WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Wednesday, January 2, 2013

PUMZIKA KWA AMANI SAJUKI,MAPENZI YA MUNGU YAMETIMIA!!!



 Alipangalo mola mwanadamu hawezi kulipangua Sajuki amekwenda.....
amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili.
Alilazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena December 2012. 

 Baada ya kurudi nchini hali yake ilikuwa nzuri tu na mwili ukaanza kurejea kama anavyoonekana kwenye picha hapo akiwa na Wastara mkewe.Pamoja na kuwa katika hali hii bado alikuwa ni mgojwa.
Mwezi wa kumi na moja 2012 Sajuki alifanya tour aliyoiita asante Tanzania kwa lengo la kuwashukuru watanzania walipomchangia.Lakini kilichokuwa nyuma ya pazia ni kwamba alikuwa akikusanya pesa ili arudi India kwa matibabu.Akiwa mkoani Arusha
katika  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini  hivi karibuni alianguka.Na yeye mwenyewe kukiri kwa kusema
“Sijisikii vizuri, hali yangu ni mbaya.”
Baadae mwenyewe alisema kuwa pamoja na kuumwa,haikuwa rahisi kurudi katika vyombo vya habari tena kwa ajili ya kuomba Watanzania kumchangia kwa ajili ya fedha za matibabu kwa awamu nyingine. na muda wa kurudi ulikuwa umefika.
 Kwa takribani wiki mbili Sajuki alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.Na ilifikia hatua ya mheshimiwa raisi Jakaya Mrisho Kikwete kuamua kumsaidia kumpeleka India kwa matibabu.
Pamoja na msaada lakini bado kulikuwa na changamoto kwamba tatizo kubwa lililomzuia Sajuki kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye huduma ya gesi.
Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo kumsafirisha mpaka India.
Sajuki alikua na tatizo kubwa la kupumua wakati huu ambapo   upumuaji wake ulikua unabadilika mara kwa mara.

 
Pole sana Wastara ulijitahidi kadri ya uwezo wako kuhakikisha mumeo anapona.Ila yule aliyetuumba ndio ameamua na akipanga lake hakuwa wa kulipangua.Pole kwa familia,mashabiki na watanzania kwa ujumla.
Msiba upo nyumbani kwao Tabata bima na mazishi kufanyika keshokutwa katika makaburi ya kisutu.
Kwa mujibu wa baba yake mzazi,marehemu alizaliwa mwaka 1986 na amefariki akiwa na umri wa miaka 27.

Mungu ailaze roho ya marehemu Juma Kilowoko mahali pema peponi,Amina.   

MAZISHI YA SAJUKI KUAMULIWA NA WAZAZI WAKE!


Hivi karibu mwigizaji Sajuki alianguka jukwaani alipokuwa kwenye tamasha la wasanii wa filamu na wale wa muziki wa kizazi kipya lililofanyika Arusha

Simon Mwakifwamba (kushoto) na wadau wengine wakimsaidia Sajuki (katikati) kutoka jukwaani baada ya kudondoka katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha mwishoni mwa mwaka jana.


INNA LILLAH WAINNA ILAIH RAAJIUN, hivi ndivyo waislam wanavyopaswa kusema unapotokea msiba. Juma Kilowoko “Sajuki”, hatunae tena, amefariki leo afajiri saa 12.
Sajuki amefariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alipokuwa amelazwa kwa zaidi ya wiki moja.
Imekuwa ngumu sana kuamini kuwa Sajuki amefariki kutokana na ukweli kuwa mara kadhaa msanii huyo amezushiwa kifo, lakini hatimaye sasa Mungu amempenda zaidi Sajuki.

Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Mohameid Said aliyekuwa analala na marehemu hospitalini hapo, hali ya Sajuki ilibadilika ghafla na kufariki alfajiri ya leo.

Mohamed ameimbia Saluti5 kuwa msiba utakuwa Tabata Bima nyumbani kwa marehemu, lakini akaongeza kuwa bado ni mapema mno kueleza Sajuki atazikwa lini na wapi.

“Kwa bahati nzuri Baba na Mama wapo hapa Dar, watatoa uamuzi baadae kama marehemu atazikwa Dar au Songea” alisema Mohamed katika maongezi yake na Saluti5.

Songea ni nyumbani kwa kina Sajuki na ndipo wanapoishi wazazi wake.
Kwa hisani ya twangapepeta.

source vijimambo blog

DHAIRA ATUA LEO SIMBA SC, KASEJA AJIENGUA KOMBE LA MAPINDUZI



Abbel Dhaira

Na Mahmoud Zubeiry
KIPA namba moja wa Uganda, Abbel Dhaira anatarajiwa kuwasili leo saa 8:00 mchana kujiunga na klabu yake mpya, Simba SC ya Dar es Salaam, akitokea kwao Uganda.
Dhaira aliyesaini mkataba wa miaka miwili wenye thamani ya dola za Kimarekani 40,000, na mshahara wa Sh. Mlioni 2 kwa mwezi, baada ya kutua Dar es Salaam atakwenda moja kwa moja Zanzibar, ambako Simba itashiriki Kombe la Mapinduzi.
Kikosi kizima cha Simba, kasoro Nahodha Juma Kaseja, Emmanuel Okwi, Amir Maftah na Amri Kiemba kitaondoka leo mchana kwenda Zanzibar, tayari kwa michuano ya Mapinduzi.
Dhaira aliyeibukia Express ya Uganda mwaka 2006, mwaka 2008 alihamia U.R.A. pia ya Uganda, ambayo aliichezea hadi mwaka 2010 alipohamia Ulaya.
Kwa kumpata Dhaira, Simba SC imepata kipa wa uhakika wa kusaidiana na kipa wake wa kwanza, Juma Kaseja ambaye amekuwa akisoteshwa peke yake bila kupumzika. Na hiyo inafuatia makipa wengine, Wilbert Mweta na Hamadi Waziri kushindwa kuonyesha uwezo wa kumsaidia Kaseja.
Katika mechi za mwishoni za mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara, Kaseja alionekana kuchoka na kudaka chini ya kiwango chake, jambo ambalo lilisababisha mashabiki wenye ‘akili mbovu’ wamfanyie fujo baada ya kufungwa mabao mawili katika mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, Simba ikilala 2-0.
Kwa sababu hiyo, Kaseja alikasirika na kujiengua kwenye kikosi cha timu hiyo akisema hataki tena kuchezea Simba.
Lakini pamoja na matatizo hayo, Kaseja ameendelea kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ambako ameendelea kufanya vizuri na kuonyesha yeye ni Tanzania One wa ukweli.

source vijimambo blog

STAA wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo


MSANII SAJUKI 

Juma Kilowoko ‘Sajuki’ enzi za uhai wake.
STAA wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ amefariki dunia leo alfajiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa anapatiwa matibabu. Kwa mujibu wa Katibu wa chama cha waongoza Filamu Wilaya ya Ilala, Rajabu Amiri ni kwamba hivi karibuni Sajuki alikuwa anasumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.…
source globalpublisher.info.
kwa taarifa zaidi tutaendelea kuwapasha kadiri tukakavyokuwa tukipokea taarifa zaidi

YANGA WAKIJIFUA UTURUKI


I

Kocha wa Magolikipa Razaki Siwa akiwawapa maelekezo magolikipa Said Mohamed, Yusuph Abdul na Ally Mustafa 'Barthez'
Wachezaji wa Young Africans wakifanya mazoezi leo katika Uwanja wa Fame Residence Football - Antalya Uturuki
Young Africans Sports Club imeanza mazoezi jana asubuhi katika viwanja vya Fame Footballl vilivyopo pemebni kidogo mwa hoteli ya Fame Residence Lara & Spa iliyopo kusini mwa mji wa Antalya ambapo imeweka kambi ya mafunzo ya wiki mbili.
Kocha Brandts akisaidiwa na kocha msaidizi Fred Felix Minziro na kocha wa makipa Razaki Siwa waliongoza mazoezi hayo yaliyoanza majira ya saa 4 kamili asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki na awamu ya pili ilianza majira ya saa 10 kamili jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
Ratiba ya mazoezi ni mara mbili kwa siku asubuhi na jioni, ambapo timu inapata huduma zote za kambi katika Hoteli ya Fame Residence Lara & Spa kuanzia chakula, malazi, mazoezi ya viungo (Gym) ufukwe kwa ajili ya mazoezi ya stamina na kujenga mwili.
Mji wa Antalya ni maarufu katiak medani ya soka kwani kwa ripoti tuliyopewa timu zaidi ya 200 zimeshafika katika mji huu kipindi cha majira ya baridi kuja kuweka kambi zikitokea katika nchi tofauti duniani.
Wenyeji wa Young Africans Team Travel wameada sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ambapo wachezaji na viongozi pamoja wenyeji wa mji huu watasherehekea pamoja. 
Wachezaji wa Young Africans wakiwa nje ya hotel ya Fame Residence tayari kwa kuelekea kuanza mazoezi
Habari kwa hisani ya Bin Zubery Blog

SIMBA YAPATA KOCHA MPYA


Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange Kaburu akisaini kwa niaba ya klabu mkataba wa kocha mpya wa klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig
Katibu wa Simba, Mtawala akiwaongoza Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange Kaburu na kocha mpya wa klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig kusaini. Nyuma ni Meneja Moshi. 
Makamu Mwenyekiti wa Simba SC, Geoffrey Nyange Kaburu akibadilishana mikataba na kocha mpya wa klabu hiyo, Mfaransa Patrick Liewig baada ya kusaini mkataba wa miezi 18 leo katika hoteli ya Spice, Lumumba, Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu wa Simba, Evodius Mtawala na nyuma ni Meneja wa hoteli ya Spice, Mzee Moshi Omar Mbury. 
Mwanasheria wa Simba, Allan Maduhu (kulia) akigonga muhuri mkataba huo
Picha kwa hisani ya Bin Zubery Blog

Tuesday, January 1, 2013

IKULU:ONA JINSI RAIS JAKAYA KIKWETE ALIVYOUKARIBISHA MWAKA MPYA 2013 KIJIJINI KWAKE MSOGA NA WANAKIJIJI USIKU WA KUAMKIA LEO




Wanakiji wa Msoga wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani wakiangalia fashifashi wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya kijijini hapo. 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakichangayika na wanakijiji wenzao wa kijijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni
 ms3:Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha kaka yake Mzee Selemani Kikwete kwa  wanakijiji wenzake  wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani, wakati wa sherehe za  kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za utamaduni
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakipeana mkono wa heri na wanakijiji wenzao wa kijiji cha Msoga, wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, wakati wa kuukaribisha mwaka mpya kwa fashifashi na ngoma za kienyeji.Picha na IKULU