WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, April 5, 2016

SERIKALI ZENYE RUSHWA NA UFISADI – KIINI CHAKE NI NINI?



Wafilipi 2: 4


Leo tujitafakari  na tujiulize kuwa je kuna serikali yeyote ya kidunia ambayo inaweza kuwa madarakani bila kuwa na kutumikia rushwa na ufisadi? Tukumbuke kuwa mwisho wa siku watumishi wa serikali bado ni raia wa nchi husika na zao la taifa husika; Je kwa mantiki hii viongozi ambao wanaunda serikali wanaweza kuepukana na vitendo vya rushwa na ufisadi? Je unakubaliana nami kuwa serikali za kidunia zimejaa rushwa na ufisadi ambao ni ubatili mtupu? Je tunaweza kuwa na serikali ambayo haina tabia hizi katika dunia hii? Bibilia inatukumbusha kuwa  serikali ambayo haitakuwa na harufu ya rushwa lazima itoke nje ya serilaki za kibinadamu;

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa serikali za kidunia ambazo hatimaye zinatawaliwa kwa rushwa na ufisadi, zinasaidiwa kuingia madarakani na raia ambao wanakuwa na malengo tofauti kwa masilahi yao binafsi; wengine wakijua wazi kuwa endapo serikali hiyo itaingia madarakani basi haja zao za kukwepa ushuru, au kuendesha biashara yao bila kufuata masilahi mapana ya nchi yatafanikiwa; hivyo na serikali itatengeneza mianya ya wao kuendelea kujinufaisha na kuwaacha wananchi wanyonge masikini katika umasikini wao kwani nguvu nyingi zitaelekezwa kwao. Tumeona sehemu kubwa za tawala hizi watu ambao ni waaminifu ndio wanaoumia zaidi.

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa ili tuweze kuangamiza rushwa na ufisadi lazima nguvu za kutokomeza zianzie kwa viongozi wa juu ambao wamepewa mamlaka juu ya nchi na Mwenyezi Mungu. Serikali yeyote ile ambayo itakuwa tayari kupambana na rushwa na ufisadi ujue kuwa itapoteza umaarufu wake; katika hili bibilia tukisoma Mhuburi 7:20 bila shaka hakuna mwanadamu mwenye haki hapa duniani, ambaye afanya mema, asifanye dhambi.

Tafakari yetu bado inatuongoza kuwa  tukiondoa wanadamu ambao sio wakamilifu; Yesu Kristo ambaye Mungu alimchagua kutawala ufalme wake, hakuweza kushawishika katika yale ambayo yalikuwa sio sahihi kutenda;  Yesu alionyesha hili pale alipokataa rushwa  kubwa ambazo alipewa na shetani juu ya kukabidhiwa utawala wote wa kinunia na fahari zake kwa kuambiwa kumsujudia shetani Mathayo 4: 8-10  kisha ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha miliki zote za ulimwengu na fahari yake; akamwambia haya yote nitakupa , ukianguka kunisujudia; Ndipo Yesu akamwambia Nenda zako shetani, kwa maana uimeandikwa msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Katika shida na mateso yote bado Yesu aliendelea kudumisha msimamo wake ulio sahihi wa kumtumikia Mungu bila kushawishiwa na mtu mwingine yeyote kwa ukombozi wetu sisi.

Ni ukweli mtupu kuwa nchi nyingi zinafanya uchaguzi ambao nadharia inaruhusu watu kuwachagua viongozi ambao wataingia ofisini/madarakani kwa ajili ya kuendesha nchi; lakini ukiangalia chaguzi nyingi na taratibu za chaguzi hizo hizo ambazo tunaona kampeni zake  nanatawaliwa kwa rushwa kwa kiasi kikubwa sana, hivyo wale wenye uwezo ndio wanaowaingiza watawala madarakani; hapa nafikiri utakubaliana na mimi vyama vya siasa ndivyo vinavyoongoza kwa matendo makubwa sana ya rushwa katika kuhakisha kuwa viongozi tukona vyama vyao ndio wanakuwa washindi ili waweze kuongoza serikali, hivyo watafanya kila hila ili waweze kushinda.

Tafakari yetu ya leo inawaasa viongozi wetu kuwa ili kuweza kuepukana na tabia zote za rushwa na kifisadi; lazima watekeleze amri kuu ya upendo ambayo ni amri ya dhahabu; kile ambacho wewe unataka ufanyiwe mfanyie mwenzako hivyo hivyo; Mathayo 7:12 Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu; nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii Mpende jirani yako kama nafsi yako. Hili kwa viongozi wetu wengi ambao ndio tegemeo la kuondoa umasikini wa watu wao wameshindwa kutekeleza hili; wao wanapenda kutendewa vizuri na kundi dogo la watu waliowaingiza madarakani na kunufaishana wao kwa wao; wameshindwa kabisa kutekeleza hii Golden Rule.

Kwa msingi huu rushwa na ufisadi unaimarishwa zaidi na choyo ya mali na ubinafsi wa kujililbikizia mali; hapa tunaona kuwa viongozi wako tayari kupokea rushwa mfano kutoka kwa makandarasi, nao makandarasi wanapata nafasi ya mwanya wa rushwa katika kutumia vifaa ambavyo havina ubora unaotakiwa ili waweze kujilipa na kupata faida kubwa; kwa msingi huu rushwa na ufisadi utaweza tu kwisha kama tutaondoka na dhana ya ubinafsi na choyo ya kujitajirisha; kama Waefeso 4:23 inavyotufundisha na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu: tunatakiwa kuvua uongo na tunatakiwa kusema kweli daima ili tuweze kuvaa utu mpya ulioumbwa katika mungu ili kutekeleza wajibu wetu ipasavyo na kuwa na hofu ya Mungu. Na ujumbe huu kutoka katika waraka wa Paulo kwa Wafilipi 2:4  ni muhimu sana ambapo anatufundishwa kuwa Kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe bali kila mtu aangalie mambo yaw engine.

Tatizo la tawala za kiduani hata kama wakati mwinginwe wanaweza patiwa elimu nzuri ya kupambana na rushwa na ufisadi bado viongozi wetu wanapenda kushiriki katika vitendo vya rushwa. Kwa msingi huu ni vigumu kwa serikali zetu kupambana na rushwa; tukumbuke mafundisho ya bibilia kuwa watu wenye uchu wa mali, na waongo hawataingia mbinguni; mara nyingi viongozi wala rushwa wana hizi tabia mbili ya Uchoyo wa mali na uongo wanapowadanganya watu wake ili kuhalalisha uovu wao na kikundi kidogo kilicho waingiza madarakani kwa masilahi yao;

Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka
Corrupt Government


.