WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Saturday, December 31, 2011

Salaam Za Mwaka Mpya Kutoka Bagamoyo!




Ndugu zangu,

Nianze kwanza kwa kuwatakia heri na fanaka za mwaka mpya wa 2012.

Ewe ndugu mwanakijiji wa blogu hii ya Mjengwa, leo tunaumaliza mwaka wa 2011. Hivyo basi, kesho ni siku nyingine tena inayotujia.Ni mwaka mpya. Hivyo,  nawe kama utakuwa umejaaliwa siha ya kuyasoma haya. Mshukuru Mungu wako kwa kukujalia hilo.

Katika dunia hii, mwanadamu unaweza kuandaa juu ya nini kifanyike siku ya kifo chako. Lakini, mwanadamu usifikiri sana kuhusu siku yako ya kufa, maana,hujui ni siku gani, lakini  itafika siku utakufa, iwe mchana au usiku.

Utakufa ndani ya siku. Ndani ya saa 24. Ndio, utakufa ndani ya mwaka wenye siku 365. Na mauti yakikufika, basi, huna tena utakaloweza kulifanya. Hali yako ya umauti itaachwa kwa wanadamu wenzako. Hivyo, mwanadamu kaa uumize kichwa kufikiri siku unayoishi, na zijazo kama utaishi. Fikiri sasa juu ya utakayoyafanya kwa mwaka huu wa 2012.

Fikiri pia utakayowaachia nyuma  wanadamu wenzako. Yale ambayo utapenda ukumbukwe nayo pale watakapotaja jina lako. Maana, si kweli kuwa yote tuyafanyao sasa, mema na mabaya, yatapotea na umauti wetu.

Jiulize; Je, mwaka mpya una maana gani kwangu?

Ndio,  nami nimejiuliza swali hilo. Nimetafakari  juu ya siku na maana yake kwetu wanadamu. Juu ya mwaka na maana yake kwa mwanadamu.

Najiuliza; siku inakuja au inakwenda? Na mwaka je? Fikra zangu zimenielekeza kwenye kuamini,  kuwa wenye kudhani kuwa siku  na miaka inakwenda wanakosea. Maana, siku  na haziendi wala hazigandi. Siku zinakuja. Vivyo hivyo kwa mwaka. Miaka haendi wala haigandi. Miaka inakuja.

Na usihangaike sana  kujiuliza; leo ni siku gani? Lililo muhimu ni kuiona siku. Unaweza hata kuamua uipe siku jina jingine badala ya  Jumapili kama ilivyo siku ya leo.

Basi, ewe mwanadamu mwenzangu, kama zawadi,  ipokee kwa mikono miwili siku hiyo iliyokujia. Ipokee kwa furaha na si kwa manung’uniko. Mshukuru na mwombe Mungu wako akuongoze katika kuitafuta busara na hekima ya kuitumia vema siku hiyo iliyokujia.

 Akuongoze kutenda yalo mema na yenye wingi wa uadilifu.  Yale yatakayokuwa na manufaa kwako na kwa wanadamu wenzako. Hivyo basi, kwa jamii unayoishi. Kwa Nchi yako. Usiwe ni mtu mwenye tamaa. Usiwe mbinafsi na mwenye tamaa ya mamlaka.

Na ndugu zangu Wakristo na hata wengine wasio Wakristo wanakitambua kisa cha Essau na Yakobo. Na tafsiri zaweza kuwa nyingi; hii ni ya kwangu. Tunasoma, kuwa Essau na Yakobo walikuwa ni wana wa Isaka.

Essau alikuwa ni mkubwa akifuatiwa na Yakobo. Essau Yule alikuwa ni mwindaji. Naye Yakobo alikuwa akipenda sana kushiriki shughuli za mapishi jikoni akiwa na mama yake.


Biblia inasema, kuwa siku moja Essau alikwenda katika mawindo yake. Alirudi mikono mitupu, hakupata kitoweo. Aliporudi nyumbali Essau alikuwa ni mwenye njaa kali, kwani, aliwinda siku nzima mwituni pasipo kula.

Nyumbani alimkuta Yakobo akiwa amepika dengu. Essau alimuomba Jakobo ampatie bakuli la dengu ili ale na kutuliza njaa yake.

Yakobo alimwambia kaka yake Essau; ” Kama unataka bakuli la dengu, basi, ukubali kuwa mdogo kwangu.” Yaani, Essau akubali kuwa, kuanzia siku hiyo, yeye Yakobo ahesabike kuwa mkubwa (mzaliwa wa kwanza) wa Isaka baba yao, na Essau awe ni mzaliwa wa pili.

Kwa vile Essau alikuwa na njaa sana, alikubali kuwa mdogo kwa Yakobo. Ndipo akapewa bakuli la dengu amalize njaa yake. Naam, tunaona, kuwa njaa ilimfanya Essau auze haki yake ya uzaliwa wa kwanza.


Na ya akina Essau na Yakobo tunayaona sasa. Kuna hata wanaouza haki za Wananchi kwa sababu ya njaa zao. Na wengine si kwamba wana njaa kali hivyo. Ni wenye njaa ya kutaka shibe kama ya mbwa mwitu. Ni watu wenye kuendekeza tamaa.

Na akina Yakobo wa sasa wenye bakuli la dengu baadhi yao ndio hao wanaoitwa wafanyabiashara. Masharti yao ya kutoa bakuli la dengu ni pamoja na kusamehewa kodi au kupewa upendeleo katika kupata tenda mbali mbali. Wamefikia hata kutoa masharti ya kutuchagulia viongozi wetu.

Na nguvu hizo tumewapa wenyewe kwa baadhi yetu kuendekeza njaa na kutaka shibe za mbwa mwitu. Na wenye bakuli la dengu wa siku hizi, hawakupi bakuli la dengu likajaa. Kwamba ule ukashiba. La, watakupa dengu kiduchu ili urudi tena kuomba bakuli lingine. Uwe tegemezi kwao.

Ndugu zangu,

Kuna wengi mlio kwenye jiko lenye giza huku mkiwa na njaa kali. Mnachohitaji kwanza ni ukombozi wa kifikra . Ukombozi huo utawapelekea kwenye kuepuka kufa na njaa. Kuepuka kuwa watumwa kwenye nchi yenu mliyozaliwa. Kwenye ardhi ya mababu zenu. Anzeni sasa kuuwasha moto. Moto huo utawapa pia mwanga kwenye jiko hilo lenye giza nene.

E nendeni mkayatafute majani makavu. Kisha muyaweke katikati ya mafiga. Tieni moto kiberiti muyawashe. Yakishawaka, anzeni taratibu kuweka vijiti na vibanzi vikavu juu yake. Na vitakaposhika moto, endeleeni kuweka kuni kubwa huku mkipulizia.

Moto utakaowaka hapo hautazimika kirahisi. Utawapa shibe ya boga au muhogo. Utawapa mwanga pia. Ni mwanga wa ukombozi wa kifikra na kiuchumi.  Heri ya Mwaka Mpya kwenu nyote.

Maggid Mjengwa,
Bagamoyo
Desemba 31, 2011

Friday, December 30, 2011

NEW YEAR RESOLUTION

If you keep going over the past, you're going to end up with a thousand pasts and no future.

We need to be flexible  just because things don't turn out as planned, we need keep going! Maybe there is another way of achieving our goal.

God Bless Tanzania in 2012

Thursday, December 29, 2011

AS WE APPROACH NEW YEAR

As one philosopher once said;
Happiness is something to someone to love something to forward to do so when happiness come your way just enjoy it.

Make 2012 a happy year in everything

Friday, December 23, 2011

IT IS MY DAY AS THE SUN SHINES ON MY FACE THIS MORNING DECEMBER 24

THIS IS THE DAY THE LORD HATH MADE; PSALM 118:24

It has been another year of Blessings when another door of life is openings in my life. I am now more than quarter of a century. Oh wow I feel good with age by knowing that age in grace and wisdom.
God has been faithful to me and to everyone else who reads this Blog. There are many people we love who didn't even see this age or even the age of 18. But we are here reading this massage and breathing by the grace and Spirit of God. I just wanted to say thank you Lord for another year another year I can share your word and your goodness to my family and friends. You've been faithful when no one else has been.

Well today is my birthday and it’s going to be a good time. I will spend most of my time in thanking God through reading the Holly Book “Bible”. As bible teaches us that “I love those who love me, and those who seek me find me”

The book of Psalm 71:6 reminds me that from birth I have relied on you; you brought me forth from my mother's womb. I will ever praise you; and it is true that No wise man ever wished to be younger.

"I always thank God for myself because of his grace given to me in all these years of my life and Second I would like to Thank my Wife Grace Peter Myamba and my Daughter Rose Turuka for helping to shape me the way I am today;


I also thank our parents Alois and Anna and Peter and Trifonia for well done job of fulfilling their role as parents in  parenting care in our life;
And all friends who always wish me and my family best wishes every single day  

I am keeping asking the Almighty God to continue to bless me as i continue knowing that the celebration of my Birthday this year is a perfect gift from God.
It is with no doubt that Birth day is really very nice to time to know, that at least once a year, some people think of Me.
As I celebrate my birth date today I am trying to define my purpose in life; to me Life is the expression of fulfillment. As one scholar wrote that “Everything has a purpose, a time and a season. When you took your first breath of life, you became a living being. The time of birth determines the quality of the power within you and reveals your purpose in life”.

Therefore Lord I thank because it is only by your grace that I am still here. Heavenly Father, Please bless me and my family for today is my birthday. Make me strong and give me the strength to make good decisions in the coming year. Keep me free from illness and sadness, for I think God I am truly good person who deserves happiness and success in all aspects of life.


We know that life is like a book. With each new chapter, we learn and grow towards what you would
have us be. Bless me with my Wife Grace and My Daughter Rose now and forever.

My MOTTO for my birthday this year LIFE HAS A PURPOSE; AND GOD HAS PURPOSE WITH US AT ALL TIMES, as Mother Teresa once wrote that;

“Life is an opportunity, benefit from it.
Life is beauty, admire it.
Life is a dream, realize it.
Life is a challenge, meet it.
Life is a duty, complete it.
Life is a game, play it.
Life is a promise, fulfill it.
Life is sorrow, overcome it.
Life is a song, sing it.
Life is a struggle, accept it.
Life is a tragedy, confront it.
Life is an adventure, dare it.
Life is luck, make it.
Life is too precious, do not destroy it.
Life is life, fight for it.”




THEREFORE “THIS IS THE DAY LORD HAS MADE, PLEASE JOIN ME IN REJOICING AND BE GLAD IN IT
In your name I pray Amen

Thursday, December 22, 2011

JE SHERIA ZETU ZINATEKELEZEKA?


MAJANGA YANAYOENDELEA KUTOKEA KATIKA TAIFA LETU; JE SHERIA ZETU NI KWELI ZINAFANYA KAZI KAMA MSUMENO?


Hivi karibuni katika siku za kuhesabu  jiji la Dar Es Salaam, limekumbwa na mafuriko ambayo yamesababisha vifo,  upotevu wa mali na ukosefu wa makazi kwa nduzu zetu watanzania waliokuwa wananaishai  katika  maeneo haya  waliyokumbwa na mafuriko; kwa tafsiri nyingine waliokuwa wanaishi sehemu za mabondeni au sehemu ambazo maji yalijaa kutokana au na “ water level” kufikia kikomo au maji kushindwa kuendelea  na safari yake kwani hayana sehemu ya kwenda kwenda kutoka na mfumo mbovu au ulio chakaa au uliokosa mwelekea wa kisanyasi katika kuyafanya maji hayo kuendelea kutambaa kwenda baharini au sehemu nyingene ambayo ni salalma kwa maji hayo kwenda.  

Kutokana na mafuriko haya kuwa makubwa katika historia ya jiji la Dar es salaam idadi ya vifo inaweza kuongezeka kadiri siku zinavyoendelea kusonga mbele;



Kama waandishi na wataalamu wengi walivyowahi kusema kuwa” miundo mbinu hafifu imetajwa kuwa chanzo kikubwa cha mafuriko katika jiji la dar es salaam na maeneo mengine nchini ambayo nayo kwa sasa yamekumbwa na mafuriko makubw aikiwemo mikoa ya mwanza na mbeya”



Mafuriko haya kwa upande mwingine ya athari kubwa sana kwani inafahamika kuwa jiji la Dar ndilo  ambalo ni kitovu kikuu cha biashara na uchumi kwa nchi; Mvua hizo zimesababisha usumbufu mkubwa sana katika swala nzima la usafir wa wananchi wa jiji hilo kutoka kuna moja kwenda kona nyingine;

Katika kipindi hiki cha kutapatapa kwa wahusika katika kushughulikia swala hili hoja tofautitofauti zitaendelea kuzungumzwa kama hizi;

·        “Tulishatangaza watu wahame mabondeni jamani, lakini bado wanaendelea kukaa tu huko na haya ndio matatizo yenyewe”

·        Gazeti la HabariLeo katika moja ya vichwa vyake lilenadika kuwa “Tusisubiri kupata hasara tuhame wenyewe mabondeni”

·        “Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Serikali ifanye nini ili ionekane inawajali watu wake?

·        Ikiwa watu hawa walishaelezwa wazi kuwa eneo hilo si maalumu kwa makazi, ni bonde na si salama hivyo wahame lakini bado wanaendelea kukaa na maafa yanapotokea lawama zinatupiwa serikali, hii si haki jamani”. 

·        “Inapotolewa tahadhari ya watu wanaoishi maeneo ya hatari kama hayo kuhama pia napo inasubiriwa Serikali iwatoe kwa nguvu? Mvua inaponyesha na maji wanaona yanaongezeka na kuzidi kujaa bado napo inasubiri Serikali iwaambie maji yanawafika viunoni ondokeni jamani! “

·        “Mimi nadhani kila mtu anatakiwa asimame katika nafasi yake, mwananchim wanasiasa na serikali kila mtu atimize wajibu wake kwa maslahi ya Taifa si maslahi binafsi.”

Hizi ni baadhi tu ya hoja kuhusiana na hali halisi ya tukio na nini kifanyike katika kufanikisha swala nzima ka kusimamia na kuwasaidia watanzania wenzetu ambao wamekumbwa na mkasa huu, sio tu kwa sasa na hata baadae;


Mimi najiuliza maswali mengi ambayo mengi kati yake sijeweza kupata majibu ya moja kwa moja kwa haraka; Najaribu kutafakari tukio hili kwa leo na matukio mengine ambayo yanafanana na haya na ambayo yanaendelea kulisababishia taifa hasara ya kubwa wa kupoteza nguvu watu kuleta hasara kubwa kwa Taifa letu kiuchumi na kulirudisha Taifa nyuma kimaendeleo na hasara ambayo tunaweza kabisa kuikabili hata kwa asilimia 80%;

·        Je ni kweli kuwa sheria zetu zimetungwa ili kumsaidia mtanzania bila kuogopa kwa manufaa na masilahi ya Taifa?

·        Sheria zimetungwa na zinafanya kazi kwa ubutu zikiishia tu katika maneno zaidi na sio utekelezaji wake?

·        Je ni kweli sheria zetu ni kama msumeno kwa maana zinatakiwa kukata mbele na nyuma na kwamba hazitakiwi kuchagua  pa kukata?

·        Je kama sheria kweli ni msumeno mbona Taifa linaendelea kushuhudia majanga yakitokea ambayo ni udhaifu wa utekelezaji wa sheria hizo?

Namkumbuka Dr. Magufuri alivyosimamia watedaji walioshindwa kufanya kazi yao inavyotakiwa kwa kujenga ofisi ya Tanroads katika hifadhi ya barabara; alisimama kidedea na kuhakikisha kuwa jingo hilo linabomolewa, na lilibomolewa; kama taifa lazima tukubali kuwa sheria  lazima iheshimiwe;

·        Je wananchi ambao wanaishi katika mabonde ambayo sio salama kwa makazi yao hasa wakati wa maafa au mafuriko kama haya, waliruhusiwa na nani?


Kama serikali ambayo ndo iriwarusuhukupitia watendaji wake kwa sababu moja au nyingine basi pamoja na maafa haya makubwa hakuna sababu ya kuwalaamu wananchi, ni jukumu la serikali kuhakikisha kuwa inawasaidia katika kuhakikisha kuwa wanakuwa salama na baada ya tatizo kutoweka maji kwisha inawajibika kuwatengenezea makao yao vizuri katika maeneo ili waweze kuendelea na maisha yao ya kila siku;

Lakini kama wananchi  na wathirika wa mafuriko haya  wanaisha katika maeneo haya kinyume cha sheria na agizo la serikali, na walivamia tu makazi haya  basi ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa Watanzania wezetu wanatafutiwa mahali salama pa kuishi na sio kuwaruhusu kuendelea kuishi katika maeneo haya ambayo sio salama hata kiafya;

·     Kwa nini tuendelee kumsikitikia Mwenyezi Mungu kwa uzembe wetu?

Siku zote sheria ni msumeno, hukata mbele na nyuma. Hivyo ni jukumu la sheria kulinda unapokuwa katika mwelekeo sahii  na kuhukumu unapoikiuka. Kwa matazamo huu niauliza tena hapa kama nilivyowahi kuuliza huko nyuma Je Msimamo wa Dr. Magufuli katika kusimamia sheria ambazo zimepindwa na watendaji wenginine ni sahihi?  Je taifa linahitaji watendaji kama Dr. Magufuli na Prof. Tibaijuka katika kuleta usawa mbele ya sheria na katika utendaji kazi wao kulingana na katiba na sheria za nchi?
Prof. Tibaijuka katika harakati zake za kusimamia sheria amekuwa akisema na kusisitiza kuwa;

·        “Tumeshatoa tangazo kwa wahusika juu ya kuhama maeneo hayo, sheria zimetungwa na kupitishwa na Bunge ili zifuatwe, hivyo jukumu letu ni kuzifuata”.

  “…Kuzitekeleza ni wajibu, safari hii tutafanya kazi bila kumwangalia mtu usoni, sheria zitafuatwa kwa wale waliojenga kinyume na sheria na maeneo ambayo si rasmi wakae chonjo,”

Nakumbuka kuwa Profesa Anna Tibaijuka, amewataka wakazi wa eneo la Jangwaji na wanaoishi eneo la Bonde la Msimbazi Dar es Salaam, wahame katika eneo hilo kabla Serikali haijawachukulia hatua.

·        “Wananchi wengi hawazijui sheria za kumiliki maeneo, ndiyo maana wengi wao wanaishi sehemu zisizo halali kwa makosa, na ndiyo maana mnaona wengine wanaishi Jangwani ingawa siyo eneo la makazi bali ni eneo maalum kwa ajili ya kuegeshwa magari.

WATAALAMU WETU WA MIPANGO MIJI BADO WANAENDELEA KULALA USINGIZI MNONO? 

Leo tunavyoendelea kushuhudia  maafa haya makubwa ya mafuriko ambayo yamesababisha maafa makubwa kwa taifa letu; je chimbuko lake nini?

Nafikiri wataalamu wa Mipango Miji  wataendelea kulaumiwa kwa sababu wao ndio waliochangia maeneo ya wazi kuvamiwa na watu bila kufuata utaratibu na kanuni za kisheria kama hawakuhusika mara moja. Kwani hata kama wananchi walivamia maeneo hayo walikuwa wanawaona na kwa nini waliamua kuwaacha waendelee kujenga na kulindikana:

Nafikiri pamoja na utaalamu wao  wameshindwa kuwaelimisha na elimu katika jamii kuhusu umiliki wa maeneo na pia hawatoa ramani zinazoonyesha maeneo ya wazi amabyo hayaruhusiwi kwa makazi.

JE WANANCHI WANAMCHANGO GANI KATIKA TATIZO HILI NA MATATIZO YANAYOFANANA?

Kama alivyosema Prof.Tibaijuka “Tumegundua wananchi wengi wanaofanya udanganyifu katika maeneo wanatumia ramani za kukopi, kitu ambacho ni udanganyifu, wanafanya hivi katika kuwaibia wananchi,”

Wananchi wakati mwingine hatujali na tunavuja sheria kusudi kwa kujua kuwa watendaji wetu wasimamizia wa sheria si wawajibikaji na wameshindwa kuthubutu katika kusimamia sheria hizo;
Wananchi wakati mwingine tumekuwa wabishi lakini tatizo likitokea kama hili majuto yanarudi kwetu na sio kwao; athari zinabaki kwa mwananchi na serikali inaendelea kuwa na utamu tu wa maneno;

Kiburi na ukorofi na urahisi wa mambo utagharimu sana maisha yetu na vizazi vyetu wananchi tunatakiwa kufuata sheria zaidi na sio kulazimisha kukaa katika sehemu ambazo zimetafitiwa sio salama kwa makazi ya kudumu ya binadamu;
Kwa kweeli sheria inatakiwa kuwa msumeno ambao unaweza kutukata pande zote mbili kuruka; na sheria kamwe isiwe jambia kuwa anayeathirika na jambia ni Yule tu anayekamata kwenye makali;

vita  ya kusimamia utekelezaji wa kweli wa sheria wahusika wanatakiwa kuwa wawajibikaji wa kweli kwani jamii imevurugwa na nguvu ya fedhakatika usimamizi wake. Hivyo, uwezekano wa kukwamishwa, kusalitiwa au kuingizwa mkenge na mafisadi kupitia kwa baadhi ya watumishi wa wizara husika wataendelea kukwazwa katika kusimamia  sheria na kanuni za kulinusuru Taifa na majanga kama haya.
   
wasimamizi wa sheria tunaendelea kuwashauri wasiogope kujitoa  muhanga iwapo watalazimika kufanya hivyo, kwani huo ndiyo utakuwa  mchango wao katika kuleta ukombozi katika ustawi wa jamii yetu  na kwa usimamizi wao ambao utakuwa umetukuka basi itakuwa rahisi sana kwa wananchi kwa umoja wetu kuunga  mkono  jitihada hizi kwa faida yetu na Taifa letu. Siasa itusaidie kuimarisha na kutekeleza sheria na tusitumie mwanya wa siasa kuogopa kusema ukweli kwa kuogopa kukosa kuchaguliwa kwa kusimamia ukweli ambao pengine utawaudhi wananchi, na kuliletea hasara taifa kama tunavyoendelea kushuhudia sasa;

Saturday, December 17, 2011

VITA YA VIJANA DHIDI YA WAZEE KATIKA UONGOZI WA NCHI


Kwa nini tunahitaji uongozi wa vijana sasa?


·        Je Ni kweli kuwa vijana ndio nguzo na uhai wa chama chochote kiwacho?

·        Je ni kweli  kuwa  Vijana wanafaa kutumikia taifa lao kwa ajili ya nguvu walizo nazo zaidi hata kama hawana elimu ya kutosha ya uongozi?

·  Je vijana wanaelewa matatizo ya vijana wenzao  na wataweza kuwasaidia  haraka katika kujinasua katika atope zito la maisha magumu pindi wapatapo nafasi ya uongozi?
Kwani nini wazee hawafai kwa sasa?



·  Hivi sasa wazee ndio chimbuko la matatizo ndani ya vyetu vya siasa?

·        wazee  kwa wakati huu  wamechoka kuongoza chama kwa umri wao na mawazo yao mgando?

·        wazee hawaoni wala hawasikii hoja zote vizuri;

·        wazee ni wazito kufanya maamuzi;

·        wazee wana huruma kupita kiasi

hoja ya wazee dhidi ya uongozi wa vijana




·     Ni kweli kuwa vijana hawana uwezo kuongoza siasa za nchi zetu?

·     ni kweli kuwa vijana hawana hekima ya kutosha katika kufanya maamuzi makubwa ya kitaifa.

· vijana wana nmatatizo bado ya kuongelea integrity (uadilifu) wa utendaji wa vyama vyao kwani wengi bado wamejiegemeza kwa kundi fulani;


· Ni ukweli kuwa maamuzi mengi ya vijana yana mwelekeo wa jazba na uharaka usio na maana?




· Ni kweli kuwa vijana wote  wanaoingizwa katika shughuli za siasa  na kushiriki katika ngazi za maamuzi, lazima wawe na back-up ya nguvu kabisa ya wazee.

Prof. Issa Shivji aliwahi kusema katika moja ya mijadala ya vijana kuwa yeye ni kijana kutokana na kuwa upeo wake wa kufikiri bado una nguvu na hutenda kazi zaidi ya ambavyo vijana kwa mujibu wa umri wao wangeweza kufanya. Tafsiri hii ya Prof. Shivji  inakuja na maswali mengi ya kujiuliza, je ujana tuuangalie katika upeo gani? Wa umri au katka uwezo wa kuamua mambo? Kwa upande wa Prof Shivji yeye anaangalia zaidi katika upande wa maamuzi; hata kama umri wako ni mkubwa lakini bado uwezo wake wa kufikiri na kufanya maamuzi  ni mkubwa; kwa tafsiri hii ya Shivji basi Mzee wetu Kingunge Kombale Mwiru kama bado anao upeo mzuri wa maamuz ni kijana;

Kwa tafsiri yangu mimi nafikiri bado Umri uchukuliwe kama ni kigezo kikubwa cha ujana;  ujana pamoja na udogo wa umri vile vile unahusisha ukakamavu, uwajibikaji wa muda mrefu hata kufikiri vizuri kwa ufasasaha kwa hiyo bado umri ni kigezo muhimu;

Kwa nini vijana wengi hutumika sana wakati wa kampeni au shughuli zote zinazohitaji utendaji imara wa muda mrefu? Kwa nini wazee wasiwe mstari wa mbele katika kampeni? Kuna tofauti kubwa kati ya mwenye umri wa miaka 45 na 70 katika kila Nyanja.  Pamoja na hoja kuwa ujana sio umri, ujana ama kijana ni upeo wa fikra pevu. Upeo wa fikra pevu ndio unaotofautisha maendeleo ndani ya nchi.

Upeo wa fikra pevu ndio utakao wafanya vijana kuwa “nguvu ya mabadiliko”. Bongo za vijana ndio chachu ya mabadiliko, na ndio chemchem ya fikra mpya na mbadala zinazotarajiwa kulitoa Taifa katika usingizi mzito wa kifikra kwa kuwa umri wao wa ujana.

Hata katika hali ya sasa ya maendeleo ya teknologia luninga, internet n.k vijana wanapata taarifa haraka, za kina na bila kuchujwa. Jambo hili limewafungua vijana kuelewa zaidi haki zao, kutambua matamanio yao na kuanza kuona kuwa na wao wanaweza kufanya vitu vinavyofanyika sehemu nyingine duniani.


·        Tatizo la mfumo wetu ni huu kwamba wazee hawa wako kwenye umri wa kustaafu lakini hawawapi vijana nafasi kwa visingizio uzoefu;

·        vijana hawana uzoefu, mtu atapataje uzoefu asipopata pa kuapitia huo uzoefu?

Kwa nini wazee wasianze kuandaa utaratibu wa kuwaandaa vijana kupata uzoefu mapema  kwa kuwaandaa katika fani za uongozi kupitia elimu na taaluma itakayowawezesha kumudu changamoto zakiuungozi bila unafiki. Pale ambapo wazee huamua kutowasaidia vijana kupata uzoefu na kuwaacha  Kujiingiza katika siasa bila elimu ya kutosha ni sawa na kujiingiza katika jambo ‘kichwakichwa’.


Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara. Kwanini viongozi wa kisiasa hawaoni haja ya kuwaendeleza kielimu vijana wanaowasafishia njia ya ushindi wao? Kwanini vijana wanabebeshwa mizogo mizito ambayo haina maslahi kwao wakati wa kampeni kwa kisingizio cha kuwa ni mkereketwa wa chama husika;
· Nafikiri kwa upepo huu vijana wanatakiwa kujitambua kuwa wao ndio kundi lenye watu  wenye nguvu na kutumia nguvu hizo ziwe na manufaa kwa jamii. 

Hebu tumwangalie  mheshimiwa Zitto Kabwe toka CHADEMA kijana msomi, mahiri wa kuzungumza na mwenye nguvu za hoja na mpigaji hodari kwa ajiri ya wananchi na maendeleo yao ndani ya Tanzania;


Ni ukweli mtupu kuwa vijana ni nguzo muhimu katika taifa letu. Hakika vijana wanaona na wanafikiri. Vijana hawa ambao wengi ni wasomi  wa hali ya Juu na hata wale wa kawaida wana uwezo wa kuchambua baina ya kauli tupu na utendaji wa kauli hizo. Vijana kama mheshimiwa Zitto Kabwe; Mheshimiwa Halima Mdee, Marehemu Amina Chifupa,  Nape Mnauye, Benno Malisa, mheshimiwa Godbless Lema, mheshimiwa January Makamba,James Mbatia, Mheshimiwa David Kafulia na wengine wengi; Naamini, endapo kweli tukiwa tunatambua nguvu, thamani na mchango wa vijana kama uliotolewa katika kipindi cha chaguzi zetu nchini,  tunaweza kuthubutu kimaendeleo kwa kuwapa nafasi za uongozi na wazee washuke katika basi la uongozi na sasa iwe zamu yao kulisukuma kutoka nje na sio ndani ;



HEBU TUWAPE NAFASI YA UONGOZI NA TUONE MAFANIKIO YAO


NUKUU ZA MWALIMU NYERERE KUHUSU KANSA YA UONGOZI TANZANIA:

·        “Viongozi wetu hivi sasa wanaogopa kutumia nguvu za hoja ili kufikia maamuzi muhimu.  Kwa sasa wanatumia hila zaidi kuliko hoja; vitisho kwao ni mbinu rahisi zaidi kuliko adha ya kutumia akili na kupata hoja safi ya kumjibu mpinzani katika mjadala “Viongozi hawa wakipewa nafasi watatumia hoja ya nguvu tu; hawatakuwa na haja ya kutumia akili.  Kichini chini baadhi yao tayari wameanza kutumia hoja ya vitisho.

·        “Kama tukiacha utamaduni wa woga ukazagaa, tutakuwa tunakaribisha udikteta. Uhuru hauji wala haudumishwi bila kuwa tayari kulipa gharama zake; na vitu vyote vyenye thamani kubwa, gharama yake ni kubwa.

Tuesday, December 13, 2011

SAKATA LA POSHO: SPIKA MAKINDA ALICHEMSHA!


Submitted by Mjengwa on 14.12.11



Ndugu zangu,

Ni dhahiri kauli ya Spika Anne Makinda kuwa wabunge wanaongezewa posho kwa vile gharama ya maisha Dodoma iko juu inaonyesha udhaifu walionao viongozi wetu wengi; kukosa uelewa wa hali halisi.

Kiukweli, kwa kauli ile, Spika Anne Makinda alichemsha.  Na ili tuelewe ni vema tukaingalia picha pana badala ya kipande cha picha. Tatizo hapa si Anne Makinda bali ni mfumo.  Ndio, Anne Makinda ni kielelezo cha tatizo la kimfumo. Kwamba mfumo wetu, mbali ya udhaifu mwingine,  unaowafanya viongozi wetu wawe ’ masultani’. Wakae kwenye nyadhifa za kisiasa na kiserikali  kwa muda mrefu sana kiasi cha kupoteza uelewa wa hali halisi za wananchi wanaowaongoza.

Kwa mfano, tangu niko shule ya msingi nimelisikia jina la Anne Makinda katika nafasi za uongozi.  Hivyo hivyo nimeyasikia majina ya akina Samwel Sitta, Malecela , Pius Msekwa na wengineo. Ndio, ni ukweli, kuwa nchi yetu ambayo asilimia kubwa ina raia vijana inaongozwa na wazee waliostahili kumpumzika na kuwaachia nafasi vijana.

Sina maana kuwa wazee hawana sifa za kuongoza, isipokuwa, tufanye sasa juhudi za makusudi za kuandaa mifumo itakayotufanya nafasi za uongozi zisishikiliwe kwa muda mrefu na watu hao hao. Tuanze sasa kufikiria kwa dhati kuandaa utaratibu wa kuwaandaa vijana ili waje kuwa viongozi bora. Vile vile, utaandae utaratibu  utakaofanya Mbunge asikae bungeni zaidi ya vipindi viwili kwa maana ya miaka kumi.

Angalia sakata hili la wabunge na posho . Kwa hakika ni moja ya mambo ya kuhuzunisha yanayotufungia mwaka. Kwamba imefika mahali wabunge wetu wamefikiria kuongezewa posho kutoka shilingi elfu sabini hadi laki mbili kwa siku, tena katika wakati huu mgumu  kiuchumi ambao mamilioni ya WaTanzania wanaupitia. Huu ni usaliti kwa nchi yetu na si kitu kingine.

Kwa Spika Anne Makinda ,  kama mwanadamu yumkini alighafirika. Ulimi hauna  mfupa na hakuna mwanadamu  asiye katika hatari ya kunena lililo baya masikioni mwa wanadamu wenzake.  Spika Makinda hajachelewa. Atoke sasa, na kwa  sauti yake mwenyewe, awaombe radhi WaTanzania. Akifanya hivyo atasamehewa. Maana atambue, ya kwamba  kuwaambia WaTanzania maisha ya Dodoma kwa Wabunge ni ya gharama ya juu  inatoa tafsiri mbaya.

 Ni kauli mbaya maana Wabunge wetu ukilinganisha na mamilioni ya WaTanzania, hata bila posho ya shilingi hamsini kwa siku, bado watakuwa na maisha ya neema kubwa kuliko wapiga kura wao wengi. Yawezekana kabisa unavyosoma  makala hii kuna mama MTanzania anayejifungua akiwa  amelala sakafuni, au kuna mtoto wa KiTanzania anayekufa kwa malaria kwa vile zahati haina dawa. Ndio hali halisi. Huu ni wakati kwa viongozi wetu kuacha kuendekeza ubinafsi.

Viongozi wakiwamo Wabunge waanze sasa kuwafikiria wananchi ambao wengi wako katika hali mbaya kiuchumi. Ni wananchi hawa ambao miongoni mwao kuna wakulima. Ni wakulima hawa ambao posho ya laki mbili kwa siku kwa mbunge ingetosha kwa mkulima huyu kununua mbolea mifuko mitatu ya kilo hamsini  kwa mfuko. Ni mbolea ya kupandia na kukuzuia kwa ekari moja. Tujiulize; tuko sasa kwenye ” Kilimo Kwanza au Wabunge Kwanza?”


Ndugu zangu, hii ni sehemu ya makala yangu ya juma hili kwenye gazeti la Raia Mwema. Nahitimisha.

Maggid,
Iringa.
Jumatano, Novemba 14, 2011



Habari hii kwa hisani ya Mjengwablogspot.com

MANUNG’UNIKO YA ONGEZEKO LA POSHO ZA WABUNGE TANZANIA.




BADO TUNAHITAJI BUSARA ZAIDI KATIKA MAAMUZI YETU KULINGANA NA HALI YETU YA UCHUMI;
  • ·“Siasa si mchezo mchafu, ila wachezaji wake ndiyo wachafu.”
  • ·      Je bunge letu linapofanya maaumuzi ya liko kwenye dhana ya “wao” na “sisi”
  •  Ni kweli kuwa  Siasa hutafasiriwa kuwa ni fikra, busara na mipango ya kuendesha nchi au ya kujinufaisha wao wenyewe?
  • ·        Litakuwa ni jambo la kuheshimiwa kwa viongozi wetu kama Waheshimiwa Wabunge wetu watakuwa wakweli na wenye Uzalendo wa kweli ndani ya mioyo kwa faida ya wananchi wao.

·   Confucius aliwahi sema kuwa  ‘Utajiri na vyeo ndivyo vitu ambavyo kila bianadamu anavitamani; lakini ikiwa njia ya kuvipata ni kwa kwenda kinyume na misingi yake, anapaswa ajiepushe navyo.’

· Rudolph Giuliani aliwahi sema kuwa ‘Kiongozi huchaguliwa kwa kuwa yeyote anayemuweka pale huwa anaamini maamuzi, tabia na uwezo wa maarifa yake – siyo ujuzi wa kufuata maoni. Ni wajibu wa kiongozi kuchukua hatua kufuatana na sifa hizo.’

·        “kiongozi ajiulize ni vipi atalitumikia Taifa na si Taifa kumtumikia yeye Kiongozi Umashuhuri na uzuri wa Kiongozi unatokana na hekima, busara, uchapakazi, ufanisi, ufuatiliaji, uimara, uungwana, uwajibikaji na unyenyekevu wake. Ama fikra endelevu na upeo wa kuongoza ni muhimu na si kauli tamu za kuwafurahisha viongozi wengine”

· Tamaa ya kujilimbikizia mali huo ni udhaifu wa mwanadamu ambao hapaswi kuupa nafasi iwapo unazingatia uadilifu wa uongozi

Demokrasia kama falsafa ya Plato ambayo inahusiana na uendeshaji wa shughuli za kisiasa inalenga zaidi katika  utumishi kwa umma na uendeshaji wa jamii na taifa. Wananchi wote hawawezi ongoza nchi kwa mara moja; Katika msingi huu wananchi kutokana na wingi wao waliridhika itakuwa sio rahisi kwa wao wote kukutana, kufanya maamuzi na kuyasimamia moja kwa moja maamuzi hayo yanayowahusu wao kama jamii; dhana ya kuwachagua viongozi wachache huzaliwa kwa chimbuko hili na kuruhusiwa kuunda serikali.


Tatizo kubwa tulilonalo kama Taifa ni ufinyu wa viongozi bora na utashi binafsi wa wachache walio katika nyanja za uongozi kwa kukosa sifa muhimu kwa viongozi. Kwani inatupasa kutambua kuwa uongozi si lelemama, ni kipaji na ni kazi ngumu. Lakini ridhaa hiyo haitolewi hivi hivi tu, inaambatana na amana, kwamba waongozi watatekeleza dhamana  na wajibu  wao kwa makubaliano na maelewano ya kufuata barabara na kuheshimu ipasavyo kanuni na maadili fulani yanayoitambulisha na kuiongoza jamii husika. 

Kwa kauli zinazotofautiana na misimamo inayotofautiana kuhusu ongezeko la Posho za waheshimiwa Wabunge hivi karibuni, tunapo yakidirifu  maisha ya kila siku ya wanasiasa ataiona siasa imejikita katika kukimbilia na kupigania nafasi, fursa na ushawishi kwa malengo ya kujilimbikizia utajiri binafsi kwa wengi ; ikumbukwe kuwa kiongozi muadilifu hakubali kufuata  au kutoa maamuzi bila kufanya ukadirifu wa hoja na hali husika. Uongozi ni kujitolea na kuweka matwakwa na maslahi ya wengine kuwa mstari wa mbele na si matakwa binafsi na kujinufaisha. Marehemu John Kennedy rais wa Marekani alitoa kauli moja maarufu iliyosema kuwa. Tuchague viongozi si kwa kuangalia vyama au sura, bali tuangalie uwezo wao wa kuongoza, kuhamasisha na kufanya kazi. Tupime kauli zao na matokeo ya kazi zao kama wanavyojinadi.


Serikali ni watu, inaundwa na watu tuliowachagua na tunawapa watu hawa na Serikali mamlaka makubwa ya kutuongoza, kupanga na kulinda Taifa na Katiba yetu. Dhamana hii imefanywa kwa kuaminiana kuwa Serikali itafanya kazi kwa manufaa ya Wananchi wake na kwa matakwa na utashi wa Wananchi wake.

Maaumuzi ya ongezeko la Posho kama kweli yamepata Baraka zote za serikali basi tujue wazi kuwa uamuzi huu haujezingatia mazingira ya Taifa letu, na uwezo wetu wa kifedha kwa wakati huu. Maaumuzi ya Bunge na kwa wabunge kuridhia kupokea posho hizo kunawafanya wananchi wajiulize maswali mengi  

· Kuna amani gani na utulivu gani katika nchi yetu wakati mioyo yetu sisi kama wananchi imevimba kwa kujaa hasira za ubinafsi?

·    Je mwananchi wana nafasi gani katika kuiendesha nchi hii? Wasubiri kuongozwa tu. Mawazo ya wabunge  ndiyo maoni yao?

Mheshimiwa Rais, busara yako inahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote kwa kuangalia hali halisi ya maisha ya mwananchi wa kawaida na mateso ya hali ngumu inayomzunguka, pengine ile aliyoisema Mheshimiwa Spika wa Bunge letu kuhusu hali ngumu ya maisha ya wabunge wetu sio kitu. busara yako Mheshimiwa Rais inahitajika sasa kuliko wakati mwingine wowote ili kudumisha amani na utulivu wa kweli


Kama ilivyo kwa umoja wa kitaifa, kiongozi muadilifu pia hufanya kila bidii kuhakikisha amani na utulivu wa kweli katika nchi vinapatikana. Amani na utulivu ni chachu ya wananchi kwa kushirikiana na Serikali yao kujiletea maendeleo. Maendeleo hayaji mahala penye magomvi na hasama. Lakini na amani na utulivu pia haviji mahala pasipo na haki na uadilifu. Uvunjifu wa amani na utulivu wa nchi hupelekea hasara ya maisha na mali ya watu na hayo hayawi malengo ya uongozi muadilifu katika nchi

Uadilifu wa uongozi unadai kuheshimu nguvu ya hoja na fikra bora na hayo yanaweza kupatikana tu iwapo nchi inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia. Hivyo, katika kutoa uongozi sahihi, kwa kuzingatia maslahi bora ya nchi na watu wake, haki, uadilifu, umoja, amani na utulivu, hapana budi kwa kiongozi kuiamini, kuiheshimu na kuifuata barabara misingi ya kidemokrasia.

Bado binadamu si mkamilifu na kwa vyovyote vile hufikia mahala akafanya maamuzi ambayo si sahihi hata kama yalifanywa kwa nia njema na kwa kuzingatia taarifa zilizopatikana wakati maamuzi hayo yanafanywa. Hayo yanaeleweka na kiongozi muadilifu anapaswa kuyakubali na kuliomba radhi Taifa. Hiki ndiyo kilele na kigezo kikuu cha uadilifu wa uongozi katika siasa. Kukubali kubeba dhamana kwa madhara yaliyotokana na maamuzi yako au yaliyofanywa kwa jina lako.

Maamuzi ya kiongozi wa kisiasa huathiri taifa zima, busara na hekima huzaa maamuzi yanayotokana na tafakuri ya kina, yanayozingatia hali halisi ya mambo na maslahi na manufaa ya muda mrefu. Kiongozi muadilifu anatakiwa ayaone haya na ayazigatie kwa kila hatua anayochukua. Kama viongozi wetu wa bunge wakikiri kuwa walikurupuka katika kufanya maamuzi hayo bila kuyafanyia kazi vizuri heshima na uwajibikaji wa kuliendesha bunge letu itarudi. Tukubali tu kuwa njia ya kusonga mbele ni kukubali kutofautiana katika fikra lakini tubaki kuwa wamoja.

Mheshimiwa Spika ni ukweli ambao haufichiki kuwa kwa sasa wananchi ndio wenye maisha magumu kuliko wabunge unaowatetea.