"Kazi ya kutengeneza
katiba ni ya wananchi, katiba ni ya wananchi, kwa manufaa ya wananchi,"
anasema Bw. Kiwanga
Kauli za makamu wa pili wa
Rais Zanzibar Mheshimiwa
Maalim Seif “Wananchi
wanapaswa kujiandaa kutoa maoni bila ya uoga, na jambo muhimu ni kuhakikisha
katika maoni yao hawamtukani mtu: Nyinyi Wazanzibari na ndugu zetu wa Tanzania
Bara ndio tuliovaa kiyatu (Muungano) na aliyevaa kiyatu ndiye anayejua msumari
unachomea wapi, au anayelala kwenye kitanda ndiye anayejua kunguni wake”,
Mheshimiwa Maalim
Seif aliendelea kueleza kuwa “katika kuzingatia mambo yenye maslahi
kwa Zanzibar wasitokee watu wakaweka maslahi binafsi mbele, alisema haitakuwa
jambo la manufaa kwa Zanzibar iwapo watajitokeza baadhi ya viongozi wakaanza
kujadili nafasi zao za Ubunge na uongozi, iwapo muundo Fulani wa Muungano
utapita”
Kauli za Mwenyekiti wa
Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia “Tunakupongeza
kwa kusimammia suala la Katiba vizuri, ni suala zito ambalo litatupa uhai
vizazi na vizazi vijavyo. Upinzani sio uadui, tunahitaji kufanya marekebisho ya
Katiba kwa amani na hoja bila kuvuruga amani yetu suala la Katiba linahitaji
ushirikiano wa pamoja kwa nia njema, kwani taifa hili ni letu sote; Ni
jambo kubwa sana, wewe ndiyo Rais wa kwanza kutengeneza sheria ya kupata katiba
mpya na kuanzisha Mchakato wa kupata Katiba Mpya.”
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John
Magufuli, “Katiba mpya izingatie matakwa ya wananchi ili kuliweka
taifa katika hali ya utulivu. Hili la Katiba mpya ni
jambo mhimu na nyeti…tunataka Katiba ijayo ikidhi matakwa ya Watanzania. Tume
itakayoundwa na rais kukusanya maoni ifanye hivyo bila konakona fulani fulani,”
Mheshimiwa John Mnyika
“Izingatiwe kuwa kwa sasa Tanzania haifanyi marekebisho ya Katiba bali
tunakwenda kufanya mapitio (review) na hatimaye kuwa na katiba mpya; hivyo
suala la ushirikishwaji wa umma sio katika kutoa maoni tu bali kuamua misingi
muhimu ya katiba ni suala lenye umuhimu wa pekee ili tuwe na katiba
inayokubalika na umma mpana isije yakajirudia tena yaliyojitokeza kwenye
kuandikwa kwa katiba ya mwaka 1977”.
Mheshimiwa Mbowe
amekuwa akisisitiza kuwa "Suala la katiba mpya limetekwa na baadhi ya
wanasiasa ambao hawajui ni fursa ya kila mtanzania, wapo wengine wanaona
chadema inapinga kuwepo kwa katiba mpya, sisi tunahitaji sana na tunachokitaka
wananchi washirikishwe na waamue wenyewe,”
Hivi karibuni tumeendelea
kuona nia njema ya Rais wetu Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akiendelea na
majadiliano na wawakilishi wa vyama mbalimbali vya siasa ambavyo vinajenga
kambi ya upinzani; kama waandishi wengi walivyoandika na kuendelea kuandika kuwa
“ Tunachotaka kusema hapa ni kwamba viongozi hao wa pande hizo mbili wametupa
matumaini mapya kwamba sasa upo uwezekano mkubwa wa kupata Katiba Mpya ya
kuipeleka nchi yetu kwenye maendeleo katika misingi ya demokrasia na utawala
bora. Tunasema hivyo kutokana na dhamira ya kweli iliyoonyeshwa na pande hizo
mbili katika mazungumzo hayo ambayo vyanzo vyetu ndani ya Serikali
vimethibitisha kuwa, mazungumzo hayo yalikuwa magumu na yasingefanikiwa iwapo
pande hizo zingetanguliza ubinafsi na itikadi za vyama vyao.”
Tunahitaji kuendelea
kuelewa kuwa tutapata katiba mpya lakini tunahitaji katiba ya aina gani? Katiba
ambayo itaelemea upande mmoja wa mlengo Fulani wa kikundi cha watu na chama
chao; jibu ni hapana tunahitaji katiba ambayo italenga mpya kuwakwamua wananchi
wa Tanzania wa pande zote bila ubaguzi; tunachohitaji sana wanasiasa wetu
katika kipindi hiki wawe kweli wanaupeo
na wawe na ukomavu wa kisiasa ambao ni pamoja viongozi kuwa na uvumilivu na
kujua jinsi ya kutatua matatizo bila kusababisha malumbano , na kujenga chuki
miongoni mwa wananchi.
Majadiliano ya hivi karibuni ya vyama vya CHADEMA, NCCR-MAGEUZI,
CUF pamoja na serikali ambayo ndio
msimamizi mkuu wa mchakato huu wa katiba ambayo sasa tunaanza kuona kuwa
inamwelekeo wa unaoleta matumaini zaidi
kwa masilahi ya Taifa na sio chama au kikundi Fulani cha watu; au kuingiza
siasa za vyama ndani ya mchakato kwa
vile katiba itabeba sheria mama ya nchi
ni vizuri kutatoa ushirikiano wa dhati katika mchakato huu kwa maslahi ya nchi
Itakuwa ni kitu cha busara
na cha kupongezwa sana kama vyama vya siasa kwa uwezo wao wa uenezi kuanza
kuwaelimisha na kuwashirikisha wananchi
katika utoaji wa maoni katika mchakato
wa kutengeneza Katiba amabayo itaweza kutuvusha
sio tu katika kuendeleza amani
bali hata katika kuleta maendeleo ambayo tunayahitaji sasa kuliko wakati
mwingine wowote; kama tutaweza kuhamasiha wananchi wetu waweze kuchangia
tutakuwa kumeipa (legitimacy ) yaani
kweli ni katiba inayokubalika kwa kila mtu na hakutakuwa na malalamiko kuwa wananchi
wameporwa mamlaka ya utengenezaji katiba.
kama wataalamu wengi walivyowahi kuseaka kuwa Demokrasia kwa ufupi ni dhana
inayolenga ushiriki wa wananchi, katika kuweka misingi sahihi ya uendeshaji wa nchi
na wao wakiwa ndio msingi wa mamlaka yote ya nchi nawalio na uwezo wa mwisho wa
kuipa serikali madaraka na mamlaka hayo ya kuongoza nchi. Kwa mantiki hii moja
ya msingi mkuu unaokuza demokrasia ya namna hii ni Katiba ya Nchi. Katiba ni
msingi mkuu wa uendeshji wa nchi,ukuaji wa demokrasia na utawala wa sheria.
Yenyewe ndiyo sheria na ni kioo cha maisha bora
ya wananchi wake:
Tunahitaji Katiba iliyomadhubuti huwa
ambayo ni msingi mkubwawa utawala bora; kwani katiba bora inazingatia uwazi, uwajibikaji na utawala
wa sheria dhana ambayo kwa ujumla ni msingi wa kwanza wa demokrasia na maendeleo ya nchi. Lazima tuendelee
kusisitiza kuwa ukweli ni kuwa katiba inayopendekezwa inatakiwa iwe ni mradi wawananchi wa Tanzania Bara na Visiwani.
Katiba mpya itakuwa ya watanzania wote na tusikubali ifanywe kuwa ya serikali
iliyopo leo na itakayokuja kesho.
Katiba mpya ikikamilika tunatamani
itufanyie haya yafuatayo:
·
Ituletea kiongozi
Mzuri pamoja na serikali yake;
·
Ituletea chama chenye
sera bora, kwa masilahi ya wanachi
·
Ituletea watumishi wa
serikali na umma ambao ni waadilifu
·
Iendelee kutudumishia
amani ambayo tumeifurahia kwa muda mrefu sasa
Nahitimisha kwa kusema hivi jamani watanzania wenzangu, wanasiasa, wananchi na
wananchi wote kwa ujumla kuwa;
"Tanzania ni yetu, hatma ya taifa hili iko mikononi mwetu,
tuwajibike, tuache woga, tujadili, tufikie mwafaka wa kitaifa. Katiba mpya ni
jibu. Jibu la kurudisha maadili ya taifa na kulinda rasilimali za taifa.
Tuchukue hatua, Hivyo Katiba inapaswa kuwa ni matokeo ya mwafaka wa kitaifa
kwenye masuala yote ya msingi ya nchi husika”