JE TAIFA LINANUFAIKA VIPI NA SENSA KILA MIAKA
KUMI (10)?
Sensa inatumika kutoa habari za hesabu (takwimu) kuhusu
watu wote wanokaakatika nchi husika.Habari hizi zinatumika na serikali, mikoa
na tawala za mitaa, biashara na jumuia za mahali na nyinginezo kusaidia katika
kufanya maamuzi kuhusu mipango ya elimu, afya, kazi, usafiri na hudumu nyingine
nyingi.
Kama viongozi wahusika wa
kuendesha shughuli nzima ya senza wanavyotuambia kuwa “Msisitizo wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu
ni kutoa kiunzi na miongozo ya kujumuisha vigezo vya idadi ya watu katika mchakato wa
maendeleo ili, hatimaye, mienendo ya idadi ya watu iwiane na mienendo mingine
ya kijamii na kiuchumi”.
Kwa
maneno mengine Sensa ni utaratibu wa kupata na
kurekodi habari kuhusu idadi ya watu fulanifulani. Ni utaratibu wa mara kwa
mara na hesabu rasmi ya idadi ya watu hao.
Msamiati hutumiwa
zaidi kuhusiana na idadi ya kitaifa na sensa ya mlango kwa mlango (kuchukuliwa
kila miaka 10 kulingana na mapendekezo ya Umoja wa Mataifa),
na ile ya kilimo na biashara. Msamiati huu umetoholewa kutoka lugha ya
Kilatini: wakati wa Jamhuri ya Kirumi sensa
ilikuwa ni orodha iliyowekwa ili kufuatilia wanaume wenye
uwezo wa kufaa kutoa huduma za kijeshi. Kitabu cha Hesabu 1:2-4 “Fanyeni hesabu
ya mkutano wote wa wana wa Israeli, kwa kuandama jamaa zao, na nyumba za baba
zao, kama hesabu ya majina ilivyo, kila mtu mume kichwa kwa kichwa; 3 tangu
mwenye miaka ishirini umri wake, na zaidi, wote wawezao kutoka kwenenda vitani
katika Israeli; wewe na Haruni mtawahesabu kwa kuandama majeshi yao. 4 Tena
mtu mume mmoja wa kila kabila atakuwa pamoja nanyi; kila mmoja aliye kichwa cha
nyumba ya baba zake.”
Swali
la msingi hapa ni hili?
Je ni kweli
kuwa Vilevile, sera hii ilitoa miongozo
itaskayo weza kutoa vipaumbele katika programu ya idadi ya watu
na maendeleo?
Je senza ikifanywa vizuri inaweza kuharakisha na
kufikia maendeleo endelevu na usawa wa ndani ya jamii?
Ukweli utabaki pale pale kuwa
Takwimu hizi kweli zititafutwa na kuzingatiwa zitatusaidia
sana katika kupanga maendeleo ndani ya jamii jamii zetu? Ni dhahiri kuwa
takwimu hizi zinaonesha uwiano wa idadi ya watu ndani ya jamii zetu hasa katika
huduma muhimu zinazotuzunguka, kama vile huduma ya hospitali zilizopo nchini.
Je sensa ni
chanzo cha maisha bora?
- Nia ni kuisadia Serikali ili iweze kupanga mipango ya maendeleo na kutunga Sheria, na kuandaa Sera kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wake kwa kutumia takwimu sahihi.
- Pia husaidia katika kutoa mwelekeo wa siku zijazo yaani 'forecasting'.
- Maendeleo endelevu na kuondoa umaskini
- Kuongeza na kuboresha upatikanaji na ufikiaji wa huduma bora za kijamii
- Kuwa na mgaosawa, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, haki ya kijamii na maendeleo kwa watu wote
- Mpangilio mzuri baina ya idadi ya watu, matumizi ya rasilimali na mazingira
Lengo kuu la Sera ya idadi
ya watu ni kuiwezesha Tanzania kufikia kiwango cha maisha kilichoboreshwa na
kufanikisha ubora wa maisha ya watu wake. Vipengele muhimu vya ubora wa maisha
ni pamoja na afya na elimu bora; chakula cha kutosha na makazi bora mazingira
imara; mgaosawa; ubora wa kijinsia, na usalama wa watu binafsi. Aidha, Sera ina lengo la kuelekeza ubunifu wa Sera
za Kisekta, na mikakati na mipango mingine
inayohakikisha maendeleo ya watu. Malengo mahsusi ya sera hii ni kufanikisha yafuatayo.
Sasa nini
tuzingatie kuelekea katika kipindi cha sense 2012?
Inafahamika kuwa sense ni
swala la kimataifa kwani katika kila nchi zoezi hili hufanyika kwa umakini kwa
mbinu tofauti kulingana na level ya uchumi ambayo nchi husika wamefikia: kwa hiyo watafiti wote duniani hutumia
takwimu zilizofanyika nyuma na kueleza ni nini kifanyike kuboresha zaidi huduma
au kukuza uchumi wa nchi kwa manufaa ya umma. Hakuna nchi duniani ambayo
haitumii takwimu za nyuma kwa ajili ya kujipima kimaendeleo. Kitaalamu
hakuna takwimu ambazo zinapitwa na wakati.
Sera inatoa miongozo ya kushughulikia
masuala ya idadi ya watu kwa namna jumuishi. Hivyo, inatambua mahusiano baina
ya mienendo ya idadi ya watu na ubora wa maisha kwa upande mmoja na ulinzi wa mazingira
na maendeleo endelevu kwa upande mwingine. Utekelezaji wake utatoa upeo mpya kwa
programu za maendeleo kwa kuhakikisha kwamba masuala ya idadi ya watu
yanashughulikiwa kikamilifu
Sensa italenga katikakulenga
kujua umaskini wa kipato cha mtu mmoja na idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi.
Itasaidia Serikali kwenye mipango yake mbalimbali, ikiwamo kutathmini Mpango wa
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKKUTA) na MKUZA, Zanzibar.
Je ni kweli
sababu ambazo serikali kuhusu maazimio ya sensa zinakidhi haja?
Sense ikitumika vizuri kwa
kuangalia uwiano wa idadi ya watu
vinaathiri maendeleo na ustawi wa mtu mmoja mmoja, familia, jumuiya katika
ngazi ndogo na katika ngazi ya wilaya, mkoa na taifa zima katika ngazi ya
jumla. Athari na miitikio ya shinikizo la idadi ya watu zinahusiana katika
ngazi zote.
Je sababu
ambazo zinaelezwa kuhusu umuhimu wa
sensa katika nchi yetu unaendana na lengo lake;
Kuna baadhi ya
wanaharakati wanaoona kuwa “Sababu zinazotolewa na Serikali kuwa zitasaidia
kufanya maamuzi sahihi si kweli, kwani Sensa nne zishafanywa na hakuna maamuzi
yalofanywa kwa kuzingatia hizo Takwimu za Sensa. Kama madawati hayatoshi,
Mikopo kwa wanafunzi haitoshi, Madawa Hakuna, Mahospitali hayatoshi,
Miundombinu karibia yote haiendani na idadi yetu. Nadhan serikali ingejikita
zaidi kutafuta vyanzo vya mapato badala ya kuchezea mapato kwa miradi isiyo na
tija”.
“Jambo ambalo ni
changamoto kwetu ni hoja ya kwamba, pamoja na jitihada hizo, taasisi za tafiti
hazijaleta matumaini makubwa hususan upande wa uchumi… miongoni mwa sababu
zinazochangia kutopungua kwa umaskini wa wananchi wengi ni pamoja na kasi kubwa
ya ongezeko la idadi ya watu ambalo haliendani na kiwango cha ukuaji wa
uchumi,”
Je sensa inasaidiaje na tatizo wa watu kuhamia mijini?
Kuongezeka kwa watu mijini
ambako kunasababishwa na wengi wao kuhama kutoka vijijini, kunaathiri shughuli
za uzalishaji za kilimo katika maeneo ya vijijini na hivyo kupunguza kipato na
hatimaye kuongeza umaskini kwa wananchi wa vijijini,”
Msongamano wa watu na magari mijini, shida ya
maji na miundombinu ya barabara na maji ni ushahidi tosha kwamba idadi ya watu
haiendani na ongezeko la kukua kwa uchumi na huduma nyingine za kijamii.
Je takwimu
zinazopatikani kweli ni sahii kwa
asilimia 100 au zina mapungufu mengi?
kama mtaalam mmoja wa sense alivyo wahi sema “tulipata shida sana kupata
takwimu sahihi za walemavu wa ngozi wakati ule kulikuwa na mauaji makubwa ya
ndugu zetu hawa, ilibidi tutume watu wakawahesabu lakini bado kulikuwa na
changamoto kubwa”.
Changamoto nyingine
inayowakabili wataalamu hao wa kutenga maeneo ni pamoja na baadhi ya maeneo
kutofikika kwa urahisi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo miundombinu duni
ya barabara, baadhi ya maeneo kuwa misitu minene yenye wanyama wakali pamoja na
miinuko mikali na mabonde katika maeneo mbalimbali hali inayowafanya wataalamu
hawa kufika kwa taabu katika maeneo hayo ili kupata vipimo sahihi.
Kutokana na utaratibu wa
kufanya kazi kwa kuchelewa na kwa kukosa uthubutu hupelekea kushindwa kufanya
kazi zao mapema kwa kuwa na maandalizi
yatasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuepuka zima moto
ilimradi kazi imalizike na kukosa takwimu sahihi kwa wakati muafaka.
- Je changamoto ya nyumba zakulala wageni au nyumba za makaazi zinazokaliwa na watu wengi wakati wa sensa zinahesabiwa vipi? mathalani nyumba moja kuwa na wapangaji wengi, kunasababisha viongozi wa eneo husika, kutojua idadi ya kaya zilizopo katika eneo husika.
Usahuri wa kawaida tu kama
Taifa lazima tuhakikishe kuwa idadi ya watu itakayo patikana mwaka huu igeuke
kuwa changamoto ya maendeleo na
kuwahakikishia wananchi wanapata maisha bora; Tusigeuze Sensa kuwa Mradi
wa kujinufaisha tu
Lazima tujenge uadilifu
katika kufanya kazi hii kwani ni kazi ambayo ni nyeti kwani wataalamu wetu wa
kuhesabu watu wanaweza tu kuamua kuto kwenda kijiji fualani kutokana na tatizo
la suafiri;
Tuhakikishe kuwa wote
watakao husika katika zoezi hili serikali tunaiomba ijitahidi kuwahudumia stahiki zao wasitumie kizingizio au kujenga
kiburi cha kushindwa kufanya kazii zao kwa umakini kwa sababu Fulani ambyo
inaweza kushughulikiwa;
Kwa naman yeyote ile sense
ni muhimu toka enzi za babu bau zetu kama nukuu hii inavyoonyesha;
- Je taarifa za sensa zinakusidiwa vile vile kutumika kwa kazi nyingine zinazolenga manufaa Chanya wa ukuaji wa Taifa?
Wakati sensa hutoa njia
muhimu ya kupata taarifa za takwimu kuhusu idadi ya watu, habari hii wakati
mwingine husababisha dhuluma, kisiasa au vinginevyo, ikiwezeshwa kwa
kuunganisha utambulisho wa kibinafsi na takwimu za faragha
Hitimisho
Ni ukweli ambao lazima
tuukubali kuwa pamoja na juhudi kubwa,
Ofisi ya Sensa haijawahi kuwa na uwezo wa kuhesabu kila mtu binafsi, kupelekea
utata kuhusu kama kutumia takwimu mbinu ili kuongeza idadi kwa baadhi ya
makusudi, kama vile hoja juu ya jinsi ya kuboresha ukusanyaji wa zoezi nzima kwa malengo yalikusudiwa kimaendeleo. Nahitimisha kwa kujiuliza maswali yafuatayo:
- Je katika hali hii taifa lifanye nini?
- Je matatizo ya kushindwa kuboresha maisha bora ya mtanzania chanzo na ukosekanaji wa takwimu sahihi za idadi ya watu?
- Je kutokana na ukosefu wa taarifa sahii watendaji wanatumia mwanya huo kujinufaisha wakitumia udhaifu wa ukusanyaji takwimu?