WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, June 21, 2016

RAISI DR. MAGUFULI NA JICHO JIPYA LA WATENDAJI KATIKA SERIKALI;



Serikali ya awamu ya tano kwa mara ya kwanza imeamua kuwatumia sana wataalamu ambao wana sifa za kielimu katika utendaji wa wake katika idara nyingi serikalini; mwelekeo ambao umekuwa wazi inajitahidi sana kuondoka na kasumba ya kuwapa watu vyeo kwa huluka ya kisiasa kwa kulindana na kurudisha fadhila. Ilikuwa jambo la kawaida hata wasomi wetu kwa sababu ya hulka ya kisiasa hata pale walipokuwa wakipata nafasi za uongozi walikuwa wanazisahau kabisa taalumu zao na kufanya kazi kwa mazoea ya siasa.

kuwa mwana siasa kwa ujumla wake sio  taaluma, ni haki ya kila mtanzania (msomi au sio) lakini lazima tofauti moja iwe bayana kuwa msomi anapongia katika siasa anaangaliwa katika jicho tofauti kwa mategemeo na matarajio kuwa anatafanya kazi kwa weledi mkubwa na kuongeza tija kwa taifa; Kitu ambacho kwa kipindi kirefu kilikuwa sio kweli. Ilikuwa ni aibu na hasara ambayo Tanzania imekuwa ikipata kwa wasomi wake kujiingiza katika siasa ambazo mchango wake kwa maendeleo ya taifa ulikuwa ni mdogo kuliko angejikita katika kufanya utafiti unaohusiana na fani yake.
Kwa wasomi wetu kuingia katika siasa ilikuwa ni mwanzo wa kuzika taaluma zao; hata pale ambapo walitakiwa kutoa ushauri ambao ungekuwa na manufaa makunwa kwa taifa, hata kama ushauri huo ungekuwa mchungu kwa serikali mara nyingi walikuwa wakitoa ushauri wenye masilahi kwa mtu au chama. Hivyo kuwa hasara kwa Taifa. Kwa wakati huo ilikuwa vyema kwa  Siasa kuwaachie wanasiasa.

Mara nyingi tumechambua kuwa siasa ni mchezo mchafu; lakini ukweli ni kuwa siasa kama mfumo hauna tatizo lolote, wenye tatizo ni wachezaji wanasiasa ambao moja ya sifa yo kubwa ni uwezo wa kuongea na kubadilisha maneno ili sio kuwasaidia wananchi ili kujinufaisha kupitia chama Fulani na uundwaji wa serikali yao; hivyo hata wasomi wetu kama raia wa Tanzania hakuna tatizo kama hao wasomi wanajiingiza kwenye siasa. Shida ni pale wanapokuwa wanasiasa waongo na wasioaminika.

Inatakiwa tufike mahali kama ilivyo kwenye nchi za mataifa yaliyoendelea kuwa utagundua wanasiasa ni wanasiasa na wataalamu huwa hawajichanganyi kwani muda wote wako wakiumiza vichwa kufikiria jinsi ya kugundua kitu fulani. Linapokuja tatizo katika jamii huwa wana wanajitahidi kutimiza wajibu wao kwa kutumia utaalamu wao katika kuleta suluhu ya tatizo.

Tunamshukuru Dr. Magufuli kwa kuanza kutaka kupata matokeo chanya kutoka kwa wasomi wetu katika awamu hii wamepewa mafasi kubwa ili weweze sasa kufanya kazi kwa utaalamu na sifa ambazo wanazo kwa faida ya Taifa na kuwaondolea wananchi wa kawaida ugumu wa maisha ambo uko mbele yao; ni kweli ilikuwa jambo la  aibu sana kuona hadi hii leo Serikali imeshindwa kutumia wasomi wake na rasilimali zilizopo kuleta ufanisi katika kuleta maendeleo kwa wananchi wake matokeo yake ni usanii wa kisiasa ndio uliowekwa mbele. Lakini kubwa zaidi ni kuona hata pale inapopatikana fursa ya ukombozi kujikwamua katika ujinga na umaskini wa kujitakia,hutokea Wasomi wetu kutusambaratisha wenyewe kwa wenyewe.

Wasomi wetu awamu hii ni kipindi chenu cha kuumiza na kushauri na kubuni mipango ya kuwafanya Watanzania katika kuleta mageuzi makubwa ya uchumi na maisha ya watu wake; Dr. Magufuli  anategemea sana ushauri na misimamo madhubuti ya wasomi ili kuisadia serikali katika kujenga Tanzania Mpya. Katika siku za nyuma ilikuwa sahihi kusema kuwa  wananchi wa nchi hii walikuwa na  shahada ambazo zilikuwa hazitumiki zilikuwa zimefungiwa kwani nafasi zao zilichukuliwa na wanasiasa ambao walikuwa hawana sifa za utendaji kwa Taalumu bali kwa siasa; Tumeona mifano ya Maprofesa wengi wasio na idadi, wengi amboa walikuwa wamekijikita kwenye siasa hivyo taaluma yao ilikuwa haina nafasi ili walazimu kucheza ngoma ya siasa na sio ngoma ya utaalamu wao katika kutoa ushauri au kutekeleza adhima ambayo ilikuwa mbele yao.

Katika mazingira yetu, tunapozungumzia Siasa, watendaji wote walilazimika kuwa chini ya mwamvuli wa maagizo ya chama na serikali yake na si vinginevyo hivyo walitakiwa kukizi zaidi zaidi matakwa na mahitaji ya watawala kuliko matakwa na mahitaji ya jamii. Ni jambo la kawaida kwa vyama vya siasa kutumia muda mchache sana kujishughulisha na matatizo/changamoto zinazokabili jamii na badala yake kujikita katika masuala yanayohusiana na uongozi na kutwaa madaraka. Lakini Mheshimiwa Dr. Magufuli anataka wasomi wetu ndio sana wawe chachu ya utawala Bora; wawe ni chimbuko la ufanisi na utatuzi wa Migogoro; wawe ndio daraja bora la maendeleo kwa taifa kwa kutumia uwezo wao wa  kuchanganua, kutambua, na kuelewa jambo. Na na ndio maana wasomi  katika jamii yoyote ile wana uwezo mkubwa wa kuona masuala mbali mbali zaidi ya mwanasiasa wa kawaida kwa  maslahi mapana ya kitaifa.

Tofauti na miaka ya nyuma, Tanzania ya leo imejaliwa kuwa na wasomi wengi sana waliotokana na vyuo vyetu vikuu. Vyuo vikuu ni taasisi zenye umuhimu wa kipekee wa kupangilia na kuendeleza kitu amhacho jamii inaweza kuakisi. Lakini kwa vile wasomi wana nafasi na uwezo wa kushughulika na masuala mbalimbali ya kijamii hawa ndio wenye jukumu kubwa la kuisaidia jamii yetu iondokane na umaskini ambao kwa mshangao mkubwa na bila aibu

kama kioo cha jamii – kwa maana ya kwamba inaipa jamii taswira yake. Wasomi wa nyanja mbali mbali wana uwezo na wajibu wa kutuelezea watanzania tunaonekana vipi kama jamii. Wasomi wana uwezo na wajibu pia kutupa tahadhari juu ya hatari iliyopo mbele yetu; na vile vile kutusaidia kutupatia maana ya vitu ambavyo wanasiasa wetu aidha wanavipotosha, hawavielewi au wanafanyia mzaa kwa faida zao binafsi. Na kwa mara nyingine nina imani kuwa katika awamu hii ile dhana iliyojengeka na jamii yetu ya kuamini wanasiasa na kuliko wasomi ina weza sasa ikapata tafsiri tofauti. 

Lakini ni wajibu wa wasomi wetu kuidhihirishia jamii kuwa wao ndio watatuzi wa kero zetu na sio wansiasa ambao walio wengi hawana taaluma inayotakiwa katika kupambana na kero tofauti tofauti.

Tukumbuke wakati wa Mwalimu alivyoweza kuwatumia wasomi wetu kwani miaka ya 1960s – 1970s, kila wakati taifa lilipokuwa linakabiliwa na changamoto mbalimbali, Mwalimu alikuwa na utamaduni wa kwenda Chuo Kikuu (Mlimani) kukutana na kujadiliana na wanafunzi. Ndio maana tofauti na leo, ilikuwa ni mara chache sana kwa serikali ya Mwalimu kukwaruzana na wasomi. Ni muhimu kwa wasomi kuendeleza juhudi za aina hii.Lengo kubwa Raisi Dr. Magufuli ni kujenge upya dhana ya utendaji kazi yenye nidhamu, uwajibikaji na weledi kwa Taifa na kuondoa utendaji kazi wa mazoea. Sasa ni wakti umefika kwa wasomi wetu ambao mmepewa dhamana ya kuongoza vitengo mbali mbali kulingana na taaluma zetu kufanya kazi katika msingi huo wa utendaji ambao utakuwa na tija kwa taifa letuna faida ya wananchi wetu na mageuzi ya kweli ya uchumi wa Taifa letu;
Mungu Ibariki Tanzania: 

Mungu Mbariki Raisi wetu na dhamira yake nzuri ambayo ameanza kuionyesha kwa Taifa.

Amina