WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Sunday, March 25, 2012

SENSA KWA MAENDELEO YA TAIFA


JE TAIFA LINANUFAIKA VIPI NA SENSA KILA MIAKA KUMI (10)?

Sensa inatumika kutoa habari za hesabu (takwimu) kuhusu watu wote wanokaakatika nchi husika.Habari hizi zinatumika na serikali, mikoa na tawala za mitaa, biashara na jumuia za mahali na nyinginezo kusaidia katika kufanya maamuzi kuhusu mipango ya elimu, afya, kazi, usafiri na hudumu nyingine nyingi.

Kama viongozi wahusika wa kuendesha shughuli nzima ya senza wanavyotuambia kuwa  “Msisitizo wa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu ni kutoa kiunzi na miongozo ya kujumuisha vigezo  vya idadi ya watu katika mchakato wa maendeleo ili, hatimaye, mienendo ya idadi ya watu iwiane na mienendo mingine ya kijamii na kiuchumi”.

Kwa maneno mengine Sensa ni utaratibu wa kupata na kurekodi habari kuhusu idadi ya watu fulanifulani. Ni utaratibu wa mara kwa mara na hesabu rasmi ya idadi ya watu hao.


Swali la msingi hapa ni hili?

Je ni kweli kuwa  Vilevile, sera hii ilitoa miongozo itaskayo  weza kutoa  vipaumbele katika programu ya idadi ya watu na maendeleo?

Je  senza ikifanywa vizuri inaweza kuharakisha na kufikia maendeleo endelevu na usawa wa  ndani ya jamii?

Ukweli utabaki pale pale kuwa Takwimu hizi  kweli zititafutwa na kuzingatiwa zitatusaidia sana katika kupanga maendeleo ndani ya jamii jamii zetu? Ni dhahiri kuwa takwimu hizi zinaonesha uwiano wa idadi ya watu ndani ya jamii zetu hasa katika huduma muhimu zinazotuzunguka, kama vile  huduma ya hospitali zilizopo nchini. 

Je sensa ni chanzo cha maisha bora?

  • Nia ni kuisadia Serikali ili iweze kupanga mipango ya maendeleo na kutunga Sheria, na kuandaa Sera kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu wake kwa kutumia takwimu sahihi.

  • Pia husaidia katika kutoa mwelekeo wa siku zijazo yaani 'forecasting'.

  • Maendeleo endelevu na kuondoa umaskini

  • Kuongeza na kuboresha upatikanaji na ufikiaji wa huduma bora za kijamii

  • Kuwa na mgaosawa, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, haki ya kijamii na maendeleo kwa watu wote

  • Mpangilio mzuri  baina ya idadi ya watu, matumizi ya rasilimali na mazingira

Lengo kuu la Sera ya idadi ya watu ni kuiwezesha Tanzania kufikia kiwango cha maisha kilichoboreshwa na kufanikisha ubora wa maisha ya watu wake. Vipengele muhimu vya ubora wa maisha ni pamoja na afya na elimu bora; chakula cha kutosha na makazi bora mazingira imara; mgaosawa; ubora wa kijinsia, na usalama wa watu binafsi. Aidha,  Sera ina lengo la kuelekeza ubunifu wa Sera za Kisekta, na mikakati na mipango mingine inayohakikisha maendeleo ya watu. Malengo mahsusi ya sera hii ni kufanikisha  yafuatayo.

Sasa nini tuzingatie kuelekea katika kipindi cha sense 2012?

Inafahamika kuwa sense ni swala la kimataifa kwani katika kila nchi zoezi hili hufanyika kwa umakini kwa mbinu tofauti kulingana na level ya uchumi ambayo nchi husika wamefikia:  kwa hiyo watafiti wote duniani hutumia takwimu zilizofanyika nyuma na kueleza ni nini kifanyike kuboresha zaidi huduma au kukuza uchumi wa nchi kwa manufaa ya umma. Hakuna nchi duniani ambayo haitumii takwimu za nyuma kwa ajili ya kujipima kimaendeleo.  Kitaalamu hakuna takwimu ambazo zinapitwa na wakati.  

Sera inatoa miongozo ya kushughulikia masuala ya idadi ya watu kwa namna jumuishi. Hivyo, inatambua mahusiano baina ya mienendo ya idadi ya watu na ubora wa maisha kwa upande mmoja na ulinzi wa mazingira na maendeleo endelevu kwa upande mwingine. Utekelezaji wake utatoa upeo mpya kwa programu za maendeleo kwa kuhakikisha kwamba masuala ya idadi ya watu yanashughulikiwa kikamilifu

Sensa italenga katikakulenga kujua umaskini wa kipato cha mtu mmoja na idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi. Itasaidia Serikali kwenye mipango yake mbalimbali, ikiwamo kutathmini Mpango wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKKUTA) na MKUZA, Zanzibar.

Je ni kweli sababu ambazo serikali kuhusu maazimio ya sensa zinakidhi haja?

Sense ikitumika vizuri kwa kuangalia uwiano wa  idadi ya watu vinaathiri maendeleo na ustawi wa mtu mmoja mmoja, familia, jumuiya katika ngazi ndogo na katika ngazi ya wilaya, mkoa na taifa zima katika ngazi ya jumla. Athari na miitikio ya shinikizo la idadi ya watu zinahusiana katika ngazi zote.

Je sababu ambazo zinaelezwa kuhusu  umuhimu wa sensa katika nchi yetu unaendana na lengo lake; 

Kuna baadhi ya wanaharakati wanaoona kuwa “Sababu zinazotolewa na Serikali kuwa zitasaidia kufanya maamuzi sahihi si kweli, kwani Sensa nne zishafanywa na hakuna maamuzi yalofanywa kwa kuzingatia hizo Takwimu za Sensa. Kama madawati hayatoshi, Mikopo kwa wanafunzi haitoshi, Madawa Hakuna, Mahospitali hayatoshi, Miundombinu karibia yote haiendani na idadi yetu. Nadhan serikali ingejikita zaidi kutafuta vyanzo vya mapato badala ya kuchezea mapato kwa miradi isiyo na tija”.

“Jambo ambalo ni changamoto kwetu ni hoja ya kwamba, pamoja na jitihada hizo, taasisi za tafiti hazijaleta matumaini makubwa hususan upande wa uchumi… miongoni mwa sababu zinazochangia kutopungua kwa umaskini wa wananchi wengi ni pamoja na kasi kubwa ya ongezeko la idadi ya watu ambalo haliendani na kiwango cha ukuaji wa uchumi,”

Je sensa inasaidiaje na tatizo wa watu kuhamia mijini?

Kuongezeka kwa watu mijini ambako kunasababishwa na wengi wao kuhama kutoka vijijini, kunaathiri shughuli za uzalishaji za kilimo katika maeneo ya vijijini na hivyo kupunguza kipato na hatimaye kuongeza umaskini kwa wananchi wa vijijini,”

Msongamano wa watu na magari mijini, shida ya maji na miundombinu ya barabara na maji ni ushahidi tosha kwamba idadi ya watu haiendani na ongezeko la kukua kwa uchumi na huduma nyingine za kijamii.

Je takwimu zinazopatikani  kweli ni sahii kwa asilimia 100 au zina mapungufu mengi?
 
kama mtaalam mmoja wa sense alivyo wahi sema “tulipata shida sana kupata takwimu sahihi za walemavu wa ngozi wakati ule kulikuwa na mauaji makubwa ya ndugu zetu hawa, ilibidi tutume watu wakawahesabu lakini bado kulikuwa na changamoto kubwa”.
Changamoto nyingine inayowakabili wataalamu hao wa kutenga maeneo ni pamoja na baadhi ya maeneo kutofikika kwa urahisi kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo miundombinu duni ya barabara, baadhi ya maeneo kuwa misitu minene yenye wanyama wakali pamoja na miinuko mikali na mabonde katika maeneo mbalimbali hali inayowafanya wataalamu hawa kufika kwa taabu katika maeneo hayo ili kupata vipimo sahihi.

Kutokana na utaratibu wa kufanya kazi kwa kuchelewa na kwa kukosa uthubutu hupelekea kushindwa kufanya kazi zao  mapema kwa kuwa na maandalizi yatasaidia kufanya kazi zao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuepuka zima moto ilimradi kazi imalizike na kukosa takwimu sahihi kwa wakati muafaka.

  • Je changamoto ya nyumba zakulala wageni au nyumba za makaazi zinazokaliwa na watu wengi wakati wa sensa   zinahesabiwa vipi? mathalani  nyumba moja kuwa na wapangaji wengi, kunasababisha viongozi wa eneo husika, kutojua idadi ya kaya zilizopo katika eneo husika.

Usahuri wa kawaida tu kama Taifa lazima tuhakikishe kuwa idadi ya watu itakayo patikana mwaka huu igeuke kuwa changamoto ya maendeleo na  kuwahakikishia wananchi wanapata maisha bora; Tusigeuze Sensa kuwa Mradi wa kujinufaisha tu

Lazima tujenge uadilifu katika kufanya kazi hii kwani ni kazi ambayo ni nyeti kwani wataalamu wetu wa kuhesabu watu wanaweza tu kuamua kuto kwenda kijiji fualani kutokana na tatizo la suafiri;

Tuhakikishe kuwa wote watakao husika katika zoezi hili serikali tunaiomba ijitahidi kuwahudumia  stahiki zao wasitumie kizingizio au kujenga kiburi cha kushindwa kufanya kazii zao kwa umakini kwa sababu Fulani ambyo inaweza kushughulikiwa;
Kwa naman yeyote ile sense ni muhimu toka enzi za babu bau zetu kama nukuu hii inavyoonyesha;

  • Je taarifa za sensa zinakusidiwa vile vile kutumika kwa kazi nyingine zinazolenga manufaa Chanya wa ukuaji wa Taifa?

Wakati sensa hutoa njia muhimu ya kupata taarifa za takwimu kuhusu idadi ya watu, habari hii wakati mwingine husababisha dhuluma, kisiasa au vinginevyo, ikiwezeshwa kwa kuunganisha utambulisho wa kibinafsi na takwimu za faragha

Hitimisho

Ni ukweli ambao lazima tuukubali kuwa  pamoja na juhudi kubwa, Ofisi ya Sensa haijawahi kuwa na uwezo wa kuhesabu kila mtu binafsi, kupelekea utata kuhusu kama kutumia takwimu mbinu ili kuongeza idadi kwa baadhi ya makusudi, kama vile hoja juu ya jinsi ya kuboresha ukusanyaji wa zoezi nzima kwa malengo yalikusudiwa kimaendeleo. Nahitimisha kwa kujiuliza maswali yafuatayo: 

  • Je katika hali hii taifa lifanye nini? 

  • Je matatizo ya kushindwa kuboresha maisha bora ya mtanzania chanzo na ukosekanaji wa takwimu sahihi za idadi ya watu? 

  • Je kutokana na ukosefu wa taarifa sahii watendaji wanatumia mwanya huo kujinufaisha wakitumia udhaifu wa ukusanyaji takwimu?

Tuesday, March 20, 2012

Mwakyembe Atinga Kazini

Dk Mwakyembe Aweka Hadharani Ugonjwa Wake





Naibu Waziri wa Ujenzi Dk. Harrison Mwakyembe, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, muda mfupi baada ya kuingia ofisini humo kuanza kazi, kutokana na afya yake kuimarika. Mwakyembe amekuwa akitibiwa nchini India kwa muda mrefu. Picha na Zacharia Osanga
 
BAADA ya utata wa muda mrefu wa ama Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe amelishwa sumu au la, jana Mbunge huyo wa Kyela, aliweka hadharani ugonjwa wake akisema unafahamika kitaalamu kwa jina la Popular Scleroderma huku akisisitiza: “Sasa nimepona kabisa.”Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo mwaka jana yalizidi kumtikisa na Oktoba 9, Serikali iliamua kumpeleka Hospitali ya Appolo, India kwa ajili ya matibabu na uchunguzi zaidi.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Dk Mwakyembe akiwa amevalia kofia ya pama alisema: “Si kwamba sijambo, bali nimepona kabisa baada ya kugundulika na maradhi hayo na kutibiwa.”“Nimerudi juzi kutoka India na daktari wangu ameniambia nimepona, nilikuwa nasumbuliwa na maradhi ya ‘Popular Scleroderma’ iliyosababisha ‘skin disorder’ (ngozi kutokuwa katika hali ya kawaida), lakini kwa nguvu za Mungu nimepona, namshukuru Mungu.”Kuhusu sumu
 
Alipoulizwa kuhusu tuhuma za kulishwa sumu, Dk Mwakyembe alikataa kuzungumzia hilo akisema anasubiri uchunguzi ulioagizwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha.Hata hivyo, Dk Mwakyembe alisema angependa kuona uchunguzi huo unakamilika haraka na ripoti yake inatangazwa kwa umma.Alisema yuko tayari na anasubiri tume hiyo ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri Nahodha imhoji ili atoa kile kilichomo katika ripoti ya daktari wake.Dk Mwakyembe alisema anachoshukuru hadi sasa ni kwamba afya yake imeimarika kutokana na shinikizo la Rais Jakaya Kikwete ambaye aliagiza Serikali kumpa kipaumbele wakati wote akiwa nchini na India hatua ambayo imemwezesha kufika hapo alipo.Kutokana na hali hiyo, Dk Mwakyembe aliwataka wananchi wote wakiwemo wa jimboni kwake Kyela kuondoa wasiwasi akisema sasa yupo imara kwa ajili ya ujenzi wa majukumu ya taifa.“Ninaomba wapiga kura wangu wa Kyela waache jazba, wawe na subira juu ya matatizo yangu. Wiki ijayo nitakwenda kuzungumza nao ili niweze kuwaeleza matatizo yaliyokuwa yananisumbua, lakini sasa hivi niko fit,” alisema.
 
SOMA ZAIDI:http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/21277-dk-mwakyembe-aweka-hadharani-ugonjwa-wake
Picha na habari kwa hisani ya Mjengwa blog

Neno La Leo: Wiki Ya Maji Na Helikopta Arumeru!



Ndugu zangu, 
Nchi yetu inaingia  gharama zisizo za lazima kama ambazo nchi inaingia kwa sasa kwa wagombea,  vyama  na hata Serikali kutumia fedha nyingi katika chaguzi ndogo. Tumeona hata helikopta zenye gharama nyingi zikiruka kilomita nyingi angani eti kwenye harakati za kusaka kura  kwenye chaguzi ndogo huku wananchi wengi wa jimbo husika wakitembea kilomita nyingi kusaka maji ya kunywa na kupikia. 

Wiki kama hii ya Maji inayoendelea sasa ilipaswa kuwa wiki ya kuomboleza uhaba wa maji unaochangiwa pia na matumizi mabaya ya rasilimali za wananchi kama haya ya kuendesha chaguzi ndogo kule Arumeru Mashariki. Na hili ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa,
Iringa.

Sunday, March 18, 2012

Neno La Leo: Mungu Hahusiki Na Umasikini Wako!


Ndugu zangu, 

Matatizo yetu mengi yanatokana na sisi wenyewe. Wenzetu Ulaya na Marekani wanasema; “Time is Money”. Kwa tafsiri ya moja kwa moja, unamaanisha kwamba muda ni pesa. Lakini, tafsiri sahihi hapo ni umuhimu wa muda.

Kwamba muda ni kitu cha thamani sana. Na hakika, kwa mwanadamu, jinsi unavyoutumia muda wako hivi leo ni ishara tosha ya jinsi kesho yako itakavyokuwa.

Tumekuwa watu wa kulalamika sana. Na tumemwachia Mungu jukumu la kutukomboa kutoka kwenye umasikini wetu. Hapana, Mungu hausiki na umasikini wako. Jukumu la kwanza la kujikomboa kutoka kwenye umasikini ni lako mwenyewe. Na hakuna njia ya mkato, bali ni kufanya kazi, kufanya kazi na kufanya kazi. Achana na ndoto za kuamka na kuvuna mamilioni. Bila kufanya kazi!
Inakuwaje basi kwa  mwanadamu mmoja awe na muda na mwingine asiwe nao?
Kuwa au kutokuwa na muda inatokana na mipangalio yako ya maisha. Binadamu unapaswa kuwa na bajeti ya muda wako. Ni jinsi unavyoutumia muda wako.  Jinsi unavyopangilia mambo yako, ratiba zako na mengineyo.
Ukiwa na utaratibu huo, basi, waweza kabisa kuwa na muda wa kutosha kufanya mambo mengine mengi uyapendayo ikiwemo mapumziko, kuwa na muda na familia yako, kuwa na muda wa kujisomea na mengineyo.
Ndio, lililo muhimu ni kuwa na vipaumbele. Unapoandika orodha ya shughuli zako za siku, juma, mwezi na hata mwaka, basi weka kipaumbele katika mambo ambayo ni muhimu zaidi. Hayo yaweke juu kabisa katika orodha yako. Kipaumbele kinaweza kutokana na umuhimu wako binafsi kwa jambo fulani.
Usiwe mtu unayesukuma mambo mbele. Mtu mwenye hulka ya kuahirisha mambo. Linalowezekana kufanyika lifanye. Kauli za ’ hili nalifanya kesho’ au ’ namwachia Mungu,’ ni kauli za mtu aliyekata tamaa kwenye mapambano ya maisha.
Wahenga walinena; ’’Linalowezekana leo lisingoje kesho!’’ Hulka ya kusukumia mbele mambo ina tafsiri moja tu; kuwa unaongeza mzigo wa mambo ya kufanya. Huna unachokipunguza. Ni mwanzo wa kupatwa na msongo (stress). Ni mwanzo wa kuchanganyikiwa. Ndipo hapo utamwona mwanadamu mwenzako akitembea huku akiongea peke yake.
Ni muhimu pia kuwa na muda na marafiki. Naam, weka bajeti ya muda. Okoa muda upate muda wa ziada. Na baadhi ya marafiki zako waweza kuwa sababu ya matumizi mabaya ya muda wako. Ndio, marafiki wengine ni marafiki wa kukupotezea muda tu. Angalia, ni marafiki wa aina gani ulio nao.
Inasemwa, ukitaka kumfahamu mtu alivyo, basi, angalia aina ya marafiki zake. Kwa mfano kama una rafiki ambaye hazingatii muda, hana miadi ya uhakika, basi,  huyo anaweza kuwa mzigo katika suala zima la matumizi ya muda.
Usiwe mtu mwenye kufuata mkumbo, eti kwa vile wengine hawazingatii muda, basi, na wewe unajifanya ni mtu usiyejali muda. Hapo utakuwa unajipoteza mwenyewe. Ni muhimu, hata unapokuwa na marafiki zako, uwe mbele katika kuhakikisha mnatumia muda wenu vizuri.

Uwe tayari na mipango kichwani hata kabla hujakutana na rafiki au marafiki zako. Kisha mshirikishe rafiki au marafiki zako katika mipango uliyoifikiria kwenye mambo ya kufanya. Na usiwe mtu mwenye kupanga mambo mia moja kwa wakati mmoja. Uwe na mipango miwili au mitatu ya kujadili na wenzako. Kesho ndio uje na mingine.
Ni bahati mbaya kwetu wanadamu, kuwa muda mwingi sana huwa tunaupoteza kutokana na kutopangilia vizuri mambo yetu. Upo umuhimu kwa mfano wa kupangilia shughuli zetu kutokana na sehemu za kijiografia.
Kwa mfano, kama una shughuli ambazo zinahitajika kufanyika mjini, hakikisha kwamba unapokwenda mjini, unazikamilisha zote kwa wakati mmoja. Kwanini uende mjini zaidi ya mara nne kwa siku?
Naam, Mungu hahusiki na umasikini wako. Muda ni mali. Panga bajeti ya muda wako, sasa! Na hili ni Neno La Leo.
( Makala haya yamechapwa kwenye gazeti Mwananchi, leo Jumapili)

Maggid Mjengwa,
Iringa.
Machi 18, 2012

Sunday, March 11, 2012

KAMA TAIFA TUKO WAPI MGOMO WA MADAKATARI




Mgomo Wa Madaktari: Ni Heri Hekima Inayokuja Kwa Kuchelewa... ( Makala Yangu Gazeti Mwananchi, Jumapili)

N

 Ndugu zangu,
Ni heri hekima inayokuja kwa kuchelewa kuliko inayokosekana kabisa.

Maana, ni heri kutibiwa na daktari aliye kazini na moyo mkunjufu kuliko kutibiwa na daktari aliyelazimishwa kwa nguvu kurudi kazini huku akiwa na kinyongo.
Wahenga walinena; unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kuyanywa maji. Hilo la mwisho ni la hiyari, kama ilivyo kwa tabasamu, kwamba unaweza kumlazimisha mwanadamu kupiga makofi, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kutabasamu, hilo la mwisho latoka moyoni.

Kuna habari za kusikitisha kwa Watanzania, kuwa madaktari wetu wamo tena kwenye mgomo.

Gazeti Mwananchi ( Mtandaoni) linaandika; ” Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Waziri Mkuu Pinda, alisema Serikali haioni sababu ya kuwawajibisha mawaziri hao kwa sasa na kueleza kushangazwa kwake na hatua ya madaktari hao kugeuza suala hilo kuwa dai namba moja hivi sasa.

“Hivi kweli mnataka nifike mahali nimwaambie Rais (Jakaya Kikwete) tunakupa saa 72 uwafukuze kazi viongozi hao? Hapana... hapana... hapana kwa lipi hasa? Siwezi kumwambia atekeleze hayo. Ingekuwa hatujafanya chochote sawa, hata angekuwa mtu yeyote hawezi kukubalina na hayo unless (vinginevyo) wenzetu madaktari watuambie wana hoja nyingine.”

Pinda alisema Dk Mponda mwenyewe anayelalamikiwa ndiyo kwanza ana mwaka mmoja na nusu kazini na hata madai mengine hayajui kwa kuwa hakuwepo wakati huo akisema shinikizo la kutaka awajibishwe ni kumuonea.

Alipoulizwa endapo mawaziri hao wataamua kuwajibika wenyewe ili kunusuru maisha ya Watanzania Serikali itakuwa tayari kwa hilo, Pinda alihoji: “Kwa lipi hasa? Naona ni vyema tusubiri majadiliano, hayo yote yatajulikana baada ya kufikia mwisho.”

Waziri Mkuu aliwataka madaktari kutumia busara, hekima na uzalendo na kuendelea na kazi kama kawaida wakati Serikali inaendelea na majadiliano na viongozi wao. ( Mwananchi Mtandaoni, Machi 8, 2012)

Naam, kinachoonekana hapa ni ukweli, kuwa mgogoro wa madaktari na Serikali umeingia katika hatua nyingine mpya. Na hii ni hatua mbaya zaidi, maana, pande zote mbili zinaonekana kujichimbia mahandakini tayari kwa kujipanga kwa vita kubwa zaidi. Vita isiyo na tija.

Huu ni mgogoro na si kitu kingine. Na majeruhi wa kwanza kwenye mgogoro kama huu ni UKWELI. Katika vita yoyote iwayo, risasi ya kwanza huelekezwa kwenye ukweli. Ni hapa ndipo propaganda huchukua nafasi yake. Lakini, kama ni vita, hii itakuwa ni vita ya kiwendawazimu, maana, haitatoa mshindi. Na katika vita hii, sote, kama taifa, tayari tumeshashindwa. Je, tunataka tushindwe mara ngapi?
Tumeona kupitia televisheni jinsi wagonjwa wanavyotahabika kwa kukosa tiba. Kwanini raia wasio na hatia wafe kwa vile watu wazima kwenye pande mbili kwenye mgogoro, zinashindwa kufikia muafaka wa namna ya kwenda mbele? Inasikitisha sana.

Ushauri wa nini kifanyike;

Hatua hii inahitaji busara na hekima zaidi. Walikofikia madaktari kwenye mapambano yao na Serikali haifikiriki kuwa watarudisha’ majeshi’ nyuma. Na walipofikishwa Serikali na madaktari haifikiriki kuwa kuna Waziri au Naibu wake atakayejiuzulu ili kumaliza mgomo. Upande wowote utakaomkubalia mwenzake katika hatua hii utatafsiriwa kuwa umeshindwa.

Na ’position’(nafasi) ya Serikali inachangiwa zaidi na hofu ya ’domino effect.’ Hilo linaeleweka ukiingia kwenye fikra za Serikali. Athari ya ’kidomino’ ina maana ya badiliko moja hata likiwa dogo linapelekea badiliko lingine, na lingine na lingine. Hatma yake ni mparaganyiko wa jumla.

Sasa basi, cha kufanya katika hatua kama hii ni kwa pande mbili kuepuka kuendesha mapambano yao hadharani. Maana, hakuna upande ulio tayari kwa sasa ’ kutua mbanji’ ( kuweka silaha chini) bila kufunika sura (face saving).

Mantiki hapa, ni kuwepo na njia ya tatu; kwamba pande zote mbili ’in a closed door dialogue’( mazungumzo yasiyoruhusu vyombo vya habari kuwepo na hata kutangaza) kufikia makubaliano ya kudumu, ya kimaandishi ya namna ya kwenda mbele; hivyo basi, kwa pamoja, na kupitia taarifa ya pamoja (joint communique) kutangaza muafaka na hivyo ’ kutua mbanji’ huku sura zao zikiwa zimefunikwa.

Kwa mantiki hiyo, wanayohitaji madaktari yafanyike yanaweza yasifanyike kesho , lakini yakaja kufanyika kwa namna nyingine, kwa makubalino kama yasipofanyika, wahusika wa upande mmoja wa kwenye makubaliano wataitaarifu pande nyingine kimaandishi na bila kupitia media, kuwa walichokubaliana kifanyike hakijafanyika na kuwa wamekubaliana kisipofanyika nini kifanyike na ndicho kitakachofanyika.


Na kitapofanyika upande mmoja utakaolalamikiwa juu ya kwanini umefanya walichokifanya, utakuwa na uthibitisho wa kuuleza umma kuwa umefanya ulichofanya kwa vile upande mwingine umekiuka makubaliano ya kimaandishi na umekubaliana nao kimaandishi juu ya hatua waliyoichukua.

Hivyo basi, tulipo sasa, pande mbili kwenye mgogoro huu hazina budi kurudi kwenye meza ya mazungumzo huku wakitanguliza busara, hekima na maslahi mapana ya taifa. Wajifungie na kuanza upya mazungumzo yatakayoleta makubaliano ya kimaandishi.

Wahenga walinena; kwenye wengi hapaharibiki neno. Ni matarajio yetu, kuwa hatma ya mazungumzo kama hayo itakuwa ni kutolewa kwa taarifa ya pamoja kwa umma, na bila shaka itakuwa ni pande zote mbili kukubaliana kwenye mambo ya msingi na kuwa madaktari wanarudi kazini.

Maana, umma wa Watanzania kwa sasa hauna haja ya kuona nani mshindi na nani mshindwa, kwa vile tulipo sasa sote tumeshashindwa. Watanzania hawana haja pia ya kuona nani, leo au kesho , anatundikwa kitanzini na kunyongwa, bali, kuwaona madaktari wao wanarudi kazini na kufanya kazi wakiwa na mioyo mikunjufu.


Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.
0788 111 765, 0754 678 252  http://mjengwablog.com

Thursday, March 8, 2012

Uchambuzi Wa Habari: " Mawaziri Hawang'oki"- Mizengo Pinda






Ndugu zangu,


Ni heri hekima inayokuja kwa kuchelewa kuliko inayokosekana kabisa.


Maana, ni heri kutibiwa na daktari aliye kazini na moyo mkunjufu kuliko kutibiwa na daktari aliyelazimishwa kwa nguvu kurudi kazini huku akiwa na kinyongo. Wahenga walinena; unaweza kumlazimisha punda kwenda mtoni, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kuyanywa maji. Hilo la mwisho ni la hiyari, kama ilivyo kwa tabasamu, kwamba unaweza kumlazimisha mwanadamu kupiga makofi, lakini kamwe huwezi kumlazimisha kutabasamu, hilo la mwisho latoka moyoni.

Kuna habari za kusikitisha kwa Watanzania, kuwa madaktari wetu wamo tena kwenye mgomo.

Gazeti Mwananchi ( Mtandaoni) linaandika; ” Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Waziri mkuu Pinda alisema Serikali haioni sababu ya kuwawajibisha mawaziri hao kwa sasa na kueleza kushangazwa kwake na hatua ya madaktari hao kugeuza suala hilo kuwa dai namba moja hivi sasa.

“Hivi kweli mnataka nifike mahali nimwaambie Rais (Jakaya Kikwete) tunakupa saa 72 uwafukuze kazi viongozi hao? Hapana... hapana... hapana kwa lipi hasa? Siwezi kumwambia atekeleze hayo. Ingekuwa hatujafanya chochote sawa, hata angekuwa mtu yeyote hawezi kukubalina na hayo unless (vinginevyo) wenzetu madaktari watuambie wana hoja nyingine.”

Pinda alisema Dk Mponda mwenyewe anayelalamikiwa ndiyo kwanza ana mwaka mmoja na nusu kazini na hata madai mengine hayajui kwa kuwa hakuwepo wakati huo akisema shinikizo la kutaka awajibishwe ni kumuonea.

Alipoulizwa endapo mawaziri hao wataamua kuwajibika wenyewe ili kunusuru maisha ya Watanzania Serikali itakuwa tayari kwa hilo, Pinda alihoji: “Kwa lipi hasa? Naona ni vyema tusubiri majadiliano, hayo yote yatajulikana baada ya kufikia mwisho.”

Waziri Mkuu aliwataka madaktari kutumia busara, hekima na uzalendo na kuendelea na kazi kama kawaida wakati Serikali inaendelea na majadiliano na viongozi wao. ( Mwananchi Mtandaoni, Machi 8, 2012)


Naam, kinachoonekana hapa ni ukweli, kuwa mgogoro wa madaktari na Serikali umeingia katika hatua nyingine mpya. Na hii ni hatua mbaya zaidi, maana, pande zote mbili zinaonekana kujichimbia mahandakini tayari kwa kujipanga kwa vita kubwa zaidi. Vita isiyo na tija.


Huu ni mgogoro na si kitu kingine. Na majeruhi wa kwanza kwenye mgogoro kama huu ni UKWELI. Katika vita yeyote iwayo, risasi ya kwanza huelekezwa kwenye ukweli. Ni hapa ndipo propaganda huchukua nafasi yake. Lakini, kama ni vita, hivi vitakuwa ni vita vya kiwendawazimu, maana, havitatoa mshindi. Na katika vita hivi, sote, kama taifa, tayari tumeshashindwa. Je, tunataka tushindwe mara ngapi?



Tumeona jana kupitia televisheni jinsi wagonjwa wanavyotahabika kwa kukosa tiba. Kwanini raia wasio na hatia wafe kwa vile watu wazima kwenye pande mbili kwenye mgogoro zinashindwa kufikia muafaka wa namna ya kwenda mbele? Inasikitisha sana.



Ushauri wa nini kifanyike;


Hatua hii inahitaji busara na hekima zaidi. Walikofikia madaktari kwenye mapambano yao na Serikali haifikiriki kuwa watarudisha’ majeshi’ nyuma. Na walipofikishwa Serikali na madaktari haifikiriki kuwa kuna Waziri au Naibu wake atakayejiuzulu ili kumaliza mgomo. Upande wowote utakaomkubalia mwenzake katika hatua hii utatafsiriwa kuwa umeshindwa.


Na position ya Serikali inachangiwa zaidi na hofu ya domino effect. Hilo linaeleweka ukiingia kwenye fikra za Serikali. Athari ya kidomino ina maana ya badiliko moja hata likiwa dogo linapelekea badiliko lingine, na lingine na lingine. Hatma yake ni mparaganyiko wa jumla.


Sasa basi, cha kufanya katika hatua kama hii ni kwa pande mbili kuepuka kuendesha mapambano yao hadharani. Maana, hakuna upande ulio tayari kwa sasa ’ kutua mbanji’ – kuweka silaha chini bila kufunika sura- face saving.


Mantiki hapa, ni kuwepo na njia ya tatu; kwamba pande zote mbili ’in a closed door dialogue’- mazungumzo yasiyoruhusu media kuwepo na hata kutangaza, kufikia makubaliano ya kudumu, ya kimaandishi ya namna ya kwenda mbele; hivyo basi, kwa pamoja, na kupitia taarifa ya pamoja- joint communique kutangaza muafaka na na hivyo ’ kutua mbanji’ huku sura zao zikiwa zimefunikwa.



Kwa mantiki hiyo, wanayohitaji madaktari yafanyike yanaweza yasifanyike kesho , lakini yakaja kufanyika kwa namna nyingine, kwa makubalino kama yasipofanyika, wahusika wa upande mmoja wa kwenye makubaliano wataitaarifu pande nyingine kiamandishi na bila kupitia media, kuwa walichokubaliana kifanyike hakijafanyika na kuwa wamekubaliana kisipofanyika nini kifanyike na ndicho kitakachofanyika.



Na kitapofanyika upande mmoja utakaolalamikiwa juu ya kwanini umefanya walichokifanya utakuwa na uthibitisho wa kuuleza umma kuwa umefanya ulichofanya kwa vile upande mwingine umekiuka makubaliano ya kimaandishi na umekubaliana nao kimaandishi juu ya hatua waliyoichukua.



Hivyo basi, tulipo sasa, pande mbili kwenye mgogoro huu hazina budi kurudi kenye meza ya mazungumzu huku wakitanguliza busara, hekima na maslahi mapana ya taifa. Wawe in a closed door na kuanza upya mazungumzo yatakayopelekea makubaliano ya kimaandishi.



Wahenga walinena; kwenye wengi hapaharibiki neno. Ni matarajio yetu, kuwa hatma ya mazungumzo kama hayo itakuwa ni kutolewa kwa taarifa ya pamoja kwa umma, na bila shaka itakuwa ni pande zote mbili kukubaliana kwenye mambo ya msingi na kuwa madaktari wanarudi kazini.



Maana, umma wa Watanzania kwa sasa hauna haja ya kuona nani mshindi na nani mshindwa, kwa vile tulipo sasa sote tumeshashindwa. Watanzania hawana haja pia ya kuona nani, leo au kesho , anatundikwa kitanzini na kunyongwa, bali, kuwaona madaktari wao wanarudi kazini na kufanya kazi wakiwa na mioyo mikunjufu.



Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika.



Maggid Mjengwa,


Iringa
 
Habari kwa Hisani ya Mjengwa Blog

DADA SHAMSA FORD STAR WA MOVIE NA SIKU YA WANAWAKE


SIKU YA WANAWAKE DUNIA


Ni ukweli ambao haufichiki kuwa katika dunia hii tunayoishi hakuna kiumbe chochote chini ya jua ambacho hakina mama,hakuna binadamu yeyote ambaye hajui umuhimu wa mama,hakuna asiyejua uthamani wa mama katika maisha yetu ya kila siku; malezi bora yanapatikana kutoka kwa mama, na kwa malezi yake bora mimi leo nimefikia katika khali hii ambayo ninairingia; Asante sana Mama wewe ni shuja wa maisha yangu; Asannte sana Mke wangu wewe ni chachu ya maendeleo yangu;

Siku ya leo dunia inasherekea mwaka wa 101 tangu sherehe hizi zilipoanzishwa rasmi: Hii ni siku ambayo wanawake walisimama kidete kudai na kutetea haki zao: msimamo huu wa wanawake ulikuwa ni changamoto kwa dunia na kwa mfumo dume; msimamo huu ulileta  changamoto kwa  Serikali mbali mbali na hata kwa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na hasa yale yanayotetea usawa wa jinsia, hii pia iliwahusisha mashirika ya kidini katika kupigania haki hizi wa wanawake.


SIKU HII INATUFUNDISHA NINI?


  • ·   Siku hii inatukumbusha  ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike  ndani ya jamii yetu na ubaguzi wa wazi wazi wa upendeleo unaofanya kwa watoto wa kiume;
·  

  •   Siku hii inatufundisha kuwa  wanawake, wananafasi sawa na wanaume katika ushiri kati ka maswala mbali mbali ya kijamii na kisiasa na kiuchumi na wanaweza kufanya vizuri sana kuliko wanauame;



  • ·   Siku hii inatumbusha kuwa wanawake wanaamini hawana silaha nyingine ya kupambana kuleta mabadiliko kuliko  umoja wao.Wanawake ni wajenzi wa amani na wanawake katika nchi mbali mbali za Kiafrika wamekuwa mstari wa mbele kulinda na kudumisha misingi ya amani na utulivu, lakini mchango wao haukupewa uzito unaostahili kutoka katika Jumuiya ya Kimataifa.

SERIKALI INATAKIWA IFANYE NINI KATIKA KUTATUA KERO ZINAZOZUNGUMZWA SANA?
·    
  • Serikali inatakiwa iendelee kuhakikisha kuwa inaandaa mazingira mazuri yatakayo hakikisha kuwa wanawake wanapata nafasi ya kushiriki   katika  kuleta maendeleo ndani ya jamii,  bila kubaguliwa  na kumpendelea mwananume kutokana na mfumu dume ambao umetawala dunia kwa kipindi kirefu.
·      
  •   Serikali uhakikishe kuwa wanawake washirikishwe katika maamuzi ili kuendelea kuwajengea  uwezo wa  wa kuchangia fikra zao ambazo jamii tunaamini kuwa ni za msingi sana kwani mwanamke ni kiongozi bora sana akipewa nafasi.
·  
  •  Serikali kwa kushirikiana na asisi zisizo za kiserikali ijiepushe kutoingiza ubaguzi na unyanyasaji, na kuendelee kupinga kwa nguvu zote mila potovu zinazolenga kumnyanyasa mwananmke na mtoto wa kike.

NINI JUKUMU LA  WANAWAKE KATIKA KUJILETEA MAENDELEO YAO?
·  
  •   wanawake wanatakiwa wao wenyewe wajithamini na kujiheshimu kwa kujilinda na anasa zinazosababisha maafa ambayo yanatokana na tabia ambazo jamii inaziona ni chafu.
·  
  •  Baadhi ya Wanawake wamekua wanavaa nguo zisizo na heshima  na hii inaharibu  kwa kiasi kikubwa heshima ambayojamii imewapa; ukilinganisha pengine na wanaumenakulingana na mfumo wa maisha yetu kosa la mwanamke linaonekana haraka zaidi kuliko wanaume ambao wanaonekana pengine wamefanya kosa sawa.
·    
  • Wanawake wamekuwa wanakwenda na wanaume hovyo bila kutumia kinga na matokeo wana athirika na maradhi mbalimbali pamoja na kushika mimba nje ya ndoa au hata wakiwa na umri mdogo na hivyo kuwasababishia matatizo kiafya na kimalezi.
·       
  •  Wanawake wamekua wauwaji wakubwa wa watoto na hii inatokana kubeba mimba hovyo bila ya kuwa na uwezo wa kuwalea.
·  
  •  Wanawake wanatakiwa wapendane na sio kuchukiana miongoni mwao, tumeendelea kuona jinsi wananwake wanavyochukiana hadharani,mifano mingi ya chuki hizi tunaweza kuiona kwa wasanii wetu wa kike.na hivyo chuki kama hizi huleta ufa mkubwa wa mshikamano miongoni mwa wanawake.
  • katika kusherekea siku hii ya leo dada yetu Shamsa Ford anawakumbusha akina dada au mama au mabinti nini kifanyike kwa maisha yaliyo bora; 

Binafsi  nimefurahishwa sana na maelezo ya Dada  Shamsa Ford ambaye ni mchezo filamu mashuhuri; ameweza kujieleza vizuri sana, nini majukumu ya wananwake kwa maendeleo yao; nafikiri kama wanawake wengi watakuwa na fikra kama zake kuna uwezekano wa kulisukumu  gurudumu hili kwa haraka sana

Hebu msikilize na ninaamini kuwa utafanikiwa kupata wazo nzuri ambalo litakuwa msaada mkubwa kwa jamii yetu.


wanawake wakipewa nafasi wanaweza kabisa kufanya maajabu katika kujiletea maendeleo yao;