Demokrasia imefafanuliwa katika namna mbalimbali; wengi wa
wanazuoni wameeleza kuwa “Demokrasia ni mfumo wa utawala ambao watu
huwachagua viongozi wa serikali yao wenyewe na kuainisha jinsi
inavyopaswa kufanya kazi”. Wakaendelea kukufafanua kuwa “ Demokrasia hukuza
ustawi wa watu wote kwani Kila raia ana haki ya kushiriki katika uendeshaji wa
shughuli za umma na katika mambo yote yanayoathiri maisha yake”.wengi wa
wanazuoni wanakubalia kuwa Demokrasia inauwezo mkubwa wa kushugulikia
uwajibishaji serikali kupitia kura za maoni na maamuzi yanayofanywa
na wawakilishi wao katika vyombo mbalimbali vya maamuzi”.
Kwa maneno mengine Demokrasia ni mkataba wa kijamii kati ya
wananchi na watawala(serikali); mkataba huu ni wa pande mbili raia wana wajibu
wa kutekeleza sehemu yao na serikali pia inawajibu wa kuwatendea raia matakwa
yao. Kwa maneno mengine ni mkataba wa kijamii unadhihirisha uaminifu na
matumaini ambayo raia wanakuwa nayo kwa wawakilishi wao ili watende kwa
niaba yao.na pale wanaposhindwa kufanya majukumu ambayo jamii iliyowachagua
imewapa wananchi wanayo nafasi ya kuwachagua wawakilishi wengine.
Swali la msingi
chimbuko la demokrasia ni nini?
Tunafahamu kuwa lengo kubwa la demokrasia ni kuleta mabadiliko kwa
wananchi wake, ili kuwaletea maisha mazuri, kuwatoa kwenye dimwi la
umasikini na kuwaletea maisha bora kwa jamii nzima na sio kikundi kidogo cha
watu; kwa msingi huu ukifuatwa vizuri na kutekeleza kwa ufanisi ni ukweli
usiopingika kwamba mfumo wa utawala wa kidemokrasia una umuhimu wake katika
maendeleo ya jamii nzima.
Je demokrasia
inatumika wakati wote?
Hili ni swali lenye changamoto kubwa; lakini ni lazima ieleweke na
tujiulize kuwa ni wakati gani demokrasia inapaswa kutumika na wakati gani
siyo muhimu kuitumia; Nasema hivyo kwa sababu siyo wakati wote ni muhimu ama
lazima kutumia mfumo wa demokrasia umaohusisha maamuzi ya wengi, ndani ya
uendeshaji wa serikali na maamuzi yake; mfano mzuri ni uamuzi ambao uliwahi
tolewa Mheshimiwa Raisi Kikwete baada ya kukutana na wawakilishi wa vyama vya
siasa na kukubaliana kuwa mchakato wa kupata katiba mpya utakao husisha maoni
ya wananchi utaendelea baada ya uchaguzi ujao. Uamuzi huu umekuwa tofauti
na uamuzi wa awali kuwa Katiba mpya itapatikana kabla ya uchaguzi 2015.
Je msingi wa
demokrasia ni nini?
Msingi wa demokrasia inawapendelea sana walio wengi kwa kukubali
mawazo ya wengi. Usahihi wa hoja mara nyingi sio jambo muhimu kuliko wingi wa
ufuasi. Walio wengi katika kufikia muafaka wa jambo kulingana na demokrasia
ndio washindi wa demokrasia hata kama hawana hoja
Je hasara ya
demokrasia ni nini?
Demokrasia inaangalia uwingi wa wawakilishi na sio lazima hoja
zinazotolewa, hata kama hoja hazina mantiki lakini zina ungwa mkono na wengi
zinafanyiwa maamuzi na hatimaye yanaonekana kuwa sahihi.
Hasara hii ya demokrasia tunaweza kulinganisha na mwenendo wa
upatikanaji wa katiba mpya ambao umekamilika huko Dodoma hivi karibuni.
kinachoangaliwa katika kufikia upatikaji wa katiba mpya umekuwa ni
wa wawakilishi ndani ya bunge la Katiba, kwa mfano katika nchi yetu ya Tanzania
“Chama cha Mapinduzi (CCM) kina wajumbe wengi katika Bunge la Katiba kwa hiyo
Msingi wa wingi wao ni ushindi walioupata katika uchaguzi halali wa
kisheria na kidemokrasia”
Kutokana na mazingira haya, mjadala wa upande mmoja uliokuwa
unaendelea bungeni ulikuwa halali, hata kama UKAWA waliamua vikao vya bunge
hilo. Walichofanya UKAWA ni mbembwe za siasa za kususia ili pengine kupata
huruma ya wananchi lakini kimsingi walitakiwa kuendelee kujenga hoja ili
kuwafanya walio wengi wabadilishe mawazo yao na wananchi weelewe msingi wao wa
hapana ni nini.
Naamini kuwa UKAWA walikuwa na hoja walitakiwa kufa kiume katika
ushindani wa hoja Bungeni; kwa maneno menginehii ndio demokrasia ya
ushindani iliyoletwa kwetu na warumi na tukaikubali na kuona ni chombo sahihi
cha maamuzi. Ndio hasara ya demokrasia lakini kwa kuwaachia wenzao uwanja
wamewanyima wananchi ushindani wa hoja za pande mbili.
Hata kama UKAWA watafanya mikutano ya kupinga katiba nje ya vikao
halali vya Bunge inakuwa ni hadithi, ni simulizi ya upande mmoja ambao hauna
usindani.
Ushindani wa hoja kati ya wanasiasa na kati ya vyama vya siasa
inatakiwa ieleweke kama ustawi wa jamii husika. Kwa kuwa tofauti ya hoja
haitakiwi ilete utengano na hatimaye migongano, bali iwe ni sehemu ya
kuleta maendeleo ndani ya jamii husika; kwani demokrasia ya ushindani itakayo
ishia katika kuleta vurugu na ugomvi ndani ya jamii itaathiri maendeleo ya
jamii na kuongeza maisha magumu kwa jamii husika hivyo kubadilisha mfumo huu na
kuingia katika mfumo wa kikatili
Utawala wa demokrasia unatakiwa utufundishe namna ya kupanua fikra
za wawakilishi wetu. Demokrasia inatakiwa iwe mkombozi wa fikra na kuwapa
wananchi uhuru wa kufikiri, uhuru wa kutenda na hata wa kwenda kinyume na fikra
za kikale. Ili jamii iweze kuendelea na iwe na demokrasia iliyopevuka ni muhimu
wananchi wawe na uhuru wa kuweza kuasi kisiasa na kuwa na fikra zisizofuata
mkondo wa fikra za kawaida za wanajamii.
Tofauti za hoja baina ya wafuasi wa vyama tofauti ndani ya
mfumo wa demokrasia huzaa chuki ambayo inajengwa kati ya watawala na wapinzani
dhidi ya wananchi kila upende ukijaribu kushinda hisia za wananchi ambao
ndio wenye nchi. Ni wajibu wa wananchi kuamka na kuwa imara na
kukataa mbwebwe za wanasiasa.
Tunatakiwa kuanza kuhoji
mambo ambayo tunaona kuwa sio ya kweli. Inafurahisha kwa sasa ndani ya Tanzania
kuwa mwamko wa wananchi wetu kwa sasa umebadilika na wananchi wameanza
kuonyesha dalili ya kuelewa Zaidi nini wanataka hasa kuhusiana na maendeleo
yao.
Tukiweza kuepukana na itikadi za matukio na polojo za
matukio na udaku: Lazima tukubali kuwa kila chama cha siasa Tanzania tupende au
tusipende kina uzuri wake na ubaya wake, lakini la msingi katika mantiki ya demokrasi
lazima tukubali kuwa chama ambacho kimefanikiwa kuingia mkataba wa hiari na
wananchi wa kuongoza nchi ndicho kimefanikiwa kupata ridhaa ya kuongoza ndipo
tunapona hasara ya demokraisa pengine matendo yao hayakubaliki na wachache
ambao wanafikiri kuwa nao wana mwelekeo tofauti na wenye tija kwa jamii. Kwa
msingi huo ni kuwa tofauti za siasa na wanasiasa katika jamii haziwezi
kuepukika na wakati mwingine unyama wao unaotokana na tofauti zao za kutamani
kuhodhi madaraka unapelekea kuiangamiza jamii ambayo haina kosa kutokana
tu na uelewa wao mdogo;
Napenda katika hitimisho la Makala yangu nimshukuru sana Mheshimiwa
Raisi Kikwete na Mheshimiwa Ally Mohamed Shein wamekuwa wasikivu, wavumilivu na walezi wa demokrasia ya kweli kwa
kuendelea kuvishirikisha vyama na asisi zote ambazo zimefika mahala na
kukinzana na serikali zetu zote mbili ili kufikia muafaka kwa kusikiliza mawazo
ya wachache bila kinyongo na hata wakati mwingine kubadilisha
msimamo wa wengi na kufuata mawazo ya wachache.
Hapa tunaona Sifa mojawapo ya demokrasia ya kweli ni kwamba:
inawapatia wachache VILEVILE nafasi ya kisheria ya kuwashawishi wengi waone
ubora wa maoni yao hata kama hawakubaliani nayo. Demokrasia ya namna hii ndiyo
njia pekee ya kuleta mawazo mapya katika jamii kwa njia ya amani na utulivu.
Hii ndio sifu kubwa ya viongozi wa serikali zetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete na Dr. Mohamed Ally Shein
Lazima tukubali kuwa demokrasia in faida na hasara yake na kamwe
sio kila mtu ataridhika na maamuzi ambayo yataendelea kutolewa katika
uwajibikaji wa pamoja.
Mungu Ibariki Tanzania