Leo tunatimiza mwaka mmoja toka mama yetu mpendwa mama Anna kinunda aka Mbuya atangulie mbele ya haki; furaha yetu kubwa ilikuwa jinsi ambavyo aliweza kuipiga vita yake kwa ushindi mkubwa; na kufanikiwa kushinda Tuzo na huku kuendelee kuilinda imani yake mpaka mwisho wa safari yake kama vile Mtume Paulo alivyoandika katika waraka 2 Timotheo 4: 5-8.
Mwaka mmoja unatukumbusha jinsi yeye alivyoyaweka maisha yake katika mwongozo wa Mungu akijua kuwa mapambano ambayo alikuwa akipitia na kuyafanya yalikuwa ni juu yake na Muumba wake na hakuna mtu mwingine yeyote ambaye angeweza kumzuia na kumshawishi tofauti ndio maana aliamini kuwa imani ameilinda: Silaha yake katika ushindi wake ilikuwa ni kutimiza amri kuu ya upendo, ambayo ukiitimiza vizuri utaishi maisha ya uaminifu; hivyo hakukuwa tayari kumpa shetani nafasi kwani aliishi maisha yake ili kumtumikia Mungu na sio maisha ya kujilinganisha na mtu au watu wengine: aliishi vile Mungu alitaka sisi tuishi:
Daima alikuwa akimpendeza Mungu zaidi; na sio kuwafurahisha watu wengine katika mambo ambayo sio ya kimungu; aliishi maisha ya kuwasaida sana wahitaji wale ambao walikuwa wakihitaji msaada; alikuwa tayari kujinyima yeye kwa faida ya taifa la Mungu hasa watoto na wazee ambalo lilikuwa likihitaji msaada;
Mbuya Anna aliishi maisha ya kutimiza wajibu wake kama mkristo kwa kumpigania Kristo: alitukumbusha wakati wote tusikae chinina kusoneneka na kujilaumu kwa makosa ya jana wajibu wetu daima ni kuomba msamaha na msaada wa Mungu; amakweli Mbuya yeye alichagua fungu lililo sahihi kama Mary katika Luka 10:41-42 : je wewe na mimi ni akina Martha tunahangaika sana na mambo ya kupita na ya Muda mfupi ya dunia hii?
Tukumbuke kuwa utawala wa Mungu kamwe hautapotea au kufa kwani juu ya mwamba atalijenaga kanisa lake na hakuna nguvu ya kuzimu ambayo inaweza kulishinda Mathayo 16:18;Mbuya alijua kuwa neema ya Mungu na thamani ya Mungu ilikuwa kuwa zaidi katika maisha yakendio maana aliipigania kwa nguvu zote; je wewe na mimi tunamsimamo gani? Ni wakati wetu sasa wa kusimama imara kumwambia shetani sasa ondoka mbele yangu; umepoteza furaha; upendo wangu; amani yangu na nuru ya uzima wa milele sasa nimesimama na kumwomba anisamehe kwani mimi narudi katika njia iliyo sahihi aipendezayo Mungu; tumwombe Mungu Msamaha kama Daudi alivyofanya katika zaburi ya 51
Tuwe kama Mwana mpotevu aliyetambua makosa yake na kuamua krudi kwa baba na kuomba msamaha wa makosa yake:Mwenyezi Mungu anafurahi pale tunaporudi kwake na kuomba msamaha ili tuweze kushiriki karamu nzuri ya mwana kondoo aliyechinywa kwa ajili yetu;
Raha ya milele mpe bwana na Mwanga wa Milele uendelee kuyangaza maisha yake katika nuru ya Kimungu kwani ameipigana vita vilivyo: Tuzo amepata; na Imani aliilinda na sasa amevikwa Taji lile ambalo alikuwa ameandaliwa pamoja na wale wote ambao wametimiza wajibu wao wa kuishi maisha yaliyompendeza Mungu
AMINA AMINA