WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, October 11, 2012

Dkt. John Magufuli-watoto wa Vigogo wako Mizani "kuiba" ndio maana "timu zinaogopa kuwakamata"



 

Habari imeandikwa na Sifa Lubasi, HabariLeo, Dodoma --- WAZIRI wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli amesema wengi wa wafanyakazi katika vitengo vya Mizani Barabarani ni watoto wa vigogo ambao wamekuwa wakipenya na kupata kazi katika vitengo hivyo wakiamini kuwa kuna ulaji mkubwa wa fedha za Watanzania.

“Ndiyo maana wakati wote ninapoagiza na kutuma timu ya kuwakamata na kuwabaini wala rushwa, timu hizo zinakosa majibu ya uhalisia kutokana na kuogopa majina ya watoto wa vigogo,” alisema Dkt. Magufuli.

Bila kuwataja majina yao, Waziri huyo alisema kazi huwa haziendi kwa mtindo huo kwani kila mmoja anatakiwa kutimiza wajibu wake kikamilifu na si vinginevyo.

Kutokana na hilo, amesema anatiwa kichefuchefu na wafanyakazi hao wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) walioko katika vitengo vya Mizani Barabarani ambao wamekuwa wakijihusisha na rushwa na kuagiza wanaobainika, wafukuzwe hata 10 kwa siku moja ili wapungue.

Dkt. Magufuli alisema hayo wakati akifungua jengo la Wakala wa Majengo (TBA) lililojengwa mjini hapa ambalo lina thamani ya Shilingi bilioni 3.1; na kuagiza kamati za mikoa na mameneja wa mikoa kuwakamata na kuwafukuza mara moja wote watakaobainika na ikibidi hata kuchukuliwa hatua za kisheria.

“Naziagiza kamati za mikoa pamoja na mameneja wa mikoa kutekeleza jukumu hilo la kuwafukuza kazi mara moja wale wote watakaobainika, wafukuzwe hata kumi kwa siku ili wapungue,” alisema na kuongeza, “Pia naagiza kuanzia leo kuwakamata na kuwafukuza kazi wafanyakazi wa Mizani watakaokutwa na simu za mkononi katika maeneo yao kwa kuwa wamekuwa wakitumia simu hizo kufanya mawasiliano.”

Akitoa mfano, alisema mwaka jana gharama za kuendesha mizani kwa nchi nzima ilikuwa ni Shilingi bilioni tatu na kiasi kilichokusanywa ni Shilingi bilioni tatu, jambo ambalo linatia shaka kubwa.

Alitaka kila mmoja kuwajibika katika kitengo chake ipasavyo na wala kusiwepo na tabia ya kuoneana aibu hata bila ya kujali mtu huyo ana nafasi ipi serikalini.

No comments:

Post a Comment