WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, November 26, 2013

Chadema ' Civil War' Imepamba Moto...!

MOTOOO_3daf8.jpg
Ndugu zangu,
Chadema ' Civil War' imepamba moto. Media imeripoti kuwa leo Chadema Makao Makuu watajibu mapigo. Bado moshi wa makombora ya Zitto haujatua. Ni juzi Zitto alitoka kwenye handaki na kajibu mapigo. Na kama ilivyotarajiwa, Chadema nao wametoka kwenye handaki. Nao wamejipanga kufanya mashambulizi leo. Naam, siasa ni burudani pia. Kuna wengi watasubiri kwa hamu.(P.T)
Bila shaka, Chadema watakwenda kuyaonyesha mashimo kwenye utetezi wa Zitto juzi. Watazama sana kwenye Katiba yao na kuonyesha walivyo makini katika kuifuata.
Ni nini kinachoendelea ?
Tafsiri yangu kiini ni mgogoro wa uongozi ndani ya Chadema. Ni mgogoro wenye kuiweka Chadema kwenye hatari ya kugawanyika. Na kama nilivyobainisha juzi, unahusu uongozi na mamlaka na hususan kuelekea 2015 na mbele zaidi.
Kuna mahali wahusika, kama watataka kupata - win-win situation, itawabidi wakae meza moja na kukubaliana. Lakini, inavyoonekana sasa, hakuna mwenye haja ya matokeo ya suluhu. Ni lazima mmoja apigwe. Na kama nilivyobainisha juzi, kuwa atakayeshindwa, basi, itakuwa ni mwanzo wa mwisho wake wa kuwepo katika hali aliyo nayo sasa.
Na nilisema, kuwa ' Vita' hii itapiganwa kwanza kwenye media. Na baada ya hapo itahamia kwenye mikutano ya hadhara. Ndio, na tuisubiri ' Kamukunji' .
Maggid Mjengwa.
Iringa.

Maalim Seif aahidi kuwaunganisha Wazanzibari

Katibu mkuu wa Chama cha wananchi (CUF),Maalim Seif Sharif Hamad
Katibu mkuu wa Chama cha wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, amesema chama chake kitaendelea na dhamira ya kuwaunganisha wananchi ili kuhakikisha kuwa Wazanzibari wanakuwa kitu kimoja katika kudai mamlaka ya Zanzibar.
Hamad alitoa msimamo huo wakati akihutubia mkutano wa hadhara wa chama chake na kusema iwapo Wazanzibari wataondosha tofauti zao na kusimamia maslahi ya nchi, maendeleo makubwa yanaweza kupatikana ikiwa ni pamoja na kuwakomboa vijana kutokana na ukosefu wa ajira.

Mkutano huo uliyofanyika kijiji cha Fumba Wilaya ya Magharibi Unguja na Maalim Seif ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar alikuwa akihitimisha ziara yake ya kichama kwa majimbo tisa ya wilaya hiyo.

“Kutafuta suluhisho la ukosefu wa ajira kwa vijana ni miongoni kwa vipaumbele katika uongozi wangu wa kisiasa, lakini napenda kuona wananchi wanaishi kwa umoja na mashirikiano,” alisema.

Alisema kuwa zipo njia nyingi za kuwakomboa vijana kutokana na tatizo hilo ikiwa ni pamoja na kuwajengea uwezo ili waweze kuajiriwa katika viwanda vidogo vidogo na vya kati kupitia kwa wawekezaji wa sekta ya viwanda, pamoja na kuwaelekeza kujishughulisha na uvuvi wa bahari kuu.

Eneo jengine alilolitaja kuweza kuwasaidia vijana kuondokana na ukosefu wa ajira ni sekta ya kilimo ambayo itawasaidia wananchi wengi kwa wakati mmoja kuondokana na tatizo hilo.
 
CHANZO: NIPASHE

Zitto ajiweka njia panda

Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amejiweka katika mazingira magumu zaidi kisiasa ndani ya chama hicho, kutokana na shaka kubwa iliyougubika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam juzi.
Zitto pamoja na viongozi wengine wawili wa Chadema; Dk Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba walivuliwa nyadhifa zao na Kamati Kuu ya Chadema baada ya kubainika kupanga mbinu za uasi, kupitia waraka ambao ulikuwa ukieleza mkakati wa kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi wakati wa uchaguzi mkuu wa ndani.(P.T)
Leo, uongozi wa Chadema umeitisha mkutano wa waandishi wa habari ambao pamoja na mambo mengine, utajibu baadhi ya hoja za utetezi ambazo zilitolewa na Zitto pamoja na Dk Kitila. Katika mkutano wa juzi, Zitto na Dk Kitila ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, walizungumzia kuvuliwa kwao madaraka, lakini maandalizi na uendeshaji wa mkutano huo yanazua shaka kutokana kuwahusisha watu wanaodaiwa kuwa ni wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (UVCCM).
Miongoni mwao, wamo waliowahi kuwa wanachama wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Habib Mchange na Mtela Mwampamba ambao walitimuliwa kwa makosa yanayofanana na yale yalizosababisha Zitto na wenzake kuvuliwa nyadhifa zao.
Mchange na Mwampamba pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Bavicha, Juliana Shonza, walivuliwa uanachama wa Baraza hilo Januari 5, mwaka huu baada ya kupatikana na hatia ya kutumia mitandao ya kijamii kukihujumu Chadema na kuwatukana viongozi wake wakuu. Baadaye walihamia CCM wanakoendeleza harakati zao za kisiasa.
Jana, Machange alipotafutwa, alisema: "Mimi sikuwahi kuondoka Chadema, nilifukuzwa kihuni kama walivyowafanyia Zitto na Kitila. Nimepeleka malalamiko yangu tangu Januari hadi leo sijajibiwa, hivyo siwezi kusema nimeondoka.
Nataka nimuunge mkono mwathirika mwenzangu kama ilivyokuwa mimi lakini nitabakia kuwa mwanachama mwaminifu.
"Mimi ni mwanaChadema na sikuwahi kujiunga na CCM au chama chochote, walioondoka ni Mwampamba na Shonza." Mwampamba alisema: "Nilijitokeza pale kuonyesha mshikamano kwa sababu mimi pia ni mwathirika. Kwa hiyo nilitaka ulimwengu ufahamu kuwa mimi ni kati ya wanaopinga siasa za aina hii... Chadema ni chama kinachojiandaa kuchukua dola, sasa kama kila mwenye mawazo tofauti anaonekana mhaini itakuwaje siku wakichukua dola? Ubaguzi huu haujalishi uko chama gani, hata kama niko CCM, hilo halinizuii kuungana na mtu aliyepatwa na tatizo kama langu."
Kuwepo kwao katika mkutano wa Zitto kunaweza kutumiwa na uongozi wa Chadema kuwa uthibitisho wa kiongozi huyo kushiriki katika uasi na kunaweza kupuunguzia nguvu utetezi unaotolewa na Dk Kitila kwamba hakuwa sehemu mpango wa kuuondoa uongozi wa sasa madarakani. Zitto, Dk Mkumbo na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba wanasubiri kukabidhiwa barua za kuvuliwa kwao madaraka na katika siku 14 wanapaswa wawe wamewasilisha utetezi wao wakieleza kwa nini wasifukuzwe uanachama kutokana na tuhuma zinazowakabili.
Dk Slaa
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa alisema jana kuwa ilikuwa lazima viongozi hao wavuliwe madaraka hasa baada ya Dk Kitila kukiri kuhusika na waraka ambao anasema ulilenga kushinda kupitia uchaguzi halali ndani ya chama hicho.
"Hata katika ya nchi ukihusika kutengeneza mbinu za siri lazima ushughulikiwe.Hakuna Katiba itakayokuruhusu kufanya mipango ya siri. Kwanza uchaguzi wa Chadema nani katangaza mpaka mipango ianzwe kutengenezwa sasa hivi?" alihoji Dk Slaa.Alikiri kwamba watuhumiwa hao hawajapewa barua za uamuzi wa Kamati Kuu na alipoulizwa sababu, alisema Katiba ya chama hicho haitoi mwisho wa mtu kupewa barua, huku akihoji: "Wao nani kawaambia waende kwa waandishi wa habari?"
"Mimi ndiye Katibu Mkuu. Katiba inasema ni lini barua iandikwe? Utatokaje kwenye kikao alfajiri na wakati huohuo uandae barua za kuwapa?" alihoji Dk Slaa.
Mkutano leo
Mkutano wa waandishi wa habari ulioitishwa leo unatarajiwa kujibu baadhi ya hoja za utetezi za viongozi hao zilizotolewa juzi. Zitto alifichua kile alichokiita tuhuma zilizotolewa dhidi yake mbele ya Kamati Kuu akimaanisha kwamba tuhuma zilizotamkwa kwenye vyombo vya habari na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazikuwa kamilifu.
Habari zinasema uongozi wa Chadema utaweka wazi kile kinachodaiwa kuwa ni "Zitto kujitungia tuhuma, kisha kuzipatia majibu", badala ya kujibu hoja ambazo zilitolewa na Kamati Kuu.
Jana, Dk Slaa akizungumzia suala hilo alisema Kamati Kuu haiwezi kuchaguliwa tuhuma za kusema na za kuacha... "Hiyo hoja walete kwenye vikao, nani anayeipangia Kamati Kuu ichukue hatua gani pale inapotaka kufanya hivyo?"
Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene akizungumza jana alisema: "Kamati Kuu ilijadili mambo mengi na hayo ndiyo tunataka umma ufahamu msimamo wetu kama chama."
Habari ambazo zimelifikia gazeti hili zinasema katika mkutano huo, huenda uongozi wa Chadema ukaweka wazi "makosa mengine" ambayo Zitto anadaiwa kuwa amewahi kuyafanya na kuonywa katika vikao vya ndani ikiwa ni pamoja na kiongozi huyo kutofika makao makuu ya chama hicho kwa zaidi ya miezi sita. "Kuna makosa mengi (Zitto) ameyafanya yenye sura ya kukiumiza chama chetu na alionywa mara nyingi tu, tena na vikao vya juu vya chama kuhusu mwenendo wake, lakini aliendelea na uasi.Sasa Kamati Kuu imechoka," alisema mmoja wa maofisa wa Chadema Makao Makuu.
Habari zaidi zinasema katika mkutano wake wa leo, chama hicho kitatoa ufafanuzi kuhusu mikutano yote ya kichama ambayo imekuwa ikifanywa na Zitto, huku kukiwa na hoja kwamba alikuwa akifanya hivyo bila kuwashirikisha maofisa wa makao makuu wala sekretarieti ambayo kimsingi ndiyo inapaswa kuiandaa.
Wasomi wanena
Akizungumzia mgogoro huo, mtaalamu wa mambo ya siasa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Mbunda alisema hali inayoendelea ndani ya Chadema ni matokeo ya vyama vya siasa kutofanya kazi kama taasisi.
"Misingi ya vyama haiweki wazi misingi ya watu kuwa viongozi. Kwa mfano, kesho nikitaka kujiunga na Chadema nitaweza kuwa Mwenyekiti? Misingi ya wazi hakuna," alisema Mbunda.Alisema hali ilivyo ndani ya Chadema kwa sasa ni furaha ndani ya CCM, kwani watu wanaona kuwa chama kilichoonekana kuwa mbadala hakiwezi hata kushughulikia mambo yake ya ndani.
Mhadhiri Mwandamizi wa Sayansi ya Siasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Alexander Makulilo alisema vyama vya siasa ni watu au kikundi cha watu wenye malengo na mitazamo tofauti.
"Ukisoma huo waraka utaona kuwa unazungumzia uongozi, upungufu uliopo kwenye uongozi na namna ya kubadili uongozi, mimi binafsi niseme ieleweke kwamba hata kwenye jumuiya yoyote mambo haya yapo hasa kwa kuwa walikuwa wanaelekea kwenye uchaguzi," alisema. Alisema haoni kwa nini Zitto na Dk Kitila waonekane wahaini kwa kupanga mikakati yao ambayo walitaka kuitekeleza kupitia uchaguzi.
"Mabadiliko ni jambo la kawaida, hali hii ya kuwaondoa kwenye nyadhifa zao inawezekana ikawagharimu Chadema na inaweza kuwagharimu zaidi wakiwafukuza uanachama," alisema Makulilo.

source: mjengwa blog

MAMIA WAMZIKA JERRY ISAACK MRUMA KINONDONI DAR ES SALAAM


Mwili wa Mtanzania Jerry Isaack Mruma  aliyekuwa akisoma Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Marekani (USIU) tawi la Nairobi nchini Kenya akichukua Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara (MBA) aliuawa wakati akitoka kwenye hafla ya usiku wa Mtanzania mjini Nairobi. Mwili  wake ulipatikana mwishoni mwa wiki iliyopita. Amezikwa leo katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam.
 Familia ya Isaack Mruma ikiwa katika ibada maalum ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika Kanisa la KKKT, Usaharika wa Mbezi Beach Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mama mzazi wa Jerry, Bi Joyce Mruma, Khan Mruma ambaye ni kaka wa marehemu, baba mzazi wa Jerry, Isaack Mruma na mdogo wake Kelvin Mruma wakiwa katika ibada hiyo. PICHA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG (P.T)

source: mjengwa Blog

Monday, November 25, 2013

TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB)- NA UONGOZI NDANI YA CHADEMA

TAARIFA YA ZITTO ZUBERI KABWE (MB) KUHUSU KUVULIWA NAFASI ZA
UONGOZI NDANI YA CHAMA CHANGU CHA CHADEMA
1. Utangulizi

i. Katika kikao chake cha siku mbili kilichofanyika tarehe 20 22
Novemba 2013,

Kamati Kuu ya CHADEMA, pamoja na mambo mengine, iliazimia kunivua
nafasi zangu zote za uongozi ndani ya chama. Kwa mujibu wa taarifa ya chama
iliyotolewa katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Ijumaa tarehe 22
Novemba 2013, ilielezwa kwamba sababu za kuvuliwa uongozi mimi na Dk
Kitila Mkumbo ni uhaini na hujuma kwa chama kutokana na waraka unaojulikana
kama mkakati wa uchaguzi 2013. Ukweli ni kwamba waraka uliotajwa si sababu
ya mimi kuvuliwa nafasi zangu za uongozi kama ilivyojadiliwa katika Kikao cha
Kamati Kuu . Sababu za kufukuzwa kwangu kama zilizojadiliwa katika kikao cha
Kamati Kuu ni tuhuma lukuki ambazo si mara yangu ya kwanza kuzisikia
zikijadiliwa ndani na nje ya vikao vya chama. Hitimisho la tuhuma hizi ni kwamba
mimi nimekuwa nikikisaliti chama kwa kutumika na CCM na Usalama wa Taifa.
Nitazianisha tuhuma hizi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa nikizijibu katika
vikao mbalimbali vyama.

ii. Ninatambua kwamba chama changu kinapita katika wakati mgumu sana sasa
hivi. Nataka nitamke mapema sana kwamba mimi Zitto Zuberi Kabwe sitokuwa
chanzo cha CHADEMA kuvunjika. Hiki ndicho chama kilichonilea na kunifikisha
hivi nilivyo. Ningependa chama hiki mtoto wangu atakapokuwa mtu mzima na
atakapoamua kujiunga na siasa aingie CHADEMA. Bado nina imani kubwa na
chama changu na ninaamini ndicho kinachostahili kuendesha nchi jana,
leo na kesho.

2. Kuhusu tuhuma mbalimbali zinazo elekezwa kwangu
Zipo tuhuma nyingi ambazo zimekuwa zikirudiwarudiwa katika vikao vya chama na
nje ya vikao na baadhi ya viongozi wenzangu. Tuhuma hizi zinalenga kuonyesha
kwamba mimi ni mbinafsi na kwamba ninapokea rushwa ili kukihujumu chama
changu. Nitazianisha tuhuma kwa kifupi na kuzijibu kama ambavyo nimekuwa
nikizijibu katika vikao mbalimbali vya chama.

i) Tuhuma kwamba sikushiriki kumpigia kampeni mgombea wetu wa urais katika
uchaguzi wa mwaka 2010. Ningependa kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:

● Mimi nilikuwa mgombea wa ubunge katika Jimbo la Kaskazini huko Kigoma.
● Pamoja na kuwa mgombea wa ubunge, nilifanya kampeni katika majimbo mengine
16 katika mikoa mbalimbali, ikiwemo Dar es Salaam, Mtwara, Pwani, Shinyanga,
Mara na Rukwa. Hakuna kiongozi yeyote wa juu aliyefanya kampeni katika majimbo
mengi kama mimi, ukiacha mgombea urais.
● Kote nilipopita nilimpigia kampeni wagombea wetu wa udiwani, ubunge na Rais.
● Katika Mkoa wa Kigoma nilizunguka na mgombea urais katika kata zote za Kigoma
Kaskazini na majimbo yote manane ya Mkoa wa Kigoma.

ii) Tuhuma kwamba katika Mkoa wa Kigoma nilishindwa kuwapigia kampeni
wagombea wetu kiasi kwamba peke yangu ndiye niliyeshinda katika uchaguzi huo.
Ukweli ni kwamba niliwapigia sana kampeni wagombea wetu, na hivyo ndivyo wapiga
kura wa Kigoma walivyoamua.

iii) Tuhuma kwamba nilishiriki kuwashawishi wagombea wetu katika baadhi ya
majimbo kujitoa katika uchaguzi wa mwaka 2010 ili kuwapisha wagombea wa CCM
wapite bila kupingwa kwa njia ya rushwa. Majimbo yanayotajwa ni pamoja na
Sumbawanga, Musoma Vijijini na Singida Mjini. Kama nilivyokwisha kueleza katika
vikao mbalimbali vya chama jambo hili si la kweli na hakuna popote ambapo watoa
tuhuma hizi wamewahi kutoa ushahidi kwamba nilifanya jambo hili. Nipo tayari kwa
uchunguzi ndani ya chama na watoa tuhuma waje na ushahidi bayana wa jambo hili. Si
afya kwa chama kuendelea kurudiarudia tuhuma hizi kila mara tangu mwaka 2010 bila
uchunguzi wowote kufanyika na jambo hili lifikie mwisho.

iv) Tuhuma kwamba nimekuwa sishiriki katika operesheni mbalimbali za chama: Ukweli
ni kwamba nimeshiriki sana katika operesheni mbalimbali za chama ndani na nje ya
nchi. Kwa mfano, mwaka 2011 tulikuwa na operesheni kubwa katika mikoa ya Kanda
ya Nyanda za Juu Kusini na nilikwenda katika mikoa yote tuliyotembelea. Mwaka 2012

baada ya hoja ya mkonge bungeni nilifanya ziara Mkoa wa Tanga. Mwaka 2012
kulikuwa na operesheni kubwa moja katika mikoa ya kusini ya Mtwara na Lindi.
Operesheni hii sikushiriki kwa sababu nilikuwa nchini Marekani kufungua matawi kwa
mwaliko wa Watanzania wanaoishi huko.

v) Tuhuma kwamba nimekidhalilisha chama kwa tamko la PAC kwamba Hesabu
za Vyama hazijakaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG): Katika jambo hili ninatuhumiwa kwamba mimi kama Naibu Katibu
nilipaswa kuwasiliana kwanza na viongozi wa chama 'kuwatonya' ili wajiandae.
Kwamba kutokuwatonya kumekidhalilisha chama na kukiweka kundi moja na CCM na
nastahili kuadhibiwa vikali kwa kuwa katika taarifa yangu nilikuwa na nia mbaya na
chama chetu. Maelezo yangu niliyoyatoa na ambayo ningependa kuyakariri hapa
kuhusu jambo hili ni kama ifuatavyo:

● Utawala bora hautaki mimi kutumia nafasi yangu ya uenyekiti wa PAC kulinda
chama changu na kuonea vyama vingine. Kufanya hivyo ni kuendeleza tabia zile zile
ambazo tunazipinga na ambazo tunapigania kuzibadilisha
● Napenda kusisitiza kwamba hakuna chama ambacho kimewahi kukaguliwa na
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG). Natambua kwamba mahesabu ya
chama changu yamekuwa yakikaguliwa na wakaguzi wa nje kwa utaratibu
tuliojiwekea. Lakini matakwa ya kisheria ni kwamba mahesabu ya vyama vya siasa
hayajakaguliwa na CAG, na hili ni kosa la kisheria, bila kujali kosa hili ni la nani.

vi) Tuhuma kwamba mimi ni mnafiki katika kukataa kwangu kuchukua Posho
za Vikao

Mtakumbuka kwamba mimi nilikataa kuchukua posho tangu mwaka 2011 kama ishara
ya kuonyesha kwa vitendo msimamo wa chama chetu wa kupinga posho za kukaa na
matumizi mengine yasiyofaa katika fedha za umma kama ilivyoanishwa kwenye Ilani
yetu ya mwaka 20102015.

Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Mheshimiwa Lema
amenishutumu kwamba kukataa kwangu kuchukua posho ni unafiki kwa sababu
ninapokea posho kubwa zaidi katika mashirika ya umma ambapo mimi ni mwenyekiti
wa kamati husika. Ninapenda kueleza yafuatayo kuhusu jambo hili:

● Sipokei posho yeyote ya vikao (sitting allowance) ndani na nje ya Bunge tangu
mwaka 2011. Hii ni pamoja na vikao vyote katika Kamati za Bunge
ninavyohudhuria. Mtu yeyote mwenye ushahidi vinginevyo auweke hadharani.
● Swala la kukataa posho (sitting allowance) ni swala la kiilani katika chama chetu, na
kwangu ni swala la kimisingi zaidi. Katika Wilaya yangu vifo vya kina mama
wajawazito ni 1900 kati ya wanawake 100,000 wenye ujauzito. Vifo hivi vinatokana
na ukosefu wa huduma kwa sababu ya bajeti finyu. Ndiyo maana nilifurahi sana kwa
chama chetu kuliweka swala la kupunguza matumizi ya Serikali katika Ilani, na
kuondoa posho za wabunge, ambao tayari wanapokea mishahara mikubwa,
kungesaidia sana kupatikana fedha ambazo zingeokoa vifo vingi vya kina mama.
● Jambo hili si suala la ugomvi baina yangu na Mheshimiwa Lema. Ni suala la
msingi katika chama chetu.
3. Usambazaji wa Ripoti ya Siri kuhusu Zitto Kabwe
Hivi karibuni kulisambazwa waraka unaoitwa ripoti ya siri kuhusu mimi ukibeba lundo la
tuhuma kwamba nimehongwa fedha nyingi ili kukihujumu chama changu. Waraka huu
ulidaiwa kuwa umechomolewa kutoka makao makuu ya CHADEMA. Jambo hili pia
lilijadiliwa katika kikao cha juzi kwa kifupi, na majibu ya viongozi wa chama ilikuwa ni
kwamba waraka huu haukuandaliwa wala kusambazwa na makao makuu. Katika
mchango wangu nililalamikia mambo matatu yafuatayo:
i. Kwamba baadhi ya waliokuwa wanasambaza waraka ule walikuwa ni viongozi wa
chama chetu. Bahati mbaya hadi leo hakuna hata mmoja ambaye
amekwishachukuliwa hatua za kinidhamu. Ninaamini kwamba kuna siku watu hao
watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu za chama chetu.
ii. Kwa kuwa chama kimekana rasmi kuhusika na waraka huu, nitaendelea na taratibu
za kisheria ili kuhakikisha kwamba wote waliohusika kutengeneza hekaya ile
wanachukuliwa hatua stahiki za kisheria.
4. Hitimisho
a) Ninatambua kwamba kuna watu walitegemea leo ningejibu mapigo na
ningewazodoa watu kwa majina kama ilivyo kawaida katika siasa za Tanzania.
Natambua pia kwamba, kama ilivyo kawaida wakati wa migogoro katika vyama vya
5.siasa hapa Tanzania, kuna watu walitegemea leo ningetangaza 'maamuzi magumu'.
Natambua kwamba wapo ambao wangependa kupata nafasi ya kuendelea
kutumia suala hili katika harakati zao za kudhoofisha mapambano ya
demokrasia na uthabiti wa siasa za ushindani nchini mwetu. Napenda
wanachama wa CHADEMA na wapenda demokrasia na siasa safi wote nchini
watambue kwamba mimi bado ni mwanachama mwaminifu wa chama hiki na
nitakuwa wa mwisho kutoka kwenye chama hiki kwa hiari yangu. Nitafuata taratibu
zote ndani ya chama katika kuhitimisha jambo hili.
b) Naomba wanachama waelewe kwamba mimi kama binadamu ninaumia
ninapopigwa. Tuhuma ninazorushiwa ni kubwa na zinanikwaza. Tuache siasa za
uzushi ili tujenge chama chetu na nchi yetu, ili hatimaye tuwakomboe Watanzania
wenye matarajio na imani kubwa kwa chama chetu.
c) Kama mwanasiasa kijana niliyekaa katika siasa kwa muda sasa yapo mengi
mazuri nimeyafanya. Lakini kuna maeneo nilipojikwaa na yapo makosa
niliyofanya kisiasa katika maisha yangu ya siasa.
d) Kinachoendelea ndani ya chama chetu ni mapambano ya kukuza demokrasia. Ni
mapambano baina ya wapenda demokrasia dhidi ya wahafidhina, waumini wa
uwajibikaji dhidi ya wabadhirifu na wapenda siasa safi dhidi ya watukuzao siasa
majitaka. Hii ni changamoto kubwa ndani ya chama chetu inayohitaji uongozi
shupavu kuikabili. Nitasimama daima upande wa demokrasia. Kama alivyopata
kunena mmoja ya wanasiasa maarufu, 'kiwango cha juu kabisa cha uzalendo katika
nchi ni kukubali kutofautiana kimawazo', na ninatamani huu ndio uwe utamaduni wa
chama chetu.
Kabwe Zuberi Zitto, Mb
Dar es Salaam.
24 Novemba, 2013

Saturday, November 23, 2013

Mtikisiko Chadema: Zitto awekwa benchi, Arfi ang'atuka, lawama zatanda

Mwenyekiti wa Chadema,Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu Maamuzi ya Kamati Kuu ya Chama hicho ya kuwavua nyazifa Naibu Katibu Mkuu,Zitto Kabwe na  Mjumbe wa Kamati Kuu Kitila Mkumbo Katikati ni Mwanasheria wa chama hicho,Tundu Lissu na Katibu Mkuu, Dk Willibrod Slaa. 

Dar es Salaam. Mgogoro ndani ya Chadema umezidi kupamba moto baada ya Kamati Kuu kuwavua uongozi Zitto Kabwe na Dk Kitila Mkumbo, huku Makamu Mwenyekiti Taifa, Said Arfi akiandika barua ya kujiuzulu.
Zitto alivuliwa uongozi wa Naibu Katibu Mkuu Taifa na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, wakati Dk Mkumbo amevuliwa ujumbe wa Kamati Kuu. Wawili hao wanatuhumiwa kukisaliti chama.
Taarifa zilisema hoja ya kukisaliti chama pia ilimkumba Arfi akidaiwa kumwezesha Waziri Mkuu Mizengo Pinda kupita ubunge bila kupingwa, katika uchaguzi mkuu uliopita na ndiyo sababu ya kuamua kuachia ngazi nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Taifa.
Mbali ya kuwavua uongozi Zitto na Dk Mkumbo, pia Kamati Kuu imewapa siku 14 wajieleze kwa nini wasifukuzwe uanachama. Kwa uamuzi huo Zitto amebaki na wadhifa wa ubunge wake wa Kigoma Kaskazini na wadhifa mwingine kwenye Kamati ya Bunge.
Zitto azungumza
Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho, Zitto aliliambia gazeti hili, “Sina cha kueleza, kikao kilikwenda vizuri na taarifa rasmi ya chama kuhusu uamuzi wa kikao itatolewa baadaye mchana (jana saa nane mchana), tusubiri Kamanda.”
Arfi ajiuzulu
Makamu Mwenyekiti wa Taifa, Said Arfi ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, jana aliwasilisha barua ya kujiuzulu nafasi ya uongozi wa chama, akisema; “…kuchoshwa na unafiki unaoendelea ndani ya chama. Napenda ifahamike pia kwangu masilahi ya wapigakura, wakazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki.
Katika barua hiyo anasema amechochwa na tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake kuwa alimsadia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kupita bila ya kupingwa  katika uchaguzi wa ubunge katika uchaguzi mkuu uliopita.
“Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutuma dhidi yangu na kutiliwa shaka uhusiano wangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu. Pamoja na kulijadili katika vikao kadhaa Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa. Huo ulikuwa uamuzi wa Wanampanda kwenu imekuwa ni tatizo, lakini hamsemi kwa nini. Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikuwa wapi na nani alaumiwe? Huu ni unafiki  wa kupindukia.
Vilevile, katika barua hiyo, Arfi anasema amechukizwa na kauli ya mwasisi wa chama hicho, aliyemtaja kwa jina moja la Mtei kuwachagulia marafiki.
“Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Mwasisi wa chama, Mhe Mtei kutuchagulia viongozi.  Naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa mali binafsi.
Kwa kusema ukweli na kusimamia ukweli daima itabakia kuwa lengo langu katika maisha yangu siku zote hata kama itanigharimu maisha yangu.”
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu barua ya Arfi ya kujiuzulu uongozi, alisema; “Mimi nimekwishaondoka ofisini.”
Taarifa ya chama
Akitangaza uamuzi wa Kamati Kuu jana Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu alisema, Zitto, Dk Mkumbo na Mwenyekiti wa Chadema mkoani Arusha, Samson Mwigamba walikuwa na mtandao wa kukiua  chama hicho, huku wakitengeneza tuhuma za kuwachafua  Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe na Katibu wake, Dk Willbroad Slaa.
Alisema kuwa kamati kuu ilibaini kuwapo kwa mkakati mkubwa wa watu hao kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013’, ambao umeandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’.
“Kikundi hicho vinara wake wapo wanne, Zitto anajulikana kama Mhusika Mkuu (MM), Mkumbo (M1), Mwigamba (M3) na mtu mwingine wa nne hatujamtambua kwa sasa yeye anatumia jina la M2” alisema Lissu.
Alisema wakati wa kuhojiwa na Kamati Kuu Dk Mkumbo alikiri kuwa mhusika mkuu wa mtandao huo ni Zitto, lakini Zitto alikana kuutambua waraka huo licha ya kueleza unamhusu kwa kuwa umetaja jina lake, kauli ambayo alidai Kamati Kuu haikutaka kuiamini.
Huku akieleza jinsi watu hao walivyokuwa wakiwasiliana na kupanga mikakati ya kuimaliza Chadema kwa siri chini ya ufadhili wa fedha kutoka kwa Zitto, Lissu alisema Naibu Katibu Mkuu huyo wa zamani alikuwa akitumiwa na Chama Tawala (CCM) kuimaliza Chadema.
“Mkakati wa Mabadiliko 2013 ni mpango haramu na ambao unaichanachana katiba ya chama chetu. Ni mkakati wa vita dhidi ya chama chetu na utaratibu wetu wa kikatiba. Hatuwezi kunyamazia mkakati huu wa kutumaliza, uvumilivu umefika kikomo,” alisema.
Uamuzi
Alisema kutokana na hali hiyo kamati kuu iliamuru wahusika wote wavuliwe nyadhifa zao zote za uongozi wa chama, kukubaliana kuunda timu ndogo ya pamoja ya watendaji wa sekretarieti ya makao makuu ya chama hicho ili kumtambua mtu wa nne (M2).
“Kamati ya Bunge imetakiwa kuchukua hatua za haraka kuhakikisha Zitto anavuliwa nafasi zote za Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, pia wote wanatakiwa kujieleza ndani  ya siku 14 kwa nini wasivuliwe uanachama na watapewa fursa ya kujitetea,” alisema.
Alisema Kamati Kuu itakutana kwa dharura kwa ajili ya kufanya uamuzi juu ya hatima ya watuhumiwa hao.
Kauli ya Mbowe
Awali Mbowe alipinga madai kuwa Zitto ameondolewa kwa kuwa alikuwa akitaka kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama hicho, akasisitiza kuwa uamuzi huo umefanyika kwa kuwa Chadema ni chama cha watu, siyo mali ya mtu binafsi.
Mvutano Zitto, Lema
Kwa zaidi ya wiki mbili Zitto amekuwa akilumbana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho.
Vita hiyo ilianzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita aliposema kuwa Zitto anafanya unafiki kukataa posho.
Alimtuhumu mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.
Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususan, mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.
Zitto alijibu kuwa tangu siku nyingi alikwishapiga marufuku kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.
Alisema tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alipiga marufuku posho na pia aliwahi kuwashtaki Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wabunge wanaochukua posho kutoka taasisi za Serikali.
  Zitto pia alipata msukosuko mwingine baada ya kusambazwa ripoti inayoitwa ‘Taarifa ya Siri ya Chadema’ iliyomtuhumu kuwa alikuwa anashirikiana na CCM na viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa kuihujumu Chadema.
Pia, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na Mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali (CAG), huku akitaka ruzuku kwenye vyama hivyo isimamishwe.
Chadema ilipinga vikali madai hayo na kueleza kuwa imekuwa inatumia taasisi binafsi kufanya kazi hiyo. Vyama vinavyopata ruzuku ya Serikali ni vile vyenye wabunge Chadema, CCM, UDP, TLP, CUF na NCCR-Mageuzi.
Mvutano kikaoni 
Wakati wajumbe wa kikao hicho wakivutana, Zitto alikuwa njiani akirejea kutoka Sudan Kusini, ambapo alienda na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa,  baada ya kuibuka sintofahamu hiyo, Mbowe aliwapoza wajumbe wa kikao hicho, akiwaeleza kuwa haitakuwa busara kumjadili mtu ambaye hayupo.
“Mbowe alipendekeza kuwa ajenda hiyo iwekwe kando na itajadiliwa baadaye kutokana na Zitto kutokuwepo katika kikao hicho,” zilieleza habari hizo.
Baadaye Zitto alituma ujumbe ambao ulitangazwa kwa wajumbe wote, kwamba alikuwa njiani kurejea Tanzania, kwamba akifika moja kwa moja atakwenda katika kikao hicho.
Zitto awasili, mzozo waibuka
Kama vile alikuwa akisubiriwa yeye, mara baada ya kufika katika ukumbi huo saa 2:23 usiku huku akisindikizwa na walinzi wanne, mvutano mkali uliibuka katika ukumbi huo na mara kadhaa walinzi wa chama hicho, Red Brigade walionekana kukaa tayari mlangoni kuzuia vurugu kama ingetokea.
Gazeti hili lilikuwa nje ya ukumbi huo na mara kadhaa lilisikia sauti za malumbano za baadhi ya viongozi wa chama hicho, akiwamo Zitto, Mbowe na Lema.
Wakati wakitoa maelezo kwa nyakati tofauti Lema na Zitto walishutumiana huku kila mmoja akimtaja mwenzake kuwa anatumia vibaya nafasi yake na mitandao ya kijamii.
“Tatizo lake ni kutumia mitandao ya kijamii kueleza mambo ya chama wakati akijua siyo utaratibu, ugomvi wangu naye kwa kiasi kikubwa uko hapo,” alisikika akisema Lema.
Kuna wakati yaliibuka malumbano makali huku sauti za juu zikisikika kutoka ndani ya ukumbi huo, kati ya Zitto, Lema na Mbowe.
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinaeleza kuwa Dk Mkumbo alikumbwa na rungu hilo baada ya kubainika kuwa alikuwa ameanda taarifa za siri ambazo zilikutwa  katika kompyuta mpakato (laptop) ya Mwigamba ambayo alinyang’anywa baada ya kudaiwa alikuwa anasambaza taarifa za kuhujumu chama hicho.
Kikao hicho kilimalizika saa 10:00 alfajiri huku maamuzi hayo yakifanywa siri na Mbowe alipoulizwa kuhusu kuwepo kwa taarifa za Zitto na Dk Mkumbo kuvuliwa uongozi,” alisema , “Taarifa zitatolewa baadaye mchana.”
Wasomi wazungumza
Akizungumza na gazeti hili jana, Profesa Gaudence Mpangala alisema Chadema ni chama kikubwa kinachoweza kushinda uchaguzi mkuu ujao hivyo kinapaswa kuwa na viongozi walioshikamana na kuwa na nia moja.
Aliongeza kuwa endapo wapo viongozi wanaoonekana kwenda kinyume na viongozi wenzao na kwenda kinyume  na misimamo ya Chama, kinayo haki ya kufanya maamuzi ya namna yoyote yenye lengo la kukinusuru.
“Chadema ni chama kikubwa kinachoweza kushika dola…kinahitaji mshikamano mkubwa kwa viongozi wake na kuhakikisha hawatokei wasaliti….kama ni kweli waliosimamishwa ni wasaliti ni halali kabisa” anasema Profesa Mpangala.
Naye aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha SAUT, Dk  Charles Kitima alisema wakati umefika kwa vyama vya siasa kutambua kuwa uwepo wa demokrasia ndani ya vyama vingi vya siasa nchini ni kusahihishana na kujisahihisha.
Dk Kitima alisema kuwa na mitazamo tofauti siyo usaliti ni demokrasia na kusema endapo mtu au kiongozi anafanya kitendo cha kuvunja katika ya nchi huyo moja kwa moja anakuwa mkosaji.
Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF), Hamad Rashid anasema matukio ya kufukuzana na kutuhumiana baina ya viongozi yanayofanywa na watendaji mkuu wa vyama vya upinzani yatasababisha upinzani uzidi kudidimia na kudumaa.
Alisema vyama vya siasa vimekuwa na usultani wa kuonekana kuwa vinapaswa kuongozwa na baadhi ya watu, na wengine wenye uwezo na mawazo mapya na yasiyopendwa na wakubwa anatafutiwa mbinu ya kuondoka.
Rashid alisema hali hiyo inasababishwa na kukosekana kwa mfumo mzuri wa uongozi ndani ya vyama vya siasa, ambapo anasema vyama haviongozwi kama taasisi na badala yake vinaongozwa kama mali za watu.
“Hili linalotokea Chadema sasa ni matokeo ya mfumo mbovu wa uongozi ndani ya vyama vya siasa nchini….vingi haviongozwi kama taasisi.” alisema.
source: mwananchi

Thursday, November 21, 2013

Simba wapewa siri ya Mzungu


Kocha Zdravok Logarusic. 

Logarusic aliwahi kuinoa Gor Mahia ambayo Mapunda anaidakia mpaka sasa.
Dar es Salaam. Kipa wa Taifa Stars na Gor Mahia ya Kenya,Ivo Mapunda amewaonya wachezaji  wa Simba wenye tabia ya uzembe kwa kuwataka wabadilishe mienendo yao vinginevyo watakabiliwa na hasira za Kocha wao mpya, Zdravok Logarusic.
Uongozi wa Simba juzi ulimtangaza Logarusic raia wa Croatia kuwa kocha mpya wa klabu hiyo akichukua nafasi ya Abdallah Kibadeni aliyefungashiwa virago na aliyekuwa msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
Logarusic aliwahi kuiona Gor Mahia ambayo Mapunda anaidakia mpaka sasa. Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Mapunda alisema Simba imelamba dume kumtwaa kocha huyo ambaye alimwelezea kama mtu mwenye msimamo na asiyependa masihara kwenye kazi.
“Mimi niwapongeze Simba kwa kumchukua Logarusic kwani ni kocha mzuri najua hata wao wamemchukua baada ya kuvutiwa na rekodi zake.
Julio aridhia na kudai chake Simba
Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ amesema amepokea kwa mikono miwili uamuzi wa kumfuta kazi uliofanywa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo. 
Kamati ya Utendaji ya Simba juzi ilitangaza kumtimua Julio pamoja na aliyekuwa Kocha Mkuu wa timu hiyo, Abdallah Kibadeni ‘King’ kutokana na kile ilichodai kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao.
Mbali na kuwaondoa Julio na Kibadeni,kamati hiyo pia ilimsimamisha Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Rage baada ya kumtuhumu kukiuka katiba ya klabu hiyo.
Julio alisema,“mimi na mwenzangu tumeupokea kwa mikono miwili uamuzi wa kutufukuza kazi, kama wao walituita na kuingia mikataba na sisi ili tuifundishe Simba  na leo wameamua kuivunja sidhani kama kuna tatizo hapo, jambo la msingi mimi nipate haki zangu tu.
Naye Kibadeni alisema hana pingamizi na uamuzi uliofanywa na kamati hiyo dhidi yake.

source: mwananchi

Yanga yatikisa nchi nzima

yanga_a573c.jpg

WATAALAMU wa hesabu wana usemi wao wanaoupenda 'Namba haziongopi'. Ukirudisha usemi huo kwenye tathimini ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lugha nyepesi unayoweza kusema ni kwamba 'hakuna kama Yanga'.

Sahau kwamba imemaliza ikiwa kileleni na pointi zake 27. Takwimu za Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), zimethibitisha kwamba Yanga imeongoza takwimu zote kuanzia mapato mpaka idadi ya mashabiki walioingia uwanjani.

Takwimu zilitolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TPL, Silas Mwakibinga, ni kuwa Yanga imekusanya kiasi cha Sh334.2 milioni katika mechi 13 za mzunguko huo. Katika takwimu hizo, Simba SC ni ya pili kwa kupata Sh304 milioni huku timu iliyopanda daraja msimu huu, Mbeya City, ikiipiku Azam FC kwa kushika nafasi ya tatu kwa kujikusanyia Sh83.8 milioni. Azam imekusanya Sh67.1 milioni.(P.T)
Nyingine na fedha zilizokusanya katika mabano ni Coastal Union (Sh65. 7 milioni), Mtibwa Sugar (Sh49.9 milioni), Ruvu Shooting (Sh46.1 milioni), Tanzania Prisons (Sh38.1milioni), JKT Ruvu (Sh36.1 milioni), Ashanti United (Sh35.7 milioni), Rhino Rangers (Sh31.1milioni), Mgambo JKT (Sh25.8 milioni), Oljoro JKT (Sh20.8 milioni) na Kagera Sugar (Sh18.5 milioni).

"Huu ni mwanzo tu wa kusimamia ligi na mpaka sasa hatujafikia lengo letu, tunataka kuona kila timu inakuwa na uwiano sawa wa makusanyo na kama kuzidiana, basi iwe kiasi kidogo, tumefurahishwa na mwenendo wa Mbeya City ambao wamefanya mambo makubwa japo wapo katika msimu wa kwanza," alisema Mwakibinga.

Kwa upande wa mashabiki walioingia viwanjani, Yanga pia imekuwa kinara kwa kuingiza mashabiki wengi katika mechi. Jumla ya mashabiki 107,890 wa timu hiyo wameingia katika mechi na kufuatiwa na Simba ambao wameingiza mashabiki 97,364 mpaka mwisho wa mzunguko huo.

Timu ya Mbeya City imezidi kung'ang'ania nafasi ya tatu na kuendelea kuitambia Azam FC kwa kuingiza mashabiki 43,439 tofauti na Azam ambao mpaka sasa wameingiza mashabiki 30,236.
Nyingine ni Coastal Union (mashabiki 27,880), Mtibwa Sugar (20,794), Rhino Rangers (20,263), Prisons (19,923), Ruvu Shooting (19,000), JKT Ruvu (16,095), Ashanti United (16,093), Mgambo (11,726) na JKT Oljoro (10,430).

Kwa mujibu wa Mwakibinga, jumla ya Sh 2.4 bilioni zimekusanywa katika mzunguko huo wa kwanza. Kiasi hicho ni ongezeko la Sh599. 5 milioni katika mzunguko wa kwanza wa msimu uliopita.
"Hii ni historia na hasa ukizingatia kuwa baadhi ya mechi zimekuwa zikionyeshwa 'laivu' katika televisheni na baadhi ya mashabiki kuangalia kupitia luninga zao, lakini bado tumezidi kupata makusanyo makubwa," aliongeza Mwakibinga.

"Haya ni matokeo mazuri ya kuzinadi mechi za ligi na mfano mzuri mechi ya Yanga na Mbeya City ambayo iliweka historia kwa kuingiza Sh100 milioni na huku tiketi zikiwa zimemalizika kufikia saa 5:00 asubuhi ya siku ya mchezo."

Kwa upande wa viwanja, Uwanja wa Taifa unaongoza kwa kukusanya fedha nyingi mpaka sasa ambapo kiasi cha Sh1.8 bilioni kimepatikana hapo, kiwango hicho ni sawa na asilimia 75 ya mapato yote ya mzunguko wa kwanza.
Uwanja wa Sokoine wa Mbeya umeshika nafasi ya pili kwa kukusanya Sh260.5 milioni na kufuatiwa na Mkwakwani wa Tanga Sh105.264 milioni.

Viwanja vingine na mapato yake ni Ali Hassan Mwinyi wa Tabora (Sh100.2 milioni), Sheikh Amri Abeid wa Arusha (Sh57.4 milioni), Azam Complex wa Dar es Salaam (Sh32.1 milioni), Kaitaba wa Bukoba (Sh26.1 milioni), Manungu wa Turiani, Morogoro (Sh9.4 milioni) na Mabatini wa Mlandizi, Pwani (Sh3.584 milioni).

Chanzo:Mwanasport mtandaoni

Babu Seya maisha yake yote jela

babuseya_d763c.jpg

Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania imetupilia mbali ombi la warufani wawili Nguza Viking na mwanaye, ambao waliomba mahakama hiyo kufanya marejeo ya uamuzi wake wa awali wa kuwapata na hatia kama ambavyo hukumu dhidi yao ilivyotolewa na mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mwaka 2004.
Nguza Viking, maarufu kama Babu Seya na watoto wake watatu walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya kubaka na kulawiti watoto.

Mwaka 2010, rufaa yao ilisikilizwa katika Mahakama ya Rufaa, na kuwaachia huru Nguza Mashine na Francis Nguza baada ya kuwaona hawana hatia katika makosa yote waliyoshitakiwa.
Baada ya rufaa hiyo, Babu Seya na mwanaye Papii Kocha walipatikana na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu ya kifungo cha maisha jela.(P.T)

Tarehe 30 Oktoba mwaka huu, Mahakama ya Rufaa iliyoketi chini ya jopo la majaji watu, likiongozwa na Nathalia Kimaro, akisaidiana na Mbarouk Mbarouk na Salum Masati walisikiliza hoja za pande zote kuhusu ombi la kufanyika mapitio ya uamuzi wa awali wa mahakama hiyo.

Alhamisi, Mahakama ya Rufaa baada ya kufanya mapitio ikiwa imeketi chini ya majaji watatu, imeendelea kuwaona warufani hao wawili kuwa na hatia na hivyo kuendelea kutumikia adhabu yao.
Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili wao Mabere Marando uliomba kupitiwa upya kwa uamuzi huo, ukidai kuwepo kasoro katika ushahidi uliowatia hatiani, ikiwemo kukosekana kwa mashahidi muhimu katika kesi hiyo.

Majaji walisema kuwa kuna uthibitisho kuwa warufani hao wawili waliwabaka watoto wa shule ya msingi mwaka 2003.
Kesi hiyo imewashtua mashabiki wa mwanamuziki Viking nchini Tanzania na kanda nzima ya Afrika Mashariki.

Mwanamuziki huyo mwenye kuimba nyimbo za Rhumba, ambaye ni mzaliwa wa DRC, ameishi Tanzania kwa miaka mingi na kuwa na mashabiki wengi.
Mwandishi wa BBC Ben Mwang'onda mjini Dar es Salaam anasema kuwa Nguza Viking na mtoto wake Johnson Nguza maarufu kama Papii Kocha ambaye pia ni mwanamuziki, walifika mahakamani hapo kusikiliza hatma yao.

Walionekana kuwa watulivu wakati majaji walipotupilia mbali ombi lao kutaka hukumu yao kubatilishwa.
Walihukumiwa kwa kuwabaka wasichana 10 wa shule ya msingi waliokuwa kati ya umri wa miaka sita na nane wote waliokuwa katika shule ya msingi ya Mashujaa wilayani Kinondoni mjini Dar es Salaam.
Wakili wa muimbaji huyo alisema kuwa mwanamuziki huyo hana matumaini tena ya kupewa rufaa kwani hili ndilo ombi lake la mwisho.

chanzo: mjengwa blog

Hofu yatanda Kamati Kuu Chadema

chadema_e1f4c.jpg
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (katikati) akiwa na walinzi wake akiwasili katika Jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, jana kushiriki kikao cha Kamati Kuu ya chama hicho. Picha na Michael Jamson
Hali ya wasiwasi iligubika eneo kinapofanyika kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kilichoanza Dar es Salaam jana.
Ulinzi mkali wa walinzi wa Chadema (Blue Guard), uliimarishwa katika ukumbi wa Ubungo Plaza kinapofanyika kikao hicho ambacho kinatarajiwa kumalizika leo, huku kukiwa na maagizo yaliyoashiria kuwapo kwa mambo mazito.
Maazimio ya kikao hicho yanasubiriwa kwa hamu na wafuatiliaji wa mambo ya siasa nchini kwani kinafanyika katika kipindi ambacho chama hicho kikuu cha upinzani nchini kinapita katika misukosuko na hasa ya malumbano baina ya makamanda wake wa juu.(P.T)
Maelekezo ya ulinzi
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliwasili ukumbini hapo saa 5.20 asubuhi na baada ya kuingia, wapiga picha waliruhusiwa kuingia kuchukua kumbukumbu ya tukio hilo kwa dakika moja tu.
Waandishi wa habari hawakutakiwa kuingia na badala yake walielezwa kuwa wangepewa taarifa baadaye.
Wakati wapiga picha wakiwa ndani, mmoja wa wajumbe wa mkutano huo alitoka na kutoa maelekezo kwa walinzi wa Chadema akiwataka kuwa makini kutekeleza kazi yao watakapopewa amri ya kumwondoa mjumbe yeyote mkutanoni.
"Kama mkipewa amri ya kuondoa mtu ingieni na mtekeleze amri hiyo mara moja," alisisitiza mjumbe huyo na kuingia ndani haraka. Walinzi hao zaidi ya 10, walipokea maelekezo hayo kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na amri hiyo.
Kikao kufunguliwa
Kikao hicho ambacho kilifunguliwa dakika nane baada ya Mbowe kuwasili, kilipangwa kujadili mambo matatu jana.
Mmoja wa wajumbe wa mkutano huo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kingepitia taarifa za vikao viwili vya Kamati Kuu vilivyopita.
Suala jingine ambalo lilipangwa kujadiliwa jana ni ushiriki wa Chadema katika uchaguzi mdogo wa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Kiembesamaki, Zanzibar na kupitia taarifa ya fedha.
Leo moto
Ajenda zinazotarajiwa kujadiliwa leo ni pamoja na ripoti ya utekelezaji wa Kampeni ya 'Movement For Change' (M4C) na hali ya siasa.
Ajenda hiyo inatazamiwa kugusa matukio ya hivi karibuni ndani ya chama hicho. Hayo ni pamoja na malumbano kati ya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, kusimamishwa kwa Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, kuvunjwa kwa uongozi wa Mkoa wa Mara na pia kuondolewa kikaoni kwa Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda.
Zitto na Lema waliingia katika vita ya maneno mwanzoni mwa Novemba kuhusiana na masuala ya posho ya vikao.
Vita hiyo ilianzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita aliposema kuwa Zitto anafanya unafiki kukataa posho.
Lema alimtuhumu Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.
Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususan, mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.
Akijibu hoja hizo, Zitto alisema tangu siku nyingi alikwishapiga marufuku kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.
Alisema tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), alipiga marufuku posho na pia aliwahi kuwashtaki Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wabunge wanaochukua posho kutoka taasisi za Serikali.
Zitto pia alipata msukosuko mwingine baada ya kusambazwa ripoti inayoitwa 'Taarifa ya Siri ya Chadema' iliyomtuhumu kuwa alikuwa anashirikiana na CCM na viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa kuhujumu chama hicho.
Ripoti hiyo inayodaiwa kuwa iliandaliwa na Idara ya Upelelezi ya Chadema, ilieleza kuwa Zitto alikuwa akipokea fedha kutoka kwa maofisa wa usalama na kuzisambaza kwa makada wengine wa chama hicho ili wafanye kazi ya kukihujumu. Hata hivyo, Chadema kupitia kwa Mnyika ilitoa taarifa kupinga vikali suala hilo.
CAG kukagua ruzuku
Pia, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na CAG. Chadema ilipinga vikali madai hayo na kueleza kuwa imekuwa inatumia taasisi binafsi kufanya kazi hiyo.
Suala jingine linalotazamiwa kujadiliwa katika kikao hicho ni kusimamishwa kwa Mwigamba na Baraza la Uongozi Kanda ya Kaskazini ambako kulizuka vurugu kiasi cha kunyang'anywa kompyuta mpakato (laptop) baada ya kudaiwa alikuwa anasambaza taarifa za kuhujumu chama hicho.
Suala lake linasubiri uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kama lile la kuvunjwa kwa uongozi wa Chadema wa Mara.
Pia kitendo cha Baraza la Kanda ya Ziwa Mashariki kumtimua Shibuda kwa madai kwamba halina imani naye nacho kina uwezekano mkubwa wa kujadiliwa.
Zitto na Mnyika wakosekana
Zitto na Mkurugenzi wa Uenezi wa chama hicho, John Mnyika walikuwa miongoni mwa wajumbe walioshindwa kuhudhuria jana.
Zitto yuko na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) huko Sudan Kusini na Mnyika pia yuko katika ziara ya kibunge Uturuki.
Kikao cha jana kilihudhuriwa na wajumbe 23 kati ya 32.
Chanzo:Mwananchi