WHATEVER YOUR ARE BE A GOOD ONE;

A nation that is afraid to let its people judge the truth and falsehood in an open market is a nation that is afraid of its people. John F. Kennedy

“Taifa letu – taifa lolote – ni zuri na mahali pazuri pa kuishi kama raia wake watalifanya liwe hivyo. Uongozi wake unaweza kuwa mzuri, mbaya au usiojali lakini kama watu wake wameamka (ki-elimu?) na wanajitambua, haitachukua muda mrefu kuwakilisha mtazamo wa jamii na kubadili mawazo na matumaini ya taifa.” Julius Kambarage Nyerere


Tuesday, July 31, 2012

DICOTA 2012 CONVENTION - AUGUST 30 - SEPTEMBER 2,2012


Dear MEMBERS OF DICOTA and FRIENDS:
You are invited to attend the DICOTA 2012 Convention – themed “Tanzania’s Diaspora - Investment, Citizenship and Relationship” – to be held at the Chicago Marriott O'Hare, 8535 West Higgins Road · Chicago, Illinois 60631 U.S.A. from 30th August to 2nd September, 2012.


The former President of Zanzibar, H.E Aman Abeid Karume is the invited Guest of Honor


The convention brings together members of the Tanzanian Diaspora in the United States America, Tanzanian private sector and government officials; key decision makers from Tanzania and U.S. businesses; financial institutions, and international organizations with vested interest in investment and growth in the country. The conference presents attendees with the latest trade and investment opportunities in all sectors of the economy, while providing a forum for potential partnership formation through many networking opportunities.
This year we will have a very important session to discuss about our inputs to the Commission which is reforming Tanzanian Constitution. Come and make your views heard and be part of this important milestone in our History.

Please make time and Plan to attend this Extra-Ordinary Convention. Click here to register, early Registration with Great discount Ends August 16, 2012. For more Information about Convention Registration, Hotel Discount Rates and Program visit us at www.dicotaus.org. You can also contact us by emailconvention@dicotaus.org or call  1-952-217-0265 to reach a convention steering committee representative.

Sincerely,
Dr. Ndaga Mwakabuta,
DICOTA - President

Monday, July 30, 2012

Zitto Ahojiwa Kwa Rushwa



SAKATA la wabunge kuhusishwa na rushwa limeingia sura mpya, baada ya Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe kuhojiwa na chama chake cha Chadema kwa saa tatu jana.
Wakati Zitto akihojiwa, kambi rasmi ya upinzani bungeni, iliwataja wabunge saba wa CCM na kueleza kuwa ndiyo wanaolichafua Bunge kwa kujihusisha na mambo yenye maslahi binafsi wakiwa watumishi wa umma.

Kadhalika, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alisema kwamba Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ilikuwa ikiendelea kuwahoji baadhi ya wabunge kuhusu tuhuma za rushwa na kwamba uchunguzi ukikamilika taarifa zitawekwa wazi.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa Tweeter kwamba alihojiwa na Sekretarieti ya chama chake kutokana na tuhuma za rushwa zinazowagusa badhi ya wabunge.
Katika maelezo yake, Zitto alisema aliiambia sekretarieti ya chama hicho kwamba Chadema kifanye uchunguzi ili kubaini ukweli wa suala hilo na kwamba yuko tayari kuwajibika ikiwa itathibitika kwamba alihusika kula rushwa.

“Kwa saa tatu nimejieleza mbele ya sekretariati ya chama kuhusu tuhuma za rushwa dhidi yangu. Niliomba kutaka kutoa maelezo kwa Katibu Mkuu, nimekiomba chama kufanya uchunguzi na ikibainika hatua zichukuliwe,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo kwenye Tweeter.

Lissu ataja wengine
Kwa upande wake, Mnadhimu Mkuu wa kambi hiyo, Tundu Lissu aliwataja wabunge wa CCM ambao wanatuhumiwa kuwa ni Nasir Abdallah (Korogwe Mjini), Mariam Kisangi (Viti Maalumu), Vicky Kamata (Viti Maalumu) na Charles Mwijage (Muleba Kaskazini) ambao hata hivyo, wote wamekanusha madai hayo.

MWANAHALISI KUFUNGIWA NI JAMII YA WA-TANZANIA AU YA WAGAGAGIGIKOKO - PROF. MBELE



Nimekuwa hapa Tanzania kwa wiki sita, na nimesoma nakala za MwanaHalisi zilizotajwa hapa. Nimejumuika na wananchi katika kujadili mambo mengi, likiwamo suala la ripoti na uchambuzi wa MwanaHalisi.

Kila mahali nilipopita, kama vile Tanga, Arusha, Dar es Salaam, na Songea, wananchi wanalipenda na kuliheshimu gazeti la MwanaHalisi. Mhariri Saeed Kubenea anaheshimiwa na kushukuriwa na wananchi kwa kazi yake anayoifanya kwa umakini. Huo ndio mtazamo wa wananchi, nilivyoshuhudia. Sasa serikali inavyodai kuwa MwanaHalisi halina tija kwa jamii, lazima niulize ni jamii gani hiyo? Ni jamii ya wa-Tanzania au ya Wagagagigikoko?

Kitendo cha serikali kulifungia gazeti hili ni kitendo cha uchochezi, kwa maana kwamba kitawaudhi au watu. Kama serikali inadhani kitendo hiki kitawaridhisha wananchi, itafakari upya.

Serikali haikatazwi kuandika makala ndefu kwenye magazeti yake, kukanusha taarifa zinazochapishwa na MwanaHalili. Ingekuwa na utaratibu wa kufanya hivyo, na kuzimisha hoja za MwanaHalisi kwa hoja, ningeiheshimu hii serikali. Lakini kwa vitendo hivi vya kutumia mabavu, serikali inajivunjia heshima mbele ya jamii.

Siku za karibuni, MwanaHalisi imekuwa ikiripoti habari za Dr. Ulimboka. Kitendo cha kulifungia gazeti hili kinatatanisha na kuzua masuali. Mungu amemnusuru Dr. Ulimboka. Wengi tunamwombea apone, atupe taarifa zaidi za yale yaliyompata. Tunahitaji kujua.

Sasa je, kama serikali inasema taarifa za MwanaHalisi ni uzushi, je serikali inapangia kumzuia Dr. Ulimboka asiwaeleze wananchi mambo hayo?

Serikali ingekuwa na busara, ingetafakari sana masuala haya ya Dr. Ulimboka kama yalivyoripotiwa na MwanaHalisi. Kulizuia gazeti hili, nahisi kutaimarisha dhana iliyozagaa katika jamii kwamba serikali inahusika katika shambulio dhidi ya Dr. Ulimboka. Inawezekana serikali haihusiki, lakini vitendo hivi vinaweza kuwa ni vya hasara kwa serikali yenyewe.

Nimalizie kwa kusema kwamba naudhika na vitendo vya kuhujumu haki yangu ya kusoma ninachotaka kusoma. Ni mtu mzima na nina akili zangu. Naweza kuchambua chochote ninachosoma. Serikali inapozuia gazeti au kupiga marufuku kitabu naona
inawatukana wananchi, kwamba hwawana akili ya kusoma na kuchambua mambo. 


Source: http://www.wavuti.com

NIMEIPENDA HII YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE


Sunday, July 29, 2012

Neno La Leo: Na Wabunge Wetu Wengine Ni Wezi, Hakyamungu!



Ndugu zangu,

Waziri Muhongo ameusema ukweli wake kule Dodoma. Nami nimefuatilia sinema hii ya Dodoma, kila inavyoendelea ndivyo ninavyozidi kuchoka. Ama hakika, tunakokwenda siko, tuna lazima ya kujipanga upya.

Namsifu Waziri Muhongo kwa ujasiri wake. Amutusaidia sana kuyajua yale ambayo yangetuchukua muda mrefu kuyajua. Kwa kusimama kwenye ukweli Waziri Muhungo ameitendea haki nchi yetu tuliyozaliwa. 

Na tulipofikia hapa ni ukweli tu ndio utakaotusaidia kutupa ahueni ya hali mbaya tuliyonayo kama taifa. Huu si wakati wa kutanguliza siasa za vyama bali kuitanguliza Nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda. Kutanguliza uzalendo.

Leo tunabaki vinywa wazi kusikia kuwa hata wachungaji, na wengine wamejiingiza Bungeni, kuwa nao wanawaibia Watanzania wenzao. Kwamba nao hawatosheki. Wanaiba huku wakitaja neno la Mungu. Leo hata wale wanaojinadi kuwa ni watetezi wa wanyonge wameanza kutiliwa mashaka. Uwezo wao wa kiuchumi unahusianishwa na ' madudu' kama haya ya Tanesco. Na kuna hata wenye ' kuwafuturisha' wenzao wenye uwezo kwa fedha walizowaibia  wananchi wanyonge. Hawa hawana cha swaumu bali wanashinda na njaa kwa dhambi ya wizi wao.

Tuna lazima sasa ya kuamka na kuwabana wezi wetu. Mwizi ni mwizi tu, hata kama ni mheshimiwa Mbunge.Na ukweli ndio unaohitajika sasa. Na si nusu ukweli, bali ukweli mzima hata kama  utatugharimu maisha yetu. 

Nimepata kusimulia   kisa cha kijana aliyehangaika sana kuusaka ukweliKatika pitapita zake akaliona duka. Kibao kimeandikwa dukani ; ” Hapa tunauza ukweli”.

Dukani hapo ukweli unauzwa kwa kilo. Bei ya robo kilo ya ukweli imeandikwa, vivyo hivyo, bei ya nusu kilo ya ukweli. Lakini, mwenye duka hakuandika bei ya ukweli mzima,  kwa maana ya kilo nzima ya ukweli.

Kijana yule akauliza; ” Mie nataka ukweli kilo nzima, mbona hujaandika bei?”
” Alaa,  unataka kilo nzima ya ukweli?” Aliuliza mwenye duka.
” Naam” Akajibu kijana yule.
” Basi, zunguka uje ndani nikuambie bei yake”.

Alipoingia ndani dukani, kijana yule akaambiwa;
” Kijana, hatukuandika bei, maana, gharama ya ukweli mzima ni uhai wako. Je, uko tayari?”

Kijana yule akatimua mbio. Nyuma aliacha vumbi. Hakuwa tayari kulipa gharama yaukweli mzima.

Katika Uislamu inasemwa;  sema ukweli, hata kama unauma na kwamba unaweza kupelekea umauti wako.

Hakika, maandiko ya kwenye vitabu vya dini zetu hizi yana ya kutufundisha. 

Na hilo ni Neno langu la Leo.

Maggid Mjengwa,
Sweden.

Thursday, July 26, 2012

SAKATA LA KUZAMA KWA MV.SKAGIT


Taarifa Kwa Umma 


Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake leo Malindi Mjini Zanzibar.

Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar imezifutia rasmi hati ya kufanya kazi Meli ya Mv.Kalama, Mv.Seagul na Mv.Sepideh kutokana na meli hizo kutokukidhi hali ya usalama wa abiria katika meli hizo.

Aidha meli hizo zimepewa muda wa mwezi mmoja kuanzia leo kuhakikisha zimeondoka katika maeneo ya Zanzibar kabla ya hatua zaidi kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa Meli hizo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Usafiri wa Baharini Zanzibar Abdullah Husein Kombo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Afisini kwake kuhusu hali ya usafiri wa baharini na usalama Zanzibar.

Amesema Mamlaka hiyo imefanya tathmini na uhakiki wa kutosha na kujiridhisha kuwa Meli hizo hazifai kufanya kazi katika maeneo ya Zanzibar jambo ambalo limepelekea kuchukua hatua za kufuta hati za kufanyia kazi meli hizo.

Amefahamisha kuwa sababu kuu zilizopelekea Mamlaka kufanya maamuzi hayo ni pamoja na uchakavu,umri wa meli hizo kuwa mrefu na kupata matatizo mara kwa mara katika safari zao.

Kombo amefahamisha kuwa Sheria ya Mamlaka ya Usafiri na Bandari Zanzibar ya mwaka 2006 kifungu cha 17.1 inampa mamlaka Msajili wa Meli kuifuta meli yoyote ambayo itakuwa haikidhi usalama wa abiria.

Kufuatia sheria hiyo Kombo amesema watawataka wamiliki wa Meli hizo kuzirudisha hati za kufanyia kazi meli hizo ili waende kutafuta sehemu nyengine za usajili kinyume na maeneo ya Zanzibar.

Akizungumzia Meli ya Mv.Serengeti Kombo amesema wamelazimika kuiagiza meli hiyo kupunguza idadi ya abiria kutoka watu 800 hadi 350 na tani za mizigo kutoka 100 hadi 50 hadi pale ambapo watajiridhisha kutokana na hali ya meli hiyo ilivyo.

Aidha amegusia kuwa Kampuni ya Bakhresa italeta Meli kubwa ya abiria itakayofanya kazi zake Zanzibar ambapo pia Serikali ya Mapinduzi nayo iko mbioni kuhakikisha wanaleta meli inayokidhi mahitaji ya wananchi wa Zanzibar.

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Tuesday, July 24, 2012

TAARIFA YA SERIKALI KUHUSU KUZAMA KWA MELI MV. SKAGIT





KAULI YA SERIKALI KUHUSU TUKIO LA KUZAMA KWA MELI YA MV. SKAGIT ILIYOTOKEA TAREHE 18.07.2012 KATIKA ENEO LA BAHARI YA CHUMBE

=======================================

Mheshimiwa Spika;

Kwa heshima naomba kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujaalia kukutana hapa leo tukiwa wazima na wenye afya njema. Pili, naomba nichukue nafasi hii adhimu kukushukuru wewe Mheshimiwa Spika kutupatia fursa hii adhimu ili kuwasilisha mbele ya Baraza lako Tukufu taarifa ya maafa ya kuzama kwa meli ya MV. Skagit iliyotokea katika bahari ya Chumbe tarehe 18.07.2012. 

1.0 Utangulizi

Mheshimiwa Spika,
Meli ya MV. Skagit ilitengenezwa nchini Marekani mwaka 1989 na imesajiliwa Zanzibar tarehe 25/10/2011, na kupewa nambari ya usajili 100144. Meli hiyo ina uzito wa GRT96 ambayo inamilikiwa na kampuni ya Seagull Sea Transport Limited ya Zanzibar.

Mheshimiwa Spika,
Mnamo tarehe 18.07.2012 majira ya saa saba na nusu za mchana ilipatikana taarifa ya ajali ya kuzama kwa meli ya MV. Skagit katika bahari ya chumbe nje kidogo ya mji wa Zanzibar. Meli hiyo ilikuwa katika safari zake za kawaida ya kutoka Dar-es-Salaam kuja Zanzibar.

Kwa mujibu wa manifest ya abiria iliyowasilishwa na wamiliki wa meli kwa Mamlaka ya Bandari Tanzania (Tanzania Ports Authority-TPA) na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini na Nchi Kavu Tanzania (Surface and Marine Transport Authority-SUMATRA), meli hiyo ilikuwa imechukua jumla ya watu 290 wakiwemo abiria watu wazima 250, watoto 31 na mabaharia 9.

Mheshimiwa Spika,
Taarifa hii inaelezea kwa kina juu ya hali halisi ya tukio pamoja na hatua zote zilizochukuliwa kuanzia tarehe 18/07/2012 hadi hivi sasa.

Mheshimiwa Spika, 
Mara baada ya tukio hili, Kamati ya Kukabiliana na Maafa ya Taifa ilikutana kwa ajili ya kuweka mikakati ya hatua za kuchukua pamoja na kuandaa taarifa rasmi ya Serikali kwa wananchi kupitia vyombo vya habari. Aidha, Baraza la Mapinduzi lilikaa usiku wa tarehe 18.07.2012, na kutoa maagizo juu ya hatua za kuchukua ikiwemo kuwepo kwa matayarisho katika hospitali ya mnazi Mmoja ya kupokea majeruhi, kutayarisha eneo la Maisara kwa ajili ya mapokezi na utambuzi wa maiti; kutayarisha eneo la kuzika miili ya marehemu huko Kama; kuweka takwimu sahihi za majeruhi na waliofariki katika ajali hiyo; pamoja na kutolewa kwa taarifa rasmi ya hali ya uokozi iliyokuwa inaendelea.


2.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Mheshimiwa Spika
Kufuatia maagizo hayo ya Serikali, hatua zifuatazo zilichukuliwa: -
  • Vituo cha mapokezi ya wahanga wa ajali hiyo vilifunguliwa katika maeneo ya Bandari ya Malindi, Hospitali ya Mnazi Mmoja na uwanja wa Maisara.
  • Vikosi vya Ulinzi na Usalama vilipelekwa katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha huduma za ulinzi na uokozi wa haraka.
  • Kazi ya uchimbaji wa makaburi katika eneo la Kama ilifanyika kwa mashirikiano makubwa ya viongozi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Vikosi vya Ulinzi na Usalama pamoja na wananchi. Jumla ya makaburi 80 yalichimbwa.
  • Sala na dua maalum ya kuwaombea marehemu wote ilifanyika baada ya sala ya Adhuhuri jana tarehe  22.07.2012 katika misikiti yote ya Unguja na Pemba na Kitaifa ilifanyika katika Msikiti wa Mwembeshauri mjini Zanzibar.
  • Kuorodhesha majina ya wale wote ambao wanasadikiwa walikuwemo ndani ya chombo kilichopata ajali na hadi sasa hawajulikani walipo. Taarifa hizi zinakusanywa kupitia ngazi ya Shehia na Wilaya kwa Unguja na Pemba na kwa Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa Tanzania Bara.
  • Kutoa huduma ya kuwasafirisha majeruhi baada ya kupata matibabu kurudi makwao.
  • Kutoa huduma za usafiri kwa walioshiriki katika shughuli zote za operesheni.
 

3.0 MATOKEO YA OPERESHENI

3.1 Shughuli za uokozi

Mheshimiwa Spika;
Kutokana na operesheni iliyofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kwa mashirikiano makubwa ya wananchi yamepelekea hadi kufika tarehe 22.07.2012 kuwa na idadi ya watu waliookolewa wakiwa hai kufikia 146 na miili ya waliofariki dunia iliyopatikana kufikia 73. Kati ya maiti hizo 68 zilipokelewa kituo cha Maisara na 5 zilipelekwa moja kwa katika eneo la makaburi la Kama kwa vile maiti hizo zilikuwa zimeshaharibika.

Kwa waliookolewa wakiwa hai waliweza kufikishwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kwa uchunguzi na matibabu. Hadi hii leo, majeruhi wote walishatibiwa na kuruhusiwa kurudi majumbani mwao.

Mheshimiwa Spika;
Katika kituo cha Maisara maiti zilipangwa ili kuwawezesha ndugu na jamaa kutambua maiti zao na kwa kurahisisha kazi hiyo, Shirika la Utangazaji kupitia kituo chake cha Televisheni kilichukua picha za sura za marehemu na kuzionyesha zikiwa tayari zimewekewa namba ili kurahisisha utambuzi na uchukuaji wa maiti hizo. Kupitia utaratibu huu, jumla ya maiti 50 zilitambuliwa na kukabidhiwa jamaa na ndugu zao kwa ajili ya mazishi. Idadi ya maiti ambao hawakutambuliwa ni 23 na mazishi yao yalisimamiwa na Serikali katika eneo la Kama. Aidha, maiti mmoja aliyetambuliwa alilazimika kuzikwa Kama kwa vile mwili wake ulikuwa umeharibika sana sambamba na ndugu wa marehemu huyo kutochukuliwa na jamaa na ndugu zake. Kila maiti alizikwa katika kaburi lake chini ya usimamizi wa mashekhe kutoka Ofisi ya Mufti na Wakfu na Mali ya Amana.

Aidha, katika kituo cha Maisara huduma za uoshaji na sala ya maiti zilitolewa na pia wale wote waliochukua maiti wao walipatiwa usafiri, sanda na ubao kwa ajili ya kuzikia.

3.2 Juhudi za kuitafuta meli na watu waliokuwa hawajaonekana

Mheshimiwa Spika,
Katika jitihada za Serikali za kuhakikisha miili zaidi ya marehemu iliyotokana na ajali ya meli inapatikana, Serikali ilivitaka vikosi vyake ulinzi na usalama vikiongozwa na KMKM kuendesha zoezi la kuitafuta meli na miili iliyosalia. Kazi ya kuendesha operesheni ya kuitafuta meli pamoja na abiria ilianza mara tu baada ya kusikia kutokea kwa ajali hiyo. Jumla ya watu waliohai 146 waliokolewa siku hiyo na maiti 31 zilipatikana.

Asubuhi ya tarehe 19.07.2012, wazamiaji kutoka KMKM, Jeshi la Wananchi wa Tanzania na makampuni binafsi walifika katika eneo la tukio kwa ajili ya kuanza kazi rasmi. Wazamiaji hao walifanikiwa kupata maiti 37 na hawakupata abiria aliye hai. Hata hivyo, wazamiaji hao hawakuweza kuiona meli.

Mheshimiwa Spika
Vikosi hivyo viliendelea na jitihada za kuitafuta meli na watu waliokuwa hawajaonekana kwa kujigawa katika makundi matatu. Makundi mawili yalihusika na kazi ya utafutaji wa watu katika maeneo ya ukanda wa eneo la tukio. Kundi jengine lilijihusisha na kazi ya uzamiaji (diving) kwa ajili ya kuitafuta meli chini ya bahari.

3.3 Kukusanya taarifa za watu waliokuwa hawajaonekana kupitia Ofisi za Masheha na Wilaya:

Mheshimiwa Spika,
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliziagiza ofisi zote za Wilaya na Shehia kuorodhesha majina ya watu waliokuwa hawajaoneka na waliofariki na kuziwasilisha orodha hizo kwa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ili kufanyiwa uhakiki na kupata orodha sahihi kwa ajili ya matumizi na kumbukumbu za baadae. Hadi kufikia tarehe 22.07.2012 zaidi ya watu 100 wameripotiwa hawakuonekana ama wakiwa hai au maiti. Hata hivyo, kwa uhakiki wa awali imebainika kwamba baadhi ya watu wameorodheshwa zaidi ya mara moja katika maeneo tofauti.

3.4 Viongozi Wakuu wa Kitaifa kutoa mkono wa pole

Mheshimiwa Spika
Viongozi Wakuu wa Kitaifa pamoja na viongozi wengine wanatarajiwa kufanya ziara za kutoa pole na kuzifariji familia zilizofiliwa na zilizopotelewa na ndugu zao kwa maeneo yote yalizoathirika Unguja na Pemba. Kazi hiyo inatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

3.5 Kuratibu upokeaji wa misaada

Mheshimiwa Spika
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa iliendelea kupokea misaada ya kifedha na vifaa kutoka kwa watu binafsi, Mashirika ya Kimataifa, Mashirika ya Umma, Mashirika yasiyo ya Kiserikali na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi.

Hadi kufikia tarehe 22.07.2012 jumla ya Shilingi320,000,000/-zimepokelewa na kuingizwa katika akaunti ya Mfuko wa Maafa Zanzibar (Zanzibar Disaster Funds) ilioko Benki ya Watu wa Zanzibar, ambayo imefunguliwa maalum kwa ajili ya michango ya aina hiyo. Aidha, vifaa na bidhaa mbalimbali zimepokelewa  kwa ajili ya kusaidia shughuli za operesheni ya uokozi.


4.0 GHARAMA ZA OPERESHENI

Mheshimiwa Spika
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliipatia Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa jumla ya shilingi milioni ishirini (20,000,000/-) kwa ajili ya kugharamia shughuli za operesheni ambapo hadi kufikia tarehe 22.07.2012 fedha zote zilikwisha tumika.


5.0 TULICHOJIFUNZA KUTOKANA NA TUKIO HILI (LESSONS LEARNED)

Mheshimiwa Spika
Kutokana na tukio hili la kuzama kwa meli ya MV. Skagit tumeweza kujifunza mambo mbalimbali ambayo ni changamoto kwetu katika kuimarisha kazi na huduma za kukabiliana na maafa nchini. Miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo: -
  • Umakini na maamuzi sahihi na ya haraka yaliyochukuliwa na viongozi wetu yameweza kuleta ufanisi mkubwa katika operesheni ya uokozi na hivyo kupelekea kuokoa maisha ya wananchi wetu wengi.
  • Muitikio wa haraka wa taasisi mbalimbali za kukabiliana na maafa, zikiwemo taasisi za Serikali, vyombo vya ulinzi na usalama, Sekta Binafsi na Jumuiya za Kiraia umepelekea watu wengi kuweza kuokolewa wakiwa hai pamoja na kupatikana kwa maiti hali ambayo imewezesha maiti wengi kuzikwa na familia zao.
  • Kutokana na wananchi wengi kutumia mtandao wa mawasiliano wa Zantel, kulisababisha ugumu wa mawasiliano kutokana na minara ya kampuni hiyo kuzidiwa na matumizi.
  • Udogo wa sehemu ya kuhifadhia maiti (motuary) ulipelekea maiti wasiotambuliwa na jamaa zao kuzikwa haraka na Serikali.
  • Uhaba wa vifaa vya kisasa vya uokozi pamoja na wataalamu wa uzamiaji (divers) umepelekea zoezi la uokozi kuwa gumu na kuchukua muda.
  • Kukosekana kwa taarifa za uwezo wetu wa ndani wa kukabiliana na maafa ikiwemo uwezo wa vifaa na wataalamu ni changamoto ambayo inapaswa kufanyiwa kazi.



6.0 SHUKRANI


Mheshimiwa Spika
Kwa mara nyengine tena kwa niaba ya Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa naomba nimshukuru Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa juhudi zake kubwa alizochukua ili kuhakikisha maisha ya wananchi yanaokolewa. Tunamshukuru kwa maelekezo yake na miongozo aliyotupatia ambayo kwa kiasi kikubwa ilitusaidia kufanikisha kazi za uokozi. Pia, tunamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maelekezo yao na msaada mkubwa walioutoa katika kukabiliana na maafa hayo. Aidha, tunamshukuru sana Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda kwa msaada mkubwa aliotupatia kupitia Ofisi yake.

Tunawashukuru pia Makamu wa Kwanza wa Rais Mheshimiwa Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa Mheshimiwa Balozi Seif Ali Iddi kwa kutupatia miongozo ya mara kwa mara katika jitihada za kuokoa maisha ya wananchi na kupunguza athari za maafa yaliyotokea.

Vile vile tunatoa shukrani za dhati kwa Baraza la Mapinduzi na Baraza la Usalama la Taifa kwa maelekezo yao juu ya hatua za kuchukuliwa katika kukabiliana na janga hili na majanga yanayoweza kutokea baadae. Shukrani za dhati pia zinatolewa kwa vyombo vya ulinzi na usalama kwa hatua zao za haraka zilizosaidia kuokoa maisha ya wananchi wengi. Pia tunaishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwa karibu nasi na kwa michango yao ya hali na mali katika kukabiliana na tukio hili la kusikitisha.

Mheshimiwa Spika
Shukrani pia zinatolewa kwa wamiliki wa vyombo vya usafiri majini, angani na nchi kavu kwa jinsi walivyoshirikiana na Serikali katika kulikabili tukio hili. Wananchi wa maeneo ya jirani hasa wavuvi na wamiliki wa hoteli na kampuni za kitalii wanapewa shukrani za pekee kwa jinsi walivyoshiriki kikamilifu tokea hatua za awali baada ya kupatikana taarifa za kuzama kwa meli ya Skagit. Tunashukuru washirika wa maendeleo na wawakilishi wa nchi marafiki kwa jinsi walivyolichukulia suala hili na kutuunga mkono katika msiba huu wa kitaifa. Vilevile tunazishukuru taasisi za kidini hasa Kamisheni ya Wakfu na Mali ya Amana na Ofisi ya Mufti kwa kusaidia maandalizi ya mazishi ya marehemu waliotokana na ajali hiyo.

Tunawashukuru madaktari na wauguzi wa hospitali ya Mnazi Mmoja kwa namna walivyoshirikiana na Kamati. Tunawashukuru wajumbe wote wa Kamati ya Kitaifa ya Kukabiliana na Maafa na wafanyakazi wa Idara ya Kukabiliana na Maafa kwa kazi kubwa waliyoifanya kwa kipindi chote toka kutokea kwa janga hili. Tunawashukuru wamiliki wa vyombo vya habari na wanahabari na wananchi wote wa Zanzibar na Tanzania kwa jumla kwa kupokea tokeo hili kwa masikitiko makubwa katika kukabiliana na janga hili. Aidha, tunawashukuru wale wote walioweza kuchangia kwa hali na mali katika msiba huu.


7.0 HITIMISHO

Mheshimiwa Spika, baada ya kutoa maelezo hayo nawaomba wajumbe wa Baraza lako tukufu waipokee taarifa hii na kutupatia ushauri ili uweze kutusaidia katika harakati za kukabiliana na maafa hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima naomba kuwasilisha.

Ahsanteni sana

………………………………

MOHAMED ABOUD MOHAMED [MBM]
WAZIRI WA NCHI
OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS
ZANZIBAR


Source: http://www.wavuti.com

Zanzibar:Waziri Ajiuzulu ; Tume Yaundwa


 


Waziri wa Mawasiliano na Miundombinu wa Zanzibar, Hamad Masoud amejiuzulu kufuatia shinikizo za watu na maandamano.

Kumekuwa na msukumo kutoka kwa makundi mbali mbali ya kutaka waziri huyo ang'atuke kufuatia kuongezeka kwa ajali za baharini kati Hatua hii imekuja kufuatia madai ya wananchi kuwa ajali za meli zimekuwa zikiongezeka mjini Zanzibar bila yeye kuchukua hatua yeyote.

Mbali na kujiuzulu kwa Hamad kama Waziri, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein ameunda Tume ya kuchunguza kiiina cha Meli hiyo ya MV Skagit kuzama na kuuwa watu.

Mwenyekiti wa tume hiyo atakuwa Jaji Abdulhakim Ameir Issa, wanachama watukiwa Meja Jenerali S.S. Omar, Komanda Hassan Mussa Mzee, Kapteni Abdulla Yussuf Jumbe, Kaptein Abdulla Juma Abdulla, Salum Taoufiq,Kaptein Hatibu Katandula, Bi. Mkali Fauster Ngowo, Ali Omar Chengo na Shaaban Ramadhan Abdalla Katibu wa Tume.

Kufuatia shinikizo hizo Siku ya Ijumaa ,tarehe 20 Julai ,Hamad Masoud alimuandikia barua rais wa Zanzibar kumuomba kujiuzu.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chama tawala cha CCM, Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein amekubali ombi la Waziri Hamad Masoud kujiuzulu.
Kufuatia kujiuzulu kwa waziri huyo, Rais ,Dk Shein amemteua Mbunge wa Jimbo la Ziwani Rashid Seif Suleiman kuwa Waziri mpya wa Miundombinu na Mawasiliano.

Taarifa kutoka ikulu zinasema kuwa, uteuzi wa Bwana Rashid Seif Suleimna utaanza mara moja.

Habari kwa Hisani ya Mjengwa Blog

Sunday, July 22, 2012

KUZAMA KWA MV SKAGIT;


JE SERIKALI ZETU ( JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NA SERIKALI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR) ZIMEGUNDUA NINI?


Kwa niaba ya Blogs ukadirifu na mungupamojanasi,  tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya ajali ya meli ya MV SKAGIT,iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar kuelekea Zanzibar, ambayo imesababisha watanzania wenzetu zaidi ya 40 kupoteza maisha yao na wengine wengi kujeruhiwa. Napenda kuungana na watanzania wote katika kutoa mkono wa pole kwa familia na ndugu zetu ambao wamepotelewa na wapendwa wao katika ajali mbaya na ya kusikitisha ya Mv. Skagit ambayo ilitokea tarehe 19 July 2012. Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema  tunaomba aendelee kuwafariji majererui wa ajali hii na kuwawezeshe kupona haraka ili waendelee na majukumu yao ya kulijenga Taifa.


Kama watanzania tutaendelea kumshukuru Mungu kwa ndugu zetu ambao wametangulia mbele ya haki kutokana na ajali hii pamoja na ukweli kuwa ajali hii ni uzembe mkubwa sana unaotokana na mikono ya baadhi ya watendaji na wasimamizi wa sheria za usalama wa abiria ambao wamekabidhiwa  Dhamana ya usimamizi wa sheria hii kwa masalahi ya Taifa; lakini kwa makusudi au katika kutimiza haja zao binafsi wanasababisha maafa makubwa kwa Taifa.

Ninajaribu kutafakari katika makala hii, matukio makubwa ya ajali za majini achana na ajali mbaya zinazohusiha barabara. Kama Mtanzania najaribu kujiuliza maswali mengi ambayo hayapati majibu; lakini swali langu kubwa ambalo litatawala makala hii ni hili:

Je baada ya tukio  baya ambalo lilikuwa kubwa na la kusikitisha sana ambalo lilihusisha Mv Bukoba May 21,mwaka 1996 ambapo zadi ya watu 800 walipoteza maisha, kwa nini sisi kama Taifa tumeruhusu ajali nyingine mbili mbaya kutokea katika pwani ya Zanzibar katika kipindi ambacho hakizidi mwaka mmoja?


Lakini kabla ya kufikiri kuwa sasa mambo yote ni sawa Hata mwaka haijapita  tangu ajali mbaya ya MV Spice Islander iliyozama pwani ya nungwi na kuua watanzania wenzetu zaidi ya 200. Na hata mwaka haujeisha wiki hii tumeshuudia kuwa  Mv. Skagit ambayo ilikuwa na abiria zaidi ya 200 nayo ikipatwa na ajali mbaya na kupoteza zaidi ya watanzania 40 katika pwani ya chumbe.

Tukijaribu kusahau ajali ya Mv. Bukoba takribani miaka kumi na tano iliyopita; pamoja na msemo wa Kiswahili usemao kuwa “ajali haina kinga” lakini ajali hizi mimi binafsi zinanirudisha katika kipengele kimoja kikubwa kuwa kama Taifa tumeshindwa kusimamia sheria zetu sihusuzo usala wa Raia wakiwa safarini; hapa mimi naweza kusema kuwa ninapima uwezo dhaifu wa wahusika ambao kama Taifa tumewapa dhamana ya kuzisimamia sheria zetu.

Tatizo nyingine kuna ugumu gani wa kutunza kumbukumbu za wasafiri ambao wanasafiri na chombo husika; tumekuwa Taifa ambalo hata takwimu za abiria ambao wamesafiri au wamehusika na ajali hazipo kama ziko haziko sahihi; Ajali ikitokea ndipo taarifa zinaanza kutafutwa; matokeo yake taarifa zinazotolewa zinatofautiana, na inakuwa ni aibu kubwa kwa pengine kuwaeleza wananchi taarifa ambazo sio sahihi:

Ama kweli ni aibu kubwa inakuwa kwa Waziri mwenye dhamana anapotamka takwimu ambazo sio sahihi na zinaendelea kubadilika kulingana na mazingira ya uokoaji; ni ikitokea kuwa mimi ni waziri mwenye dhamana na sina uhakika na usahihi wa takwimu hizo, sitaweza kutamka takwimu hizo kwani kwa kufanya hivyo tunaendelea kuimarisha mfumo mbovu  wa ukusanyaji wa takwimu za wasafiri.

  • Je vyombo vyetu vya majini hufanyiwa ukaguzi wa kina vinapoingizwa nchini wakati wa kusajiliwa, kubaini kuwa chombo kinafaa kwa matumizi ya kweli ya binadamu?


  • Je wakaguzi wa wizara hufanya nini au hukagua nini kabla ya chombo kuondoka?


  • Je usalama wa Taifa ambo wanakuwa katika bandari zetu wnafanya nini wananagalia nini yaani hata abiria wakijazwa wao hubaki kimya bila kutoa taarifa katika ofisi husika?


  • Kwa maneno mengine kwamba vyombo vyetu vinapoondoka bandarini havikaguliwi?


  • Watanzania wengi tunaendelea kujiuliza kwa nini meli ijaze kupita kiasi?


  • Ni nani msimamizi wa meli zetu na kwa nini meli zetu zisichukue watu kulingana na uwezo wake?


  • Sasa tufanye nini katika kuzuia ajali hizi zisiendelee kumaliza Taifa letu katika siku za usoni?


Lazima tukubali kuwa kujifunza kutokana na ajali hizo kuwa vyombo vingi vya usafiri vibovu ambavyo vinanunuliwa kuletwa kwetu baada ya kutumika sana katika nchi husika na kisha hupakwa rangi na kufanyiwa matengenezo madogo ka msingi huu vimekuwa vimepoteza sifa ya kusafirisha abiria na mizigo yao; kwa sababu ya ubovu wa vyombo hivyo na kwa sababu ya ukiukwaji wa sheria ambao huwafanya wamiliki kupakia abiria wengi kuliko uwezo wake nap engine ikitokea hali ya hewa mbaya (upepo ambo utasababisha mawimbi makubwa) chombo kama hicho hakiwezi kuhimili kishindo itaishia kukosa mwelekeo na hatamaye kupinduka tu.

Wengi tunajiuliza ilikuwaje mamlaka zinazohusika zikaruhusu meli iliyobeba abiria zaidi ya uwezo wake ikaruhusiwa kusafiri?  Au pengine wahusika wa usalama wa abiria bandari walipokea chochote ndipo wakaruhusu meli kuondoka? Lazima tukubali kukosolewa ajali hizi zote sababu yake kubwa ni uzembe wa utendaji kazi wetu;  uzembe huu ulisababisha yaliyotokea Mv Bukoba, mv spice islander na sasa Mv Skagit bado tumekuwa wagumu wa kujifunza.

Je Professionality ya manahodha wetu iko wapi?  Ningekuwa mimi    nahodha  ningethubutu kusema hatuondoki hapa mpa abiria wapunguzwe. Vile vile katika hali mbaya ya hewa ninge sitisha safari kwa usalama wa Watanzania wenzangu. Tumeyaona haya katika nchi za wenzetu ambao wanaheshimu sheria za usalama wa abiria:

Je Concord baada ya ajali ziko wapi? Nimeshangaa tu kwa nini mnjanja mmoja hajezinunua na kuzileta kwetu kwenye nchi ya majaribio ya vitu chakavu na vyema matatizo ya kiufundi:

Ni aibu kubwa sana kwa wataalamu ambao ndio wanatumaliza kwa tamaa zao binafsi ambao wanashindwa kuwashauri wamiliki wa meli aina gani ya meli wanunue wameshindwa kutumia  maadili ya kazi zao katika kuwasaidia wamiliki kufanya uamuzi sahihi. Sasa fikiria taarifa za kuwa Mv. Skagit kabla ya kuja kwetu; Undani wa ajali ya meli hii ni kama ifuatavyo: Meli iliponunuliwa ilikuwa tayari imekwishatumika. Meli hii ina miaka zaidi ya 35 ya uhai wake sasa mmiliki wa chombo hiki alipata ushauri kabla ya kununua chombo hiki au alipuuzia ushauri?

Tunaomba serikali zetu ziangalie zaidi katika Viwango (standards)  za meli zetu hapa naendelea kujiuliza kuwa je kweli tuna meli zenye viwango kulingana na bahari Zetu?


Wataalamu wetu naamini kabisa wanao uwezo uwezo wa kuangalia mambo haya kisayansi na kuyaelewa na kuja na mapendekezo ya kisayansi  yanaweza kutunaweza kuondokana kwa kiasi kikubwa cha ajali hizi kama tutafanikiwa kuandaa utaratibu wa Usimamiaji wa sheria za usalama wa abiria kwa msingi wa maadali yake; pamoja na kuzingatia Usimamiaji na ubora wa vyombo vya usafiri na ukaguzi wa kuona kama vinafikia kiwango kinachostahili
Je sisi watanzania ni kweli wavivu wa kufikiri na  kufanya maamuzi sahihi kama abiria kwani chombo cha usafiri kikijaa tunalazimishwa kupanda?


Jamani kwani sisi kama wananchi huru tunakuwa tayari kupanda chombo wakati tunaona hali ya chombo? Na wala sio shetani kama tunavyojiambia na tunayaweka maisha yetu rehani tena kwa makusudi na lolote baya likitokea tunaanza kulaumiana.

baada ya matukio haya yoye pengine ni wakati muufaka kwa serikali kufikiria ununuzi wa meli kubwa kama ilivyokuwa huko nyuma ambayo inaweza kukidhi haja ya watanzania wanyonge. Pengine kwa njia hii tunaweza kujenga msingi madhubuti kuhakikisha uzembe wa aina yoyote ule unaepukwa kulinda isije kutokea ajali kama hizi.

Kama mheshimiwa Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dk. Shein ambaye alisema kuwa “Nimesikitishwa sana na msiba huu, Katika wakati huu si vema tukaanza kulaumiana jambo la muhimu hivi sasa  ni kuokoa maisha ya watu”  maneno haya ni mazito lakini hatutatenda haki kama hatutaendelea kuwakumbusha watendaji husika umuhimu wa kurekebisha vyanzo vya ajali  kama nilivyoainisha hapo juu ili kuliepusha taifa hili kuwa na wasimamiaji wabovu wa sheria na kuiepusha nchi yetu nzuri Tanzania katika majanga ya ajali za kila siku;

Nina amini kuwa kama nchi (Tanzania); ni nchi ambayo wananchi wake wanaishi sio katika nchi inayotawaliwa na sheria za msituni, bali hutawaliwa na sheria halali na tuliepushe Taifa hili na mbinu za wenye nguvu ndio wanaofaidika kwa nguvu zao na kufanya chchote wanachotaka kwa faida binafsi. Kama Taifa wakati umefika wa sisi kama wananchi kuamka na kujitambua. 


MUNGU IBARIKI TANZANIA

Thursday, July 19, 2012

JK Na Mama Salma Kikwete Watua Zanzibar Kutoa Rambirambi




Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimsikiliza Bw.  Kitwana Makame Haji, mmoja wa majeruhi walionusurika katika ajali ya meli waliolazwa katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja mjini Unguja jioni ya leo.
Rais Jakaya Kikwete akimpa pole Bi Salome Abeli, mfanyakazi wa Tanzania Automic Energy Commission jijini Arusha, aliyekuwa njiani kuelekea Pemba kikazi kabla ya kupatwa na ajali hiyo ya meli. Amesema hali yake inaendelea vyema hapo katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakipita mbele ya miili ya waliokufa katika ajali hiyo ya meli jana karibu na kisiwa cha Chumbe. Hapa ni uwanja wa Maisara ambako miili huletwa kwa kutambuliwa.


TAIFA LINAPOENDELEA KUOMBOLEZA KUFUATIA AJALI NYINGINE MBAYA YA MELI HEBU TUJIKUMBUSHE "POST HII YA SEPTEMBER 16/2011


SHERIA ZETU TUNAPOZIPA MUHALI NI UWAJIBIKAJI AU UZEMBE?


KUFUATIA AJALI YA MELI YA “MV SPICE ISALANDER “SISI KAMA TAIFA TUFANYE NINI KUEPUSHA HALI HII ISITOKEE TENA?

Mwishoni mwa wiki kulitokea ajali mbaya ya kupinduka kwa Meli na kuzama, ajali ambayo imesababisha vifo vya watanzania wenzetu zaidi ya 200 wengi wao wakiwa wananwake na watoto, ajali ambayo ilitokea katika bahari ya Hindi katika eneo lenye mkondo mkali wa Nungwi ikiwa inaelekea Pemba;

Msiba huo ni mkubwa kitaifa kwani umekatisha maisha ya watanzania wenzetu ambao ni nguvu kazi yetu kwa maendeleo yetu; wengi wa aliofariki ni wazazi wa familia zetu na watoto ambao walikuwa wanaandaliwa kwa ajili ya maendeleo yetu ya kesho.

Kwa mara nyingine nachukua nafasi hii kutoa pole kwa  kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa wazazi kwa msiba huu mkubwa. Na kwa viongozi wetu wakuu wa taifa letu Raisi wa Serikali ya Mapinduzi Ya Zanzibar pamoja na timu yake yote ya uongozi; Raisi wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania na timu yake vile vile;

Swali ambalo limenigusa sana siku hii ya leo ni hili kwa nini ajali hii ilitokea?

Ni kweli imekuwa ajali kama ajali ambayo imekuja bila hodi na haikuwezekana kabisa kuepukwa?

Je ni ajali ambayo imechangiwa na uzembe wa usimamizi wa wajibu wetu kama watendaji?

Je ni tatizo la uwajibikaji na kuweka rehani ya maisha ya watanzania  kwa kuendekeza “ muhali” na kushindwa kusimamia na kukemea sheria katika atendaji pale panapohitaji kufanya hivyo?

Je ni tatizo la tamaa ya wamiliki wa vyombo na wasimamizi wa miradi hivyo kushindwa kufuata taratibu zinazoongoza biashaya zao?

Mwananchi wa kawaida atajiuliza lakini serikali zetu ziko wapi katika kuwajibika?

Au zinasubiri kuwajibika baada ya tatizo kutokea au hufanya kazi vipi ( management in crisis or management after crisis or crisis management)?

Leo naungana na kauli ya Waziri katika Afisi ya Makamo wa pili wa Rais, Mhe Mohamed Aboud Mohamed

 “amesema,kuwa kamati maalum itaundwa ili kuchunguza juu ya ajali hiyo na ikibainika kuwa uzembe umepatikana sheria itachukua mkondo wake”. ..
”kuwa tatizo kubwa la wazanzibari ni muhali, na amesema ili utendaji mzuri uwepo, lazima suala hili la muhali liwekwe upande ili nchi ipige hatua za maendeleo, na ikibainika kuna watu wanafanya uzembe wa kikazi lazima hatua za sheria zichukuliwe”

Tunaipongeza kauli hii ya awali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuwa itawachukulia hatua za kisheria wale wote watakaobainiika kufanya uzembe uliosababisha kuzama kwa meli ya Spice Islanders huko katika mkondo wa Nungwi na kusababisha vifo vya watu watanzania wenzetu zaidi ya 200.

Wasiwasi wangu ni huu kuwa, pamoja na kusisitiza umuhimu wa kuangalia na kukagua kila mara vyombo vya usafiri ili kunusuru ajali ambazo zinaweza kuepukika. 


Je wakibainika kwa uzembe huu watachukuliwa hatua za kweli ambazo zitakuwa fundisho kwa wamiliki na watendaji wengine?

Tatizo letu kama taifa siku zote tume zinazoundwa zinaishia kuwa ni viini macho tu na hakuna msukumo wa kweli wa adhabu ambazo zinakidhi haja na haki kwa wafiwa;

Kwa nini meli hiyo ilipakia kupita uwezo wake? Kwa nini captain alikubali kuendelea na safari? Kama yuko hai inapasa awajibishwe kulingana na uzito wa madhara ambayo yametokea  tusimwonee muhari;

Je tunaweza kuthubutu kama serikali ya China inavyothubutu kwa raia wake ambao wanasababisha hasara kwa taifa? Wao hawana mchezo;

Kama tukiweza kuthubutu kwa wavunjaji sheria, uwajibishaji huu tutaweza kuzilinda na kuzitekeleza sheria  na kanuni ambazo zimewekwa kwa ajili ya vyombo vya usafiri ili kudhibiti na kuzuia ajali zisitokee, kwa bahati mbaya sana baadhi ya wamiliki wa vyombo hivyo huacha kufuata kanuni hizo ama kwa makusudi na masilahi binafsi.

Ni kweli kuwa ajali haziepukiki, lakini ajali nyingine husababishwa na uzembe wa wamiliki pamoja nawatendaji wake na hili ndilo lilitokea wiki iliyopita huko Nungwi. 

Natoa wito kwa wadau wote kushikamana katika kuhakikisha vifo vinavyosababishwa na ajali vinapungua kama si kumalizika kabisa kama tukisimama pamoja na kukataa kuburuzwa na wenye mali na kuweza kuwakatalia wengine kupanda kwenye ambacho kimejaa kulingana na uwezo wake tutakuwa tumeweza kuthubutu kwa masilahi ya taifa. 

udhaifu wa usimamiaji wa sheria na muhali umetupa wakati mgumu wa kujua meli hiyo ilikuwa na abiria wangapi? Kwa nini kunakuwa na taarifa ya idadi inayotofautiana? Huu ni uzembe ambao kwa kweli hautakiwi kuendelea kuvumiliwa;

Mwisho tunaiomba Serikali  yetu ambayo ndio muhimili wa maisha bora ya raia wake na usalama wao kuhakikisha inasimamia  utekelezaji wa sheria zake; serikali lazima ithubutu katika  kuwawajibisha wote waliohusika na kuwachukulia adhabu kali na kuacha MUHALI