WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Thursday, September 25, 2014

BALOZI SEIF ALI IDD AKANUSHA MADAI MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA GAZETI LA MTANZANIA .

PIX_1[1]
PIX_2.[1]
PIX_3.[1]
PIX_4.[1]
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akikanusha taarifa zilizoandikwa na gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014.
PIX_5.[1]
PIX_6.[1]
Waziri Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Mohammed Aboud akichangia mada wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kukanusha taarifa zilizoandikwa na Gazeti hilo.
PIX_7.[1]
PIX_8.[1]
PIX_9.[1]
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo wakifutailia kwa makini taarifa toka Balozi Seif Ali Idd.
BALOZI SEIF ALI IDD AKANUSHA MADAI MBALIMBALI YALIYOTOLEWA NA GAZETI LA MTANZANIA KUHUSU KUJIUZULU KWA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR.
 Na Benedict Liwenga, MAELEZO-Dodoma.
 
MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd amekanusha madai mbalimbali yaliyotolewa na Gazeti la Mtanzania la Jumatano 24 Septemba, 2014 ambalo liliandika kuwa ‘Siri zavuja za AG Zanzibar kujiuzulu’.
 
Akikanush taarifa hizo, Mhe. Balozi Idd amesema kuwa Mhe. Othman alitakiwa ashiriki katika kamati kama Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa upande wa Zanzibar lakini kutokuwepo kwake katika Kamati sio kikwazo cha kupatikana kwa Katiba, kwani waliokuwepo ndani ya kamati kwa upande wa Zanzibar walitosheleza kuiwakilisha Zanzibar kikamilifu.
 
Mhe. Balozi Idd alifafanua kuwa Mjumbe kuchaguliwa katika kamati na kukataa kuhudhuria ni maamuzi yake binafsi na hakuna lazima ya mjumbe kuchaguliwa kuingia katika kamati fulani ikawa ndiyo kifungo licha ya kwamba atakuwa na wajibu wa kuendelea kufanya kazi katika kamati hiyo hadi mwisho.
 
“Sisi kama Serikali tunakanusha suala la sintofahamu iliyoandikwa na gazeti hilo ambayo imedai kwamba Viongozi wa juu wa CCM walikutana kwa dharura na kuazimia kumfukuzwa kazi kwa Mwanasheria huyo kwa kile walichodai amekisaliti Chama”, alisema Balozi Idd.
 
Akizungumzia juu ya uwepo wa hoja 17 ambazo zilitakiwa kuwasilishwa na Mwanasheria Mkuu huyo, aisema kwamba Mwanasheria hiyo tayari alishaziwasilisha n azote ziliingizwa katika Rasimu ya Katiba isipokuwa Hoja Nne ambazo bado zinafanyiwa kazi.
 
Aidha ameongeza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali hatakiwi kuwa muumini wa Chama chochote cha siasa na ndiyo maana hata vikao vya chama hatakiwi kuhudhuria, hivyo Mwanasheria huyo wa Serikali si mteule wa chama bali ni mteule wa Mhe. Rais was Zanzibar na ndiyo mwenye maaumuzi ya kumuondoa ama kutomuondoa.
 
Akizungumzia kuhusu tuhuma za kufanyika kwa kikao cha Mawaziri wote wa SMZ wakiongozwa na Dkt. Shein ili kuelezwa taarifa ya Mwanasheria huyo juu ya masuala 17 aliyotaka yaingizwe katika Rasimu ya Katiba alikanusha kuwa, suala hilo sio kweli kwani baadhi ya waandishi wa habari hawafahamu Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ina Mfumo wa Umoja wa Kitaifa ambao umeundwa na CCM na CUF.
 
“Kama inavyoeleweka CUF hawamo katika Bunge Maalum la Katiba, sasa itakuwaje washiriki kuchangia masuala ambayo wao kama sehemu ya UKAWA hawakubaliani na kuendelea kwa Bunge hilo?”, alihoji Balozi Idd.
 
Mhe. Balozi Idd amevitaka Vyombo vya habari kuandika habari zenye ukweli na amewataka kupuuzia uvumi unaoenea katika mitandao ya kijamii kuhusu vitisho vitolewavyo na baadhi ya watu wenye nia ya kuwatisha baadhi ya wajumbe wa bunge hilo kwani vyombo vya dola linafahamu juu ya uwepo wa vitisho hivyo na inavifanyia kazi.

source: matukiotz.com

Tuesday, September 23, 2014

Maximo awaomba radhi Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga,Mbrazil Marcio Maximo

Kocha Mkuu wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo ameawaomba radhi wanachama na mashabiki wa Yanga baada ya timu yake kuanza vibaya msimu huu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL).

Kikianza na wachezaji wanne wa kimataifa, Wanyaruanda Haruna Nyinzoma na Mbuyu Twite, Mganda Hamis Kizza na Mbrazil Genilson Santos Santana ‘Jaja’, Kikosi cha Yanga kilijikuta kikikubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya timu isiyo na mchezaji hata mmoja wa kimataifa, Mtibwa Sugar katika mechi yao ya kwanza ya VPL msimu huu iliyopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Maximo, kocha wa zamani wa timu ya Taifa (Taifa Stars) amelazimika kuwaomba radhi Wanajangwani kutokana na kipigo hicho huku akiahidi kufanya vizuri katika mechi zinazofuata.

“Maximo anawaomba radhi wapenzi, mashabiki na wanachama wa Young Africans (Yanga) waliojitokeza kwa wingi mjini Morogoro kushangilia timu yao kwa matokeo mabaya ya kupoteza mchezo wa kwanza.

Ameahidi kuhakikisha kuwa timu inajipanga vizuri ili kupata pointi zote tatu katika mechi inayofuata,” inasomeka sehemu ya taarifa ya uongozi wa Yanga iliyowekwa kwenye mtandao wa klabu hiyo.

Taarifa hiyo pia inaeleza kuwa Maximo amesema amekubaliana na matokeo, lakini hakuridhishwa na maamuzi ya marefa wa mechi hiyo.

Lakini, Kanuni za Ligi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) haziruhusu makocha kutoa maoni kuhusu uchezeshaji wa marefa wa mechi husika.

Mabao ya Mtibwa katika mechi hiyo iliyoshuhudiwa mshambuliaji mpya wa Yanga kutoka Brazil Jaja akikosa penalti mwanzoni mwa kipindi cha pili, yalifungwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Mussa Hassan Mgosi na Ame Ali aliyekuwa mwiba mkali kwa Yanga siku hiyo.

Kipigo hicho ni mwendelezo wa ‘uteja wa Yanga kwa Mtibwa’ kwani Yanga haijawahi kuwafunga mabingwa hao wa 1999 na 2000 wa Tanzania Bara kwenye uwanja huo tangu Septemba 19, 2009 Wanajangwani waliposhinda 2-1, mabao yakifungwa na Mrisho Ngasa na Nurdin Bakari.

Kikosi cha Yanga, ambacho kinatiwa nguvu na kupona kwa kiungo mpya kutoka Brazil Andrey Coutinho, kinaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi inayofuata.

Mabingwa hao mara 24 wa Tanzania Bara, watakuwa wenyeji wa Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Jumapili wakati Kagera Sugar watakuwa wageni wa JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Azam siku hiyo.

Jumamosi vinara wa msimamo wa ligi hiyo kwa sasa, Ndanda FC watavaana na wababe wa Yanga, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Manungu uliopo Turiani, Kilometa 100 kutoka mjini Morogoro wakati Simba watashuka tena kwenye Uwanja wa Taifa kuwakabili Polisi Morogoro walioanza kwa kipigo cha 3-1 dhidi ya Azam FC.

Mechi nyingine za Jumamosi zitawakutanisha mabingwa watetezi, Azam FC dhidi ya Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Azam, Stand United walioanza kwa kipigo cha 4-1 dhidi ya Ndanda FC watasafiri kutoka mjini Shinyanga hadi jijini Tanga kuwavaa Mgambo Shooting walioanza kwa kuichapa Kagera Sugar 1-0.

Mabingwa wa 1988 wa Tanzania Bara, Coastal Union ambao juzi waliishika Simba katika sare ya mabao mawili, watakuwa wageni wa kikosi cha kocha Juma Mwambusi cha Mbeya City kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
 
CHANZO: NIPASHE

Bunge la Katiba:Kura kupigwa ughaibuni

Mbunge wa Bunge Maalum la Katiba, Said Arfi, akichangia hoja ya kurekebisha kanuni za bunge hilo jana ili kutoa nafasi kwa wajumbe walio nje ya bunge hilo kupiga kura. Picha/ Khalfan Said.

Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, ametumia ‘ubabe’ kuongoza Bunge hilo kufanya marekebisho ya kanuni ili kuruhusu wajumbe watakaokuwa nje ya Bunge siku ya kupiga kura wafanye hivyo kwa kutumia mtandao.

Hali hiyo ilijitokeza wakati wajumbe waliokuwa wakipinga kufanyika kwa marekebisho hayo alipokuwa akiwaingilia na kuwakatisha na wakati mwingine kuwatuhumu kuwa ni waongo na wanazua kwamba, azimio hilo ni la kulazimisha ili wapige kura. 

Alifanya hivyo wakati wajumbe watatu kwa nyakati tofauti walipokuwa wakichangia kuhusu marekebisho ya kanuni za Bunge hilo jana.

Mjumbe wa kwanza kukumbana na hasira na ubabe Mwenyekiti huyo wa Bunge alikuwa Ezekiah Oluoch, aliyeambiwa kuwa ni muongo.

Wengine ni Said Arfi, ambaye alilazimika kukatisha muda wake baada ya kulumbana na Mwenyekiti alipotamka kuwa haoni sababu ya kuwalazimisha na kuwatafuta watu waje kupiga kura kwa kuwa siyo matakwa ya demokrasia.

Kauli hiyo ilimfanya Mwenyekiti kumkatisha kwa kumtaka Arfi aeleze ni nani anawalazimisha wajumbe hao walio nje ya Bunge kupiga kura. 
“Nani anakwambia wanalazimishwa, nani anakwambia wanalazimishwa? Hakuna mtu anayewalazimisha,” alisema.

Kitendo cha Mwenyekiti kuingilia mara kwa mara michango ya wajumbe wanaopinga marekebisho ya kanuni, ilimfanya Arfi kumweleza kuwa wananchi wanaomsikiliza akiwaingilia wajumbe wakati wa michango yao, wanampima.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, unapotuingilia katika michango yetu, Watanzania wanakupima kama unafaa kuliongoza taifa hili,” alisema Arfi.

Hali hiyo ilimfanya Mwenyekiti naye kumweleza Arfi ‘kiutu uzima’ kuwa anaheshimika sana, lakini anachozungumza wakati mwingine siyo sawasawa.

Arfi alisema hakubaliani na azimio hilo kwa sababu kanuni ya 38 ya Bunge hilo ilikuwa tayari imeshaweka utaratibu mzima na hakuna sababu ya kuifanyia marekebisho. 

“Jambo hili tunalofanya ni kubwa sana. Kuandika Katiba ya taifa letu ni lazima tuwe na nia zilizokuwa njema ili tuweze kulipatia taifa hili Katiba ambayo itaridhiwa na Watanzania,” alisema.

Alisema haoni sababu zozote za msingi za kutaka wajumbe, ambao hawamo ndani ya Bunge hilo kupewa fursa ya kupiga kura.

“Kwa uzoefu wa mabunge mengi duniani, inapofika wakati wa kupiga kura, hupiga kura wajumbe, ambao wamo ndani ya ukumbi wa Bunge…huu ndiyo utaratibu unaotumika dunia nzima. Sasa hii ya kwenda kuwatafuta watu huko waliko na huna uhakika kwamba, huyu anayepiga kura ndiye yeye, ni shaka tupu, alisema.

Oluoch alituhumu kauli za mkanganyiko, ambazo zilitolewa bungeni kwa nyakati tofauti na mwenyekiti wa Bunge hilo pamoja na Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Asha-Rose Migiro, kuhusu utata wa akidi ya wajumbe.

Hali hiyo inasababisha kushindwa kujulikana kwa idadi halisi ya wajumbe wanaopaswa kupiga kura.

“Waziri wa Sheria na Katiba alipotoa taarifa yake wiki iliyopita alilijulisha Bunge hili kuwa waliopo ndani ya Bunge hili wapo 500. Mwenyekiti uliposimama kuelezea tatizo, ambalo hivi sasa umelileta kwetu, ulieleza kwamba, wanaotakiwa kupiga kura ni watu 460. Asubuhi hii uliposimama umetuambia waliopo hapa ni kama watu 480,” alisema Oluoch.

Hata hivyo, Mwenyekiti alimkata kauli kwa kusema kuwa takwimu alizozitoa ni za makadirio, huku akimtuhumu Oluoch kwa kusema uongo.

Oluoch alisema licha ya Mwenyekiti kumwita mwongo, haungi mkono hoja ya kufanya marekebisho ya kanuni kwa sababu anaamini inavunja sheria za nchi na haijawahi kutokea katika mabunge mahali popote duniani kwa mtu kupiga kura akiwa nje ya ukumbi wa Bunge.

Alisema kutunga kanuni inayopingana na sheria mama ya nchi ni uvunjaji wa sheria, ambao hatakubaliana nao hata kama atabaki peke yake katika suala hilo.

“Mwenyekiti, naeleza hili kwa misingi hii kuwa kila raia ana haki ya kupiga kura, katiba yetu inaeleza ilimradi awe na miaka 18. Lakini haki hiyo imewekewa pia utaratibu wa kisheria. Taratibu tulizonazo katika nchi hii, hazijaweka utaratibu wa kwamba mtu, ambaye hayupo kwenye eneo la kupigia kura akaruhusiwa kupiga kura…hatujawa na sheria hiyo mheshimiwa mwenyekiti,” alisema.

Hata hivyo, mwenyekiti aliendelea kumkata kauli Oluoch kwa kumuuliza ni aina gani ya kura anazozungumzia.

“Kura zipi, ambazo wewe unazungumzia? Ebu nionyeshe kifungu…unasema uwongo mtupu…wewe unazungumzia sheria ya uchaguzi. Tunamchagua nani hapa?” alihoji Mwenyekiti wa Bunge hilo.

Oluoch alisema: “Haya Mheshimiwa Mwenyekiti, ngoja na mimi niendelee japokuwa umeniita muongo…” na kuongeza:
  “Ninaomba kwamba, kama kanuni zetu zitaruhusu na kuna jambo, ambalo linaleta utata, anaweza akaitwa mtu akalitolea ufafanuzi.”

Alikiomba kiti kumpeleka bungeni Sheikh Mkuu wa Tanzania ili awafafanulie wajumbe wa Bunge hilo kama wajumbe waliokwenda Hijja wanaweza kupata muda wa kupiga kura.

“Mimi siungi mkono jambo hili. Na uamuzi huu wa kuwataka waliokwenda Hijja, ambao hawapo ndani ya Bunge hili kupiga kura. Mimi siliungi mkono,” alisema.

Alisema uamuzi wowote ambao utafanywa na Bunge hilo kwa ajili ya utashi wa kisiasa kwa jambo linalopingana na sheria, atasimama peke yake ndani ya Bunge kulikataa.

Mjumbe wa mwisho kufanyiwa ‘ubabe’ na Mwenyekiti, alikuwa Ally Omar Juma, ambaye alishambuliwa kwa kudai kuwa azimio hilo linalenga kulazimisha wajumbe kupiga kura. 

Omar Juma alisema msingi wa maridhiano ndiyo chemchem ya kuanzishwa kwa Katiba mpya.Alisema nguvu yoyote, vitisho au husuda havitasaidia kitu katika katiba hiyo.

 “Nashauri busara zako. Mimi nakuamini, sina ugomvi na wewe na nakuheshimu sana…hivyo Mwenyekiti, Katiba hii ni maridhiano ya nchi mbili huru.

Si busara, hasa kwa maslahi ya taifa letu kuharakisha kupiga kura kwa watu, ambao hawapo ndani ya Bunge hili. Ni mvurugano mkubwa wa kisheria, ambao utaleta ufa mkubwa wa kisheria kama ambavyo ufa huo umeshajitokeza ndani ya Bunge hili baina ya sisi tuliomo ndani ya Bunge hili na upande wa Ukawa, ni hasara kwa taifa,” alisema.

Alisema haungi mkono azimio linalotaka kupitishwa la kufanya marekebisho ya kanuni ili kuruhusu wajumbe, ambao wapo nje ya Bunge hilo kupiga kura kwa sababu waliokwenda Hijja hawatakuwa na muda wa kupiga kura.

 “Mheshimiwa mwenyekiti, mimi ni muumini wa dini ya Kiislamu. Moja ya nguzo muhimu katika dini ya Kiislamu ni Ibada ya Hijja katika nguzo tatu za Kiislamu…kumpelekea mtu, ambaye yupo Hijja, amekwenda maalumu kwa ajili ya shughuli za ibada, ukiwa katika ibada ile kuna masharti yake…hata kukata kucha unapokuwa pale au kunyoa nywele huruhusiwi,” alisema.

 Aliwaomba wajumbe kusitisha suala la kupiga kura ili kutoa fursa pana zaidi ya mashauriano kwa ajili ya wajumbe wote ili wahudhurie katika Bunge hilo.


Kwa upande wa wajumbe, ambao michango yao ilionyesha kuwa wanakubaliana na hoja ya kufanya marekebisho ya kanuni za Bunge hilo ili kutoa fursa kwa watu walio nje ya Bunge kupiga kura, walidai kutokana na wajumbe wenzao kushiriki kwenye mjadala mzima ni busara na haki kuwapatia fursa ya kuhitimisha kazi hiyo kwa wao pia kupiga kura hata kama wako nje ya nchi.

WAJUMBE WAUNGA MKONO 
Goodluck Ole Madeye pamoja na kuunga mkono marekebisho ya kanuni hizo, alishauri Bunge hilo kuweka utaratibu wa kuainisha vituo vya kupigia kura ndani na nje.

Alisema hali hiyo itaonyesha uwazi na kuwapa wajumbe uhakika wa kweli kwamba kura hizo zinapigwa toka maeneo hayo.Mwingine kuunga mkono hoja hiyo, ni Pindi Chana, ambaye alidai iwapo wataruhusiwa wajumbe walio nje ya Bunge kupiga kura itakuwa ni moja ya utekelezaji wa haki za binadamu.

“Wajumbe watakaokuwa nje watatekeleza haki yao kwa kupiga kura katika ofisi za balozi zetu,” alisema.Alisema utaratibu wa upigaji wa kura nje ya nchi uliopitishwa na Bunge hilo ni tofauti na ule wa uchaguzi.

Sheikh Thabit Jongo, kwa upande wake, aliunga mkono kwa wajumbe kupiga kura nje ya nchi, lakini akijikita zaidi kwa wajumbe, ambao watakuwa wameenda kuhiji Macca.

Alilazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuzuka kwa mvutano miongoni mwa wajumbe kuhusu uhalali wa wajumbe hao kupiga kura wakiwa wameenda kuhiji hoja, ambayo awali ilipingwa na mjumbe Ally Omary Juma, ambaye alisema wakiwa kwenye hija waumini wa dini hiyo hawaruhusiwi kufanya kitu chochote nje ya suala la hija.

“Kwa kuwapo Macca na Madina, wajumbe wetu wanaweza kupiga kura, kuna wakati, ambao wanaruhusiwa kufanya hivyo, isipokuwa tarehe 3 Oktoba,” alifafanua.

Wengine waliounga mkono hoja hiyo ni Paul Makonda, Suleiman Jaffu, Sixtus Mapunda, Mohammed Raza, Dk. Khamis Kigwangalla, Lucas Charles Malunde na Constantine Akitanda.

MAREKEBISHO YA KANUNI BUNGE LA KATIBA
Mapema akiwasilisha azimio la Mwenyekiti wa Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalumu, Pandu Ameir Kificho, mjumbe wa kamati hiyo, Amon Mpanju, alisema marekebisho hayo yanalenga kumuwezesha mjumbe aliye nje ya maeneo ya Bunge hilo kwa ruhusa ya maandishi ya mwenyekiti kupiga kura.

Alisema ni haki ya kila mjumbe wa Bunge hilo kujadili rasimu ya katiba na hatimaye kupiga kura kwa lengo la kupitisha ibara za sura za rasimu ya katiba zilizoandikwa upya kwenye rasimu ya mwisho ya Katiba.

Mpanju alisema haki hiyo haiondolewi na jambo lolote isipokuwa kama mjumbe mwenyewe amehiari kutoitumia haki hiyo au kifo.

Alisema mchakato wa kufanya marekebisho hayo unazingatia kanuni ya 59 (1) ya kanuni za Bunge hilo, ambayo inatoa mamlaka ya kupeleka mapendekezo ya kuzifanyia marekebisho au mabadiliko kanuni zake katika Kamati ya Kanuni na Haki za Bunge Maalum.

Mpanju alisema mwenyekiti alitumia mamlaka hayo kuwasilisha kwenye kamati mapendekezo ya kuzifanyia mabadiliko kanuni ya 36 na 38.

Alisema kanuni ya 36 (1) inaweka sharti kwamba, sura za rasimu ya katiba zilizoandikwa upya zitapigiwa kura ibara kwa ibara, kwa muda usiozidi siku saba.

Mpanju alisema uzoefu uliopatikana wakati wa kamati za Bunge hilo zilipokuwa zikipiga kura ibara kwa ibara ulidhihirisha kwamba, zoezi hilo linachukua muda mrefu zaidi ya muda uliowekwa na kanuni.

“Hivyo kuna haja ya kurekebisha kanuni ya 36 kwa lengo la kupendekeza utaratibu mwepesi wa kupiga kura utakaokidhi mahitaji ya kanuni.“Marekebisho yanayopendekezwa yataruhusu wajumbe kuzipigia kura ibara zote za sura moja au zaidi.

“Chini ya utaratibu huo, mjumbe anayepiga kura ya wazi, atalazimika kutamka ibara anazozikubali na asizokubali na mjumbe anayepiga kura ya siri, ataonyesha kwenye karatasi ya kupigia kura, ibara anazozikubali na asizozikubali,” alisema.

Alisema utaratibu unaopendekezwa utawawezesha wajumbe wote kupiga kura ndani ya muda ulioainishwa kwenye kanuni ya 36 (1).“Haki hiyo haiondolewi na jambo lolote isipokuwa, kama mjumbe mwenyewe amehiari kutoitumia haki hiyo au kifo,” alisema.

Kuhusu kanuni ya 38 alisema imeweka utaratibu wa kupiga kura utakaotumiwa na wajumbe waliomo ndani ya ukumbi wa mkutano wa Bunge Maalum pekee.

RASIMU YA KATIBA JUMATANO
Hatimaye Kamati ya Uandishi ya Bunge, ambayo ipo chini ya Mwenyekiti wake, Andrew Chenge, ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), kesho (Jumatano) inatarajiwa kuwasilisha rasimu ya tatu ya Katiba bungeni na baadaye wabunge kupata muda wa kuipitia.

Mwenyekiti wa Bunge hilo, alisema jana kuwa baada ya kamati hiyo kuwasilisha bungeni rasimu hiyo, wabunge kupitia kwenye kamati zao 12, watapata nafasi ya kuijadili ili kuona kama yaliyomo ni sahihi.

Alisema baada ya hapo kamati hiyo itaandika upya wakijumuisha hoja mbalimbali, ambazo awali zilikuwa zimeachwa au kufanyiwa marekebisho na kwamba, kazi hiyo itafanywa kwa siku mbili, kuanzia Septemba 27 hadi 28, mwaka huu.

Alisema baada ya hapo, wajumbe wataanza kuipigia kura rasimu hiyo, kuanzia Septemba 29 hadi Oktoba 2, mwaka huu.
Imeandikwa na Emmanuel Lengwa, John Ngunge, Jacqueline Massano na Editha Majura, Dodoma.
CHANZO: NIPASHE

MAZIKO YA MAREHEMU IDDI PANDU HASSAN MJINI ZANZIBAR LEO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein (wa nnne kulia) akiwepo na Rais Mstaafu wa Zanzibar DK.Amani Abeid Karume wakijumuika na waisalmu katika kumswalia Marehemu  aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan katika Msikiti wa Mchekeni Magomeni Mjini Zanzibar leo na Kuzikwa kijijini kwao Makunduchi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein na Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ALhaj Dk. Mohamed Gharib Bilali waliungana na wananchi mbali mbali katika maziko ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Iddi Pandu Hassan aliyezikwa kijijini kwao Kipunguni Makunduchi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein alipofika nyumbani kwa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwapa pole wafiwa leo kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Ndugu wa Marehemu Iddi Pandu Hassan aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali alipofika kuwapa pole wafiwa nyumbani kwa marehemu Magomeni Mjini Zanzibar leo kabla ya kufanyika mazishi huko kijijini kwao Makunduchi.
Baadhi ya akina mama walioshiriki katika mazishi ya aliyekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Marehemu  Iddi Pandu Hassannyumbani kwake Magomeni Mjini Unguja. Picha na Ramadhan Othman Ikulu.
source: matukiotz.com

Monday, September 15, 2014

RAIS DKT. SHEIN APOKELEWA COMORO

IMG_4092RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.ALI MOHAMED SHEIN AKISALIMIAANA NA BALOZI COMORO NCHINI TANZANIA ALIPOWASILI KATIKA UWANJA WA NDEGE WA COMORO AKIWA KATIKA ZIARA YA KISERIKALI AKIWA AMEFUATANA NA MKEWE MAMA MWANAMWEMA SHEIN NA VIONGOZI MBALI MBALI [PICHA NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU.]

IMG_4102RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI DK.ALI MOHAMED SHEIN  AKIWA NA MAKAMO WA KWANZA WA RAIS WA COMORO MOAMED  ALI SOILIHI WAKATI WIMBO WA TAIFA WA JAMHURI YA MUUNGANO WAA TANZANIA NAWIMBO WA MUUNGANO WA COMORO UKIPIGWA 

[PICHA NA RAMADHAN OTHMAN,IKULU.]

source: matukiotz.com

TUTENGENEZE KATIBA INAYOLENGA KUTATUA MATATIZO YA WANANCHI WETU KWA MIAKA 50 IJAYO. PROF:MWANDOSYA.

Mwandosya akizungumza 1
MJUMBE wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Mark Mwandosya ameeleza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2055 Tanzania itakuwa imeachana na umaskini katika nchi ya uchumi wa kwanza endapo kutakuwa na dhamira ya dhati hususani kuwa kuandika Katiba yenye kuleta nafuu kwa watanzania kwani kila kitu kwa Waafrika kinawezekana pasipo kuwa na Wazungu.
 Prof. Mwandosya alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa katiba ndani ya Bunge Maalum, ambapo alisisitiza umuhimu wa kuwa na katiba itakayozingatia vipaumbele ambavyo vinaweza kumkwamua mwananchi wa kawaida kuondokana na umasikini na kuliinua Taifa kiuchumi.
 Mhe. Mwandosya amesema kuwa kuhusu changamoto na kero zinazohusu mambo ya Muungano, katiba imejaribu kuzizingatia karibia zote, huku akieleza kuwa hali ya Muungano ni imara na itaendelea kuwa imara.
 Ili kufanikisha nchi inapiga hatua baada ya kuwa na Katiba bora, Mhe. Mwandosya amefafanua kuwa, watumishi wote wa Umma hawana budi kuliletea tija Taifa hili kwa kuwa misingi imewekwa ndani ya rasimu ya katiba  na kusisitiza kuwa Mtumishi wa Umma sio mtawala na mambo yanayohusu miiko na maadili ya mtumishi huyo yenye kumtumikia mwananchi serikali Katiba imeweza kuyazungumzia.
 
“Tumezungumzia kuhusu rushwa ambaye ni adui wa haki, kwamba hili tulitambue katika Katiba ili katika Sheria likasimamiwe vilivyo na pia tumezungumzia pia wale wanaouhujumu uchumi”, alisema Mhe. Mwandosya.
 Kuhusu haki za vijana, Mhe. Mwandosya ameeleza kuwa katika Rasimu ya Katiba wamezungumzia juu ya haki za vijana, haki za walemavu, haki za wazee, pamoja na haki za watoto, huku akiwashangaa baadhi ya wajumbe walioko nje ya bunge hilo wanapotoa shutuma kuwa wanapoteza wakati kana kwamba hawazungumzii mambo yanayowahusu wananchi.
 “Nawaomba wananchi watusikilize na wayazingatie haya tunayoyasema”. Alisema Mhe. Mwandosya.
 Akizungumzia kuhusu Vyombo vya Usalama, amesema kuwa Katiba inawalinda na kuwatambua viongozi wa usalama, ambapo sheria inawapa haki hata baada ya kustaafu ili wakaweze kuishi maisha bora kwa kuchukua dhamana kubwa, hivyo kwa dhamana hiyo viongozi hao wanapostaafu wanatakiwa kujiepusha na masuala ya kisiasa kwasababu.
 “Usalama wa Taifa, Jeshi, Polisi, Magereza na Uhamiaji, hawa tunawatengezea mambo mazuri sana wanapostaafu, kwahiyo tafadhari sana mkishatoka tusaidieni, toeni ushauri lakini mkijiingiza katika siasa na mafaili yetu huku mmeyashika hamtutendei haki”, alisema Mhe. Mwandosya.
 Aidha, ameomba kuwepo na Randama kwani hiyo inaandikwa katika lugha ambayo mwananchi anaweza kuisoma tofauti na katiba kwani hiyo inaandikwa kwa lugha ya kisheria, kwahiyo amependekezo kuwepo na randama kwa ajili ya wananchi.
 Mwandosya ameongezea juu ya suala la amani kuwa ni jambo kubwa sana, amewananga watu wenye tabia ya kutaka wananchi kuandamana wakapigwe risasi hao ni watu wasioitakia mema nchi, hivyo amewaasa wananchi walipinge kwa nguvu zao zote kuhusu suala hilo.
 “Nina ushauri kwa viongozi wenye kutaka wananchi wakapigwe risasi na Polisi, naomba watangulie wao wajipige risasi, unapotaka kuwa Shujaa anzia kwanza wewe mwenyewe, usiwapeleke vijana ambao ni matumaini ya nchi yetu, ndugu zangu hili jambo siyo la busara hata kidogo na wananchi mnapokwenda kuandamana, vijana mseme mnaandamana kwa nini? Kwasababu gani? Na kwa misingi gani na kwasababu ya nani? Ukishajibu haya maswali kwakweli mtaona nchi yetu kuwa ni nzuri sana, nchi ya amani”, alisisitiza Mhe. Mwandosya.

source: matukiotz.com