Serikali ya awamu ya tano kwa mara ya kwanza imeamua kuwatumia sana
wataalamu ambao wana sifa za kielimu katika utendaji wa wake katika idara
nyingi serikalini; mwelekeo ambao umekuwa wazi inajitahidi sana kuondoka na
kasumba ya kuwapa watu vyeo kwa huluka ya kisiasa kwa kulindana na kurudisha
fadhila. Ilikuwa jambo la kawaida hata wasomi wetu kwa sababu ya hulka ya
kisiasa hata pale walipokuwa wakipata nafasi za uongozi walikuwa wanazisahau
kabisa taalumu zao na kufanya kazi kwa mazoea ya siasa.
kuwa mwana siasa kwa
ujumla wake sio taaluma, ni haki ya kila
mtanzania (msomi au sio) lakini lazima tofauti moja iwe bayana kuwa msomi
anapongia katika siasa anaangaliwa katika jicho tofauti kwa mategemeo na
matarajio kuwa anatafanya kazi kwa weledi mkubwa na kuongeza tija kwa taifa;
Kitu ambacho kwa kipindi kirefu kilikuwa sio kweli. Ilikuwa ni aibu na hasara
ambayo Tanzania imekuwa ikipata kwa wasomi wake kujiingiza katika siasa ambazo
mchango wake kwa maendeleo ya taifa ulikuwa ni mdogo kuliko angejikita katika
kufanya utafiti unaohusiana na fani yake.
Kwa wasomi wetu kuingia
katika siasa ilikuwa ni mwanzo wa kuzika taaluma zao; hata pale ambapo
walitakiwa kutoa ushauri ambao ungekuwa na manufaa makunwa kwa taifa, hata kama
ushauri huo ungekuwa mchungu kwa serikali mara nyingi walikuwa wakitoa ushauri
wenye masilahi kwa mtu au chama. Hivyo kuwa hasara kwa Taifa. Kwa wakati huo
ilikuwa vyema kwa Siasa kuwaachie
wanasiasa.
Mara nyingi tumechambua
kuwa siasa ni mchezo mchafu; lakini ukweli ni kuwa siasa kama mfumo hauna
tatizo lolote, wenye tatizo ni wachezaji wanasiasa ambao moja ya sifa yo kubwa
ni uwezo wa kuongea na kubadilisha maneno ili sio kuwasaidia wananchi ili
kujinufaisha kupitia chama Fulani na uundwaji wa serikali yao; hivyo hata
wasomi wetu kama raia wa Tanzania hakuna tatizo kama hao wasomi wanajiingiza
kwenye siasa. Shida ni pale wanapokuwa wanasiasa waongo na wasioaminika.
Inatakiwa tufike mahali
kama ilivyo kwenye nchi za mataifa yaliyoendelea kuwa utagundua wanasiasa ni
wanasiasa na wataalamu huwa hawajichanganyi kwani muda wote wako wakiumiza
vichwa kufikiria jinsi ya kugundua kitu fulani. Linapokuja tatizo katika jamii
huwa wana wanajitahidi kutimiza wajibu wao kwa kutumia utaalamu wao katika
kuleta suluhu ya tatizo.
Tunamshukuru Dr. Magufuli
kwa kuanza kutaka kupata matokeo chanya kutoka kwa wasomi wetu katika awamu hii
wamepewa mafasi kubwa ili weweze sasa kufanya kazi kwa utaalamu na sifa ambazo
wanazo kwa faida ya Taifa na kuwaondolea wananchi wa kawaida ugumu wa maisha
ambo uko mbele yao; ni kweli ilikuwa jambo la aibu sana kuona hadi hii leo Serikali
imeshindwa kutumia wasomi wake na rasilimali zilizopo kuleta ufanisi katika
kuleta maendeleo kwa wananchi wake matokeo yake ni usanii wa kisiasa ndio
uliowekwa mbele. Lakini kubwa zaidi ni kuona hata pale inapopatikana fursa ya
ukombozi kujikwamua katika ujinga na umaskini wa kujitakia,hutokea Wasomi wetu
kutusambaratisha wenyewe kwa wenyewe.
Wasomi wetu awamu hii ni
kipindi chenu cha kuumiza na kushauri na kubuni mipango ya kuwafanya Watanzania
katika kuleta mageuzi makubwa ya uchumi na maisha ya watu wake; Dr. Magufuli anategemea sana ushauri na misimamo madhubuti ya
wasomi ili kuisadia serikali katika kujenga Tanzania Mpya. Katika siku za nyuma
ilikuwa sahihi kusema kuwa wananchi wa
nchi hii walikuwa na shahada ambazo
zilikuwa hazitumiki zilikuwa zimefungiwa kwani nafasi zao zilichukuliwa na
wanasiasa ambao walikuwa hawana sifa za utendaji kwa Taalumu bali kwa siasa; Tumeona
mifano ya Maprofesa wengi wasio na idadi, wengi amboa walikuwa wamekijikita
kwenye siasa hivyo taaluma yao ilikuwa haina nafasi ili walazimu kucheza ngoma
ya siasa na sio ngoma ya utaalamu wao katika kutoa ushauri au kutekeleza adhima
ambayo ilikuwa mbele yao.
Katika mazingira yetu,
tunapozungumzia Siasa, watendaji wote walilazimika kuwa chini ya mwamvuli
wa maagizo ya chama na serikali yake na si vinginevyo hivyo walitakiwa kukizi
zaidi zaidi matakwa na mahitaji ya watawala kuliko matakwa na mahitaji ya
jamii. Ni jambo la kawaida kwa vyama vya siasa kutumia muda mchache sana
kujishughulisha na matatizo/changamoto zinazokabili jamii na badala yake
kujikita katika masuala yanayohusiana na uongozi na kutwaa madaraka. Lakini
Mheshimiwa Dr. Magufuli anataka wasomi wetu ndio sana wawe chachu ya utawala
Bora; wawe ni chimbuko la ufanisi na utatuzi wa Migogoro; wawe ndio daraja bora
la maendeleo kwa taifa kwa kutumia uwezo wao wa kuchanganua, kutambua, na kuelewa jambo. Na na
ndio maana wasomi katika jamii yoyote
ile wana uwezo mkubwa wa kuona masuala mbali mbali zaidi ya mwanasiasa wa
kawaida kwa maslahi mapana ya kitaifa.
Tofauti na miaka ya nyuma, Tanzania ya leo imejaliwa kuwa na wasomi wengi sana waliotokana na vyuo vyetu vikuu. Vyuo vikuu ni taasisi zenye umuhimu wa kipekee wa kupangilia na kuendeleza kitu amhacho jamii inaweza kuakisi. Lakini kwa vile wasomi wana nafasi na uwezo wa kushughulika na masuala mbalimbali ya kijamii hawa ndio wenye jukumu kubwa la kuisaidia jamii yetu iondokane na umaskini ambao kwa mshangao mkubwa na bila aibu

kama kioo cha jamii – kwa
maana ya kwamba inaipa jamii taswira yake. Wasomi wa nyanja mbali mbali wana
uwezo na wajibu wa kutuelezea watanzania tunaonekana vipi kama jamii. Wasomi
wana uwezo na wajibu pia kutupa tahadhari juu ya hatari iliyopo mbele yetu; na
vile vile kutusaidia kutupatia maana ya vitu ambavyo wanasiasa wetu aidha wanavipotosha,
hawavielewi au wanafanyia mzaa kwa faida zao binafsi. Na kwa mara nyingine nina
imani kuwa katika awamu hii ile dhana iliyojengeka na jamii yetu ya kuamini wanasiasa na
kuliko wasomi ina weza sasa ikapata tafsiri tofauti.
Lakini ni wajibu wa wasomi
wetu kuidhihirishia jamii kuwa wao ndio watatuzi wa kero zetu na sio wansiasa
ambao walio wengi hawana taaluma inayotakiwa katika kupambana na kero tofauti
tofauti.
Tukumbuke wakati wa Mwalimu alivyoweza kuwatumia wasomi wetu kwani miaka ya 1960s – 1970s, kila wakati taifa lilipokuwa linakabiliwa na changamoto mbalimbali, Mwalimu alikuwa na utamaduni wa kwenda Chuo Kikuu (Mlimani) kukutana na kujadiliana na wanafunzi. Ndio maana tofauti na leo, ilikuwa ni mara chache sana kwa serikali ya Mwalimu kukwaruzana na wasomi. Ni muhimu kwa wasomi kuendeleza juhudi za aina hii.Lengo kubwa Raisi Dr. Magufuli ni kujenge upya dhana ya utendaji kazi yenye nidhamu, uwajibikaji na weledi kwa Taifa na kuondoa utendaji kazi wa mazoea. Sasa ni wakti umefika kwa wasomi wetu ambao mmepewa dhamana ya kuongoza vitengo mbali mbali kulingana na taaluma zetu kufanya kazi katika msingi huo wa utendaji ambao utakuwa na tija kwa taifa letuna faida ya wananchi wetu na mageuzi ya kweli ya uchumi wa Taifa letu;

Mungu Ibariki Tanzania:
Mungu Mbariki Raisi wetu na dhamira yake nzuri ambayo ameanza kuionyesha kwa
Taifa.
Amina