mwingine viongozi mbali mbali ambao hawana shahada ya juu wanaweza kwa namna moja au nyingine wakawa ni wasomi wakubwa sana ambao wanaweza kutatua matatizo ya jamii kuliko hata kama wengekuwa wamesomea kozi husika. Tuchukue utambuzi ambao Kenya waliona na kuamua kumtunukia Mheshimiwa Kikwete shahada ya heshima kupitia  chuo kikuu cha kenyatta,” kwa ujasiri wake wa kusuluhisha ugonvi wa kibaki na oginga 2008; suluhu hii ya ugomvi ilikuwa na maana kubwa sana katika nchi ya Kenya baada ya vifo vya wenyewe kwa wenyewe;

Je unafikiri kuwa “baadhi ya maelezo” ya hapo chini  yana mpa sifa  
Dr. Kikwete kutunukiwa shahada hizo zote za heshima?

Dr. Kikwete kama kiongozi wa chama na serikali ametumia muda wake mwingi kukemea Ufisadi unaofanywa ndani ya chama twawala na , serikali yake

Dr. Kikwete amekuwa mbele katika  kuimarisha utawala bora miongoni mwa  jamii;

Dr.Kikwete ariruhusu kuundwa kwa  tume huru ya kuchunguza mikataba mibovu katka sekta mbalimbali  zenye kulalamikiwa na wananchi

Kuhusu demokrasia, Kikwete amepiga hatua kwa kuruhusu kwa wazi mijadala mbalimbali. Vyombo vya habari na wananchi wamekuwa huru kuibua hoja mbalimbali zikiwamo hata zile zinazodhalilisha serikali pamoja na  kuagizi kuandikwa upya kwa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania iweze kuendana na miaka hamsini ya uhuru

Rais Kikwete ameendelea kuwa msikivu na kupokea hoja zilizotolewa na makundi mbalimbali ya Watanzania na kuzitafutia majibu kulingana na mipaka yake na bila kuingilia chombo kingine cha maamuzi.

Dr. Kikwete ameweza kuiagiza chombo kinachuhusika kutenda haki kwa watuhumiwa wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA)  na wale wote waliotumia madaraka yao vibaya; uamuzi huu wa busara unatoa  matumaini kwamba rais kweli amedhamiria kupambana na ufisadi ambao unatishia uhai wa uchumi wa nchi yetu,

Kikwete kwa kiasi kikubwa kaonyesha kutoingilia Bunge wala Mahakama katika utendaji, ndiyo maana baadhi ya mambo yamefanikiwa.

Dr. Kikwete amesaidia kuleta suluhu Kenya na Zimbabwe na kuuweka uongozi wa umma Comoro, baada ya kutuma vikosi vyetu huko.

Amesimamia muafaka kati ya CCM na CUF  mpaka serikali ya umoja wa kitaifa imepatika na inafanya kazi kwa kushirikiana vizuri sana.

Lakini ikumbukwe kuwa hata wasomi ambao wanakaa darasani katiki kusomea shahada kama aliyopewa mheshimiwa Kikwete wanakabilia na “ challenges”; na kwa msingi huu Si rahisi kwa binadamu akawa na mazuri matupu; hakuna aliye mkamilifu kwani sisi si malaika na Mheshimiwa Kikwete kadhalika,kama binadamu anayomapungufu yake;

Rais Kikwete kwa mazuri aliyofanya anastahili heshima hiyo kwa  pamoja na mapungufu yake na kama kiongozi bado ana muda wa kurekebisha kasoro zilizojitokeza katika uongozi wake kwa kuendelea kuwabana watendaji wake walio chini yake; lakini tusisahau kuwa nasi tunamchango wa kufanikisha maendeleo yetu tukishirikiana na Mheshimiwa Rais wetu.

HONGERA SANA MHESHIMIWA DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA KUTUNIKIWA SHAHADA ZA JUU ZA  HESHIMA  NJE NA NDANI YA NCHI

Karibu tujadili kwa maendeleo ya Taifa letu

Friday, October 21, 2011

LEADERSHIP ACCOUNTABILITY VS 50 YEARS OF INDEPENDENCE


WHEN I GET THE BUS FARE

A SONG BY MRISHO MPOTO  
    

ANALYSIS BY       ROSE EMMANUEL TURUKA
KALAMAZOO CHRISTIAN HIGH SCHOOL     OCTOBER     2011

This song is about a man in the village who desperately wants to visit his uncle in the city. He wants to remind his uncle what he is left behind, but he doesn’t have the bus fare.

The author Mrisho Mpoto shows rather irony and metaphor in singing this song. He starts off with “if I receive a bus fare I will come and visit you uncle” he continues by saying “it is better to build a bridge than a wall” literally we would say that Mwisho is longing to see his uncle, he has sort to put that into his first priority that he doesn’t have money to visit him but if he had he would;  instead Mwisho is still converting the message through  song to the President to whom he calls “uncle” advising him on the ways to control the government , because the government is not doing enough to help the people of  are indeed

Mwisho says “it is better to build a bridge than a wall” he is trying to make him understand that a wall separates individuals, the wall he builds between the people and himself call for no communication rather separation. It is an obstacle that blinds you from the reality from another side of the wall and fills you with the fantasy to believe that the other side which you don’t see there is no problems. So he says” it is better to build a bridge “for then people will be able to go from one point to another and will be able to communicate for you will be able to see sides, the reality and fantasy. He then goes on in saying “spring water is not forceful. If you want to drink it's  water you must bend down to it”. Here Mwisho is establishing the point that in order to get the water to drink you must follow the rules and everything that comes with it. You have to get close to the spring water. I believe Mwisho is trying to send the message that, for the President to lead this country effectively, he must not sit in his office waiting for the details to come to him, he should go out and search for the details himself, and not to wait until campaign time. It is true that when President is interacting with people in day to day activities President can see what people are needed truly; Mrisho caution leaders not to wait and appeal to citizens it, what can be changed and how it can be improved changes during voting time.

Mwisho uses the line” you just want the world to be like a village; congratulations”. As the irony of how poor the work of leaders have become the emphasis they give, doing the campaigns is not the work they produce after being in the office. Mwisho says” congratulations” as the irony that it is a poor job, thinking about globalization while village people are suffering for poverty and nothing has improved and the country is falling. Why you just want the world to be like a village, why you want  to focus on external policy while the country is poor, no improvement, no direction, no good leaders, because that is what is happening. There is no good leader to take care of the nation that we are deteriorating slowly.

In the second verse Mwisho asks” uncle do you know your team? Do you know who is loyal and who is not? Character is like skin of the body difficulty to change, remember that the child of snake is not being taught how to bite if you laugh with the monkey you will get the flu”. Mwisho is raising the awareness to the President on the people he takes advice from and operates with. He says the child of a snake is not taught to bite, the leaders who are corrupt not necessary will teach their children how to, they will grow up with it; perhaps they have grow up with it too. So if he stays and do nothing about and laugh with them instead, he will also be contaminated by their disease of corruption practices. And so it is better to take precautions before your get sick.

In this song Mwisho Mpoto establishes the ideas that president should take his responsibilities and matters and look at the issue closely, work so close with people in order to improve the country and people’s conditions. This song is so powerful, Mwisho sees social oppression and is trying to awaken citizen’s mind through the massage to his “Uncle”. I believe that many social movements and social transformation processes have always use music as a tool for social change.

ROSE EMMANUEL TURUKA