WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, September 30, 2012

RAIS MSTAAFU ALI HASSANI MWINYI NA MOYO WA UPENDO KWA WANANCHI WA KWADELO



 Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omari Kariati akimsalimia Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwa Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi (kushoto), Mikocheni jijini Dar es Salaam. kabla ya hafla ya wananchi wa Kata hiyo kukabidhiwa tangi la maji na kidanda cha kujifungulia kina mama, iliyofanyika nyumbani hapo, leo.

Diwani Kariati akiongozana na Mzee Mwinyi na Mama Sitti Mwinyi kwenda eneo la tukio

 Kisha mzee Mwinyi na mkewe wakasongea pamoja na waalikwa pahala vilipokuwa vitu vya kukabidhi. Hapa anakabidhi kitanda

 Kwa furaha baada ya kukabidhiwa, mama mmoja wa Kwadelo akakifanyia majaribio kidogo kitanda hicho.

Kisha Mzee Mwinyi akakabidhi tangi la lita 5000 kwa Mwadham Msami (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerereng'ombe, palepale Kwadelo. Naye Omari Kariati akishuhudia

Baada ya kurejea meza kuu, Mzee Mwinyi akakabidhi sh. 200,000 kwa kijana, Kassim Omar kwa ajili ya kumalizia masomo yake ya ualimu Chuo cha Ununio, Bagamoyo.

 "Kwanza tunamshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya pili Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi kwa kutukaribisha nyumbani kwake kukamilisha hafla hii. Shughuli iliyotuleta hapa ni Mzee wetu kuwakabidhi wana-Kwadelo tangi kubwa la maji la sh. 650,000 na kitanda cha kujifungulia kina mama, kisha atamapatia sh. 200,000 kijana wetu aliyemuahidi kwa ajili ya kukamilisha masomo yake ya ualimu pale Ununio" akasema Diwani wa Kwadelo Omari Kariari kufungua shughuli. pembeni ni Mzee Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, wakimsikiliza.

"Karibuni Chai" akasema Mama Sitti kuwakawakabisha wageni mwishoni mwa shughuli

Kisha Mzee Mwinyi akaeleza yake ya moyoni kuwahusia wana Kwadelo na Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.

 Wageni wakachangamkia chai.Picha Zote na Francis Dande habari kwa hisani ya Haki Ngowi blog.