BUSARA ALIYOIONYESHA MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE YA
KUANZA KUKUTANA NA VYAMA VYA UPINZANI KUJADILI MCHAKATO WA KATIBA MPYA
TUMEzIPOKEA KWA FURAHA KUBWA;
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumanne, Novemba 29, 2011, ametia saini
Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011. Hatua hiyo ya
Mheshimiwa Rais kutia saini Muswada huo inakamilisha safari ya kutungwa kwa
Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 baada ya Bunge kuwa limepitisha
Muswada huo uliowasilishwa na Serikali katika kikao kilichopita cha Bunge. Aidha,
kutiwa saini kwa Muswada huo ili uwe Sheria ni hatua kubwa na muhimu katika
safari ya kutungwa kwa Katiba mpya ya Tanzania kama ilivyoahidiwa na Mheshimiwa
Rais Kikwete katika salamu zake za Mwaka Mpya kwa wananchi Desemba 31, mwaka
jana, 2010.”
Kama taifa inatupasa
kukumbuka kuwa mabadiliko ya katiba ni
madai ya msingi na matakwa ya lazima kama nchi hii inataka kujenga na kudumisha
amani ya kweli na kuleta maendeleo kwa watu wake; wazo la serikali na vyama vya
siasa na zsasi zingine zinazojishughulisha na sheria ni msingi kuendelea kutambuka kuwa Safari hii ya utungaji wa katiba ni ya Muhimu sana ;
hivyo ni wajaibu wao kuhakikisha kuwa
wananchi waweze kujua zaidi kuhusu katiba, wawe tayari kutoa mawazo ili tume au
kamati itakapowatembelea wawe na kitu cha kusema, watakapoachwa hivi hivi
hawatakuwa na cha kuzungumza; je vyama na asasi kwa sasa hivi zimeandaa mkakati
gani wa kuwaelimisha wananchi kuhusu umuhimu wa kuchangia maoni; tatizo
nilionalo kama vyama vitaendelea kulumbana vyenyewe vuifahamu kuwa havina
nafasi ya kumsaidia mwananchi wa katika kujinasua katika hali duni kwani katiba
na utungaji wake itabakia kwa wanansiasa, wasomi na wanjanja wachache.
Tukiangalia wenzetu kama
Marekani pamoja na uwezo wao na maendeleo yao bado Katiba ni chombo cha
wananchi na sio chombo cha chama Fulani, na katiba yao imejengwa katika
msingi mkubwa sana wa uhuru ambao umewekwa katika katiba yao.
Jukumu la wanasiasa
kuwaelimisha wananchi kuhusu marekebesho ya
kutungwa kwa katiba mpya ni la muhimu sana kwani wananchi wengi hawajui katiba ya zamani inamabo gani ni ina
matatizo gani, hivyo wasipoelimishwa hata mabadiliko yanayokusudiwa hayatakuwa
na msisimko wowote kwao na itabaki tu kuwa je watawezaje kutoa maoni ya katiba mpya wakati hawajui mapungufu amabayo yamo katika katiba
iliyotumika kwa ktakribani miaka hamsini sasa.
Kwa serikali vyama vya
siasa, vyama vya upinzani na Asasi zinazojihusiha na maswala ya katiba,
tunaviomba sana katika mchakato huu mzima wa uandikaji wa katiba mpya vitumie nafasi hii vizuri kwa kujadiliana juu
ya Katiba mpya, kwa kudumisha utamaduni wa kuvumilia maoni yanayotofautiana,
sambamba na kuwa na mtazamo chanya na kutanguliza taswira nzuri ya Taifa kwa
masilaha ya wananchi wote, vijana, akina mama, wanaume, wazee, matahira na
wengineo wote, kwa maana ndiyo inayosimamia maisha yao.
Nakumbuka Profesa Shivji katika moja ya mikutano ya
changamoto ya katiba mpya ya Tanzania aliwahi sema kuwa “mchakato wa upatikanaji wa kabisa mpya ni
fursa muhimu ya kurejesha mwafaka kwa majadiliano kuliko ilivyo sasa ambako
kuna kila dalili za kuelekea katika magomvi na mapambano”
Kwa maneno mengine
Professor Shivji anatukumbusha kuwa
Katiba inatakiwa Ni ya wananchi, ndio
wananchi lazima wawe wenye uamuzi wa aina ya serikali wanayotaka
kuwa nayo na inawaongozaje, wananchi ndio msingi wa madaraka yote nchini. Kwa
maneno mengine Katiba inatakiwa itoke kwa wananchi. Siyo katika kuipigia kura
tu bali katika uandikaji wake. Katiba ambayo haitoki kwa wananchi na haiweki
ushiriki wa juu kabisa wa wananchi kutoka mwanzo haiwezi kudai kuwa ni katiba
ya wananchi hao.
Kwa mtazamo wangu na wengine wengi ambao sio
wanansiasa au wasomi tunatamani kuwa Katiba
Mpya iwe ni kumbu kumbu endelevu na kwamba, kasoro zilizojitokeza kiasi cha
kutibua mori na hali ya watanzania, iwe ni changamoto ya kuwa makini zaidi
katika mchakato mzima wa uandikaji wa Katiba Mpya, mzaha wowote unaweza
kulitumbukiza Taifa katika maafa makubwa lazima usipewe nafasi kwani tunatamani
katiba yetu iwe kama ile ya Merakani ambayo imesimama na inatekelezeka.
Kama Mwalimu Nyerere
alivyowahi sema katika moja ya mikutano yake kuwa Katiba ni sheriamama, iguse msingi wa mambo
makuu yatakayoongoza sheria, sera na mifumo ya kitaifa. Hii ni dhamana nyeti
inayopaswa kuwashirikisha wataalam kutoka katika medani mbali mbali za maisha
nchini Tanzania. Wanasiasa waepuke kishawishi cha kudhani kwamba, wao ndio
wanaopaswa kusimamia na kuongoza mchakato huu, wajitahidi kushiriki kama
watanzania wengine kwa kuchangia mawazo yao
Katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba tuzingatie,
· Tunaomba Busara na hekima za Rais wetu zitumike sana wakati
huu;
· Katiba Mpya inapaswa kuwa ni mali ya
watanzania wote kwa kuwa mchakato mzima unawashirikisha watanzania wengi zaidi
kwa njia ya moja kwa moja au uwakilishi wao. Chombo kitakachopewa dhamana ya
kusimamia kuandika Katiba Mpya, kwanza kabisa kikubalike na watanzania wengie,
hii itakuwa ni hatua kubwa hata kuweza kuridhia kile kitakachoandikwa. Miongozo
itolewe katika lugha inayoeleweka na fasaha ili kuwa na tafsiri sahihi na
rahisi kwa watanzania wa kawaida kabisa
·
Washauri wa mheshimiwa Rais tunawaomba
wamshauri Mkuu wetu wa nchi kwa masilahi ya Taifa na sio vinginevyo
wakizingatia kuwa serikali yetu kwa hivi sasa inaingia katika kipindi muhimu
sana cha kulipitisha Taifa letu katika wakati huu kwa maendeleo ya wananchi
wote na sio kikundi kidogo cha watu;
· Katiba yetu ikamilishwe kutungwa kwa
majadiliano na makubaliano ya umoja wa kitaifa na sio kwa vitisho vya Migomo na
maandamano na shinikizo la vyama kwa masilahi binafsi.
· ili kupata Katiba makini inayozingatia
mafao ya wengi kuna haja kwanza kabisa kuwa na utulivu wa kimawazo, busara na
hekima vitumike zaidi, kwa kuzingatia umoja wa kitaifa na upendo kati ya watu.
Masilahi ya taifa yapewe kipaumbele cha kwanza na kamwe ubinafsi usiruhusiwe
kutawala zoezi nyeti kama hili.
·
Ebu tuache malumbano wakati huu ni mzuri kwa vyama vya
siasa tanaznia pamoja asasi zanazojishughulisha
na mambo ya sheria kutumia muda huu kuwafundisha
wananchi katiba ya zamani na waone hayo mapungufu
yake halafu wapate kutoa maoni yanayolingana
na mahitaji yao na sio kufuata mkumbu wa mahitaji ya wanasiasa kama
inavyoendeleahivi sasa;
HITIMISHO;
Kwa msingi huu vyama vyote
yaani CCM, CHADEMA, CUF, NCCR, TLP na
Vyama vingine vya siasa vikumbuke kuwa “Katiba ya nchi si mali ya chama au mtu
binafsi na wala si mali ya kiongozi fulani, ni mali ya watu wote raia wa
Tanzania na wala katiba isipatikane kwa shinikizo la kukundi chochote cha watu”
kama Dk Salim Ahamed
Salim aliwahi sema kuwa “Chama tawala na chama kikuu cha upinzani
vijue tunaangalia mustakhabali wa taifa letu, lazima uelewano uwepo malumbano
si mazuri japokuwa ni sehemu ya siasa, lakini akaonya kwamba yasiruhusiwe
yakasababisha nchi ikafika pabaya. Ninachoomba chama tawala na Chadema
wafikirie mwafaka na kuangalia mustakhabali wa taifa, kama hakuna maafikiano si
jambo zuri kwa taifaKwa hali ya kisiasa hivi sasa ni lazima mjadala uwe wa nia
njema lengo ni kuendeleza makubaliano na si kuhitilafiana. Tujenge na kuimarisha
undugu na mishikamano wetu na kuonyesha uzalendo na uongozi madhubuti wa taifa
letu,”
kwa hiyo tunavyoelekea
kupata katiba mpyaa ifikapo mwaka 2015 kama serikali ilivyohaidi, Tanzania kama
nchi ambayo imeingia katika mfumo wa vyama vingi miaka ya 90, inahitaji
mabadiliko au katiba mpya yenye misingi YA UPANA NA UWAZI WA DEMOKRASIA na
misingi mipya ya kuongoza vyama vingi na mawazo mapya ya Jamii kwa msingi huu
kama sisi kama Taifa tutafanikiwa kupata katiba mpya basi tukakuwa tumejijengea katiba iwapo vile vile tutaweza kujumuisha kwenye
uandikaji wa katiba mpya kwa maoni ya wananchi hapo tutakuwa tumejijengea Utawala wa Demokrasia ya umma.
Tunaendelea kumpongeza
mheshimiwa Rais kwa busara yake ya kuanza kukutana na vyama vya upinzani
CHADEMA, katika kufikia muafaka na kushauriana katika kuboresha uandikaji wa
katiba mpya; tunamwomba mheshimiwa Rais aendelee kukutana na wale wote wenye
nia njema, katika kuboresha katiba yetu mpya;
MUNGU IBARIKI
TANZANIA KATIKA MAANDALIZI YA KATIBA MPYA